Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, March 26, 2015

UKURASA WA 85; Jipe Miadi.

Kwa mfano ukataka kuonana na mimi ili tuzungumze jambo lolote, tutawekeana miadi. Kwamba siku fulani na muda fulani tutakuwa pamoja tukizungumzia jambo fulani. Na tunapokutana hatutegemei kuwa na usumbufu mwingine wowote, ni mimi na wewe.

Nikikupigia simu sasa hivi, utaacha jambo lolote ambalo unafanya na kujibu simu hiyo, hata kama nitakuwa nakuambia jambo lolote ambalo sio muhimu sana kwako. Utanipa muda wako kwa jambo lolote ambalo nataka mimi.

SOMA; Maswali ambayo huulizwa mara nyingi kuhusu uwekezaji katika hisa.

Unatoa muda wako kwa mambo mengi sana. Watu wanakutumia meseji unazijibu, watu wanaandika vitu kwenye mitandao ya kijamii unavijibu, unachangia na kadhalika. Watu wanakutumia meseji za vichekesho na wewe unazituma kwa wengine. Sijasema lolote hapa ni baya ila kuna kitu kimoja muhimu sana unakisahau.

Upo tayari kumpatia mtu yeyote muda wako. Ila je upo tayari kujipatia wewe muda? Upo tayari kuipatia nafsi yako muda?

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu hawajawahi kuzipatia nafsi zao muda. Na wewe ni mmoja wao.

Ipe nafsi yako muda, jipe miadi wewe mwenyewe. Kutana na nafsi yako na jadili mambo yote muhimu kwenye maisha yako. Muda huu unaoipa nafsi yako ni tofauti na muda wa kupumzika, huo pia unapaswa kuwa nao.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

Tenga muda kila siku ambapo utakaa wewe mwenyewe, kwenye utulivu wa hali ya juu na kuyaangalia maisha yako kwa jicho la ndani zaidi. Katika muda huu hakikisha hakuna wa kukusumbua, yaani usiwe na simu kabisa. Fanya kama hii ni sehemu ya kuitoroka dunia.

Muda huu unaweza kuwa dakika tano, kumi, robo saa, nusu saa na hata saa nzima. Katika muda huu weka matatizo yako pembeni kwanza, acha kufikiria kuhusu mtu mwingine yeyote na fikiria kuhusu maisha yako wewe, yalipotoka yalipo na yanapokwenda.

Kwa zoezi hili dogo sana utaweza kuona mabadiliko makubwa unayoweza kuyafanya kwenye maisha yako.

SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.

TAMKO LA LEO;

Kila siku nitatenga muda wa kukaa mwenyewe na nafsi yangu na kutafakari maisha yangu. Najua nafasi hii ni muhimu sana kwenye maisha yangu ili kujua nimetoka wapi, nipo wapi na ninaelekea wapi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 86 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment