Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, January 16, 2015

Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Kama utaamua kupuuza ushauri mwingine wowote ambao unausoma sehemu mbalimbali basi shika ushauri huu mmoja tu. Shikilia ushauri huu na kila siku jikumbushe maana ni muhimu sana kwako ili kuweza kufikia ndoto zako.

Hii ni kwa sababu tunaishi kwenye jamii ambayo inajaribu sana kuturudisha nyuma.

Huenda mwaka huu 2015 umeweka malengo makubwa ambayo unajua kama ukiwez akuyafikia maisha yako yatabadilika kwa kiasi kikubwa sana. Lakini nakuhakikishia ukiwaeleza watu kumi malengo yako uliyojiwekea watu saba watakuambia haiwezekani, wawili watasikiliza hawatakuambia kwamba haiwezekani kwa sababu wanaogopa kukuumiza ila ndani ya nafsi zao wanaamini huwezi kuyafikia. Mmoja atakupa moyo kwamba unaweza japo na yeye anaweza kuwa hana uhakika sana.

Ukweli ni kwaba unapokuwa na malengo makubwa watu wengi watakuambia huwezi, haiwezekani, haijawahi kufanywa, kuna wenzako walijaribu wakashindwa na utaambiwa kila aina ya hadithi ya kukuonesha ni jinsi gani haiwezekani.

Cha kushangaza watu hawa wanaokuambia haiwezekani hawajawahi kujaribu na wala hawana uhakika na wanachoongea. Na mbaya zaidi wakishakuambia hivyo wanasahau baada ya dakika tano.

Yaani dakika tano baada ya mtu kukuambia kwamba lengo lako la kuwa bilionea haliwezekani, anasahau alichokwambia na anaendelea kufikiria matatizo yake mwenyewe kwenye maisha yake.

Sasa kitu muhimu cha kukumbuka kila siku ni kwamba hakuna anayeweza kukuambia ni nini unaweza au nini huwezi. Wewe mwenyewe ndio unaamua unafanya nini na maisha yako na kisha kufanya.

Ukiendelea kuwasikiliza watu kila siku hutafanya lolote, wakati watu hao wanasumbuliwa na matatizo yao wenyewe.

Maisha ni yako uchaguzi ni wako, chagua kuwasikiliza watu na uishie kuwa na maisha ya hovyo, au chagua kujisikiliza mwenyewe na uwe na maisha unayotaka wewe mwenyewe.

Chukua hatua… JISIKILIZE.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment