Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Showing posts with label FIKRA TOFAUTI. Show all posts
Showing posts with label FIKRA TOFAUTI. Show all posts

Tuesday, March 3, 2015

Nikiwa Mkubwa Nataka Kuwa Muosha Magari.

Katika pita pita zangu kwenye mtandao nimekutana na habari moja ambayo Mh January Makamba alishirikisha watu.

Alikutana na watoto wa mtaani, mmoja anasoma mwingine hasomi. Alimuuliza yule asiyesoma akiwa mkubwa anataka kuwa nani, yeye akajibu anataka kuwa muosha magari.

kuosha magari

Habari nzima ni ya kusikitisha, kwa sababu watoto hawa wana maisha magumu sana kama ilivyo kwa watoto wengine wa mtaani.

Lakini kilichonifanya niandike hapa ni jibu la mtoto huyo ambalo limenifanya nifikiri zaidi, na nione kuna shida kubwa kwenye jamii yetu kwa sasa.

Zamani mtoto alikuwa akiulizwa anataka kuwa nani, haijalishi kama ameenda shule au la alijibu bila ya wasi wasi kwamba angependa kuwa rubani, daktari, mwalimu, askari, dereva na mengine mengi.

Kwa sasa naona mashujaa wa watoto wanapungua sana, ndio maana unaweza kuona mtoto mdogo anafikiria akiwa mkubwa awe muosha magari. Hii inaweza kutokana na ukweli kwamba watu pekee anaowaona karibu yake ni waosha magari, au jamii imeshamwambia kwamba watu wa aina yako wanaishia kuosha magari.

Hatudharau kazi ya kuosha magari, maana kuna wanaoifanya kitaalamu na inakuwa biashara nzuri. Ila kwa akili ya mtoto na kwa mazingira ya kitanzania wote tunajua kwamba uosha magari anaoufikiria yeye ni upi.

Lengo la makala hii na wito wangu ni turudi kujenga mashujaa kwa vizazi vijavyo. Fanya kazi unayofanya au biashara unayofanya kwa ubora wa hali ya juu kiasi kwamba mtoto wako au wa jirani yako au wa ndugu yako atatamani sana kuwa kama wewe.

Ila kama wewe baba au mama au ndugu kazi yako ni chanzo kikuu cha matatizo kwako hakuna mtoto atakayependa kuishia kwenye matatizo kama yako.

Je upo tayari kuwa shujaa wa mtoto mmoja tu? Tuanze na tutaona mabadiliko makubwa kwenye jamii zetu.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Friday, January 30, 2015

Hakuna Kitu Chenye Maana...

Hakuna kitu chenye maana duniani,
Ila sisi wenyewe ndio tunavipa vitu maana.
Ukiweza kulijua hili, utajipunguzia matatizo mengi sana.
Kwa mfano kama unaona dhahabu ina maana, kuliko shaba, kumbuka vyote hivi ni madini ambayo yanapatikana kwenye ardhi. Tumeweka maana kubwa kwenye dhahabu kwa sababu haipatikani kirahisi kama shaba.
Kama nyama choma ni chakula cha maana, kumbuka huyu ni mnyama ambaye ameuawa na kuchomwa, hiyo maana nyingine tumeweka wenyewe.
Kama unaona pombe na mivinyo ya bei kali ni vitu vya maana, kumbuka haya ni matunda yaliyochachishwa, lakini sisi tumevipa maana.
Kitu chochote ambacho kina maana au kina thamani kubwa, hakijajipa thamani hiyo chenyewe.
Thamani hiyo tumevipa sisi wenyewe, hivyo usikubali kuteseka kwa sababu unaona huna vitu hivyo.
Chagua ni vitu gani cya maana kwako na vifanyie kazi.

Thursday, January 29, 2015

Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

Kama mpaka sasa huna utaratibu wa kujifunza kila siku, tayari upo nyuma sana katika kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako.

Kujifunza kila siku ni hitaji la chini sana la wewe kuweza kufikia mafanikio. Na tunaposema kujifunza kila siku ni kila siku kweli, jumatatu mpaka jumapili na kurudia tena na tena na tena.

Pamoja na umuhimu wa kujifunza kila siku, bado tunaishi kwenye jamii ambayo haitupi nafasi kubwa ya kujifunza. Hii ni kutokana na kuzungukwa na mazingira yenye changamoto nyingi zinazozuia kujifunza kila siku.

Kutokana na changamoto hizi ndio kulikonisukuma kutumia muda wangu kukupatia wewe nafasi ya kujifunza zaidi. Kupitia blog ya MAKIRITA AMANI utaweza kupata nafasi ya kujifunza kila siku, jumatatu mpaka jumapili.

Kila siku utaianza siku yako kwa neno la siku, hili ni neno ambalo litakupa hamasa ya kuweza kuifanya siku yako kuwa bora zaidi. Na pia kila siku kwa mwaka huu 2015 utapata ukurasa mmoja katika safu ya kurasa 365 za mwaka 2015. Kama bado hii haitoshi, unapata nafasi ya kupata kauli za kuhamasisha kutoka kwa viongozi na watu mashuhuri ambao wamefanikiwa sana. Na pia utaweza kupata hadithi za mafunzo ambapo utawez akujifunz akupitia visa mbalimbali.

Pamoja na haya yote utakuwa ukipata makala zenye fikra za kukuchokoza. Hizi ni zile ambazo zinaniingia kwenye fikra zangu kutokana na mawazo mbalimbali yanayonifikia katika kutafuta njia za kufanya maisha yangu na ya wewe msomaji kuwa bora zaidi kila siku.

Kwa kifupi wewe kutembelea blog hii ni sawa na kuwa na mimi pembeni yako, kwani utapata kitu kizuri kutoaka kwangu pale unapokihitaji.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za mbalimbali za kukufundisha na kukuhamasisha kila siku bonyeza hapa na uweke email. Kila siku kwenye email yako utapata mambo haya moja kw amoja.

Siku yako itakuwa bora sana kwa kuwa karibu na blog hii nzuri kwako.

Kama ningekuwa natoza wasomaji fedha kulingana na elimu ninayoitoa hapa, kila msomaji angetakiw akulipa tsh elfu moja kila siku. Hivyo kwa mwaka ungetakiw akulipa tsh 365,000/= ili kupata elimu hii muhimu sana kwako. Lakini sijataka wewe uingie gharama yoyote, gharama yako ni wewe kufungua blog, kusoma makala na kufanyia kazi yale unayojifunza.

Ombi moja muhimu sana kwako ni wewe kuwaalika watu wengi zaidi kusoma blog hii. Haina gharama yoyote na wala haitakuja kuw ana gharama yoyote. Tafadhali tuma makala hii kwenye email za watu watano, itume kama ilivyo halafu nikopy kwenye email hiyo utakayotuma, tumia email makirita@kisimachamaarifa.co.tz kama hujui jinsi ya kukopi, wakati unaweka email ya unayemtumia chini yake kuna cc, hapo weka email yangu. Na mimi nitakupa zawadi nzuri sana ya kitabu cha mabadiliko ambacho bado nakiandika.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya kuboresha maisha yako.

TUPO PAMOJA SANA.

 

KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

Huwa tuna utaratibu wa kupunguza ukali wa maneno, kwa kiswahili tunaita tafsida.

Yaani badala ya kusema mtu amezaa tunasema amejifungua, japokuwa yote ni yale yale tu, ila kujifungua linapunguza ukali wa uhalisia wenyewe.

Maneno kama kujisaidia, kufanya tendo la ndoa na mengine mengi ni maneno mazuri yanayotumika badala ya maneno halisi ya vitendo hivi. Uzuri wa maneno haya ni kwamba yanapotumika kila mtu anajua maana ni ile ambayo unafichwa.

SOMA; Ushauri Kwa Wajasiriamali Kutoka Kwa Mwanzilishi Wa Facebook.

Sasa kuna neno moja ambalo lina tafsida yake, ila watu huwa wahaielewi kabisa hii tafsida. Neno hilo ni KAWAIDA.

KAWAIDA ni neno ambalo linatumika kuficha ukweli halisi ambao ni HOVYO.

Ukisema unafanya kazi kawaida maana yake unafanya HOVYO, kwa kiwango cha chini sana ambacho hakuna anayeweza kuvutiwa.

Ukisema wewe ni mfanya biashara wa kawaida maana yake wewe ni mfanyabiashara wa HOVYO ambae hujui unakoelekea na unafuata tu upepo.

SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Kinachokurudisha Nyuma.

Usikubali kabisa kuwa wa kawaida, namaanisha kuwa hovyo.

Chochote unachofanya, kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana ili yeyote atakayeona avutiwe, ashawishike kujua zaidi na hapa ndio thamani yako inaongezeka. Hata kama unafanya kazi ambayo unaona haiwezi kufanywa kwa kipekee wewe ibadili na ifanye kwa kiwango cha hali ya juu sana. Utaona mabadiliko makubw akwenye kazi yako na hata maisha yako kwa ujumla.

Ukikubwali kuwa wa kawaida, yaani kuwa HOVYO, umeamua kutopata mafanikio ambayo yanakusubiri. kuwa bora, kuwa tofauti, kuwa wa kipekee na utaona mafanikio yakikufuata wenyewe.

Kuanzia leo jiwekee marufuku kuwa HOVYO.

SOMA; Mambo 10 Unayotakiwa Kujua Kuhusu Uwekezaji.

Tuesday, January 27, 2015

Unataka Kuiona Dunia? Vua Miwani…

Unachokiona sasa hivi sio dunia halisi, bali ni dunia unayotaka kuiona wewe.

Hii ni kwa sababu kila mtu ni kama amevaa miwani yake ambayo inamuonesha kile anachotaka kuona.

Umewahi kuvaa miwani ya rangi? Unaonaje kitu unapokiangalia? Je unaonaje kitu kile unapovua miwani?

Hiko ndio kinachotokea kweye maisha yako ya kila siku. Unaona vitu kutokana na mtazamo wako, mawazo yako na hata matamanio yako.

SOMA; Njia Kumu(10) Za Kupata Utajiri Na Mafanikio.

Hali yoyote inayotokea, jinsi unavyoichukulia na jinsi utakavyokwenda nayo itategemea wewe unaionaje dunia .

Kama unataka kuiona dunia ya uhalisia, vua miwani, ondoa matarajio yote, ondoa hisia zinazoegemea upande mmoja na iangalie dunia kama vile ilivyo.

Utajifunza mengi na utaona fursa nyingi ambazo kwa sasa huzioni.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

Friday, January 23, 2015

Kitu Muhimu...

KITU MUHIMU NI KUKIFANYA KITU MUHIMU KUWA KITU MUHIMU...
Unaweza kuona sentensi hiyo ni rahisi sana ila pale unapojikuta umezama kati kati ya vitu ambavyo sio muhimu hapo ndio pa kuanzia.
Na mara kwa mara utajikuta unafanya kitu ambacho sio muhimu kwako.
Gundua haraka na fanya kitu muhimu.

Monday, January 19, 2015

Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Binadamu tunapenda kulalamika sana na hata kuwalaumu wengine. Hakuna mtu anayependa aonekane kwamba yeye ndio amechangia kusindwa kwa jambo fulani. Hivyo katika jambo lolote lile linalotokea watu hukimbilia kumtafuta mchawi, yaani mtu wa kulaumu.

SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku.

Sasa kwa tabia hii ya kulalamika na kulaumu inakurudisha sana wewe nyuma katika maendeleo ya maisha yako.

Huwezi kufikia mafanikio kama kila mara wewe ni mtu wa kulalamika na kulaumu wengine.

Leo hii nataka ufanye changamoto moja ambayo itakuwezesha kuondokana na tabia hii ili uweze kufikia mafanikio.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Kwa siku kumi kuanzia leo, jiepushe kulalamika au kumlaumu yeyote. Hakikisha siku nzima imesiha bila ya kulalamika au kulaumu. Ikitokea umefanya siku ya kwanz aila ya pili ukajisahau na kulalamika, unafuta na kuanz atena upya. Endelea hivi mpaka siku kumi ziishe bila ya kulalamikia kitu chochote.

Pia katika siku hizi kumi usimseme mtu kwa jambo lolote baya, yaani usisengenye, usishiriki majungu na wala usifanye umbea. Hizi ni tabia ambazo zinakurudisha sana nyuma.

SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Fanya changamoto hii na kama ukifanikiwa kukamilisha siku kumi nitumie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz kunijulisha umeionaje hali hiyo na pia nitakuwa na zawadi nzuri kwako.

Na changamoto ianze, tutakutana upande wa pili, KARIBU SANA.

Saturday, January 17, 2015

Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku.

Dunia ina maajabu mengi sana, na sehemu kubwa ya maajabu hayo hayapo mbali sana kwani unayafanya wewe mwenyewe kwenye maisha yako kila siku.

Ni maajabu kwa sababu haiingii akilini unawezaje kufanya mambo hayo kwenye maisha yako na huku ukishindwa kufanya mengine ya muhimu zaidi kwenye maisha yako.

Unaweza kupanga kikosi cha machester united, arsenal, simba au yanga ila huwezi kupanga maisha yako. Yaani unajua kabisa ni wapi kocha amekosea mpaka timu ikashindwa ila hujui ni wapi wewe umekosea mpaka maisha yako hayaendi kama ulivyotegemea.

SOMA; Hii Ndio Hasara Ya Kutokuwa Na Malengo.

Unajua Dimond analipwa kiasi gani, ana magari mangapi mazuri, ana wapenzi wangapi ila hujui utawezaje kuboresha kipato chako, hujui maisha yako ya kesho yatakuwaje na huna malengo yoyote unayoyafanyia kazi kila siku.

Unaweza kukosoa ni jinsi gani kila mtu anayejaribu kitu kipya anakosea, ni jinsi gani hataweza kufanikiwa na kwa nini asiendelee kupoteza muda wake. Ila cha kushangaza hujawahi kujaribu kufanya kitu chochote kipya kwenye maisha yako, umejawa na hofu ya kufanya makubwa na hujiamini.

Haya ni maajabu ya dunia, maana hakuna njia nyingine tunayoweza kuyaita.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

Jali maisha yako, sikukatazi kufuatilia haya ila weka kipaumbele kwanza kwenye maisha yako, maana hayo mengine yatapita, ila maisha yako yatabaki kuwa na wewe. Kama yatakuwa magumu yataendelea kuwa na wewe mpaka mwisho.

Maisha Yako, Chaguo Lako..

Makirita Amani.

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Wednesday, January 14, 2015

Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

Kuna kauli nyingi ambazo watu wengi hupenda kutumia.
Katika kauli hizi kuna ambazo hutusukuma mbele na kutufanya tufikie malengo yetu.
Pia kuna kauli nyingine zinaashiria kushindwa na kukata tamaa. Kauli hizi zinaweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa.
Zifuatazo ni kauli mbili za kuacha kutumia leo ili kuweza kifikia malengo yako.
1. Liwalo na liwe.
Hii ni kauli ya kuashiria kutojali watu wengine na kujali maslahi yako tu. Kauli hii inaweza kukufanya uchukue hatua ambayo utaijutia sana baadae. Acha kutumia kauli hii na acha kufanya mambo yanayokunufaisha wewe tu na kuwaumiza wengine.
2. Kama ipo ipo tu.
Hii ni kauli inayoashiria kukata tamaa na hivyo kuacha kufanya juhudi ili kufikia malengo yako. Unaposema kama ipo ipo tu maana yake unakubali kwamba huwezi kutengeneza maisha yako. Maana yake unapokea chochote kinachokuja mbele yako. Kama unakubali chochote ni vigumu sana kufikia mafanikio.
Kumbuka kufikia mafanikio unahitaji malengo ambayo utayafanyia kazi kila siku. Usikate tamaa, endelea kuweka juhudi hata pale mambo uyanapoonekana kuwa magumu.

Monday, January 12, 2015

Ni Nini Hasa Kinakuzuia Mpaka Sasa?

Huenda malengo uliyoweka mwaka huu uliweka pia mwaka jana, na mwaka mwingine kabla ya mwaka jana.
Umekuwa ukiweka malengo hayo hayo na muda mfupi unayasahau.
Unaanza mwaka kwa shauku...
Mwaka huu nitaanza kufanya mazoezi...
Mwaka huu nitaacha ulevi...
Mwaka huu nitaanzisha biashara...
Mwaka huu nitaboresha maisha yangu.
Ila mwezi wa kwanza unapoisha tu, malengo yako hukumbuki tena.
Unasubiri mwaka mwingine kuweka tena malengo.
Hebu leo kaa chini na UFIKIRI TOFAUTI...
Hebu acha mchezo huo wa kupanga ma kuacha.
Lazima kuna kitu ambacho mpaka sasa kinakuzuia hujafikia malengo unayopanga kufikia..
Je unakijua? Kama hukijui utaendelea na mchezo huu miaka nenda miaka rudi.
Kama umechoka na mchezo huu kaa chini leo na ujue kipi kinakukwamisha.
Kisha chukua hatua.

Saturday, January 3, 2015

Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya

Kazi yenyewe ni kufikiri vizuri(GOOD THINKER)
Kwa nini ni muhimu sana wewe kuwa mtu wa kufikiria(GOOD THINKER)
1. Watu wanaofikiria wanahitajika sana, mtu anayejua JINSI YA KUFANYA hakosi kazi, ila anayejua KWA NINI INAFANYWA anakuwa bosi wake.
2. Watu wanaofikiri wanatatua matatizo na hawakosi mawazo ya kujenga taasisi.
3. Watu wanaofikiri ni vigumu kujikuta kwenye matatizo yanayosababishwa na watu wengine. Ni vigumu watu kuweza kuwatumia kwa faida zao wenyewe.
Adolf Hitler amewahi kunukuliwa akisema; ni raha iliyoje kwa watawala kwamba watu hawafikiri.
Kuna aina kumi na moja za kufikiri ni muhimu sana kuzingatia zote maana kila moja ina umuhimu wake ili uweze kufikia mafanikio.
1. Kufikiria kwa pica kubwa
2. Kufikiria kwa kuepuka usumbufu
3. Kufikiria kwa ubunifu
4. Kufikiria kwa uhalisia
5. Kufikiria kimkakati
6. Kufikiria kwa uwezekano
7. Kufikiria kwa kutafakari yaliyopita
8. Kufikiria kwa umaarufu
9. Kufikiria kwa kushirikiana
10. Kufikiria kwa kuepuka ubinafsi
11. Kufikiria kwa undani.
Uanzie wapi ili na wewe uwe mtu wa kufikiri
1. Soma vitabu, majarida na vitu vingine vitakavyokuongezea ufahamu.
2. Kaa na watu ambao nao wanafikiria.
3. Andika mawazo yanayokuja kichwani kwako. Njia rahisi ni kuandika mawazo kumi kila siku.
Ukifanya hivi utakuwa kiwanda cha kuzalisha mawazo mazuri na utakuwa wa thamani sana.

Friday, January 2, 2015

Kuwa Kawaida Ni Kupoteza Muda Wako Na Siri Moja Ya Mafanikio Mwaka 2015

Ukipanda ndege kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ukafika hilo sio jambo la kushangaza, ndio ulichotegemea.
Lakini ukipanda ndege na ukapata huduma nzuri sana, ukapewa vyakula na vinywaji ya bei ghali kama upo kwenye hoteli ya nyota tano utafurahia na huenda utamsimulia kila mtu utayekutana naye.
Hii inamaanisha nini?
Ukifanya kile ambacho unategemewa kufanya hakuna atakayegundua kwa sababu ni kawaida, kwa sababu ndicho walichotegemea.
Ila unapofanya cha ziada zaidi, unapoweka ubunifu zaidi, unapoweka jitihada zaidi hapo ndio watu wanagundua, wanaona tofauti, wanawaambia wengine na ghafla kazi yako au huduma yako inakuwa bora na maarufu sana.
Mara zote fanya kwa ziada, nenda maili ya ziada, utasimama kwa tofauti.
Hii ndio siri ya mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya, iwe ni baba/mama, mume/mke, mwanafunzi, mfanyakazi, mfanyabiashara, msanii.

Monday, November 24, 2014

Hivi ndivyo shauku inavyokufanya kuwa mteja bila ya kupenda.

Sasa hivi tumekuwa watu wa kuendeshwa na shauku inayotokana na hisia. Na hii imetufanya tuwe wateja kwa wanaoweza kuzitumia hisia na shauku zetu.
Kwa mfano;
Kuna tofauti gani kwa anayenunua simu mpya iliyotoka leo kwa kusubiria muda mrefu na atakayekuja kuinunua kesho wakati kumetulia?
Kuna tofauti gani kati ya anayesikia habari mpya leo, BREAKING NEWS na atakayeisikia kesho?
Kuna tofauti gani kwa atakayekuwa wa kwanza kusambaza habari na ambae hatakuwa na haraka hiyo?
Yote haya na mengine mengi hayana tofauti ila yanatufanya tuwe wateja wa matoleo mapya, habari zilizovunjika na mbaya zaidi kusambaza habari ambazo hatuna uhakika nazo ili tu uwe wa kwanza......
Huna haja ya kuwa wa kwanza katika mambo haya, ni kujiongezea tu msongo.