Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, March 22, 2015

KITABU; SHERIA 48 ZA NGUVU KATIKA UONGOZI.

Katika moja ya matatizo yanayoisumbua nchi yetu na hata bara la Africa kwa ujumla ni ukosefu wa uongozi mzuri. Tunao viongozi ambao wamepewa nafasi za kuongoza ila hawajapata mafunzo mazuri ya uongozi. Kuongoza kwa utashi kila mtu anaweza, lakini hakumwezeshi kiongozi kuweza kupambana na changamoto mbalimbali za zama hizi.

Kwa sababu hii kiongozi anapaswa kujifunza mbinu bora zaidi zitakazomwezesha kufanikiwa kwenye uongozi wake.

Tumeona vijana wengi wanaochipukia kwenye uongozi wakipotea ghafla katika kipindi ambacho wanakuwa wapo juu kiuongozi. Yote haya yanapelekea kupoteza ndoto zao na kushindwa kuonesha ule uwezo mkubwa ambao upo ndani yao.

Ni katika hali hii nimefikiria ni jinsi gani tunaweza kusaidiana ili kujiandaa kuwa viongozi bora. Sio lazima uwe kiongozi wa siasa tu, unahitaji kuwa kiongozi wa familia yako, unahitaji kuwa kiongozi kwenye kazi yako na pia unahitaji kuwa kiongozi kwenye biashara yako.

Katika kufikiria huku nimeona sio vibaya kama tutashirikishana mafunzo mazuri ya uongozi kutoka kwenye kitabu THE 48 LAWS OF POWER. Hizi ni sheria 48 za nguvu katika uongozi, zimetokana na historia ya viongozi maarufu waliofanikiwa sana siku za nyuma.

Nimeandaa utaratibu ambao kila siku kwa siku 48 utajifunza sheria moja kupitia blog hii MAKIRITA AMANI na pia nitawashirikisha kitabu hiko ili uweze kujisomea zaidi.

Kwenye kila sheria nitaeleza kwa kifupi kwa lugha rahisi ya kiswahili ili kila mmoja wetu aweze kuelewa bila ya kujali lugha anayotumia. Atakayehitaji kusoma kwa undani zaidi ataendelea kusoma kwenye kitabu.

Mpango huu utaanza tarehe 01/04/2015 na utaendelea kila siku. Ili kuhakikisha unapata makala hizi ambazo zitakujenga sana kiuongozi bonyeza hapa na uweke email na kisha idhibitishe kwenye email utakayotumiwa. Ni bure kabisa, hakuna malipo yoyote, ni utayari wako tu wa kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo unajifunza.

Karibu sana kwenye mafunzo haya mafupi ambayo yatakuandaa kuwa kiongozi bora.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment