Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, July 4, 2015

UKURASA WA 185; Bila Kuwajua Watu Hawa Watatu Na Kumalizana Nao, Sahau Kuhusu Mafanikio.

Kuna watu watatu ambao kwa wewe kujua au kutokujua wamekuwa wanakuzuia kufikia mafanikio.
Sio kwamba wao wanakuja na kukuzuia wewe kufikia mafanikio, ila kwa sababu yao wewe mwenyewe umeshindwa kufikia mafanikio kwenye maisha yako.
Aina ya kwanza ya watu hawa ni watu ambao unataka kuwalinda. Kuna watu ambao wewe unataka kuwalinda na hivyo unajizuia kufikia mafanikio ili uendelee kuwalinda. Kuna baadhi ya watu wanaogopa kufikia mafanikio kwa sababu wanataka kuendelea kuwa na watu wanaowazunguka. Kuna wafanyakazi ambao wanaogopa kuonesha ubora wao kwenye kazi zao kwa sababu wanaogopwa kuchukiwa na wenzao au kuonekana ni hatari kwa mabosi zao.
SOMA; Wajue Watu Hawa na Waepuke Kwenye Maisha Yako.
Aina ya pili ni watu ambao unajaribu kuwaadhibu. Kuna watu ambao unaweza kuwa unataka kuwaadhibu na hivyo ukajizuia wewe kufikia mafanikio. Labda wazazi wako hawakukupatia kile ulichofikiri kingekuwa bora kwako. Na hivyo unataka uwaoneshe kwamba walikosea na hivyo wewe huwezi kufikia mafanikio kama ya wengine.... kwa sababu ya kutojali kwao.
Aina ya tatu ni watu ambao unataka kuwafurahisha. Hawa ni watu ambao unataka kuwafurahisha ili waendelee kukuona kama wanavyopenda kukuona na hivyo kujizuia kufikia mafanikio. Kuna watu ambao wanalazimika kuvaa mavazi ya bei ghali, kuendesha magari ya bei ghali na hata kuishi maeneo fulani ili tu waonekane.
Wajue watu hawa watatu kwenye maisha yako na malizana nao, hakikisha unaishi maisha uliyochagua wewe mwenyewe, yatakayokufikisha kwenye mafanikio unayotaka na sio kuwalinda watu, kuwaadhibu au kuwafurahisha.
TAMKO LA LEO;
Nimeamua sasa kwamba sitaki tena kuwalinda watu, kuwaadhibu au kuwafurahisha. Nahitaji kuishi maisha ambayo yatanipa furaha na kunifikisha kwenye mafanikio na sio maisha ambayo yatanirudisha nyuma. Nitaweka juhudi na maarifa ili niweze kuwa bora zaidi ya nilivyo sasa.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment