Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, March 12, 2015

UKURASA WA 71; Angalia Nyuma Kwa Lengo Moja Tu…

Mpaka uje kufikia kile unachotaka kwenye maisha yako, utafanya makosa mengi sana.

Kuna mambo mengi utakayofanya na kukosea, na kushindwa.

Ili ufanikiwe unahitaji kurudia tena na tena na tena.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Saa Hili moja Kufikia Mafanikio Makubwa.

Lakini pia ni rahisi sana kuangalia nyuma, kuona makosa uliyofanya. Katika kuangalia huku nyuma unaweza kuanza kujilaumu kwa makosa uliyofanya.

Tatizo ni kwamba hata kama utajilaumu hakuna utakachoweza kufanya kabadili makosa uliyofanya jana.

Angalia nyuma kwa lengo moja tu, kujifunza na kujua kama unasonga mbele au kurudi nyuma.

Usiangalie nyuma kwa lengo jingine lolote zaidi ya hilo, labda kama unataka kuendelea kunasa kwenye makosa uliyofanya huko nyuma.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia sasa nitaangalia nyuma kwa lengo moja tu, nalo ni kujifunza na kuona kama nasonga mbele au naendele akufanya yale niliyofanya nikashindwa. Sitaangalia nyuma ili kujutia makosa niliyofanya. Sina muda wa kupoteza kwa jambo ambalo halitanipa faida.

SOMA; NENO LA LEO; Unachotakiwa Kusema Unaposhinda Na Unaposhindwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 72 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment