Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, March 7, 2015

NENO LA LEO; Ili kushinda Unahitaji Hiki, Na Kama Huna Utakipata Hivi.

To be a great champion you must believe you are the best. If you're not, pretend you are. -Muhammad Ali

Kuwa mshindi ni lazima uamini kwamba wewe ni bora. Na kama sio bora basi jifanye kuwa bora.

Ushindi unaanzia ndani yako, kwa kuamini kwmaba wewe ni bora na unaweza kufanya mambo makubwa.

Hata kama unajua kweli wewe sio bora au huwezi, usikubali kubaki hivyo. Anza kujiona wewe ni bora na endelea kujiboresha kila siku.

Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa bora, wote unaowaona bora leo walianza wakiwa hawajui kabisa.

Hata wewe unaweza, anza sasa kufanyia kazi uwezo wako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Adui Yako Anaanzia Hapo Ulipo Na Anaanza hivi.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment