Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, March 3, 2015

TAFAKARI; Unachagua Upande Upi?

Maisha ni kuchagua, ndio unalijua hili.
Kuna wakati ambao unachagua ukijua, na kuna wakati ambao hujui kma umechagua ila unakuwa umeshachaguliwa.
Maisha yana pande pili katika kila jambo.
Kuna kuishi, kuna kufa. Kuna kuwa na afya, kuna kuumwa. Kuna kupata faida, kuna kupata hasara. Na pia kuna kufanikiwa na kunakushindwa.
Katika pande zote hizo mbili, upande uliopo sasa umechagua mwenyewe iwe kwa kujua au kwa kutokujua.
Kama huna mafanikio maana yake hujachagua kupata mafanikio, hujishughulishi kupata mafanikio, sasa utabaki na nini?
Kama unaumwa, maana yake umeamua kutochagua afya na hivyo kubaki na magonjwa. Unajua kabisa kuna mbu, hujikingi unapata maleria. Unajua kabisa chipsi unazokula mara kwa kara sio nzuri. Unajua kabisa utaratibu wako wa kutofanya mazoezi sio mzuri, lakini umechagua kubaki nao.
Kama unafanya biashara na unapata hasara, ndio umechagua hasara. Maana hujachukua muda kujifunza kuhusu biashara yako, kujua kwa nini unapata hasara na mengine mwengi.
Kwa hiyo basi, hebu kaa chini leo na uchague upya, kwenye kila eneo la maisha yako. Halafu ukishachagua usilalamike fanya kile ulichochagua.
Na kama utaamua kutokuchagua, yaani pamoja na yote haya ukaona huna muda wa kukaa na kuchagua upya, nina habari njema kwako, tayari umeshachaguliwa, na ulichochaguliwa sio kizuri san kwako.
TAFAKATI HILI HALAFU LIFANYIE KAZI.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment