Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, March 14, 2015

NAFASI MOJA YA KAZI; Changamkia haraka.

Kuna mtu anahitaji kufanya mazoezi ya mwili ila ratiba yake imembana sana hivyo anakosa muda wa kufanya mazoezi.
Hivyo anatafuta mtu yeyote ambae yupo tayari kumsaidia kufanya mazoezi na atamlipa kiasi atakachohitaji.
Kwa hiyo kama unaweza kufanya mazoezi na huyu mtu akanufaika kwenye mwili wake, nafasi ipo.
Swali ni je unaiweza kazi hii?
Na kama huiwezi je unafikiri inawezekana?
Kwa pamoja tutakubaliana kwamba hiki ni kitu ambacho hakiwezekani.
Unajifunza nini hapa?
Kikubwa kilichonifanya nikushirikishe hili ni wewe ujifunze kwamba kuna vitu huwezi kufanyiwa na mtu kwenye maisha yako. Vitu muhimu kwako unahitaji kuvifanya mwenyewe.
Hakuna mtu atakayeweza kukufanyia kazi wewe ili upate mafanikio, ni lazima utumie akili yako na nguvu zako kuyapata mafanikio.
Tambua kwamba vitu muhimu kwenye maisha yako vinakutegemea wewe mwenyewe. Weka juhudi na maarifa. Hakuna mtu anayeweza kukufanyia wewe mazoezi halafu ukawa na afya njema. Hili ni jukumu lako, usilikwepe.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment