Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, January 17, 2015

Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku.

Dunia ina maajabu mengi sana, na sehemu kubwa ya maajabu hayo hayapo mbali sana kwani unayafanya wewe mwenyewe kwenye maisha yako kila siku.

Ni maajabu kwa sababu haiingii akilini unawezaje kufanya mambo hayo kwenye maisha yako na huku ukishindwa kufanya mengine ya muhimu zaidi kwenye maisha yako.

Unaweza kupanga kikosi cha machester united, arsenal, simba au yanga ila huwezi kupanga maisha yako. Yaani unajua kabisa ni wapi kocha amekosea mpaka timu ikashindwa ila hujui ni wapi wewe umekosea mpaka maisha yako hayaendi kama ulivyotegemea.

SOMA; Hii Ndio Hasara Ya Kutokuwa Na Malengo.

Unajua Dimond analipwa kiasi gani, ana magari mangapi mazuri, ana wapenzi wangapi ila hujui utawezaje kuboresha kipato chako, hujui maisha yako ya kesho yatakuwaje na huna malengo yoyote unayoyafanyia kazi kila siku.

Unaweza kukosoa ni jinsi gani kila mtu anayejaribu kitu kipya anakosea, ni jinsi gani hataweza kufanikiwa na kwa nini asiendelee kupoteza muda wake. Ila cha kushangaza hujawahi kujaribu kufanya kitu chochote kipya kwenye maisha yako, umejawa na hofu ya kufanya makubwa na hujiamini.

Haya ni maajabu ya dunia, maana hakuna njia nyingine tunayoweza kuyaita.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

Jali maisha yako, sikukatazi kufuatilia haya ila weka kipaumbele kwanza kwenye maisha yako, maana hayo mengine yatapita, ila maisha yako yatabaki kuwa na wewe. Kama yatakuwa magumu yataendelea kuwa na wewe mpaka mwisho.

Maisha Yako, Chaguo Lako..

Makirita Amani.

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment