Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, January 4, 2015

NENO LA LEO; Hawa Ndio Watu Wenye Furaha Zaidi.

Remember that the happiest people are not those getting more, but those giving more. –H. Jackson Brown, Jr.

Kumbuka kwamba watu wenye furaha zaidi sio wale wanaopokea vingi bali wale wanaotoa vingi.

Huwezi kuwa na furaha kwa kuwa mtu wa kupokea tu. Ukishakuwa mtu wa kupokea tu unaweza kujiona wa chini, ya kwamba huna msaada kwa wengine bali wewe ndio wa kusaidiwa.

Unapokuwa mtu wa kutoa unakuwa na furaha sana kwa sababu unaona na wewe una mchango kwenye maisha ya watu wengine.

Anza sasa kutoa zaidi ya unavyopokea, uzuri ni kwamba jinsi unavyotoa ndio jinsi unavyozidi kupokea, hii ni sheria kama huamini jaribu.

Huna cha kutoa? Toa chochote, iwe upendo, iwe tabasamu, iwe ushauri mzuri au hata kwa kumtumia rafiki yako ujumbe huu au kushare kwenye facebook hapo chini, utakuwa umetoa kitu kwa wengine na utapokea zaidi na zaidi.

Nakutakia siku njema.

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment