Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, March 24, 2015

NENO LA LEO; Acha Kupoteza Nguvu Zako Kwenye Kitu Hiki Unachopenda Kufanya.

“Don't waste your energy trying to change opinions ... Do your thing, and don't care if they like it.” ― Tina Fey, Bossypants

Usipoteze nguvu zako kwa kujaribu kubadili maoni ya wengine. Fanya kile unachofanya na usijali kama watakipenda au la.

Katika kitu chochote, watu watakuwa na maoni tofauti tofauti. Kuna wengine watakubaliana nacho, kuna wengine watakipinga. Kuna wengine watakupa moyo, kuna wengine watakukatisha tamaa.

SOMA; Usijaribu Kumfurahisha Kila Mtu.

Ukianza kusikiliza kila mtu au kuanza kubishana nao kwamba unachofanya ni sahihi, utapoteza nguvu nyingi na bado watu hawa hawatobadilika. Badala yake tumia nguvu hizo kufanya unachofanya kwa ubora wa hali ya juu.

Watakapoona matokeo mazuri wote wanaokupinga na kukukatisha tamaa watakaa kimya. Ila utakapokazana kuwabadili maoni yao kwa kubishana nao utapoteza nguvu zako na utashindwa kufanya kile ulichochagua na wao watakuwa sahihi.

Kumbuka watu hawataacha kusema, hata ungefanya kiasi gani. Ni sawa na mfano uliotolewa na mfalme mmoja kwamba hata ukitembea juu ya maji kuna watu watasema anatembea juu ya maji kwa sababu hajui kuogelea.

Tumia nguvu zako kufanya mambo ya msingi kwako na sio kubadili maoni ya wengine. Acha majibu mazuri yafanye kazi hiyo.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Unachohitaji Kufanya Ili Dunia Nzima Ikukubali.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment