Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, March 31, 2015

UKURASA WA 90; Kila Sehemu Utakayokwenda Utawakuta Watu Hawa.

Mtu mmoja alikuwa amechoshwa na watu kwenye mji aliokuwa anaishi. Kutokana na kuchoshwa huku aliona sulhisho pekee ni kuhama mji ule maana watu wale walifanya maisha yake kuwa magumu sana.

Alichagua mji mmoja wa kwenda na kabla ya kuhamia mji ule alitaka kuchunguza kwanza watu wa mji ule wana tabia gani. Alikwenda kwa mzee mmoja mwenye busara na kumwambia kwamba anataka kuhamia mji ule ila anapenda kujua watu wa mji ule wakoje.

SOMA; Mabadiliko; Yalikuwepo, Yapo Na Yataendelea Kuwepo.

Mzee yule mwenye busara alimuuliza swali moja, huko unakotoka watu wa huko wakoje? Alimjibu kwamba wana roho mbaya, ni wabinafsi na wana majungu sana. Mzee yule alimjibu kwamba hata kwenye mji ule anaotaka kuhamia watu wana tabia hizo hizo.

Dhana kubwa hapa ni kwamba kama unaona watu ulionao ni wabaya, wana roho mbaya, wabinafsi na mengine mengi, sehemu yoyote utakayokwenda utakutana na watu wa aina hiyo. Popote unapokwenda utakutana na watu ambao umechagua kuwaona.

SOMA; USHAURI; Hii Ndio Changamoto Kubwa Inayokuzuia Wewe Kutatua Changamoto Zako.

Ukiona kwmaba watu ni wazuri, wana roho nzuri, wanapend akusaidia, hiko ndio utakachokiona kila sehemu utakayokwenda.

Ukweli ni kwamba tunapata kile ambacho tunatarajia. Hivyo kama tunatarajia kupata mazuri kutoka kwa watu tutayapata na kama tunatarajia kupata mabaya pia tutayapata.

TAMKO LA LEO;

Najua matatizo makubwa hayapo kwa watu ninaowaona bali yapo ndani yangu mwenyewe. Kila sehemu nitakayokwenda, nitakutana na watu ambao natarajia kukutana nao. Kubadili mtizamo wangu juu ya watu, kutanisaidia sana ili kuweza kuishi maisha ya furaha.

SOMA; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini

Tukutane kwenye ukurasa wa 91 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kitu Kimoja Unachohitaji Kuondoa Ili Kufanikiwa.

“You crave winning and fear losing instead of just doing. To succeed you must remove your self-imposed limitations.” ― Wayne Gerard Trotman

Unatamani kufanikiwa na unahofia kushindwa badala ya kufanya. Ili kufanikiwa unahitaji kuondoa vikwazo ulivyojiwekea mwenyewe.

Hakuna ambaye hatamani kufanikiwa, lakini kutamani tu hakutakuletea mafanikio unayotazamia.

Watu wengi sana wana hofu ya kushindwa. Wanaogopa kufanya jambo kwa sababu wanafikiria kama watashindwa hali itakuwaje? Wanaona kama watapoteza au maisha kuwa magumu zaidi.

SOMA; BIASHARA LEO; Mwisho Wa Ufalme Wa Mteja.

Hapo ulipo kuna vikwazo vingi sana ambavyo umejiwekea mwenyewe. Kumbuka yale maneno unayojiambia kwamba huwezi kufanya biashara kwa sababu huna mtaji, huwezi kufikia uhuru wa kifedha kwa sababu huna elimu kubwa. Na mengine mengi, yote haya yanakurudisha nyuma.

Mafanikio yanatokana na kufanya, yanatokana na vitendo.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia Malengo Yako Kwa Haraka.

Monday, March 30, 2015

UKURASA WA 89; Sheria Tatu Muhimu Za Kufanikiwa Kwenye Maisha.

Watu hupenda kusema kwamba maisha hayana kanuni, yaani hakuna kanuni moja ambayo kila mtu akiifuata basi atakuwa na uhakika wa kuwa na maisha anayotaka. Pamoja na hii kuwa kweli, bado kuna sheria mbalimbali ambazo kama ukizifuata maisha yako yanakuwa bora na inakuwa rahisi kwako kufikia mafanikio.

SOMA; Biashara Unayofanya Sasa, Au Utakayoanza Sasa Sio Biashara Utakayofanya Milele.

Leo tutaangalia sheria tatu za msingi na muhimu sana ili kuwa na maisha bora na yenye mafanikio.

Sheria ya kwanza; Kama hutakiendea kile unachotaka hutokipata. Kwa urahisi ni kwmaba kama unataka mafanikio, halafu hufanyi jambo lolote la kukuletea mafanikio unayotaka, hutayapata. Kama kuna kitu unakitaka kwenye maisha yako, kifanyie kazi, kitafute na utakipata.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Sheria ya pili; Kama hutauliza, jibu ni hapana. Kama kuna kitu ambacho unataka kumuuliza mtu, halafu ukaogopa kuuliza basi jibu tayari unalo, ambalo ni hapana. Usisite au kuogopa kuuliza au kuomba chochote, kabla hujaomba jibu ni hapana, hivyo omba na jibu likiwa hapana, halibadilishi chochote na kama jibu likiwa ni ndio utapata unachotaka.

SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Sheria ya tatu; Kama hutapiga hatua kwenda mbele, utaendelea kubaki hapo ulipo. Kama hutabadilika, kama hutafanya chochote cha kukusogeza mbele, utaendelea kuwa hapo ulipo, utaendelea kuwa na maisha uliyonayo.

Fanyia kazi kile unachotaka, omba au uliza unachotaka, piga hatua kwenda mbele.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia sasa nitafanyia akzi kile ninachotaka ili niweze kukipata, nitauliza au kuomba kile ninachotaka kwa sababu najua nisipofanya hivyo jibu ni hapana. Na pia nitapiga hatua kwenda mbele kwenye kila eneo la maisha yangu. Sitakubali kubaki hivi nilivyo, nataka kuwa bora zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 90 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Haya Ndio Mambo Matatu Yatakayokuletea Matokeo Ya Kushangaza.

“Extra miles, extensive preparation and exhaustive efforts usually show astonishing results.” ― Roopleen

Kwenda hatua ya ziada, kujiandaa vyema na kuweka juhudi kubwa mara zote kutakuletea matokeo makubwa na ya kushangaza.

Jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako na ambalo unataka likufikishe kwenye mafanikio makubwa ni muhimu sana uweke mambo haya matatu muhimu.

Nenda hatua ya ziada, usifanye tu kile ambacho kila mtu anafanya. Weka ubunifu zaidi, kuwa wa tofauti, ogopa sana kuwa kawaida. Maana kuwa kawaida ni sumu kubwa ya mafanikio.

SOMA; Kitu Hiki KImoja Kitakufanya Ushindwe Kwenye Biashara.

Kuwa na maandalizi ya kutosha. Jiandae vizuri kwa jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako. Kuna changamoto nyingi sana kwenye maisha hivyo kama huna maandalizi ni rahisi sana kukata tamaa. Ila maandalizi haya yasiwe kikwazo kwako kuanza, anza huku ukiendelea kujiandaa zaidi.

Weka juhudi kubwa. Juhidi ndio zinazleta mafanikio. Hata kama ungekuw ana mipango mizuri kiasi gani, kama hutaifanyia kazi na kama hutaweka juhudi kubwa, hakuna chochote kitakachobadilika kwenye maisha yako.

SOMA; Nilichojifunza Leo; Zoezi Moja Litakalobadili Maisha Yako Kabisa.

Nakutakia siku njema.

Sunday, March 29, 2015

UKURASA WA 88; Usinunue Matatizo Ya Watu.

Binadamu ni viumbe wa kujumuika, yaani tunaishi vizuri kwenye jamii, kwa kusaidiana hapa na pale.

Lakini katika kusaidiana huku kuna wakati ambapo tunatoa msaada ambao unatuumiza sana sisi na pia haumsaidii sana yule ambaye tunampatia.

Msaada huu ni pale ambapo unanunua matatizo yya mtu.

SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia Malengo Yako Kwa Haraka.

Unanunuaje matatizo ya watu?

Mtu anakuwa na tatizo, ambapo unashawishika kulitatua lakini katika kulitatua na wewe unaingia kwenye matatizo au hali yako inakuwa mbaya kuliko ilivyokuwa mwanzo. Unajikuta na wewe unaingia kwenye huzuni, unaanza kuona tatizo lile kama ni lako moja kwa moja.

Kama utafanya hivi kwa matatizo ya watu wengi, ni vigumu sana kuweza kuwa na maisha yenye furaha.

SOMA; Matatizo Yote Kwenye Maisha Yako Yanatokana Na Kitu Hiki.

Sikiliza matatizo ya watu, toa msaada kama unaweza, ila usizame moja kw amoja kwenye tatizo hilo. Kwa kufanya hivyo unakuwa umenunua tatizona litakusumbua sana wewe. Na pia kama huwezi kusaidia tatizo la mtu usiondoke nalo na likaendelea kukusumbua. Tambua ya kwmaba kila mtu ana matatizo yake na huwezi kutatua matatizo ya kila mtu.

Kwa hili haimaanishi kwmaba hujali matatizo ya watu, ila hubebi matatizo hayo na kuyafanya sehemu ya maisha yako. Wewe mwenyewe una matatizo yako yanayokusumbua, pambana na hayo kwanza.

SOMA; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini

TAMKO LA LEO;

Kuanzia sasa sitanunua tena matatizo ya watu. Sitachukua matatizo ya watu na kuyafanya sehemu ya maisha yangu. Nitasikiliza matatizo hayo na kama nitaweza kusaidia nitafanya hivyo, kama siwezi nitakiri kwamba siwezi na sitakubali nimezwe na matatizo haya.

Tukutane kwenye ukurasa wa 89 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kama Tayari Una Ndoto Hiki Ndio Unatakiwa Kufanya.

“If you have a dream, don’t just sit there. Gather courage to believe that you can succeed and leave no stone unturned to make it a reality.” ― Roopleen

Kama una ndoto, usikae tu na kufikiri utaifikia. Kusanya ujasiri wa kuamini kwamba unaweza kufanikiwa na usiache jiwe lolote halijageuzwa kwenye kutimiza ndoto zako.

Karibu kila mmoja wetu ana ndoto kubwa sana kwenye maisha yake. Ila watu wengi hukaa na ndoto zao bila ya kufanya jitihada zozote kubwa za kutimiza ndoto hiyo.

SOMA; Nilichojifunza Leo; Zoezi Moja Litakalobadili Maisha Yako Kabisa.

Mtu anaweza kukuambia nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa. Ukimuuliza umeshafanya nini ili kufikia ndoto hiyo anaanza kukuletea sababu. Mara mtaji sina, mara sijapata wazo na mengine mengi. Kama kweli ndoto yako ni kuwa mfanyabiashara mkubwa, unatakiwa kuanza kuhangaika huko na kule, kuhakikisha unapata pa kuanzia. Unaongea na watu wengi, unajaribu vitu vingi mpaka unapata kitu kimoja cha kukomaa nacho.

Nakutakia siku njema.

SOMA; BIASHARA LEO; Biashara Unayofanya Sasa, Au Utakayoanza Sasa Sio Biashara Utakayofanya Milele.

Saturday, March 28, 2015

Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuishinda Hofu.

Ili kuishinda hofu, rudisha mawazo yako kwenye wakati uliopo sasa. Maana hofu kubwa unaipata pale unapofikiri mambo yaliyopita ambayo huwezi kuyabadili na kuwaza mambo yajayo ambayo huwezi kuyabadili pia.
Acha kuwaza mambo ambayo yameshapita, huwezi kuyabadili. Yatakuumiza na kukupa hofu kubwa.
Acha kufikiria mambo yajayo na kuyahofia. Bado hujayafikia na mambo hayatakuwa mabaya kama unavyofikiria sasa.
Weka mawazo yako sasa, kwenye wakati uliopo na utapata ujasiri mkubwa wa kufanya kile unachotaka kufanya.
Kumbuka ili kuwa na maisha mazuri ya kesho unatakiwa kuwa na maisha mazuri leo. Hivyo badala ya kuhofia kesho itakuwaje, tumia muda huo kuishi vizuri leo na kesho mambo yatakwenda vizuri.

UKURASA WA 87; Kuna Jambo Moja La Ziada La Kufanya.

Inapokuja kwneye kazi, biashara au jambo lingine tunalofanya ili kutengeneza kipato, mara zote huwa kuna kuwa na jambo moja la ziada la kufanya.

Kwa mfano kama umesema leo utafanya vitu fulani vitatu, utakapomaliza kufanya vitu hivyo utaona kuna kitu kingine cha ziada cha kufanya.

SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia Malengo Yako Kwa Haraka.

Ukiwa unatembelea mitandao ya kijamii, facebook, instagram, twitter, na hata wasap. Kuna kitu kimoja cha ziada cha kuangalia, kuna picha moja ya ziada ya kuangalia, kuna kundi moja la ziada la kuangalia.

Tatizo kubwa haliishii hapa kwenye kitu cha ziada cha kuangalia, bali linakuwa kubwa pale kitu hiki kimoja cha ziada, kinazaa kitu kingine na kingine na kingine.

Ulifikiri kitu hiki kimoja cha ziada unachotaka kufanya kingechukua dakika tano, unashangaa nusu saa imepita, mara saa moja imepita na bado unafanya kitu kile ulichofikiri ni cha ziada. Na kwa bahati mbaya sana kitu hiki cha ziada sio muhimu sana na kingeweza kusubiri.

SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.

Hasara kubwa zaidi ya kitu hiki cha ziada tunachotamani kufanya inakuja pale kinapotumalizia muda wetu wa kupumzika, muda wa kuwa na wale tunaowapenda na muda wa kufanya mambo ambayo ni muhimu zaidi kwetu.

Ili kuondokana na hali hii, kwanz akuwa na ratiba ya vitu unavyotaka kufanya kwenye siku na vifanye hivyo tu. Pili jua kwmaba sio lazima ufanye kila kitu na vitu vingine vinaweza kusubiri. Tatu kuwa na muda maalumu wa kutembelea mitandao ya kijamii na heshimu muda huo, yaani usizidishe hata dakika moja.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwmaba vitu vya kufanya huwa haviishi. Kila wakati nitakuwa na jambo moja la ziada ambalo nitahitaji kulifanya. Mara nyingi jambo hili sio muhimu sana na linanipotezea muda. Nitaepuka hali hii kwa kuwa na ratiba ninayoiheshimu na kuwa na muda maalumu wa kutembelea mitandao ya kijamii.

Tukutane kwenye ukurasa wa 88 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Hii Ndio Hatari Kubwa Kuliko Zote.

“Being comfortable with who you are is the ultimate threat.” ― Sean Beaudoin

Kuridhika na vile ulivyo ndio hatari kubwa kuliko zote.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha yako kama kuridhika na vile ulivyo, kuridhika na hali uliyofikia.

Hii ni sumu kubwa sana ya wewe kufikia mafanikio makubwa.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

Kuridhika na vile ulivyo maana yake hutofanya juhudi za kujiboresha zaidi na hatimaye kuachwa nyuma na mabadiliko yanayotokea kila siku.

Kuwa makini pia, hii haimaanishi ujidharau na kujiona hufai. Unatakiw akujiamini na kupenda maisha yako ila usije ukaridhika na pale ulipo sasa. Miaka michache ijayo mambo mengi yatakuwa yamebadilika.

Soma kitabu JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA na utajifunza mbinu bora za kujiandaa na mabadiliko.

Nakutakia siku njema.

Friday, March 27, 2015

UKURASA WA 86; Jifunze Kusikiliza.

Tuna masikio mawili na mdomo mmoja kwa sababu moja kubwa sana. Kusikiliza ni bora kuliko kuongea. Yaani unahitaji kusikiliza mara mbili ya unavyoongea.

Lakini kwenye maisha yetu ya kawaida mambo ni kinyume kabisa na hapo. Watu wanaongea mara mbili ya wanavyosikiliza. Kila mtu anakazana kuongea na mwishowe hakuna tena mazungumzo mazuri.

SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.

Maongezi mengi yamekuwa sio ya kujifunza na kuelewa zaidi bali yamekuwa ni maongezi ya mtu kusubiri wakati wake wa kuongea. Yaani wakati mtu mwingine anaongea wewe husikilizi kwa makini kile anachoongea bali unafikiria utamjibu nini au utaongea nini.

Katika hali hii hakuna mawasiliano mazuri kati ya watu wanaongea na hivyo ujumbeuliotakiwa kufika unashindwa kufika.

SOMA; Maswali ambayo huulizwa mara nyingi kuhusu uwekezaji katika hisa.

Hasara za kuongea kuliko unavyosikiliza zipo nyingi sana ila kuna hii moja ambayo ni kubwa sana na yenyewe ni KUTOJIFUNZA. Kama katika maongezi yoyote uliyopo wewe ndio muongeaji sana maana yake unajiambia vitu ambavyo tayari unavijua. Lakini unaposikiliza unajifunza vitu vipya ambavyo hukuwahi kuvijua kupitia wengine wanaoongea.

Punguza kuongea na anza kusikiliza kwa makini, hata kama mtu anakosea, utajifunza ni nini cha kufanya ili na wewe usikosee.

SOMA; Hizi Ndizo Gharama Unazotakiwa Kuzilipia, Ili Uweze Kupata Kile Unachokihitaji Katika Maisha Yako.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia leo nitakuwa nasikiliza mara nyingi ya zaidi ya ninavyoongea. Na katika kusikiliza kwangu nitasikiliza kwa makini ili kujifunza na sio kusikiliza ili nijue kipi cha kujibu. Najua kwa kuongea mimi mwenyewe sijifunzi kitu kipya, ila ninapowasikiliza watu wengine najifunza mambo mengi sana mapya. Nitasikiliza kwa makini sana maongezi yoyote nitakayokuwepo.

Tukutane kwenye ukurasa wa 87 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Jambo Muhimu La Kufanya Wakati Unapia Magumu.

“In the darkest hours we must believe in ourselves.” ― Terry Goodkind

Katika nyakati ngumu, unatakiwa kujiamini wewe mwenyewe.

Kila mmoja wetu anapitia nykati ngumu kwenye maisha yake. Inaweza kuwa kwenye kazi, kwenye biashara, kwenye familia na hata maeneo mengine muhimu kwenye maisha yako.

Huu ni wakati ambapo malengo na mipango yako unaona kama haviendi kabisa na wakati mwingine unaona kama haviwezekani.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Katika nyakati hizi jambo muhimu kabisa la wewe kufanya ni kujiamini wewe mwenyewe. Ukishindwa kujiamini unajua ni kitu gani kinafuata? Kukata tamaa. Na ukishakata tamaa na mambo yako ndio yamekwisha.

Jiamini katika nyakati ngumu, jikumbushe ni wapi unatoka na pia jikumbushe ni wapi unapokwenda. Kwa hiki kidogo tu unaweza kupata hamasa kubwa ya kuweza kuendelea na mapambano.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

Thursday, March 26, 2015

UKURASA WA 85; Jipe Miadi.

Kwa mfano ukataka kuonana na mimi ili tuzungumze jambo lolote, tutawekeana miadi. Kwamba siku fulani na muda fulani tutakuwa pamoja tukizungumzia jambo fulani. Na tunapokutana hatutegemei kuwa na usumbufu mwingine wowote, ni mimi na wewe.

Nikikupigia simu sasa hivi, utaacha jambo lolote ambalo unafanya na kujibu simu hiyo, hata kama nitakuwa nakuambia jambo lolote ambalo sio muhimu sana kwako. Utanipa muda wako kwa jambo lolote ambalo nataka mimi.

SOMA; Maswali ambayo huulizwa mara nyingi kuhusu uwekezaji katika hisa.

Unatoa muda wako kwa mambo mengi sana. Watu wanakutumia meseji unazijibu, watu wanaandika vitu kwenye mitandao ya kijamii unavijibu, unachangia na kadhalika. Watu wanakutumia meseji za vichekesho na wewe unazituma kwa wengine. Sijasema lolote hapa ni baya ila kuna kitu kimoja muhimu sana unakisahau.

Upo tayari kumpatia mtu yeyote muda wako. Ila je upo tayari kujipatia wewe muda? Upo tayari kuipatia nafsi yako muda?

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu hawajawahi kuzipatia nafsi zao muda. Na wewe ni mmoja wao.

Ipe nafsi yako muda, jipe miadi wewe mwenyewe. Kutana na nafsi yako na jadili mambo yote muhimu kwenye maisha yako. Muda huu unaoipa nafsi yako ni tofauti na muda wa kupumzika, huo pia unapaswa kuwa nao.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

Tenga muda kila siku ambapo utakaa wewe mwenyewe, kwenye utulivu wa hali ya juu na kuyaangalia maisha yako kwa jicho la ndani zaidi. Katika muda huu hakikisha hakuna wa kukusumbua, yaani usiwe na simu kabisa. Fanya kama hii ni sehemu ya kuitoroka dunia.

Muda huu unaweza kuwa dakika tano, kumi, robo saa, nusu saa na hata saa nzima. Katika muda huu weka matatizo yako pembeni kwanza, acha kufikiria kuhusu mtu mwingine yeyote na fikiria kuhusu maisha yako wewe, yalipotoka yalipo na yanapokwenda.

Kwa zoezi hili dogo sana utaweza kuona mabadiliko makubwa unayoweza kuyafanya kwenye maisha yako.

SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.

TAMKO LA LEO;

Kila siku nitatenga muda wa kukaa mwenyewe na nafsi yangu na kutafakari maisha yangu. Najua nafasi hii ni muhimu sana kwenye maisha yangu ili kujua nimetoka wapi, nipo wapi na ninaelekea wapi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 86 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kitu Kimoja Kinachoangusha Watu Wengi Kuliko Vingine Vyote.

“Fear defeats more people than any other one thing in the world.” ― Ralph Waldo Emerson

Hofu inaangusha watu wengi kuliko kitu kingine chochote duniani.

Hofu ndio inaua ndoto za watu wengi sana.

SOMA; Hizi ndio Hofu mbili ulizozaliwa nazo, nyingine ni uongo.

Hofu ndio inawafanya wengi washindwe kuchukua hatua za kuboresha maisha yao.

Hofu imewafanya wengi kuwa na maisha magumu sana.

Ni hofu ya kushindwa na hofu ya kukataliwa zinazoongoza kuwafanya wengi washindwe kuchukua hatua.

Ondokana na hofu hizi kwa sababu sio kitu cha kweli. Ni hali ya akili yako kutokuwa tayari kufanya jambo fulani.

Kama unataka mafanikio, anza kuishinda hifu.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Adui Yako Anaanzia Hapo Ulipo Na Anaanza hivi.

Wednesday, March 25, 2015

UKURASA WA 84; Pata Muda Wa Kuishi.

Kwa masikitiko makubwa sana naomba kukuambia kwamba bado hujapata muda wa kuishi. Na kama hutachukua hatua mapema basi utajikuta mpaka siku unakufa hujapata muda wa kuishi.

Kuna usemi maarufu unasema kwamba maisha ni kile kinachoendelea wakati wewe unaweka mipango mingine.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Huu ni ukweli kabisa. Tumekuwa watu wa kuweka mipango tukiamini kwamba mpango huu ukikamilika basi ndio tutaanza maisha yetu vizuri. Ukiwa shuleni unafikiria nikimaliza tu masomo na kuanza kazi basi maisha yangu yatakuwa mazuri. Ukimaliza shule na kupata kazi unasema nikishaoa/olewa na kuwa na familia yangu basi maisha yangu yatakuwa mazuri sana. Unapooa/olewa unasema nikishamaliza kulea watoto maisha yangu yatakuwa viuzuri.

SOMA; NENO LA LEO; Hiki Ndio Chanzo Cha Nguvu Zako.

Unaendelea kusogeza maisha mbele kama vile kuna siku moja utaamka na mipango yote uliyoweka ikawa imetekelezwa.

Ukweli ni kwamba maisha hayaendi hivyo. Hakuna siku ambayo utakuwa umemaliza mipango yako yote. Na kwa bahati mbaya sana mipango hii inaendelea kuongezeka kila siku.

Kumbuka maisha ni sasa, maisha ni hapo ulipo. Pata muda wa kuishi maisha yako. Pata muda wa kuyafurahia kwa hapo ulipo na hivyo ulipo. Furahia kila wakati wa maisha yako kwa sababu huna wakati mwingine, unaweza kufa kesho, nani ajuaye?

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

TAMKO LA LEO;

Nitahakikisha napata muda wa kuishi. Najua ni rahisi sana kukosa muda huu kama nitakuwa naweka maisha baada ya mipango yangu. Pamoja na mipango mizuri niliyojiwekea, maisha ni sasa hata kabla sijakamilisha mipango hii.

Tukutane kwenye ukurasa wa 25 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kinachoamua Maisha Yako Sio Unachozungumza, Bali Hiki…

It’s not what you say out of your mouth that determines your life, it’s what you whisper to yourself that has the most power!” ― Robert T. Kiosaki

Sio kile unachoongea ndio kinabadili maisha yako, ni kile unachojinongoneza mwenyewe ndio kina nguvu kubwa.

Unaweza kuzungumza chochote unachopenda mbele ya watu. Unaweza kuwahakikishia kwmaba utapambana na hutakata tamaa mpaka pale utakapofikia mafanikio.

Lakini kama unapokuwa mwenyewe unajinongoneza kwamba huwezi, haiwezekani, vikwazo ni vingi. Unafikiri kati ya vitu hivi viwili ni kipi chenye nguvu? Maneno uliyowaambia wengine au yale uliyojinongoneza?

Uliyojinongoneza yana nguvu sana. Hakikisha unatumia nguvu hii kufikia malengo yako.

Jiambie unaweza, jiambie utapambana na jiambie hutokata tamaa mpaka upate kile unachotaka.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini

Tuesday, March 24, 2015

UKURASA WA 83; Unahitaji Kuwa Sahihi Au Kuwa Na Furaha?

Kuwa sahihi na wakati huo huo kuwa na furaha ni kama vitu viwili ambavyo haviwezi kutokea kwa wakati mmoja. Na hii ni sahihi sana hasa kwenye maisha yako na mahusiano yako na watu wengine.

Ni vigumu sana wewe kuonesha kwamba upo sahihi na wakati huo huo ukawa na furaha.

Hii inatokea sana kwenye mahusiano yetu na watu wengine. Mtu anaweza kuwa anafanya jambo ambalo huenda hukubaliani nalo, au sio sahihi kwa upande wako. Kwa kumpinga na kumwambia yeye hayupo sahihi ila wewe ndio upo sahihi, kutamfanya atetee sana upande wake. Katika hali hii mahusiano yanakuwa mabovu na wote mnakosa furaha.

SOMA; Siri Kubwa Unayotakiwa Kujua Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara.

Kutaka kuwa sahihi bila ya kujali furaha inayotokana na mahusiano mazuri imekuwa ndio chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano mengi ya kirafiki na hata ndoa pia.

Badala ya kutaka kuonekana kwamba wewe ndio sahihi sana, hebu wape wengine nafasi ya kukosea, hebu wape wengine nafasi ya kufanya kile wanachoona ni sahihi kwao na furahia mahusiano mazuri mnayoendelea kuwa nayo.

SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Kinachokurudisha Nyuma.

Mara nyingi vitu ambavyo watu wanabishania kuonekana sahihi ni vidogo sana na havistahili kukuzwa kiasi hiko mpaka kupelekea mahusiano kuwa mabaya na hata kuvunjika.

TAMKO LA LEO;

Najua kwenye mahusiano niliyonayo na watu wengine, ni vigumu sana kuwa sahihi na wakati huo huo kuwa na furaha. Najua vita ya kutaka kuonekana nipo sahihi zaidi itaniondolea furaha yangu kwa kuvunja mahusiano niliyonayo. Nitawapa wengine nafasi ya kujiona wapo sahihi, nitawapa nafasi ya kukosea na nafasi ya kufanya kile ambacho ni sahihi kwao.

SOMA; NENO LA LEO; Ufunguo Muhimu Wa Ufunguo Wa Mafanikio.

Tukutane kwenye ukurasa wa 84 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Acha Kupoteza Nguvu Zako Kwenye Kitu Hiki Unachopenda Kufanya.

“Don't waste your energy trying to change opinions ... Do your thing, and don't care if they like it.” ― Tina Fey, Bossypants

Usipoteze nguvu zako kwa kujaribu kubadili maoni ya wengine. Fanya kile unachofanya na usijali kama watakipenda au la.

Katika kitu chochote, watu watakuwa na maoni tofauti tofauti. Kuna wengine watakubaliana nacho, kuna wengine watakipinga. Kuna wengine watakupa moyo, kuna wengine watakukatisha tamaa.

SOMA; Usijaribu Kumfurahisha Kila Mtu.

Ukianza kusikiliza kila mtu au kuanza kubishana nao kwamba unachofanya ni sahihi, utapoteza nguvu nyingi na bado watu hawa hawatobadilika. Badala yake tumia nguvu hizo kufanya unachofanya kwa ubora wa hali ya juu.

Watakapoona matokeo mazuri wote wanaokupinga na kukukatisha tamaa watakaa kimya. Ila utakapokazana kuwabadili maoni yao kwa kubishana nao utapoteza nguvu zako na utashindwa kufanya kile ulichochagua na wao watakuwa sahihi.

Kumbuka watu hawataacha kusema, hata ungefanya kiasi gani. Ni sawa na mfano uliotolewa na mfalme mmoja kwamba hata ukitembea juu ya maji kuna watu watasema anatembea juu ya maji kwa sababu hajui kuogelea.

Tumia nguvu zako kufanya mambo ya msingi kwako na sio kubadili maoni ya wengine. Acha majibu mazuri yafanye kazi hiyo.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Unachohitaji Kufanya Ili Dunia Nzima Ikukubali.

Monday, March 23, 2015

Changamoto Inayokusumbua Kwenye Biashara.

Habari mpenzi msomaji,
Naandika kitabu kinachohusu biashara. Hii ni kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi sana zinazozuia watu wengi kuingia kwenye biashara au kufanikiwa zaidi kupitia biashara.
Vitabu vingi vya kibiashara havijaangalia upande wa pili wa tatizo ambapo ni mtu mwenyewe.
Hivyo kitabu hiki kitaanza na mapinduzi ya mfanyabiashara mwenyewe ndio aweze kuleta mapinduzi kwenye biashara yake.
Nachukua nafasi hii kukuambia kwamba kama una changamoto yoyote ambayo inakuzuia kuingia kwenye biashara au ambayo inakufanya ushindwe kufanikiwa unaweza kuileta na ikajibiwa kwenye kitabu hiki.
Unachotakiwa kufanya ni kuandika changamoto yako kwa mfumo wa swali na kutuma kwa email ushauri@kisimachamaarifa.co.tz
Swali au changamoto yako itajibiwa kwenye kitabu hiki ambacho kitatoka muda sio mrefu.
Chukua hatua haraka ya kuuliza changamoto yako kwa sababu muda ni mfupi.
Nakutakia kila la kheri.
TUPO PAMOJA.

Je Umepata Kitabu Chako?

Siku kadhaa zilizopita niliweka ujumbe ambao nilikuomba wewe kama msomaji uwatumie watu wa tano kwenye email zao.
Na pia niliahidi ukifanya hivyo nitakupa zawadi ya kitabu kinachohusu mabadiliko.
Watu wengi walitikia ombi lile na ujumbe ulitumwa kwa watu wengi sana.
Jana kitabu kilikamilika na wewe uliyetuma ujumbe kwa wengine ulikuwa wa kwanza kutumiwa.
Naandika hapa nikotaka kujua kama umepata kitabu ulichotumiwa.
Kitabu kimetumwa kwa watu 33 ambao waliitikia wito ule.
Kama ulituma ujumbe na hujapokea kitabu tafadhali nijulishe kupitia email makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Nakupenda na kukuheshimu sana wewe msomaji wangu hivyo napenda kutimiza kile ninachokuahidi.
Pia nitumie nafasi hii kutangaza kwamba zoezi la kutuma ujumbe ule na baadae kupewa zawadi limefungwa rasmi.
Ila nakuomba uendelee kutuma jumbe hizi nzuri kwa watu wako wa karibu na washauri kujiunga nasi. Usitake kupata mambo haya mazuri peke yako, tusambaze elimu hii ili iwafikie wengi zaidi.
Asante na nakutakia kila la kheri.
TUPO PAMOJA.

UKURASA WA 82; Mambo Madogo Ndio Muhimu Sana.

Wakati unafikiria kuhusu mafanikio kwenye maisha unafikiria mambo makubwa sana.

Kama unafikiria kuhusu fedha unafikiria mamilioni na mabilioni.

Kama unafikiria kuhusu nyumba unafikiria hekalu, au nyumba kubwa sana yenye kila kitu.

Kama unafikiria usafiri unafikiria magari mengi na ya kifahari.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Mambo yote haya ni mazuri sana na hakuna asiyependa vitu vizuri.

Ila ukweli unakuja kwamba, mambo madogo ndio yanayojenga maisha yetu. Yaani mambo madogo madogo ndio yana athari kubwa sana kwenye maisha tunayoishi.

Sio milioni mia moja au bilioni moja itakayokupa wewe uhuru wa kifedha, bali unawezaje kuitumia shilingi elfu moja vizuri, ikatimiza mahitaji yako na ukaweza kuweka akiba kidogo.

Sio jumba kubwa sana ambalo litaweza kukuletea furaha kwenye maisha, bali ni maisha gani unayoishi kwenye nyumba yoyote uliyopo sasa. Kama ni maisha ya amani na upendo yatakusukuma wewe kufikia jumba hilo kubwa hata kama unaanzia kwenye chumba kimoja.

SOMA; Haya Ndio Mapinduzi Makubwa Tunayohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Kilimo.

Vitu hivi vidogo vidogo ukiweza kuvizingatia vitakuletea mafanikio makubwa. Ukishindwa kuvizingatia maisha yako yatakuwa hovyo hata kama ungekuwa na vitu vikubwa kiasi gani.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba vitu vidogo ndio muhimu sana kwenye maisha, ndio vinapelekea mambo makubwa kuwa muhimu kwetu. Nitaendelea kuzingatia mambo haya madogo ili maisha yangu yawe bora zaidi kila siku.

Tukutane kwenye ukurasa wa 83 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Kama kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho hapa duniani ni kwamba dunia inabadilika kila siku. Ukiangalia historia ya dunia tulikotoka na tulipo sasa kumetokea mabadiliko makubwa sana. Zilianza zama za mawe, zikaja zama za chuma, yakaja mapinduzi ya viwanda na hata sasa tupo kwenye mapinduzi ya kiteknolojia.

Jambo moja la kushangaza ni kwamba pamoja na mabadiliko haya kuwa wazi bado watu wengi ni wagumu sana kubadilika. Watu hawapendi mabadiliko, wanapenda kufanya kile walichozoea kufanya na wanataka maisha yaendelee vile yalivyokuwa jana na leo. Kitu ambacho ni ndoto isiyowezekana.

Katika zama zote ambazo dunia imepita, kuna watu ambao waliweza kubadilika haraka na kupata faida ya mabadiliko, wengine walilazimishwa kubadilika na hivyo kuburuzwa na kuna ambao waliachwa na mabadiliko na hivyo kupotea. Waliofaidika na mabadiliko ni wale waliokuwa tayari kubadilika, walioburuzwa na mabadiliko ni wale ambao walikuwa hawajui kama kuna mabadiliko ila wanakwenda tu na hali ilivyo. Walioachwa na mabadiliko ni wale ambao hata baada ya kuona mabadiliko wao waligoma kubadilika, waliendelea kung’ang’ania kile walichozoea na hatimaye kuachwa nyuma na kupotea.

mabadiliko cover EDWEB

Mabadiliko ni jambo muhimu sana lakini watu wengi hawajalipa msisitizo kwenye maisha na hii inapelekea wengi kuachwa nyuma na mabadiliko haya.

Ni kutokana na umuhimu wa jambo hili nimekuandalia kitabu kinachoitwa JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Katika kitabu hiki utajifunza mambo yafuatayo;

1. Historia fupi ya mabadiliko kwenye maisha ya mwanadamu hapa duniani na kwa nini mabadiliko yataendelea kutokea.

2. Mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye elimu, kazi na hata biashara.

3. Makundi ya aina tatu ya watu ambao wanazalishwa na mabadiliko, kundi linalonufaika na mengine yanayopoteza.

4. Mambo kumi muhimu sana ya kufanya ili na wewe uingie kwenye kundi ambalo linanufaika sana na mabadiliko ambayo yanaendelea kutokea

5. Mabadiliko makubwa yanayokuja kwenye mfumo wa elimu, mfumo wa ajira na hata biashara na ujasiriamali.

Kitabu hiki kitakuandaa wewe na kukupa mbinu za kuweza kuboresha maisha yako zaidi na kufanikiwa licha ya mabadiliko yanayoendelea.

Kitabu hiki ni muhimu sana kwa makundi yafuatayo;

1. Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanasoma ila hawana uhakika wa kupata ajira. Kitawawezesha kujiandaa mapema ili kujua njia watakayochukua na hivyo kutopoteza muda wakisubiri ajira ambazo hazipo.

2. Wafanyakazi ambao wamekuwa kwenye kazi kwa muda mrefu lakini hawaoni manufaa ya kazi zao kwenye maisha yao.

3. Wafanyabiashara ambao wamefanya biashara kwa muda mrefu ila wako pale pale miaka nenda miaka rudi.

4. Wafanyakazi ambao wamestaafu kazi, wamefukuzwa kazi, wamepunguzwa kazi au wameamua kuacha kazi wenyewe.

5. Watu ambao umri wao umekwenda kiasi na wanaamini kwamba mambo waliyokuwa wanafanya zamani ni bora kuliko yanayofanyika sasa, na wanaendelea kuyafanya licha ya kushindwa kupata majibu makubwa.

6. Mtu yeyote ambaye anataka kuboresha maisha yake zaidi, kwa kujua mambo yanayoendelea na ni yapi yanakuja kwa siku za mbeleni.

Ni muhimu sana wewe kupata na kusoma kitabu hiki, kitaleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako kama utakuwa tayari kufanyia kazi yale ambayo utajifunza.

JINSI YA KUPATA KITABUJINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy yaani pdf na unaweza kukisoma kwenye simu yako kama ni smartphone, unaweza kukisoma kwenye tablet na pia unaweza kukisoma kwenye kompyuta. Kurasa zake zinasomeka vizuri kwenye vifaa hivyo vya aina tatu tofauti.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu tano(5,000/=), gharama hii ndogo sio kwa sababu kina mambo madogo ila ni kwa sababu kitabu hiki ni muhimu sana na kila mtu ni muhimu akisome, hivyo gharamaisiwe kikwazo cha watu kushindwa kukisoma.

Kupata kitabu unafanya malipo ya tsh 5,000/= kupitia namba 0717396253 au 0755953887 na kisha unatuma email yako kwenye moja ya namba hizo na unatumiwa kitabu mara moja.

Mambo sasa hivi yanakwenda kidigitali zaidi na huna haja ya kubeba mizigo mingi, kwa kuwa na simu yako tu unaweza kuendelea kujifunza mambo mengi sana.

Karibu sana upate kitabu hiki mapema, kwa sababu jinsi unavyozidi kuchelewa kukipata, mabadiliko yanaendelea kutokea na yanakuacha nyuma. Jinsi utakavyoweza kuchukua hatua haraka ndivyo unavyoweza kuiokoa na kuimarisha kazi yako au biashara yako. Chukua hatua haraka kwa kusoma kitabu hiki leo.

Pia tembelea blog ya VITABU VYA UJASIRIAMALI NA MAFANIKIO ili kupata vitabu vingine vingi na vizuri vya kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo lolote unalofanya.

Jipatie kitabu chako leo, maisha hayakusubiri wewe uwe tayari.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako, na kitabu hiki kiwe nguzo muhimu sana kwako.

TUPO PAMOJA.

MAKIRITA AMANI

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

NENO LA LEO; Huu Ndio Ufunguo Wa Maisha, Na Sio Elimu.

“The key to life is accepting challenges. Once someone stops doing this, he's dead.” ― Bette Davis

Ufunguo wa maisha ni kuzikubali changamoto. Mtu atakapoacha kuzikubali changamoto, amekufa.

Hakuna maisha ambayo hayana changamoto, kwa kifupi hakuna mtu ambaye hana matatizo. Ukiwa huna fedha unakuwa na matatizo, ukiwa na fedha unakuwa na matatizo.

Njia moja ya kuweza kupambana na changamoto unazokutana nazo, kutatua matatizo unayokutana nayo ni kuyakubali kwanza.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

Kubali kwamba changamoto hii ni yako. Kubali kwamba uko kwenye matatizo. Na unaweza kuanzia hapa kujua unawezaje kujinasua kwenye matatizo haya.

Unaposhindwa kukubali, au ukaanza kukimbia changamoto na matatizo, yanazidi kuwa mengi zaidi na yatakumeza mzima mzima.

Nakutakia siku njema.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Sunday, March 22, 2015

KITABU; SHERIA 48 ZA NGUVU KATIKA UONGOZI.

Katika moja ya matatizo yanayoisumbua nchi yetu na hata bara la Africa kwa ujumla ni ukosefu wa uongozi mzuri. Tunao viongozi ambao wamepewa nafasi za kuongoza ila hawajapata mafunzo mazuri ya uongozi. Kuongoza kwa utashi kila mtu anaweza, lakini hakumwezeshi kiongozi kuweza kupambana na changamoto mbalimbali za zama hizi.

Kwa sababu hii kiongozi anapaswa kujifunza mbinu bora zaidi zitakazomwezesha kufanikiwa kwenye uongozi wake.

Tumeona vijana wengi wanaochipukia kwenye uongozi wakipotea ghafla katika kipindi ambacho wanakuwa wapo juu kiuongozi. Yote haya yanapelekea kupoteza ndoto zao na kushindwa kuonesha ule uwezo mkubwa ambao upo ndani yao.

Ni katika hali hii nimefikiria ni jinsi gani tunaweza kusaidiana ili kujiandaa kuwa viongozi bora. Sio lazima uwe kiongozi wa siasa tu, unahitaji kuwa kiongozi wa familia yako, unahitaji kuwa kiongozi kwenye kazi yako na pia unahitaji kuwa kiongozi kwenye biashara yako.

Katika kufikiria huku nimeona sio vibaya kama tutashirikishana mafunzo mazuri ya uongozi kutoka kwenye kitabu THE 48 LAWS OF POWER. Hizi ni sheria 48 za nguvu katika uongozi, zimetokana na historia ya viongozi maarufu waliofanikiwa sana siku za nyuma.

Nimeandaa utaratibu ambao kila siku kwa siku 48 utajifunza sheria moja kupitia blog hii MAKIRITA AMANI na pia nitawashirikisha kitabu hiko ili uweze kujisomea zaidi.

Kwenye kila sheria nitaeleza kwa kifupi kwa lugha rahisi ya kiswahili ili kila mmoja wetu aweze kuelewa bila ya kujali lugha anayotumia. Atakayehitaji kusoma kwa undani zaidi ataendelea kusoma kwenye kitabu.

Mpango huu utaanza tarehe 01/04/2015 na utaendelea kila siku. Ili kuhakikisha unapata makala hizi ambazo zitakujenga sana kiuongozi bonyeza hapa na uweke email na kisha idhibitishe kwenye email utakayotumiwa. Ni bure kabisa, hakuna malipo yoyote, ni utayari wako tu wa kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo unajifunza.

Karibu sana kwenye mafunzo haya mafupi ambayo yatakuandaa kuwa kiongozi bora.

UKURASA WA 81; Achana Na Ubishi, Hautakusaidia Lolote.

Ukishaamua ni kitu gani ambacho unataka kufanya kwenye maisha yako, basi hapo ndio unafunga mjadala. Usijiingize kwenye ubishi kuhusiana na kile unachofanya.

Kama umeshaamua kwamba wewe utakuwa mjasiriamali, anza kufanya ujasiriamali, jua kabisa mpaka unakufa wewe utakuwa mjasiriamali. Kuanza kuingia kwenye ubishi kama mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa hakutakusaidia lolote. Kuanza kuingia kwenye ubishi kwamba kama kweli utaweza kufanikiwa kwenye ujasiriamali au la hautakusaidia chochote.

SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.

Waache wasiojua matumizi ya muda wao waendelee kubishana, wewe tumia muda huo kufanya kile unalichopanga kufanya.

Kama kuna kitu hujui, jifunze.

Kama kuna mahali unakwamba omba msaada, angalia wengine walifanyaje.

Usiingie kwenye ubishi, iwe na mtu au na nafsi yako mwenyewe. Usianza kujiuliza kama maamuzi uliyofanya ni sahihi au la. Jua kwamba hayo ndio maisha uliyochagua kuyaishi na anza kuyaishi haraka sana.

Muda wako ni mfupi sana na una vitu vingi vya kufanya, una vitu vingi vya kujifunza na una watu wengi wa kuwahudumia.

Epuka ubishi ambao hautakuongezea maarifa zaidi, au fursa zaidi au fedha zaidi. Asilimia 99 ya ubishi unaingia hapo, achana nao.

SOMA; Mambo KUMI Ya Kufanya Ili Usiishi Maisha Ya Majuto.

TAMKO LA LEO;

Nimeshaamua kitu ambacho ninakitaka kwenye maisha yangu. Sitarudi tena nyuma na kuanza kujihoji kama nilifanya maamuzi sahihi au la. Sitoingia kwenye mabishano kama naweza au la. Nitatumia muda wangu vizuri kufanya kile ambacho nimechagua kufanya na nina hakika nitafikia mafanikio makubwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 82 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Hiki Ndio Chanzo Cha Nguvu Zako.

“Look well into thyself; there is a source of strength which will always spring up if thou wilt always look.” ― Marcus Aurelius

Angalia vizuri ndani ya nafsi yako na utaona chanzo kikubwa cha nguvu ambacho kitaendelea kububujika kama utaendele  kukitumia.

Kama unafikiri huna nguvu, kama unafikiri huna ujasiri basi unakosea sana.

una nguvu kubwa sana ambayo ipo ndani yako, lakini nguvu hii hutaweza kuitumia mpaka utakapojua kwamba ipo na utakapojua jinsi ya kuitumia.

SOMA; SIRI YA 6 YA MAFANIKIO; Tumia Nguvu Yako Kuchagua.

Pata muda wa kutulia na kuangalia ndani yako, kuongea na nafsi yako na utapata chanzo kikubwa sana cha nguvu ambayo utakuwa nayo maisha yako yote.

Nguvu tayari unazo, ni wewe kuzijua na kuanza kuzitumia.

Nakutakia siku njema.

SOMA; SIRI YA 23 YA MAFANIKIO; Kama Una Matumaini Ya Baadae Una Nguvu Leo.

Saturday, March 21, 2015

UKURASA WA 80; Utabiri Mzuri Wa Kesho.

Je unahitaji mtu wa kukusaidia kuitabiri vizuri kesho yako? Huna haja ya kwenda kwa wapiga ramli au watabiri wa nyota, kwani mtabiri bora kabisa tayari upo nae hapo ulipo. Mtabiri huyo ni wewe mwenyewe.

Unafikiria kama biashara unayofanya itakuletea mafanikio makubwa baadae?

Unafikiria kama kazi unayofanya utadumu nayo kwa muda mrefu?

Yote haya hayahitaji wewe kwend akwa mtabiri anayesifika, yanahitaji wewe ufanye jambo moja tu, ishi vizuri leo.

SOMA; Kesho Jua Litachomoza Tena...

Kama ukiishi vizuri leo, unakuwa umefanya maandalizi ya kuishi vizuri kesho. Kama utafanya biashara yako vizuri leo, unakuwa umetengeneza mazingira mazuri ya kufanikiwa kwenye biashara yako kesho. Kama ukifanya kazi yako vizuri leo unakuwa umetengeneza mazingira mazuri ya kufanya kazi nzuri zaidi kesho.

Kila kitu kitakwenda vizuri kesho kama utafanya vizuri leo.

Hivyo badala ya kuhofu kwamba mambo yatakwendaje kesho, badala ya kupoteza muda kutafuta watabiri, tumia muda huo kuishi vizuri leo na utatengeneza mazingira mazuri ya kesho.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba mtabiri mzuri wa maisha yangu ya kesho nu mimi mwenyewe na jinsi ya kufanya utabiri huu ni kuishi vizuri leo, kufanya kilicho chema leo na kesho mambo yatakwenda vizuri. Sitapoteza muda kuhofu kesho itakuwaje au kutafuta mtu wa kunitabiria, nitatumia muda huo kufanya vizuri leo na nina hakika kesho mambo yatakuwa mazuri sana.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Za Watu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 81 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Umuhimu Wa Kuchukua Hatari.

“Risk anything! Care no more for the opinion of others ... Do the hardest thing on earth for you. Act for yourself. Face the truth." ― Katherine Mansfield,

Kuchukua hatari ndio kila kitu. Usijali maoni ya wengine… Fanya vitu ambavyo ni vigumu sana kwako. Fanya mambo yako. Ukabili ukweli.

Kuna wakati mtu unaogopa kuchukua maamuzi ukiona kwamba ni maamuzi ya hatari sana kwako. Nikuambie kwamba maamuzi ya hatari ndio yanayoweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.

Kuna wakati ambao unaacha kufanya mambo magumu, unafanya mambo ambayo ni rahisi kwako. Nikuambie kwamba mambo magumu ndio yatakayokuletea manufaa makubwa kwenye maisha yako, yafanye hayo. Hakuna kitu rahisi.

SOMA; TAFAKARI YA LEO; Urefu Wa Muda Sio Mrefu.

Ukisikiliza maneno ya kila mtu, hutafanya jambo lolote kubwa kwenye maisha yako, maana watu hawakosi la kusema, hata kama ungefanya nini.

Fanya mambo yako, ukabili ukweli. Hakuna kinachoweza kuupinga ukweli, hata ukiukwepa kuna siku mambo yote yatakuwa wazi.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

Friday, March 20, 2015

TAFAKARI YA LEO; Urefu Wa Muda Sio Mrefu.

Utaanza lini kutekeleza mipango mizuri uliyoweka? Muda sio mrefu.
Karibu kila mmoja wetu ameshaingia kwenye mtego huu, wa kufikiria muda sio mrefu.
Lakini swali la msingi ni urefu wa muda sio mrefu ni upi?
Yaani unaposema muda sio mrefu, kiuhalisia unamaanisha nini? Kesho? Wiki ijayo? Mwezi ujao? Mwaka ujao?
Kulingana na mtazamo wako mwenyewe muda sio mrefu unaweza kuwa touti.
Sasa tafakari yetu ya leo ni UPI UREFU WA MUDA SIO MREFU?
Kwa maana hii usiseme tena nitaanza muda sio mrefu, sema nitaanza jumatatu ijayo, au tarehe kumi ya mwezi ijao au mwezi wa tatu wa mwaka ujao.
Hapo utakuwa na kitu cha kukusuta, kama hutoanza. Na itakusukuma kuanza.
#TUTAFAKARI.

UKURASA WA 79; Usitegemee Nyundo Tu, Kuna Zana Nyingine Pia.

Wenye busara walipata kusema maneno haya mazuri sana;

Kama zana pekee uliyonayo ni nyundo, basi kila kinachokuja mbele yako kitaonekana kama msumari.

Umeielewa vizuri kauli hiyo? Kama hujaielewa tafuta mtoto mdogo halafu mpe nyundo akae nayo tu na uone atakuwa anafanya nini. Atagonga kila kitu.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

Sawa najua wewe huna nyundo tu na pia najua tukikupa nyundo hutagonga kila kitu. Ila umekuwa unafanya kosa hili karibu kila siku kwenye maisha yako.

Fikiria ni matatizo mangapi ambayo umeshakutana nayo kwenye maisha yako, je umekuwa unajaribu kuyatatuaje? Ni hatua zipi ambazo umekuwa unachukua pale unapokutana na changamoto?

Kama utakuw amuwazo na nafsi yako utaona kwamba umekuwa unatatua matatizo yako yote kwa aina moja ya kufikiria. Umekuwa ukipambana na changamoto zako zote kwa mbinu moja.

Bado unashangaa kwa nini matatizo hayaishi, au kwa nini changamoto zinakushinda? Ni kwa sababu unatumia nyundo tu, una aina moja ya mawazo ya kutatua matatizo yako. Una mbinu moja ya kupambana na changamoto zako na hivyo umekuwa ukishindwa na kama utaendelea kuitumia utaendele akushindwa.

SOMA; Hatua TANO Za Kuongeza Uzalishaji Wako Ili Kufikia Mafanikio.

Anza kupata mawazo tofauti tofauti kwenye tatizo unalokutana nalo. Badala ya kufikiria wewe ndio upo kwenye tatizo hebu fikiria kama usingekuwa kwenye tatizo hilo, ungemshauri nini aliyepo kwenye tatizo hilo? Kama ingekuwa wewe sio muathirika wa tatizo hilo je ungelichukuliaje? Aina hizi tofauti za kufikiria zitakupatia picha kubwa itakayokusaidia kuchukua hatua nzuri.

Unapokutana na changamoto kabla hujairukia na kuanza kuitatua kaa chini kwana na ufikirie mbinu gani inafaa kwa changamoto hiyo. Jua nini chanzo cha changamoto hiyo. Jua ni kwa kiasi gani inakuathiri. Na jua wengine waliokutana na changamoto hiyo walitumia njia gani wakashindwa na walitumia njia gani wakafanikiwa kupambana nayo.

Njia muhimu kabisa ya kupata mawazo tofauti, ya kupata mbinu tofauti ni kujifunza, kusoma. Jifunze kutokana na makosa yako mwenyewe, jifunze kutoka kwa wengine pia. Na muhimu zaidi soma kila siku.

SOMA; Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.

TAMKO LA LEO;

Najua kuna zana nyingi nazoweza kutumia kutatua matatizo yangu, kupambana na changamoto zangu. Sitatumia tena zana moja ambayo nimezoea kuitumia kila siku, kwa sababu kila tatizo, kila changamoto ina utofauti wake na inahitaji mbinu tofauti. Nitajifunza na kujisomea kila siku ili niweze kuongeza zana zangu za kuniwezesha kufanikiwa kwenye maisha.

Tukutane kwenye ukurasa wa 80 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Sio Lazima Ufanye Maamuzi Sahihi.

“I do not believe in taking the right decision, I take a decision and make it right.” ― Muhammad Ali Jinnah

Siamini kwenye kufanya maamuzi sahihi, nafanya maamuzi kisha nayafanya yawe sahihi.

Kuna wakati ambao unaacha kufanya maamuzi kwa sababu huna uhakika kama maamuzi hayo yatakuwa sahihi au la. Au wakati mwingine unajua kabisa kwamba maamuzi yako hayatakuwa sahihi, hivyo hufanyi maamuzi.

SOMA; UKURASA WA 78; Hiki Ndio Kitu Unachoweza Kufanya, Bila Ya Kujali Uwezo Wako.

Kwa kutofanya maamuzi unaweza kuona uko salama, lakini kama unataka kufikia mafanikio makubwa, hiki ni kikwazo kikubwa sana kwako. Ili kufikia mafanikio unatakiwa kufanya maamuzi mengi na wakati mwingine kwa haraka. Unahitaji kuchukua nafasi ambazo wakati mwingine ni hatari.

Badala ya kusubiri uwe na uhakika ndio ufanye maamuzi fanya maamuzi kisha yafanye yawe sahihi. Fanya maamuzi yoyote ambayo yatakupelekea kufikia lengo lako, kisha yafanye maamuzi hayo kuwa sahihi. Kwa njia hii utaweza kuvuka vikwazo vingi sana na kufikia mafanikio.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.

Thursday, March 19, 2015

UKURASA WA 78; Hiki Ndio Kitu Unachoweza Kufanya, Bila Ya Kujali Uwezo Wako.

Jambo moja la kushangaza kwetu binadamu ni kwamba kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na kuna vitu ambavyo hatuwezi kufanya.

Vitu ambavyo tunaweza kufanya ni vile vitu ambavyo tumekuwa tunafanya kila siku, au tunaona watu wengine wakiwa wanavifanya. Hii inatupa imani kwmaba vinawezekana kufanyika na tunaweza kuvifanya bila ya tatizo.

SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.

Kwa upande wa pili kuna vitu ambavyo hatuwezi kufanya. Vitu hivi vimegawanyika katika makundi mawili, ila hatuyajui. Kundi la kwanza ni vitu ambavyo ni kweli kabisa hatuwezi kuvifanya kutokana na kukosa baadhi ya vitu tunavyohitaji. Na kundi la pili ni vitu ambavyo hatuwezi kuvifanya kwa sababu hatujawahi kufanya au hatujawahi kumuona mtu akivifanya.

Asilimia 99 ya vitu tunavyoona hatuwezi kufanya vipo katika kundi la pili, yaani tunaona hatuwezi kufanya, sio kwa sababu haiwezekani kabisa, ila kwa sababu hatujawahi kufanya au hatujamuona mtu mwingine anafanya.

SOMA; Njia KUMI Za Kuboresha Maisha Yako Ya Kibiashara.

Badili sasa mtizamo wako kuhusu vitu ambavyo unafikiri huwezi kufanya. Unapopata wazo lolote, badala ya kuliua kwa kusema hii haiwezekani au siwezi kufanya, sema nawezaje kufanya kitu hiki? Kwa kujiuliza swali hili unaipa akili yako nafasi ya kuchambua na kama unajiamini utapata majibu mengi sana ya jinsi unavyoweza kufanya.

Kitu unachoweza kufanya bila ya kujali hali yako ni kile ambacho unaamini unaweza kufanya.

Kitu usichoweza kufanya ni kile ambacho unaamini huwezi kufanya. Ni hivyo tu.

SOMA; Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwmaba hatua ya kwanz aya kuwez akufanya kitu ni kuamini kwamba kinawezekana kufanyika, naweza kukifanya. Kuanzia sasa kila nitakapopata wazo la kuboresha kazi au biashara zangu sitasema haiwezekani ila nitajiuliza itawezekanaje? Swali hili litafungua akili yangu na kunipa majibu mengi zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 79 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

NENO LA LEO; Haya Ndio Maafa Unayojitengenezea Mwenyewe.

“As long as you look for someone else to validate who you are by seeking their approval, you are setting yourself up for disaster. You have to be whole and complete in yourself. No one can give you that. You have to know who you are - what others say is irrelevant.” ― Nic Sheff

Kama bado unasubiri wengine wakukubali vile ulivyo kwa kufanya wanachotaka wao, umejiandalia maafa. Unahitaji kuwa vile ulivyo wewe mwenyewe, hakuna anayeweza kukupa hilo. Unatakuwa kujua wewe ni nani, wanayosema mengine hayana maana.

SOMA; Jinsi ya kuchagua Kampuni ya kuwekeza katika Soko la Hisa

Wewe ni wewe, hakuna mwingine kama wewe dunia nzima.

Usikubali kuiga kile wengine wanachofanya ili tu wakukubali, kuwa ulivyo wewe na kama wanakujali watakukubali vile ulivyo na watakuheshimu sana.

Ila ukianza kutengeneza maisha tofauti ili tu watu wakukubali, hawatakukubali na watakudharau kabisa. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayependa mtu ambaye sio halisi.

Kuwa halisi, kuwa wewe, jiamini, jikubali. Fanya kile unachofanya vizuri, wanaokujali watakuwa pamoja na wewe, wasiokujali, hata ungefanya nini bado usingeweza kuwashawishi.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Za Watu.

Wednesday, March 18, 2015

UKURASA WA 77; Kama Watu Hawakupingi Unakosea Sana.

Kwenye kazi au biashara unayofanya, au hata maisha unayoishi kuna kipimo rahisi sana cha kuweza kujua kama unachofanya ni cha tofauti au ni cha kawaida.

Kipimo hiko ni muitikio wa watu kwa kile unachokifanya. Kama kila mtu anakubaliana na wewe kwa kile unachofanya na jinsi unavyofanya basi utakuwa unafanya makosa makubwa sana. Utakuwa unafanya kitu ambacho ni cha kawaida sana kwao na hivyo hakitawafanya hata wajali.

SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

Lakini kama watu watakupinga, watakuambia haiwezekani, watakupa ushahidi wa waliojaribu wakashindwa, watakupa hata historia ni jinsi gani haiwezekani basi hapo furahia sana maana unaanza kufanya jambo ambalo sio la kawaida.

Na uzuri wa kufanya jambo ambalo sio la kawaida ni kwamba unaleta mabadiliko makubwa, unapata mafanikio makubwa na unawasaidia wengi zaidi.

Kumbuka jambo tunalozungumzia ufanye hapa lisiwe kinyume na sheria au taratibu za kawaida za maisha ya binadamu. Kwa kifupi lisiwe na madhara kwa watu au eneo unalofanyia.

SOMA; NENO LA LEO; Furahia Kupingwa…

Kufanya jambo jipya, ambalo halijazoeleka kunahitaji ujasiri mkubwa sana. Ni ujasiri huu ndio unaoweza kukutenga na wale ambao hawataweza kufikia mafanikio makubwa. Kama na wewe umekosa ujasiri huu mtaendelea kuwa pamoja, hamuendi mbali na mnaendelea kurudishana nyuma.

Kama unataka kuamini huna jambo kubwa na la tofauti unalofanya kwenye maisha jaribu moja kati ya haya, jaribu wka wiki moja tu halafu utaona muitikio wa watu ukoje.

1. Kama umeajiriwa, wahi kazini mapema sana kabla ya watu wengine wote. Fanya kazi zako kwa makini na kamilisha kwa wakati, mapumziko yakiisha rudi kwenye kazi yako haraka. Watu wakiwahi kuondoka, ongeza muda kidogo, yaani kuwa wa mwisho kuondoka. Kukitokea jambo lolote linalohitaji msaada kuwa wa kwanz akujitolea. Fanya hivi na utaona ni jinsi gani watu watakavyokupinga na kukusema vibaya, japo hujaingilia maisha yamtu yeyote.

2. Kama unatumia pombe na una marafiki ambao huwa unakunywa nao, waambie wewe hunywi tena pombe, ukikutana nao agiza maji, au juisi na baada ya muda omba ruhusa ya kuondoka ili uwahi kufanya mambo yako mengine. Utaona jinsi ambavyo watakupinga, japo ni marafiki zako na unalolifanya ni jema kwa maisha yako.

3. Kama unafanya biashara, fanya kwa utofauti, toa huduma za kipekee kwa wateja wako, hakikisha hawezi kuzipata popote. Zungumza nao vizuri, unacheka nao, unawasiliana nao. Halafu utaona wafanyabiashara wengine watakavyokupinga, na wengine kudiriki kusoma unatumia uchawi.

Fanya zoezi moja hapo kwa wiki moja tu, halafu uone muitikio wa watu ukoje. Halafu ukikamilisha wiki moja, ongeza nyingine na nyingine na nyingine mpaka huo utakapokuwa utaratibu wako wa maisha, na watu watazoea tu, na wakishazoea inakuwa ni kawaida, itabidi utafute kingine cha kufanya ambacho watu hawajazoea.

SOMA; UKURASA WA 40; Amua Kuwa Wewe…

TAMKO LA LEO;

Najua kabisa kwamba kama ninafanya jambo la tofauti ambalo watu hawajalizoea nitapingwa na kukatishwa tamaa. Hivyo kipimo changu cha kujua kama ninachofanya ni cha tofauti ni muitikio wa watu. Kama jambo lolote ambalo nafanya hakuna hata mmoja anayepinga au kushangazwa, basi ni jambo la kawaida sana na nitaachana nalo.

Tukutane kwenye ukurasa wa 78 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

NENO LA LEO; Unachohitaji Kufanya Ili Dunia Nzima Ikukubali.

“Because one believes in oneself, one doesn't try to convince others. Because one is content with oneself, one doesn't need others' approval. Because one accepts oneself, the whole world accepts him or her.”― Lao Tzu

Kwa sababu mtu anajiamini mwenyewe, hajaribu kuwashawishi wengine. Kwa sababu mtu ameridhika na nafsi yake, hahitaji idhini ya wengine. Kwa sababu mtu amejikubali mwenyewe, dunia nzima inamkubwali.

Kama hujiamini wewe mwenyewe hakuna mtu mwingine anayeweza kukuamini. Unahitaji kuanza kujiamini wewe mwenyewe na wengine watakuamini, kwa sababu kujiamini hakujifichi.

Kama hujaridhika na nafsi yako, utakazana kupata idhini ya watu wengine, waone kwamba umeridhika. Kumbe sivyo na maisha yako yanakuwa magumu sana.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Za Watu.

Kama utajikubali wewe mwenyewe, basi dunia nzima haina budi bali kukukubali, bila ya kujali wewe ni nani, unatokea wapi na una rangi gani.

Dunia inakupa kile unachotoa, kile unachotaka na haina upendeleo. Kama kuna kitu unataka ila hujapata, basi jua hujakitaka vya kutosha au hujatumia njia sahihi za kukipata.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…

Tuesday, March 17, 2015

Huu Ndio Ukoma Wa Zama Hizi, Na Jinsi Unavyoweza Kuuepuka.

Moja ya magonjwa ambayo yamewahi kuisumbua sana dunia ni ugonjwa wa ukoma.
Huu ni ugonjwa ulioua watu wengi sana na kuacha wengine wakiwa kwenye hali mbaya sana.
Changamoto kubwa ya ugonjwa huu ni kwamba ulikuwa wa kuambukizwa. Yaani ukikaa na mtu mwenye ukoma na wewe unapata ugonjwa huu.
Kwa hiyo njia kubwa ya kujikinga na ugonjwa huu ilikuwa ni kujitenga na watu wenye ugonjwa huu.
Kwa bahati nzuri sana ugonjwa huu umetokomezwa kabisa duniani.
Ila kwa bahati mbaya sana kuna ukoma mpya umeingia duniani. Ukoma huu unaua watu wengi sana lakini wengi bado hawajaujua.
Ukoma huu ni mawazo hasi.
Mawazo hasi yamekuwa yanawarudisha watu wengi sana nyuma.
Yamekuwa yakizima ndoto nzuri za watu na hata kuharibu maisha yao kabisa.
Mawazo hasi yanasambaa kwa kasi kuliko hata ukoma, hasa kwenye ulimwengu huu ambao mawasiliano yamekuwa rahisi sana.
Jiepushe na ugonjwa huu kwa kukagua kila wazo unalopokea kabla ya kuliingiza kwenye akili yako na kuliufanyia kazi.
Epuka sana mawazo hasi, ni sumu kubwa kwa mafanikio yako.

UKURASA WA 76; Jinsi Ushauri Unavyoweza Kufanya Kazi Kwako

Tunaishi kwenye jamii ambazo kila mtu anaweza kutoa ushauri kwenye jambo lolote lile. Usipokuwa makini unaweza kuchukua ushauri ambao sio mzuri na ukakuingiza kwenye matatizo makubwa au kukupotezea muda.

Kuna ushauri ambao ni wa bure, ambao unatolewa na kila mtu. Hiki ni kitu hatari sana, usikimbilie kuufuata, utaumia.

SOMA; USHAURI ADIMU; Chukua Ushauri Kwa Mtu Huyu Tu, Achana Na Wengine Wote.

Aina za ushauri huu ni kama; biashara fulani inalipa kweli, ona fulani kaanza kuifanya juzi juzi tu na sasa hivi ana mafanikio. Ubaya wa ushauri huu utapew ana mtu ambaye hafanyi hiko anachokushauri na wala hajachukua muda kuchunguza na kujua ni hatua gani mtu huyo amepitia mpaka akapata mafanikio hayo. Unapopata ushauri kama huu usikimbilie kufanya, bali chukua muda wako kufanya utafiti wa kile ulichosikia, asilimia 80 ni uongo.

SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Kuna ushauri kutoka kwa watu ambao wanafanya kitu, au wamefanya utafiti wa kutosha kuhusu kitu fulani. Hawa ndio watu ambao unatakiwa kusikiliz ana kuchukua ushauri wao. Na hata utakapouchukua bado huwezi kuutumia moja kwa moja, utahitaji kuangalia ni jinsi gani unaweza kuboresha zaidi na kulingana na uwezo wako na mazingira yako.

Usitegemee ushauri wowote utakaopokea utafanya kazi kwa silimia 100, wewe una nafasi kubwa sana ya kuufanya ushauri huo ufanye kazi. Usiwe mvivu wa kufikiri, kupanga na kutekeleza mipango yako. Hakuna ushauri utakaoweza kufanya kazi kwako kama wewe hutafanya kazi.

Pamoja na kupata ushauru mzuri, bado unahitaji kufanya kazi kubwa sana ya kuufanya ushauri huo ukuzalishie matunda mazuri.

SOMA; NENO LA LEO; Ushauri Bora Unaoweza Kutoa Kwa Rafiki Yako.

TAMKO LA LEO;

Najua suahuri wa bure una gharama kubwa sana kama nitauchukua biala ya kufanya utafiti na kuona nitautumiaje. Ushauri wowote nitakaopokea kutoka kwa watu, nitaufanyia utafiti kwanza na kuona ni jinsi gani naweza kuutumia vizuri. Najua hakuna ushauri unaoweza kufanya kazi kwa asilimia 100, hivyo nafasi yangu ni kubwa sana kwenye kufanyia kazi ushauri.

Tukutane kwenye ukurasa wa 77 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Ukishafanya Kitu Hiki Kimoja, Utajua Jinsi Ya Kuishi.

“As soon as you trust yourself, you will know how to live.” ― Johann Wolfgang von Goethe

Mara utakapojiamini, utajua jinsi ya kuishi.

Ni vigumu sana kujua jinsi ya kuishi kama wewe mwenyewe hujiamini. Utahangaika kufanya mambo mengi na utaishia kushindwa na kukata tamaa.

Unapojiamini unajua ni kitu gani hasa unataka na utang’ang’ana mpaka ukipate, kwa kuwa una uhakika ni lazima utakipata.

Je ni nini kinakufanya usijiamini? Hutaki kujua jinsi ya kuishi maisha yako vizuri?

Nakutakia siku njema.

SOMA; Nyasi Za Upande Wa Pili Ni Za Kijani Zaidi…

Monday, March 16, 2015

UKURASA WA 75; Kila Mtu Ana Matatizo…

Kuna wakati ambao unakuwa na matatizo mengi sana kwenye maisha yako na kufikiri  kwamba kama ungekuwa kama mtu fulani huenda usingekuwa na matatizo.

Labda huna kazi, unafikiri kama ungekuwa na kazi kama watu unaowaona wana kazi basi maisha matatizo yako yangekwisha.

Labda wewe ni mfanyakazi wa kawaida na unafikiria kwamba kama ungekuwa bosi basi matatizo yako yote yangeisha.

SOMA; Njia Mbili Za Uhakika Za Jinsi Ya Kupata Fedha.

Au unafanya biashara na kuona biashara yako haiendi vizuri, unafikiria kama ungekuwa unafanya biashara wanazofanya wengine basi matatizo yako yangekwisha…

Unaweza kufikiria hivi utakavyo, lakini ukweli ni kwambaaa

Kila mtu ana matatizo.

SOMA; USHAURI; Umuhimu Na Jinsi Ya Kutofautisha Biashara Na Maisha Ya Kawaida.

Unaweza kuona ukiwa na kazi hutakuwa na matatizo, lakini wafanyakazi wengi sana wana matatizo kuliko hata ambayo unayo wewe.

Unaweza kuona bosi wako hana matatizo, ila ukweli ni kwamba anaweza kuwa na matatizo makubwa kuliko uliyonayo wewe.

Unaweza kuona biashara za wengine hazina matatizo kama unayopata wewe, ila ukipewa biashara hizo unawez akukimbia kabisa.

Kwa kuw akila mtu ana matatizo kwa hiyo tufanyeje sasa?

Fanya hivi, acha kuangalia nani hana matatizo, acha kuangalia matatizo yako sana na anza kuangali ni jinsi gani unaweza kuboresha maisha yako, ni jinsi gani unaweza kuyatyumia matatizo yako kuwa bora zaidi.

SOMA; Hizi Ndio Siri 21 Za Mafanikio

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba kila mtu ana matatizo. Naweza kuona kwamba watu fulani hawana matatizo kama mimi ila nikipewa maisha yao nitashindwa kuyaendesha. Nitawekeza nguvu zangu kuboresha maisha yangu kila siku na kuangalia ni jinsi gani naweza kuyatumia matatizo ninayopitia kufaidika zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 18 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Ufunguo Muhimu Wa Ufunguo Wa Mafanikio.

One important key to success is self-confidence. An important key to self-confidence is preparation. -Arthur Ashe

Ufunguo muhimu wa MAFANIKIO ni KUJIAMINI. Ufunguo muhimu wa KUJIAMINI ni MAANDALIZI.

Kama unataka kufikia mafanikio makubw akwneye maisha yako unahitaji kujiamini. Hakuna mtu ambaye hajiamini anayeweza kufanikiwa. Kwa sababu ili ufanikiwe lazima watu wegine wakuamini ili waweze kushirikiana na wewe, sasa kama wewe mwenyewe hujiamini ni vigumu sana wengine kukuamini.

SOMA; Huu Ni Uwekezaji Wa Uhakika Ambao Hautakuangusha.

Ili uweze kujiamini unahitaji kuwa na maandalizi ya kutosha. Kama hujajiandaa utakuwa na wasi wasi na utendaji wako na hii itakuondolea kujiamini.

Kwa maana hiyo basi ili uweze kufikia mafanikio unahitaji kuw ana maandalizi mazuri.

Anza maandalizi leo, kama kweli unataka kufikia mafanikio.

Nakutakia siku njema.

SOMA; SIRI YA 10 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujiamini.

Sunday, March 15, 2015

Huu Ni Uwekezaji Wa Uhakika Ambao Hautakuangusha.

"A man who empties his purse into his head never goes broke."
Kama unatumia kipato chako kujiemdeleza zaidi huwezi kufilisika.
Kwa maana hiyo kama una shilingi elfu kumi labda na hujui uifanyie nini. Ushauri wa uhakika na ambao hutausikia popote ni huu. Katafute kitabu kinachohusiana na jambo lolote unalopenda kufanya, kinunue, kisome ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho. Rudia kukisoma tena kwa mara ya pili.
Andika vitu 20 ulivyojifunza kwenye kitabu hiko.
Chagua vitu kumi utakavyoanza kuvifanyia kazi mara moja ulivyojifunza kwenye kitabu hiko.
Anza kuvifanyia kazi.
Ni hivyo tu, miaka kumi ijayo utashukuru sana maamuzi uliyochukua leo.
Kama hutafanya chochote miaka kumi ijayo hutakuwa tofauti sana kama ulivyo leo.
Kila la kheri,
TUPO PAMOJA.
www.amkamtanzania.com

UKURASA WA 74; SAMEHE…

Labda tuseme kuna mtu amekuudhi sana kwenye maisha yako, amekufanyia jambo baya sana kiasi kwamba maisha yako yameharibika sana, una haki ya kumchukia, si ndio?

Labda tuseme mtu huyu alifanya jambo ambalo lilikupa hasara kubwa sana kwenye maisha. Au kuharibu maisha yako sana. Au hata kujaribu kuondoa uhai wako, ila kwa njia moja au nyingine ukapona.

SOMA; Fanya Mambo haya matatu kuwa na maisha bora na yenye furaha.

Una haki ya kumchukia mtu huyu, kuwa na kinyongo naye na wakati wowote unapomuona kuchukia. Una haki kabisa ya kukataa kukutana nae, na hata kutokutaka kushirikiana nae tena. Au hata kutoongea nae hata kama ataomba msamaha.

Unaweza kuona hili ni suluhisho kwako au una haki ya kufanya hivi, ila leo nakuambia kwamba unafanya makosa makubwa sana kwenye maisha yako.

Wewe ndiye unayeendelea kuumia kwa hali hiyo ya kuwa na kinyongo. Wewe ndiye unayeshindwa kufanya mambo yako vizuri kwa sababu ya kujiwekea kinyongo. Wakati kwa upande wa pili mwenzako anaendelea na maisha yake.

SOMA; NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Msamaha

SAMEHE mtu yeyote ambaye umemuwekea kinyongo mpaka sasa. Ondoa kabisa kinyongo kwenye moyo wako na endelea na maisha yako. Hata kama hutaki kushirikiana nae tena, usiendelee kuweka kinyongo. Msamehe kwa yote aliyofanya na endelea na maisha yako.

Kwa kufanya hivi utakuwa umenunua uhuru ambao uliupoteza kwa kuweka kinyongo.

TAMKO LA LEO;

Leo hii nawasamehe wote ambao wamewahi kunikosea kwenye maisha yangu(wataje majina). Naondoa vinyongo vyote ambavyo nilikuwa nimeweka na sasa nimekuwa mtu huru. Sitakuja kuweka tena kinyongo kwenye maisha yangu. Mtu anaponikosea naachana nae na kuendelea na maisha yangu. Muda wangu ni wa thamani sana kuupoteza kwa kushikilia vinyongo vya watu ambao hawanijali.

SOMA; UKURASA WA 68; Furaha Ya Leo Ni Kikwazo Maisha Yako Yote…

Tukutane kwenye ukurasa wa 75 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.