Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Showing posts with label MBINU ZA MAFANIKIO. Show all posts
Showing posts with label MBINU ZA MAFANIKIO. Show all posts

Friday, June 5, 2015

Mabadiliko Kwenye Blog Zinazoendeshwa Na AMKA CONSULTANTS.

Habari za leo mpenzi msomaji wa blog za AMKA CONSULTANTS, naamini unaendelea vizuri na harakati zako za kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. AMKA CONSULTANTS ipo pamoja na wewe kwenye safari hii ya kuboresha maisha yako na inakupatia maarifa na ushauri muhimu utakaokusaidia kwenye safari hii.
Kwa kuwa lengo letu AMKA CONSULTANTS ni kukuwezesha wewe kufikia ule uwezo mkubwa ulio ndani yako, kila mara tunaangalia njia bora ya kukuwezesha wewe kufikia uwezo huu mkubwa sana. Tunajua kwamba wewe hufanani na mtu mwingine, licha ya kudanganywa hivi kwa muda mrefu. Hivyo tunafanya kila linalowezekana ili kukupatia wewe maarifa na ushauri utakaokuwezesha kutumia uwezo wako na mazingira yako kuboresha maisha yako.
http://www.amkamtanzania.com/p/kuwa-tajiri.html
Ili kuhakikisha unapata kilicho bora, kuna mabadiliko makubwa yatakayofanyika kwenye baadhi ya blog za AMKA CONSULTANTS. Mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuboresha zaidi ili iwe rahisi kwako kufikia kile unachotaka kufikia kwenye maisha yako.
Yafuatayo ni mabadiliko yatakayofanyika mapema.
KISIMA CHA MAARIFA,
Kisima cha maarifa ni blog ya kulipia inayoendeshwa na AMKA CONSULTANTS. Blog hii ina makala nyingi sana na nzuri zinazokupatia wewe maarifa ya biashara, mafanikio na hata uchambuzi wa vitabu. Blog hii ilikuwa na uanachama wa aina tatu, BRONZE(tsh elfu 10), SILVER(tsh elfu 30) na GOLD(tsh elfu50).
Kwa sasa kutakuwa na mabadiliko yafuatayo.
Kutakuwa na makala moja kwa kila siku ya juma. Jumatatu makala ya biashara/ujasiriamali, Jumanne makala ya tabia za mafanikio, jumatano makala ya world class, alhamisi makala ya uchambuzi wa vitabu na ijumaa makala ya uongozi na usimamizi. Kipengele cha uongozi na usimamizi kimeongezwa ili kuweza kukujenga wewe kuwa kiongozi bora na hata msimamizi mzuri pia. Unapokuwa kwenye biashara, unahitaji kuwa kiongozi na wakati huo huo kuwa msimamizi. Utajifunza yote haya kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Makala za uchambuzi wa vitabu hazitakuwa tena kama zamani ambapo kitabu kimoja kilikuwa kinachambuliwa kwa muda, bali kila wiki kitachambuliwa kitabu kimoja. Hii itakuwezesha wewe kujifunza mambo mengi zaidi ya kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa.
Kwenye makundi ya uanachama kutakuwa na mabadiliko pia. Kundi la BRONZE litaondoka na hivyo tutabaki na SILVER ambapo ada yake ni tsh elfu 30 kwa mwaka na GOLD ambapo ada yake ni tsh elfu 50 kwa mwaka. Waliopo kwenye GOLD wataendelea kupata nafasi ya kuwa kwenye kundi la wasap. Wanachama wa bronze wa sasa wataingia kwenye silver bila ya kuongeza kiwango kingine cha fedha. Lakini wakati w akufanya malipo mapya watalipia kwa ada ya silver au gold kama watapenda. Usikose nafasi hii nzuri ya kujifunza. Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza maandishi haya.
Pia kuna kundi moja litaongezeka ambalo litakuwa ni PLATNUM. Kundi hili ni la watu wachache ambao watahitaji kufuatiliwa kwa karibu sana kwa kile wanachofanya ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea. Kundi hili linahitaji mtu aliyejitoa kweli na yupo tayari kwenda hatua ya ziada ili kupata kile anachotaka. Gharama za kuwa kwenye kundi hili ni kubwa na zinatofautiana kulingana na mahitaji ya mtu. Kama utahitaji kuwepo kwenye kundi hili tuwasiliane.
EMAIL LIST.
Mpaka kufikia sasa tuna watu elfu mbili waliojiunga na email list ya AMKA CONSULTANTS. Watu hawa wamekuwa wanatumiwa email tatu kwa wiki na email hizi zimekuwa zinatokana na makala zinazowekwa kwenye AMKA MTANZANIA. Lakini ni sehemu ndogo sana ya watu walioweka email zao wanafungua email zinazotumwa. Na sisi tunaingia gharama kutuma email hizi. Hivyo hatua ya kwanza kabisa ni kufuta email zote ambazo hazijafunguliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja. Kama tungu mwezi wa nne umetumiwa email ila hujaifungua utafutwa. Tunataka tubaki na watu wenye kiu kweli ya kujifunza ili tuweze kwenda pamoja.
Kutakuwa na mabadiliko kwenye email zinazotumwa, kwanza hazitatumwa mara tatu kwa wiki kama ilivyokuwa mwanzo, sasa zitatumwa mara mbili kwa wiki, jumanne na alhamisi. Labda kama kutakuwa na jambo muhimu ndio kutakuwa na email zaidi ya hapo kwa wiki. Email zitakazotumwa sasa sio za makala iliyopo kwenye blog, bali yatakuwa mazungumzo ya moja kw amoja kutoka kwangu kuja kwako. Nitakuwa nakushirikisha mambo mbalimbali ambayo naona yanaweza kukusaidia sana. Na mwisho nitakuwekea link ya makala zilizopo kwenye blog.
Nitakuwa natoa mafunzo makubwa sana kupitia email nitakazokuwa natuma na yatakuwa na thamani kubwa sana. Ungehitaji kulipia gharama kiasi kupata mafunzo haya, lakini gharama yako itakuwa ni kufungua email na kusoma kwa wakati. Ukishindwa kufungua email kumi kwa mfululizo, moja kwa moja unaondoka kwenye mfumo wetu wa email. Na sio sisi tunakuondoa bali ni mfumo unakuondoa wenyewe kwa jinsi tulivyouweka.
Hivyo fungua email yako kila siku ya jumanne na alhamisi uweze kujifunza. Kama bado hujajiunga na mfumo huu wa email bonyeza maandishi haya.
AMKA TV.
Kwa sasa utakuwa unapata video mbalimbali za mafunzo na kuhamasisha kupitia mtandao wa YOUTUBE. Video hizi zitakuwa kwneye channel inayoitwa AMKA TV. Bado tunaifanyia kazi chanel hii ili kuweza kukuleta mafunzo bora zaidi kwa sasa tunaanza na video za kutengeneza wenyewe ila baadae tutakuwa tunafanya mahojiano na watu mbalimbali ambapo utajifunza mambo mengi na mazuri. Ingia kwenye channel ya AMKA TV kwa kubonyeza maandishi haya na hakikisha unasunscribe(kujiunga) nayo ili ufahamishwe kila video mpya inapowekwa.
Makala kwenye AMKA MTANZANIA na JIONGEZE UFAHAMU zitaendelea kuwepo kila siku ya juma na kwa utaratibu uliopo sasa. Kuna vitu vingine vizuri bado tunavifanyia kazi na vitakapokuwa tayari tutawashirikisha. Lengo ni wewe uweze kufikia malengo na mipango uliyojiwekea kwenye maisha yako.
Nakukaribisha sana kwenye AMKA CONSULTANTS, karibu ujifunze na uhamasike ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
TUPO PAMOJA.
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Saturday, May 2, 2015

Hii Ni Nafasi Ya Mwisho Kabisa, Usiikose Tena.

Kwanza niwashukuru sana wale wote ambao wameshajiunga na semina ya MAFANIKIO KATIKA BIASHARA  mwaka 2015. Umefanya maamuzi sahihi sana kujiunga na semina hii na utajifunza mambo mazuri ambayo kama utayatumia utaboresha zaidi biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

Nimepokea ujumbe kutoka kwa watu wengi jana kusumbuliwa na mtandao hivyo kushindwa kutuma malipo ya ada ya semina. Na jana hiyo ndio ilikuwa mwisho w akujiunga na semina hii ya kipekee ambayo mtu hawezi kuipata mahali pengine. Kutokana na changamoto hii ya kukamilisha ambayo wengi imewazuia kukamilisha malipo, nimeona ni busara kuongeza siku ya leo kufanya malipo.

Kama ulikwama kufanya malipo au kama ulikuwa bado hujaamua kujiunga unaweza kutumia siku ya leo jumamosi tarehe 02/05/2015 kukamilisha malipo yako na kujiunga. Nyongeza hii ya siku za kuijunga ni kwa leo tu hivyo itumie vizuri kama hutaki kupitwa na semina hii.

Kama ndio unapata ujumbe huu kw amara ya kwanza habari iko hivi; AMKA CONSULTANTS wamekuandalia semina ya biashara inayokwenda kwa jina MAFANIKIO KATIKA BIASHARA na semina hii inaendeshwa kwa njia ya email kwa kipindi cha mwezi mmoja. Katika mwezi huu ni kama unapata nafasi ya kuwasiliana na mimi moja kwa moja kila siku, kujifunza, kuuliza maswali na kupata majibu. Ada ya kujiunga na semina hii ni tsh elfu 30, na ili kujiunga tuma ada hiyo kwa namba 0717396253/0755953887 na kisha tuma ujumbe wenye jina lako na email kwenye moja ya namba hizi na utaunganishwa.

Hii ni semina ambayo hupaswi kuikosa labda kama umeamua kubaki pale ambapo upo kwa sasa.

Tumia siku hii ya leo kukamilisha malipo yako ili uweze kuingia kwenye semina hii. Uzoefu ambao nimekuwa nao kwenye maandalizi ya semina hizi ni kwamba watu wengi hutaka kujiunga pale ambapo semina inakuwa imeshaanza. Inakuwa ni changamoto sana kwa muundo tunaotumia kutoa mafunzo, mfumo huu unahitaji washiriki wawe wamepangwa vizuri kabla ya masomo kuanza kutolewa. Hivyo kama utashindwa kujiunga leo, hutaweza kujiunga tena hasa pale mafunzo yatakapoanza. Hivyo kama hukuona ujumbe huu na ntingine zilizopita ndio tayari umeshakosa mambo haya mazuri.

Karibu sana tujifunze ili kuweza kuwa bora zaidi na kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA.

Wednesday, April 29, 2015

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Biashara Kubwa Kwa Kuanzia Chini Kabisa, Hata Kama Huna Kitu.

Semina ya mafanikio kupitia biashara mwaka 2015 imebaki siku mbili tu ili uweze kujiunga. Kama unapitia changamoto zozote kwenye biashara yako au hata kama huna changamoto ila ungependa kufikia mafanikio makubwa usikose kujiunga na semina hii. Mwisho wa kujiunga ni ijumaa hii tarehe 01/05/2015. Baada ya hapo hutapata tena nafasi ya kujiunga na mafunzo hayo ambayo ni muhimu sana kwenye maisha yako na biashara yako pia. Kujiunga tume fedha ya ada ambayo ni tsh elfu 30 kwenye namba 0717396253/0755953887 na kisha tuma ujumbe wenye jina lako na email yako. Semina itafanyika kwa mwezi mzima wa tano na kwa njia ya email. Kuna vitu unaweza kuvikosa kwenye maisha yako, ila sio semina hii, utakosa mengi na utaendelea kushindwa kufika hatua ya juu kabisa kwenye biashara yoyote ambayo unafanya au unatarajia kufanya.

Kwenye makala ya leo nataka nikushirikishe mbinu ambazo unaweza kutumia na kutengeneza biashara kubwa sana na yenye mafanikio hata kama unaanzia chini kabisa, yaani huna kitu chochote cha kuanzia.

Katika hali ya kawaida watu wengi sana huwa wanalalamika kwamba wanataka kufanya biashara ila hawana mtaji. Wengine wanafikiri wanakosa elimu kubwa ndio maana hawawezi kuingia kwenye biashara. Wengine wanafikiri wangepata ‘connection’ nzuri tu basi biashara zao zingefika mbali sana. Ni kweli vitu vyote hivyo ambavyo watu huwa wanavilalamikia ni muhimu sana ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara. Ila ukweli muhimu zaidi ni kwamba, haimaanishi kwa kukosa vitu hivyo basi wewe umelaaniwa na huwezi kufanikiwa kwenye biashara.

Unaweza kufikia mafanikio makubwa sana kwenye biashara yako hata kama huna mtaji, huna elimu kubwa na hata kama hakuna anayekujua. Inawezekanaje hivyo? Tutajifunza kwa undani sana kwenye semina inayokwenda kuanza wiki ijayo, ila leo hapa nitakuonesha kwa mfano rahisi jinsi gani unaweza kufanya hivyo. Twende pamoja kwenye mfano huu rahisi na unaweza kuutumia kwenye biashara nyingine yoyote.

Tuseme labda wewe ni kijana ambaye umekuwa na wakati mgumu sana kifedha. Unajaribu kutafuta kazi hupati na pia umefikiria sana kufanya biashara ila tatizo limekuwa mtaji. Na pia ukifikiria hakuna mtu yeyote anayeweza kukuunganisha na watu wa kazi au watu wa biashara. Ukifikiria mkopo, hupati jibu kabisa kwa sababu huna chochote cha kuweka dhamana.

Ila kwa kuwa wewe ni mtu ambaye hukatishwi tamaa haraka, unaamua kufikiria zaidi. Unajiuliza ni shida gani ambayo mtu anaweza kuwa nayo na wewe ukaweza kuitatua na akakupa japo fedha kidogo? Kwa kufikiria kwa kina na kutokana na hali uliyonayo, unapata jibu moja ambalo linakuonesha mwanga. Unagundua kwamba sehemu unayoishi watu wana magari, ila hawapati huduma nzuri za kuoshewa magari yao. Unaona hapa ndio unapoweza kuanzia, kuosha magari kwa mtindo tofauti kabisa na wanavyofanya wengine.(Tafadhali usiishie hapa baada ya kuona nakuambia ukaoshe magari, hii ni hatua ya mwanzo tu, utafikia biashara kubwa sana baadae). Baada ya kuwa na wazo hili unaweza kulikuza hatua kwa hatua kama ifuatavyo.

Nenda kwa kila jirani mwenye gari, na mweleze kwamba ungeomba umwoshee gari yake bure kabisa. Unamwambia unataka kuanzisha biashara ya kuosha magari ambayo itakuwa tofauti kabisa na inavyofanyika sasa. Mwambie kwamba kwa ufahari wa huduma hii anafanyiwa akiwa nyumbani kwake, kwa siku ambayo amepumzika. Utahitaji kutoa maelezo ya kina ili uonekane kwmaba unajua kile ambacho unakwend akufanya. Kuna ambao watakataa, ila wengi watakubali, kwa sababu hakuna gharama yoyote wanayoingia na kama umewapa maelezo mazuri, watajaribu kupima waone kama kweli huduma unayokwend akuwapa ni ya tofauti.

Baada ya hapo jifunze kila aina ya gari unaloona majirani zako wanalo. Kama umeweza kusoma hapa, maana yake unawez akufungua mitandao mbalimbali inayohusiana na magari. Jifunze ubora wa gari husika, tafuta kitu chochote unachoweza kukisifia kwenye gari la mteja wako. Jua vitu muhimu unavyoweza kumshauri kuhusiana na gari lake hilo ili liweze kudumu kwa muda na lisimsumbue. Wakati huo huo jifunze kuhusu uoshaji wa magari, Jifunze ni kemikali gani nzuri unazoweza kuzitumia na zisilete madhara kwenye rangi ya gari au vitu vingine kwenye gari. Mambo yote haya muhimu utamweleza mteja wako siku ya kwanza unapoomba kuosha gari bure na hata siku ya kufanya kazi hiyo. Pia waeleze ni jinsi gani itakuwa fahari kwao kw akupata mtu wa kuwaoshea magari huku akiwapatia maelekezo yote ya msingi kuhusiana na magari yao.

Baada ya kupata nafasi ya kuosha gari bure kwa siku ya kwanza, hapa sasa unatoa ofa yako ambayo mteja hawezi kuikataa kutokana na huduma nzuri uliyompatia siku hiyo ya kwanza. Mwambie mteja kwamba unaweza kumfanyia huduma hiyo mara moja kila wiki kwa gharama ya tsh elfu tano tu. Utamfanyia usafi wa uhakika na kumpa maelekezo yote muhimu kuhusiana na gari lake.

Labda tuseme kwenye mtaa unaokaa kuna watu 30 ambao wanamiliki magari yao. Kwa kuongea nao wote 20 wanaweza kukubali kukupa nafasi ya kuwaoshea magari yao bure. Baada ya kutoa huduma hii ya kwanz a bure na kuwapa ofa yako, tuseme 10 ndio watakaosema ndio. Hii ni sawa na tsh elfu 50 kwa wiki, kwa kuanzia, sio mbaya ukilinganisha na sasa ambapo huna kipato kabisa. Na kumbuka huu ni mwanzo tu, unaendelea kuwaambia wengine wengi zaidi, maliza mtaa unaokaa na nenda mtaa mwingine. Na hawa wateja wako waambie wawaambie na marafiki zao kwamba unatoa huduma hiyo. Uzuri ni kwmaba mtu mwenye gari atakuwa na marafiki ambao nao pia wana magari na kama ukiwapa huduma nzuri hawatasita kuwaambia wenzao kwamba kuna kijana anatoa huduma nzuri sana ya kusafisha magari.

Hata kama umepata mteja mmoja, endelea kuongea na wengine wengi. Hata kama wote wamekataa, endele akuongea na wengine wengi, na kama utakuwa unatoa maelezo yako vizuri kuna mtu atakuambia NDIO na huyu ndio wa kumtumia vizuri.

Kumbuka katika mchakato wote huu hujatumia fedha nyingi sana, hujahitaji kuw ana eneo kwa sababu huduma hii unaitolea kwa mteja. Labda utahitaji kuwa na ndoo mbili, na vifaa vingine vya kawaida vya kuoshea na sabuni au kemikali nyingine nzuri ya kuoshea magari ambayo sio ya bei ghali sana. Gharama za vitu hivyo vichache haiwezi kuzidi tsh elfu 20.

Haya yote tuliyojadili hapo juu ni hatua ya kwanza kabisa ya wewe kufanikiwa kwenye biashara, bado kuna hatua nyingi sana ambazo bado hujatumia. Na changamoto kubwa ni kwmaba watu wengi huwa wanaishia hatua hii ya kwanza ndio maana wanakuwa watumwa wa biashara zao. Unakuta mtu anauza duka lile lile kwa kiwango kile kile kwa zaidi ya miaka 10, hakuna mafanikio hapa. Sasa wewe hutaki kuosha magari kwa maisha yako yote. Hivyo unakwenda hatua nyingine muhimu kabisa ya ukuaji wa biashara yako. Anza kutoa huduma za ziada kwenye magari unayoosha, badilisha oil au maji au chochote ambacho kutakuongezea kipato cha ziada kutoka kwa mteja wako ambaye sasa anakuamini sana. Unaweza pia kuchukua jukumu la kuwatafutia fundi wa uhakika kwa matatizo wanayokutana nayo kwenye magari yao. Yaani wewe unakuwa zaidi ya muosha magari kwao, wanapopata shida yoyote kwenye magari yao, mtu wa kwanza kuja kwenye akili yao ni wewe na hivyo kukutafuta uwashauri vizuri.

Baada ya kupata wateja wa uhakika tafuta vijana wengine ambao wapo tu mtaani na hawana cha kufanya. Chagua unaoona wanaweza kufanya akzi kwa uaminifu, wafundishe kile unachofanya na wafenye kuwa wasaidizi wako. Walipe kadiri wanavyoweka juhudi zao kwenye kazi unazowapangia. Endelea kwenda mbele, endelea kukua, endelea kuongeza wateja mpaka unafikia wateja 1000 kwa mwezi ambao wapo tayari kukupa sio chini ya shilingi elfu tano kila mmoja. Hii itakuwa ni milioni tano, ukiondoa gharama zote za uendeshaji, bado utabaki na zaidi ya nusu ya kiwango hiko. Sasa niambie ni nani angekuajiri akupe mshahara wa milioni mbili, ndani ya mwaka wako wa kwanza wa kazi. Kumbuka hapa bado una nafasi kubwa ya kuendelea kukua zaidi na zaidi na hakuna kikomo isipokuwa unachojiwekea mwenyewe.

Hivyo ndio unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kw akuanzia chini kabisa. Maelezo hayo yanaonekana rahisi ila utekelezaji unahitaji moyo, unahitaji muda maana hiyo haitotoke amara moja tu, watu watataka wakuamini kwanza ndio waweze kufanya kazi na wewe. Unahitaji uaminifu wa hali ya juu sana, unahitaji kujitoa na kutokujali wengine wanakuchukuliaje kwa sababu umeamua kuosha magari. Unahitaji uvumilivu, kuna watu watakuambia hapana, kuna wengine watakusumbua kwenye malipo. Lakini kama utakomaa, kama utaweka juhudi na maarifa na ukatoa huduma ambayo mtu hajawahi kuipata kokote, lazima utakuwa na bishara, hata kama hutofikia mamilioni, lakini utapata cha kukutoa hapo ulipo.

Sasa hebu niambie, unafikiri ni kitu gani kinachokuzuia mpaka sasa? Ni wewe mwenyewe tu.

Mfano huu tuliotumia hapo juu unawez akuweka kitu kingine chochote unachoweza kufanya, iwe ni kutangaza biashara za watu wengine kwenye mtandao, iwe ni kutoa huduma ya kukusanya taka taka, iwe ni kutoa huduma ya kufundisha watoto majumbani na mengine mengi. Unachohitaji ni wewe kukaa chini, kuweka mipango na kuanz akuitekeleza mara moja.

Kupitia semina inayoanza wiki ijayo, utajifunza mengi zaidi na jinsi unavyoweza kubadili wazo lolote kuwa biashara itakayokulipa.

Kama wewe ni kijana na huna fedha kabisa ila umependezwa na wazo hilo hapo juu na unafikiria kulifanya, jiunge na semina hii halafu tutapata muda wa kuendeleza wazo hilo na nitakupa nafasi ya kuwa msimamizi wako mpaka biashara yako itakapokomaa. Kwa hiyo unahitaji shilingi elfu 50, elfu 30 ya semina na elfu 20 ya kuanzia biashara yako. Kama kwa kufikiria wkako kote unaona huwezi kupata shilingi elfu 50, fanya hivi, angalia ni vitu gani unavyomiliki ambavyo huna matumizi navyo makubwa na unaweza kuuza na kupata fedha hiyo. Kama huna, angalia katika ndugu zako na watu wengine wa karibu, chagua watu kumi ambao utaomba kuonana nao na utawaomba wakupe shilingi elfu kumi tu kila mmoja, waambie kuna kitu cha tofauti unataka kujaribu na kitakuw ana manufaa kwako. Katika 10 utakaowaomba, hutakosa watano watakao kupatia. Usikubali kirahisi, pambana mpaka uhakikishe umepata kile ambacho unakitaka.

Nikukaribishe sana kwenye semina inayoanza wiki ijayo na mwisho wa kujiunga ni ijumaa hii. Ukiikosa hii, unakuw aumejikosesha mambo mengi sana na mazuri.

Nakutakia kila la kheri katika biashara unayofanya au unayotegemea kufanya.

TUPO PAMOJA

Makirita Amani 

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322

Monday, April 20, 2015

Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

Huu ni wakati ambao karibu kila mtu anahitaji kuingia kwenye biashara. Haijalishi mtu ameajiriwa au hana ajira, haijalishi kiwango cha elimu mtu alichonacho na wala haijalishi umri wa mtu, kwa sasa kila mtu anahitaji kuwa kwenye biashara.

Ajira zimekuwa za shida kupatikana na hata wale wanaozipata bado haziwawezeshi kuyamudu maisha. Changamoto ni nyingi sana. Njia ya uhakika ya kuweza kupambana na changamoto hizi ni kuingia kwenye biashara,

Mazingira ya kuingia kwenye biashara nayo yamebadilika pia. Tofauti na zamani ambapo ilihitaji mtu kuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha ndio aweze kuingia kwenye biashara, sasa hivi unaweza kuingia kwenye biashara kwa mtaji kidogo sana.

Pamoja na umuhimu huu wa kuingia kwenye biashara na urahisi wa kufanya biashara, bado kuna changamoto kubwa sana wkenye biashara. Biashara nane kati ya kumi zinazoanzishwa zinakuwa zimeshakufa ndani ya miezi 18. Na hata zile ambazo zinapona kipindi hiki, nyingi hazifikii mafanikio makubwa.

Watu wengi wanaweka juhudi kubwa sana kwenye biashara ila bado hawaoni mafanikio waliyotarajia. Hili linawaangusha wengi sana na wengi kukata tamaa.

Matatizo haya mengi yanatokana na kukosekana kwa elimu sahihi ya biashara, kukosa mtazamo sahihi wa kufanikiwa kwenye biashara, kutokujua mbinu za mafanikio kwenye biashara na kufanya biashara kwa mazoea.

Ili kuwasaidia wafanyabiashara na wale ambao wanapanga kuingia wkenye biashara kuweza kuondokana na changamoto hizi, AMKA CONSULTANTS imeandaa SEMINA YA MAFANIKIO KWENYE BIASHARA 2015. Semina hii itakupatia wewe elimu sahihi, mbinu muhimu na mtazamo sahihi utakaokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara yako.

Hii sio semina ya kukosa kwa sababu imejaa mambo mengi ambayo hujawahi kuyapata sehemu nyingine yoyote.

Semina hii imeandaliwa kuweza kukidhi mahitaji ya kufanikiwa kwenye biashara kwa mazingira yetu ya kitanzania. Semina hii itakuwezesha wewe kutoka hapo ulipo sasa na kupiga hatua kubwa sana kibiashara.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao na itaendeshwa kwa kipindi chote cha mwezi wa tano.

Washiriki wa semina hii watatumiwa email ya mafunzo kila siku asubuhi, kupata nafasi ya kuisoma na kuweza kuuliza swali popote ambapo hajaelewa. Email hizi zitakuwa na mafunzo yaliyofanyiwa utafiti w akina pamoja na mifano ambayo itamwezesha mshiriki kpata mawazo tofauti anayowez akuyatumia kwenye biashara yake na akafanikiwa sana.

Semina hii itafundisha mambo yafuatayo;

SEMINA YA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA.

Anza, kuza na fanikiwa kupitia biashara.

Yatakayofundishwa;

1. Utangulizi

1.1. Huu ni wakati mzuri wa wewe kuwa kwenye biashara.

1.2. Unawezakufanikiwa kwenye biashara.

1.3. Utakachokipata kwenye kozi hii.

2. Wazo la biashara

2.1. Biashara sahihi kwako kufanya

2.2. Jinsi ya kupata wazo bora la biashara

2.3. Jinsi ya kuboresha wazo lako la biashara

2.4. Baadhi ya mawazo ya biashara.

3. Mchanganuo wa biashara.

3.1. Umuhimu wa mchanganuo

3.2. Vitu muhimu vya kuweka kwenye mchanganuo wako

3.3. Udhaifu na uimara wako

3.4. Utafiti wa biashara yako

3.5. Ushindani.

3.6. Kuajiri wasaidizi bora kwenye biashara yako.

4. Mtaji na vyanzo vyake.

4.1. Aina za mtaji unaohitaji kwenye biashara

4.2. Mtaji wa fedha na vyanzo vyake

4.3. Njia bora za wewe kupata mtaji wa biashara.

5. Urasimishaji wa biashara

5.1. Umuhimu wa kusajili biashara yako.

5.2. Aina za usajili na faida zake

5.3. Hatua za kusajili biashara yako

5.4. Umuhimu na jinsi ya kulinda biashara yako.

6. Thamani ya biashara yako

6.1. Maandalizi ya bidhaa au huduma

6.2. Upatikanaji na upakiaji wa bidhaa au huduma

6.3. Upangaji wa bei.

7. Masoko na uuzaji.

7.1. Chagua soko la biashara yako

7.2. Mpango bora wa kutangaza biashara yako.

7.3. Njia rahisi za kutangaza biashara yako.

7.4. Mbinu za kuongeza mauzo kwenye biashara yako.

8. Mzunguko wa fedha.

8.1. Mauzo na faida.

8.2. Gharama muhimu za biashara

8.3. Gharama za kuepuka kwneye biashara

8.4. Kujilipa wewe mwenyewe.

8.5. Hesabu za fedha na umuhimu wa mhasibu.

9. Huduma kwa wateja.

9.1. Lengo la biashara ni kutengeneza wateja.

9.2. Jinsi ya kutoa huduma bora kwa mteja.

9.3. Mfanye mteja atangaze biashara yako.

9.4. Mteja ni mfalme na mwisho wa ufalme wake.

10. Changamoto za biashara.

10.1. Changamoto zinazoua biashara nyingi

10.2. Umuhimu wa mabadiliko

10.3. Mbinu za kufufua biashara inayokufa.

11. Mafanikio ya biashara yako

11.1. Jifunze kila siku

11.2. Matumizi mazuri ya muda

11.3. Kujihamasisha mwenyewe

11.4. Mafunzo kwa wafanyakazi wako

11.5. Usimamizi mzuri wa biashara yako.

11.6. Kununua uhuru wako kutoka kwenye biashara yako.

Gharama za kushiriki semina hii ni tsh elfu 30(30,000/=), ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii tuma fedha za kushiriki kwa Mpesa 0755953887 au tigo pesa/airtel money 0717396253 kisha tuma majina yako na email kwenye moja ya namba hizo na utaandikishwa kwenye semina hii. Uandikishaji unaanza leo tarehe 20/04/2015 na utasitishwa tarehe 01/05/2015. Wahi kujiandikisha mapema kwani nafasi ni chache na zitakapojaa utakosa nafasi hii adimu ya kupata maarifa ya kukuwezesha kufanikiwa kwenye biashara yako.

Kumbuka semina inafanyika kwa njia ya mtandao hivyo popote ulipo Tanzania na hata nje ya Tanzania unaweza kushiriki semina hii.

Semina itaanza rasmi tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima.

Karibu kwenye semina hii ambayo itakupatia kila unachohitaji ili kufanikiwa kwenye biashara yako.

Kumbuka maarifa ni nguvu, pata maarifa sahihi kupitia semina hii ili uweze kuwa na nguvu za kutosha na zitakazokuletea mafanikio makubwa.

Karibu sana na hakikisha hukosi semina hii kwa sababu yoyote ile.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani 

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322

Wednesday, April 1, 2015

MIAKA MIWILI YA AMKA MTANZANIA; Kwa Nini Ipo Na Itaendelea Kuwepo Na Mambo Mazuri Yanayokuja.

Tarehe 31/03/2013 ilikuwa ndio siku ya kwanza kwa makala ya kwanza kwenda hewani kwenye mtandao huu wa AMKA MTANZANIA. Kipindi hiko wakati naanzisha mtandao huu mambo hayakuwa kama sasa, watu walikuwa na muamko mdogo wa kusoma habari za aina hii na hata kujisomea vitabu. Leo hii miaka miwili tu mbele, mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana

Leo hii, miaka miwili baadaya kuanzishwa kwa mtandao huu nimeona ni vyema tukashirikishana kwa nini mtandao huu upo, utaendelea kuwepo na mambo makubwa yanayokuja.

Moja ya makala za mwanzo kabisa kwenye AMKA MTANZANIA;

UTARATIBU WA KUJISOMEA VITABU

USIMLAUMU YEYOTE, ANZA KUJILAUMU WEWE

ZOEZI ZURI LA KUFANYA KILA SIKU

Kwa nini mtandao huu upo?

Miaka miwili kabla ya kuanz akwa mtandao huu, nilikuwa naishi kwenye hadithi nzuri ambayo tumekuwa tukidanganywa. Hadithi kwamba nenda shule, soma kwa bidii, faulu vizuri na utapata kazi nzuri na kuwa na maisha mazuri. Nilisoma kwa bidii kweli na kufaulu vizuri sana masomo yangu ya kidato cha sita. Baada ya hapo nilipata nafasi ya kusomea udaktari wa binadamu. Kwa nafasi hii niliamini ndio nimepata tiketi ya maisha mazuri.

Lakini mambo yalibadilika sana baadaya ya kuanza masomo haya ya udaktari. Baada ya kuona kile nitakachokwenda kufanya na mazingira ya kukifanya na hata maisha ya madaktari wengine, sikushawishika sana kama mwanzo kwamba kuwa daktari ndio tiketi ya maisha bora.

Changamoto kubwa zaidi ilitokea mwaka 2011 ambapo nilijikuta nje ya mfumo wa elimu, huku sina degree wala chochote cha kuniwezesha kupata kazi ya kujikimu kwenye maisha yangu. Mbaya zaidi hakuna aliyeweza kunielewa kwenye kipindi hiki kwa sababu kila mtu anayenifahamu aliona nimefanya makosa makubwa sana kwenye maisha, sijui ninachofanya na mengine mengi. Ni hapa ndio nilipoamua kushika hatamu ya maisha yangu. Nilikaa chini na kuamua kwamba kama nitakwenda kufanikiwa kwenye maisha yangu, basi hiyo ni juu yangu. Na nilijiambia kabisa kwamba mafanikio kwenye maisha hayahitaji degree au elimu yoyote kubwa.

Ni baada ya maamuzi haya ndipo niliacha kulalamika na kuanz akuchukua hatua juu ya maisha yangu. Nilitafuta kazi yoyote ninayoweza kufanya ili angalau iniwezeshe kuendelea kuwepo mjini. Nilipata kazi hiyo na sio kwa sababu ya kuwa nimesomea kazi hiyo, au kwa sababu ya kujulikana, bali kwa ushawishi niliokuwa nautoa kwenye maombi ya kazi hiyo.

Baada ya hapa niliamua kujifunza na kuangalia ni kitu gani ninachopendelea kufanya. Nilianza kujifunza mambo yanayohusiana na teknolojia ya habari(IT) ambapo nilijifunza jinsi ya kutengeneza tovuti, blog, programu za kompyuta na vitu vingine vingi. Yote haya sikuwa na darasa la kufundishwa, bali nilitafuta vitabu na kujisomea kisha kufanyia kazi yale ambayo nimeyasoma. Uzuri ni kwamba nilikuwa naona matokeo mazuri kila ninapojifunza na kufanya kitu.

Baada ya mwaka mmoja wa kujifunza vitu vya kitaalamu na pia kujisomea vitabu vyakujijenga na kujihamasisha niliona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yangu. Kwanza nilijikuta katika hali kubwa ya kujiamini, nikiwa na vyanzo mbalimbali vya mapato kutoka kwenye shughuli mbalimbali ambazo nilikuwa naweza kufanya. Ni katika wakati huu ambapo niliona makosa makubwa niliyokuwa nafanya kwenye maisha yangu na jinsi nilivyoweza kuyarekebisha.

Ni wakati huu pia ambapo niliona watu wengi wanafanya makosa haya na kunafanya maisha yao yawe magumu sana. Ndio maana niliona kuna umuhimu wa kuwashirikisha vitu hivi vizuri ambavyo nimefanya kwenye maisha yangu na ninaendelea kuvifanya ili nao waweze kuboresha maisha yao. Hapa ndipo mtandao huu wa AMKA MTANZANIA ulipozaliwa. Lengo kubwa la mtandao huu ni kumsaidia kila mtanzania ambaye ameamua kushika hatamu ya maisha yake kuweza kufikia malengo na mipango aliyojiwekea kwenye maisha yake.

Kwa nini nimekushirikisha sehemu hiyo ndogo ya maisha yangu na historia ya mtandao huu?

Nimefanya hivi kwa sababu najua kuna kijana wa kitanzania ambaye amemaliza masomo yake ila hajapata ajira. Kijana huyu amekaa nyumbani na hajui afanye nini, kwani hata biashara anasema hana mtaji. Nataka kukuambia wewe kijana mwenzangu kwamba AMKA na uchukue hatamu ya maisha yako, utakapoamua kuamka hakuna linaoshindikana.

Najua kuna mfanyakazi ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu sasa ila haoni kitu kikubwa ambacho amefanya kwenye maisha yake. Maisha yake yamekuwa ya kuamka, kwenda kazini, kurudi nyumbani na kesho pia kufanya hivyo. Kipato anachopata pia hakioni kwa sababu kinaishia kulipa madeni na kulipia gharama za maisha. Nataka kukuambia wewe mtanzania mwenzangu, haijalishi kazi yako ni ya chini kiasi gani, haijalishi umeifanya kw amuda gani, kuna njia nzuri sana za wewe kuweza kuyabadili maisha yako na kuwa bora sana zaidi ya sasa ambapo unayaona yanakwenda tu.

Pia najua kuna mfanyabiashara ambaye amekuwa anafanya biashara zake kwa muda mrefu ila haoni mabadiliko yoyote kwenye biashara hiyo. Au ameanza biashara na kupata hasara hivyo kuamini kwmaba biashara haiwezekani. Napenda kukuambia kwamba kuna mbinu nzuri sana za kufanya biashara zako na kama ukiamua kuzitafuta na kuzifuata maisha yako yatakuwa tofauti sana na yalivyo sasa.

Maisha yoyote ambayo unapitia sasa, hata yawe magumu kiasi gani, unayo nafasi kubwa sana ya kuyabadili wewe mwenyewe. Huna haja ya kulaumu serikali, kulaumu wazazi au kulaumu mtu mwingine yeyote unayefikiri ndio anakuletea maisha hayo magumu. Leo nakuambia kwamba, maisha magumu uliyonayo, yataondolewa na wewe mwenyewe.

Kwa nini AMKA MTANZANIA itaendelea kuwepo.

AMKA MTANZANIA itaendelea kuwepo kwa sababu bado watanzania wengi hawajaamka. Bado watanzania wengi wamekabidhi maisha yao kwa waajiri wao, kwa serikali, kwa jamii na wameruhusu taasisi hizi zifanye maamuzi muhimu kwenye maisha yao. Hii ndio maana wanaona maisha yao yakienda tu na hivyo kuishia kulaumu pale ambapo kile walichotarajia hakijatokea.

Bado watanzania tunahitaji maarifa muhimu sana ya kuweza kuboresha maisha yetu na kufanikiwa zaidi. Sehemu kubwa sana ya watanzania wanafanya mambo kwa mazoea. Wanafanya kazi kwa sababu ndio kazi ambayo wamekuwa wanaifanya kila siku. Wanafanya biashara kwa sababu wamezoea kufanya biashara hiyo. Hii ni sumu kubwa sana ya kufikia mafanikio makubwa kama unavyoweza kuisoma vizuri kwenye kitabu JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA.

Mtandao huu utaendelea kuwepo na kutoa makala na mafunzo mazuri yatakayomwezesha kila aliyeamua kuboresha maisha yake kuweza kufikia lengo hilo.

Mambo mazuri yanayokuja kwenye AMKA CONSULTANTS.

Ilianza AMKA MTANZANIA ambayo ilikuwa na jukumu kubwa la kukupa wewe taarifa muhimu unazohitaji kuwa nazo ili kuboresha maisha yako. Mwaka mmoja baadae ikaja KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni sehemu maalumu kwa wale ambao wako tayari kufikia mafanikio makubwa sana kwenye maisha yao. Kupitia KISIMA CHA MAARIFA watu wanajifunza tabia za mafanikio, mbinu za kufikia mafanikio, biashara na ujasiriamali na hata kupata uchambuzi wa vitabu vizuri. Kupitia KISIMA CHA MAARIFA pia unapata nafasi ya kukutana na watanzania wengine ambao nao wanaelekea kwenye safari ya mafanikio.

Kuna mambo mengi na mazuri ambayo yataendele akukujia kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Endelea kutembelea mitandao hii na washirikishe wengi zaidi ili nao wapate mambo haya mazuri.

Kuna kipengele muhimu kitakachokuja kwenye AMKA MTANZANI ambapo tutapata shuhuda za watu mbalimbali ambao maisha yao yamebadilika sana baada ya kujifunza kupitia AMKA MTANZANIA na kuamua kufanyia kazi yale ambayo wamejifunza. Shuhuda zipo nyingi mpaka sasa. Kama na wewe ungependa kuwashirikisha watanzania wenzako ushuhuda mzuri kutokana na uliyojifunza kwenye mtandao huu tafadhali andika maelezo yako kwa kujitambulisha, kueleza ulipotoka, ulipo sana na unapokwenda na jinsi gani AMKA MTANZANIA imekusaidia kisha tuma kwenye email makirita@kisimachamaarifa.co.tz Tafadhali fanya hivi na utakuwa sehemu ya mabadiliko ya nchi yetu na watanzania wenzetu.

Ufanye nini ili maisha yako kuwa bora ziadi?

Kwanza kabisa chukua maamuzi juu ya maisha yako, jua kama utakwenda kufanikiwa basi ni kwa juhudi zako na hakuna atakayekuletea mafanikio hayo.

Pili amua kujifunza sana kuhusiana na hiko unachofanya na maisha yako kwa ujumla. Jisomee vitabu mbalimbali vinavyotumwa kwenye mtandao huu na endelea kusoma mtandao huu kila siku kwa sababu kila siku kunakuwa na makala nzuri za kukuwezesha kuboresha maisha yako.

Tatu, jiunge na KISIMA CHA MAARIFA, kwa kuwa ndani ya kisima utajifunza mbinu nyingi sana za kukuwezesha kufikia mafanikio na pia utapata nafasi ya kukutana na watanzania wengine ambao wameamua kuchukua hatamu ya maisha yao. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na weka taarifa zako kisha lipa ada ya uanachama na utapata nafsi ya kupata maarifa hayo adimu. Kuhakikisha unapata mambo yote mazuri lipia ada ya GOLD MEMBER.

Naomba nichukue nafasi hii kukushukuru sana wewe msomaji ambaye umekuwa na mtandao huu mpaka sasa. Ni kwa sababu yako ndio maana mtandao huu umeendelea kukua na kuwafikia wengi zaidi. Umekuwa ukiwashiriksiha wengine habari za mtandao huu na kuwafanya wautembelee pia. Tafadhali endelea kuw abalozi mzuri wa AMKA MTANZANIA na hakikisha kila mtu unayemfahamu naye amefahamu kuhusu mtandao huu ili na yeye autembelee na kujifunza.

Pia niseme kwamba sisi sote tunaendelea na safari ya kujifunza, hakuna anayejua zaidi bali tunajifunza na wakati mwingine tunafanya makosa. Mimi na waandishi wengine wa mtandao huu sio kwamba ndio mabingwa sana kwenye kile tunachoandika, ila tunapenda kujifunz ana kutumia mambo haya na maisha yetu yanakuwa bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda. Na wewe usikose nafasi hii ya kuboresha maisha yako kila siku hata kama ni kidogo kiasi gani.

Nakutakia kila la kheri katika kuboresha maisha yako. Kumbuka kwamba kila kitu kinawezekana kama ukiamua kuchukua hatua. Kama kuna jambo lolote ambalo linakupa changamoto na ungependa kupata ushauri zaidi karibu sana tuwasiliane. Unaweza kupiga simu kwenye namba 0717396253 na tukaona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana kwenye jambo hilo.

TULIKUWA PAMOJA, TUPO PAMOJA NA TUTAENDELEA KUWA PAMOJA. Tafadhali tuma makala hii kwa njia ya email kwa watu watano na nicopy(weka email yangu makirita@kisimachamaarifa.co.tz kwenye sehemu ya cc) kwenye email hiyo na nitakutumia zawadi nzuri ya kitabu cha kufaidika na mabadiliko.

kitabu-kava-tangazo4322

Monday, March 23, 2015

Changamoto Inayokusumbua Kwenye Biashara.

Habari mpenzi msomaji,
Naandika kitabu kinachohusu biashara. Hii ni kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi sana zinazozuia watu wengi kuingia kwenye biashara au kufanikiwa zaidi kupitia biashara.
Vitabu vingi vya kibiashara havijaangalia upande wa pili wa tatizo ambapo ni mtu mwenyewe.
Hivyo kitabu hiki kitaanza na mapinduzi ya mfanyabiashara mwenyewe ndio aweze kuleta mapinduzi kwenye biashara yake.
Nachukua nafasi hii kukuambia kwamba kama una changamoto yoyote ambayo inakuzuia kuingia kwenye biashara au ambayo inakufanya ushindwe kufanikiwa unaweza kuileta na ikajibiwa kwenye kitabu hiki.
Unachotakiwa kufanya ni kuandika changamoto yako kwa mfumo wa swali na kutuma kwa email ushauri@kisimachamaarifa.co.tz
Swali au changamoto yako itajibiwa kwenye kitabu hiki ambacho kitatoka muda sio mrefu.
Chukua hatua haraka ya kuuliza changamoto yako kwa sababu muda ni mfupi.
Nakutakia kila la kheri.
TUPO PAMOJA.

Je Umepata Kitabu Chako?

Siku kadhaa zilizopita niliweka ujumbe ambao nilikuomba wewe kama msomaji uwatumie watu wa tano kwenye email zao.
Na pia niliahidi ukifanya hivyo nitakupa zawadi ya kitabu kinachohusu mabadiliko.
Watu wengi walitikia ombi lile na ujumbe ulitumwa kwa watu wengi sana.
Jana kitabu kilikamilika na wewe uliyetuma ujumbe kwa wengine ulikuwa wa kwanza kutumiwa.
Naandika hapa nikotaka kujua kama umepata kitabu ulichotumiwa.
Kitabu kimetumwa kwa watu 33 ambao waliitikia wito ule.
Kama ulituma ujumbe na hujapokea kitabu tafadhali nijulishe kupitia email makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Nakupenda na kukuheshimu sana wewe msomaji wangu hivyo napenda kutimiza kile ninachokuahidi.
Pia nitumie nafasi hii kutangaza kwamba zoezi la kutuma ujumbe ule na baadae kupewa zawadi limefungwa rasmi.
Ila nakuomba uendelee kutuma jumbe hizi nzuri kwa watu wako wa karibu na washauri kujiunga nasi. Usitake kupata mambo haya mazuri peke yako, tusambaze elimu hii ili iwafikie wengi zaidi.
Asante na nakutakia kila la kheri.
TUPO PAMOJA.

KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Kama kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho hapa duniani ni kwamba dunia inabadilika kila siku. Ukiangalia historia ya dunia tulikotoka na tulipo sasa kumetokea mabadiliko makubwa sana. Zilianza zama za mawe, zikaja zama za chuma, yakaja mapinduzi ya viwanda na hata sasa tupo kwenye mapinduzi ya kiteknolojia.

Jambo moja la kushangaza ni kwamba pamoja na mabadiliko haya kuwa wazi bado watu wengi ni wagumu sana kubadilika. Watu hawapendi mabadiliko, wanapenda kufanya kile walichozoea kufanya na wanataka maisha yaendelee vile yalivyokuwa jana na leo. Kitu ambacho ni ndoto isiyowezekana.

Katika zama zote ambazo dunia imepita, kuna watu ambao waliweza kubadilika haraka na kupata faida ya mabadiliko, wengine walilazimishwa kubadilika na hivyo kuburuzwa na kuna ambao waliachwa na mabadiliko na hivyo kupotea. Waliofaidika na mabadiliko ni wale waliokuwa tayari kubadilika, walioburuzwa na mabadiliko ni wale ambao walikuwa hawajui kama kuna mabadiliko ila wanakwenda tu na hali ilivyo. Walioachwa na mabadiliko ni wale ambao hata baada ya kuona mabadiliko wao waligoma kubadilika, waliendelea kung’ang’ania kile walichozoea na hatimaye kuachwa nyuma na kupotea.

mabadiliko cover EDWEB

Mabadiliko ni jambo muhimu sana lakini watu wengi hawajalipa msisitizo kwenye maisha na hii inapelekea wengi kuachwa nyuma na mabadiliko haya.

Ni kutokana na umuhimu wa jambo hili nimekuandalia kitabu kinachoitwa JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Katika kitabu hiki utajifunza mambo yafuatayo;

1. Historia fupi ya mabadiliko kwenye maisha ya mwanadamu hapa duniani na kwa nini mabadiliko yataendelea kutokea.

2. Mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye elimu, kazi na hata biashara.

3. Makundi ya aina tatu ya watu ambao wanazalishwa na mabadiliko, kundi linalonufaika na mengine yanayopoteza.

4. Mambo kumi muhimu sana ya kufanya ili na wewe uingie kwenye kundi ambalo linanufaika sana na mabadiliko ambayo yanaendelea kutokea

5. Mabadiliko makubwa yanayokuja kwenye mfumo wa elimu, mfumo wa ajira na hata biashara na ujasiriamali.

Kitabu hiki kitakuandaa wewe na kukupa mbinu za kuweza kuboresha maisha yako zaidi na kufanikiwa licha ya mabadiliko yanayoendelea.

Kitabu hiki ni muhimu sana kwa makundi yafuatayo;

1. Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanasoma ila hawana uhakika wa kupata ajira. Kitawawezesha kujiandaa mapema ili kujua njia watakayochukua na hivyo kutopoteza muda wakisubiri ajira ambazo hazipo.

2. Wafanyakazi ambao wamekuwa kwenye kazi kwa muda mrefu lakini hawaoni manufaa ya kazi zao kwenye maisha yao.

3. Wafanyabiashara ambao wamefanya biashara kwa muda mrefu ila wako pale pale miaka nenda miaka rudi.

4. Wafanyakazi ambao wamestaafu kazi, wamefukuzwa kazi, wamepunguzwa kazi au wameamua kuacha kazi wenyewe.

5. Watu ambao umri wao umekwenda kiasi na wanaamini kwamba mambo waliyokuwa wanafanya zamani ni bora kuliko yanayofanyika sasa, na wanaendelea kuyafanya licha ya kushindwa kupata majibu makubwa.

6. Mtu yeyote ambaye anataka kuboresha maisha yake zaidi, kwa kujua mambo yanayoendelea na ni yapi yanakuja kwa siku za mbeleni.

Ni muhimu sana wewe kupata na kusoma kitabu hiki, kitaleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako kama utakuwa tayari kufanyia kazi yale ambayo utajifunza.

JINSI YA KUPATA KITABUJINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy yaani pdf na unaweza kukisoma kwenye simu yako kama ni smartphone, unaweza kukisoma kwenye tablet na pia unaweza kukisoma kwenye kompyuta. Kurasa zake zinasomeka vizuri kwenye vifaa hivyo vya aina tatu tofauti.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu tano(5,000/=), gharama hii ndogo sio kwa sababu kina mambo madogo ila ni kwa sababu kitabu hiki ni muhimu sana na kila mtu ni muhimu akisome, hivyo gharamaisiwe kikwazo cha watu kushindwa kukisoma.

Kupata kitabu unafanya malipo ya tsh 5,000/= kupitia namba 0717396253 au 0755953887 na kisha unatuma email yako kwenye moja ya namba hizo na unatumiwa kitabu mara moja.

Mambo sasa hivi yanakwenda kidigitali zaidi na huna haja ya kubeba mizigo mingi, kwa kuwa na simu yako tu unaweza kuendelea kujifunza mambo mengi sana.

Karibu sana upate kitabu hiki mapema, kwa sababu jinsi unavyozidi kuchelewa kukipata, mabadiliko yanaendelea kutokea na yanakuacha nyuma. Jinsi utakavyoweza kuchukua hatua haraka ndivyo unavyoweza kuiokoa na kuimarisha kazi yako au biashara yako. Chukua hatua haraka kwa kusoma kitabu hiki leo.

Pia tembelea blog ya VITABU VYA UJASIRIAMALI NA MAFANIKIO ili kupata vitabu vingine vingi na vizuri vya kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo lolote unalofanya.

Jipatie kitabu chako leo, maisha hayakusubiri wewe uwe tayari.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako, na kitabu hiki kiwe nguzo muhimu sana kwako.

TUPO PAMOJA.

MAKIRITA AMANI

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Friday, March 13, 2015

Hizi Ndizo Siku Za Wiki Zenye Bahati Sana, Hakikisha Unaweka MIpngo Yako Kwenye Siku Hizi.

Ijumaa ni moja ya siku za wiki zenye bahati sana. Ni siku ambayo unaweza kuanza jambo lako kubwa na likafanikiwa sana.

Ni siku ambayo unaweza kupata faida kubwa sana kwenye biashara kama utaweka juhudi na maarifa.

SOMA; UKURASA WA 39; Jitengenezee Bahati Yako Mwenyewe…

Ni siku ambayo unaweza kuweka juhudi za ziada kwenye kazi yako na ukaongeza thamani yako na hata ukaweza kuongeza kipato chako.

Hii ni siku ya wiki ambayo hupaswi kuiacha ipite hivi hivi maana ina mambo mengi sana na mazuri kwako.

Ukiacha ijumaa siku nyingine za wiki ambazo zina bahati sana ni jumanne, alhamisi, jumatatu, jumamosi, jumatano na jumapili.

Usiziache siku hizi zipite bila yakufanya jambo kubwa na muhimu. Utaweza kufikia mafanikio makubwa sana.

Itumie siku ya leo yenye bahati sana kufanya jambo ambalo hujawahi kufanya ili ujiweke kwenye nafasi bora sana.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Kama Ulikuwa Hujui Bahati Inavyopatikana Soma Hapa.

Saturday, February 7, 2015

Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.

Karibu mataizo yote ya binadamu chimbuko lake ni fedha.
Watu wanachukuiana, watu wanauana na watu wanafanya mambo ya hatari sana kwa ajili ya fedha.
Ili kuondokana na matatizo haya mengi, anza kwa kutatua tatizo kuu ambalo ni fedha.
Kama unataka kutatua tatizo lako la fedha hasa kwa baadae anza leo kwa kuweka akiba asilimia 10 ya chochote unachopata. Na baadae wekeza akiba hiyo kwenye sehemu ambapo itaweza kuzalisha zaidi.
Ndio hivyo, weka pembeni asilimia 10, isahau kabisa. Kadiri miaka inavyokwenda utashangaa kuona uwekezaji wako unakua na matatizo ya fedha yanakwisha.

Sunday, February 1, 2015

Kitu Kimoja Cha Kufanya Kila Siku Ili Ufikie Malengo Yako 2015…

Mpaka sasa umeshajifunza mbinu nyingi sana za kukuwezesha kufikia malengo uliyojiwekea kwa mwaka huu 2015.

Kama una malengo na mipango tayari ni muhimu sana kutumia yale unayojifunza ili uweze kufikia malengo yako.

Mpaka kufikia leo kuna watu ambao tayari wameshasahau malengo waliyokuwa wamejiwekea kwa mwaka huu 2015. Hii inatokana na kuweka malengo kishabiki na kutokufuata kanuni muhimu z akuweza kuyafikia.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Ili uweze kufikia malengo yako unahitaji kuyafanya yawe kwenye akili yako kila siku na kila mara. Bila ya kujali ni hali gani unayopitia hutakiwi kuondoa mawazo yako kwenye malengo yako.

Leo utajifunza mbinu moja muhimu sana itakayokuwezesha kuyaweka malengo yako kwenye akili yako kila mara.

Mbinu hii ni kujiwekea utaratibu wa kuandika malengo yako kila siku asubuhi kabla ya kuianza siku yako. Yaani kila siku unapoamka andika malengo yako makubwa kwenye karatasi(ni vyema ukawa na kitabu) na tarehe ambazo utakuwa umefikia malengo hayo.

SOMA; Kozi 1100 Unazoweza Kujifunza Bure Kupitia Mtandao.

Kwa kufanya hivi utaianza siku yako kwa kufikiria ni nini cha kufanya ili uweze kufikia malengo hayo. Malengo yako yanakuwa kwenye akili yako muda wote na inakuwa rahisi kwako kuziona fursa za kukuwezesha kufikia malengo hayo.

Kumbuka kila siku kuandika malengo yako, haitakuchukua muda mrefu, dakika chache tu ila itakuletea faida kubwa. Usione ni kitu kidogo, kina matokeo makubwa kwako.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia malengo yako kwa mwaka huu 2015.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Ni Muda Unaenda Haraka Au Wewe Unaenda Taratibu?

Kufumba na kufumbua mwezi wa kwanza hatunao tena...
Tuko mwezi wa pili na siku sio nyingi tutauanza mwezi wa tatu.
Ni majuzi tu tulikuwa tunasherekea mwaka mpya, sasa hivi ni kama umechakaa.
Muda unakwenda haraka eh?
Hiki ndio kila mtu anachosema, kwamba muda unakwenda haraka sana.
Lakini je ni kweli?
Ni kweli muda unakwenda haraka au sisi tunakwenda taratibu?
Kipimo cha muda tunachotumia ni kile kile ambacho tumetumia miaka mingi iliyopita.
Iwe ni kwa kutumia saa, machweo na mawio na hata mzunguko wa mwezi. Vyote hivi havbijabadilika.
Ila sisi tunaona mabadiliko, muda unakwenda haraka sana.
Kwa dhana hii ya kwamba vipimo vyetu vya muda havijabadilika, ni dhahiri kamba sisi ndio tunakwenda taratibu.
Na kama tusipogundua mapema tutazidi kubaki nyuma.
Tufanye hima, muda hautusubiri.

Saturday, January 31, 2015

Huu Ni Mwaka Wa Kuacha Unafiki...

Umefika wakati wa kuacha unafiki..
Maana kuendelea na unafiki huu hakuwezi kukusaidia tena.
Swali la msingi; wakati unazaliwa au unakua ni nani alikuambia maisha yatakuwa rahisi? Kwamba utapata kila kitu kwa urahisi? Kwamba kutakuwa na njia za mkato za wewe kupata unachotaka?
Hakuna popote umewahi kuambiwa hivi.
Lakini kwa unafiki umeamua kulalamikia mambo hayo.
Kwamba maisha ni magumu, kwamba hupati njia ya mkato ya kufikia mafanikio.
Achana na unafiki huu,
Maisha ni magumu ndio, lakini ugumu wa maisha ndio unayafanya yawe mazuri kuishi.
Hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio, na kutokuwepo kwa njia hii ndio kunafanya safari ya kuelekea kwenye mafanikio kuwa nzuri.
Furahia kila hatua ya maisha yako.
Jifunze kutokana na changamoto unazopitia.
Acha kulalamika.

ADUI NAMBA MOJA WA MAFANIKIO YAKO...

Friday, January 30, 2015

Je Upo Tayari Kupata Unachotaka? Siri Ni Hii Moja…

Unataka nini kwenye maisha yako?

Maana kama hujui unachotaka tayari umeshakikosa.

Je upo tayari kupata hiko unachotaka?

Ni nini kinakuzuia mpaka sasa hujakipata?

Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza. Maana kuna kitu ambacho kimekufanya mpaka sasa hujapata unachotaka na kushindwa kujua kitu hiko kitaendelea kukuzuia.

Jua kikwazo ni nini na anza kukishughulikia.

Anza na vikwazo hivi;

Kwa watanzania waliowengi, vikwazo vinafanana na baadhi ya vikwazo hivyo ni;

1. Kutokujiamini.

2. Hofu

3. Kulalamika

4. Kutegemea kuna mtu atakuja kukutoa hapo ulipo.

5. Matumizi mabaya ya hela.

6. Uvivu, kutokuwa na ubunifu. Kuiga

7. Kukosa uvumilivu na kukata tamaa mapema.

8. Kutafuta njia ya mkato

9. Kukosa uaminifu

10. Kupanga malengo na mipango ila kushindwa kuchukua hatua.

Anza kufanyia kazi mambo hayo kumi na utaona ilivyo rahisi kupata chochote unachotaka.

Thursday, January 29, 2015

Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

Kama mpaka sasa huna utaratibu wa kujifunza kila siku, tayari upo nyuma sana katika kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako.

Kujifunza kila siku ni hitaji la chini sana la wewe kuweza kufikia mafanikio. Na tunaposema kujifunza kila siku ni kila siku kweli, jumatatu mpaka jumapili na kurudia tena na tena na tena.

Pamoja na umuhimu wa kujifunza kila siku, bado tunaishi kwenye jamii ambayo haitupi nafasi kubwa ya kujifunza. Hii ni kutokana na kuzungukwa na mazingira yenye changamoto nyingi zinazozuia kujifunza kila siku.

Kutokana na changamoto hizi ndio kulikonisukuma kutumia muda wangu kukupatia wewe nafasi ya kujifunza zaidi. Kupitia blog ya MAKIRITA AMANI utaweza kupata nafasi ya kujifunza kila siku, jumatatu mpaka jumapili.

Kila siku utaianza siku yako kwa neno la siku, hili ni neno ambalo litakupa hamasa ya kuweza kuifanya siku yako kuwa bora zaidi. Na pia kila siku kwa mwaka huu 2015 utapata ukurasa mmoja katika safu ya kurasa 365 za mwaka 2015. Kama bado hii haitoshi, unapata nafasi ya kupata kauli za kuhamasisha kutoka kwa viongozi na watu mashuhuri ambao wamefanikiwa sana. Na pia utaweza kupata hadithi za mafunzo ambapo utawez akujifunz akupitia visa mbalimbali.

Pamoja na haya yote utakuwa ukipata makala zenye fikra za kukuchokoza. Hizi ni zile ambazo zinaniingia kwenye fikra zangu kutokana na mawazo mbalimbali yanayonifikia katika kutafuta njia za kufanya maisha yangu na ya wewe msomaji kuwa bora zaidi kila siku.

Kwa kifupi wewe kutembelea blog hii ni sawa na kuwa na mimi pembeni yako, kwani utapata kitu kizuri kutoaka kwangu pale unapokihitaji.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za mbalimbali za kukufundisha na kukuhamasisha kila siku bonyeza hapa na uweke email. Kila siku kwenye email yako utapata mambo haya moja kw amoja.

Siku yako itakuwa bora sana kwa kuwa karibu na blog hii nzuri kwako.

Kama ningekuwa natoza wasomaji fedha kulingana na elimu ninayoitoa hapa, kila msomaji angetakiw akulipa tsh elfu moja kila siku. Hivyo kwa mwaka ungetakiw akulipa tsh 365,000/= ili kupata elimu hii muhimu sana kwako. Lakini sijataka wewe uingie gharama yoyote, gharama yako ni wewe kufungua blog, kusoma makala na kufanyia kazi yale unayojifunza.

Ombi moja muhimu sana kwako ni wewe kuwaalika watu wengi zaidi kusoma blog hii. Haina gharama yoyote na wala haitakuja kuw ana gharama yoyote. Tafadhali tuma makala hii kwenye email za watu watano, itume kama ilivyo halafu nikopy kwenye email hiyo utakayotuma, tumia email makirita@kisimachamaarifa.co.tz kama hujui jinsi ya kukopi, wakati unaweka email ya unayemtumia chini yake kuna cc, hapo weka email yangu. Na mimi nitakupa zawadi nzuri sana ya kitabu cha mabadiliko ambacho bado nakiandika.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya kuboresha maisha yako.

TUPO PAMOJA SANA.

 

Tuesday, January 27, 2015

Hii Ndio Faida Ya Kuboresha Maisha Yako...

Unapoboresha maisha yako, kila kitu kinachokuzunguka nacho kinakuwa bora.
Hii ni sheria ya asili.
Kazana kila siku kuboresha maisha yako na utajikuta unazungukwa na kila kilicho bora.
Kumbuka hili ni zoezi la kila siku, hakikisha leo unakuwa bora kuliko ulivyokuwa jana.

Unataka Kujifunza Kitu Chochote Unachoona Ni Kigumu? Fanya Hivi...

Njia bora kabisa ya kujifunza ni kufanya, kutenda.
Utasoma vitabu vyote, utafundishwa na walimu waliobobea ila kama hutatendea kazi yale uliyojifunza ni kazi bure.
Hakuna mtu aliyewahi kujifunza na akajua kuendesha baiskeli kwa kusoma vitabu tu. Hata baada ya maelekezo ulihitaji kuipanda baiskeli, kuanguka na hata kuumia ndio ukajua kuendesha baiskeli.
Sasa nini kinakuzuia wewe kuchukua hatua sasa? Hujajifunza? Anza kufanya.
Unataka kujifunza biashara, anza kufanya biashara, anza kidogo kidogo.
Unataka kujifunza kuandika makala nzuri anza kuandika, anza maneno matano nenda kumi, ishirini, mia...
Unataka kujifunza kilimo, nenda tafuta shamba, anza kulima.
Unataka kujifunza maisha, anza kuishi, sio kuishi kama kila mtu anavyoishi, bali kuishi kama ambavyo unataka kuishi.
Mwaka huu ni JUST DO IT.
Chochote unachotaka kwenye maisha yako, anza kukifanyia kazi. Hakuna kitakachokushinda.

Sunday, January 25, 2015

Mambo Matatu Muhimu Ya Kufanya Siku Ya Jumapili Ili Kuwa Na Wiki Yenye Mafanikio

Jumapili ni siku muhimu sana kama unataka kuwa na wiki yenye ufanisi mkubwa.
Ni siku ambayo kama ukiitumia vizuri utakuwa na wiki yenye mafanikio na kama ukiitumia vibaya utakuwa na wiki mbaya na ya kupoteza muda.
Kuna vitu vitatu unavyoweza kufanya siku ya jumapili ili kuwa na wiki yenye ufanisi mkubwa na mafanikio makubwa.
1. Tafakari wiki inayoisha.
Fikiria jinsi ambavyo wiki yako ilikwenda. Angalia ni mambo gani ulifanikiwa kufanya na yakakusogeza mbele. Na pia angalia ni mambo gani ulishindwa kufanya na nini kilisababisha ukashindwa.
2. Panga wiki inayoanza.
Angalia wiki inayoanza na panga ni vitu gani unataka kukamilisha kwenye wiki hiyo. Panga mambo muhimu na weka vipaumbele kwenye matumizi ya muda wako.
3. Pata muda wa kupumzika.
Kama unafanya kazi wiki nzima, angalau tenga siku ya jumapili upumzike. Hata kama sio siku nzima, pata masaa machache ambayo utapumzisha mwili wako. Pia lala mapema ili uamke ukiwa na nguvu za kuanza vyema wiki yako.
Fanya mambo hayo matatu kila jumapili na utaona jinsi wiki yako itakavyokuwa bora.
Usipofanya hayo utajikuta kila jumatatu kwako ni BLUE MONDAY, jumanne ni hovyo, jumatano haisomeki, alhamisi angalau na ijumaa unafurahia maana wikiendi imekaribia tena.
Maisha ya aina hii hayatakufikisha kwenye mafanikio.

Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.

Muda una thamani kubwa sana kuliko fedha, hii ni kwa sababu ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine ila ukipoteza muda huwezi kuupata tena.
Ila muda na fedha vina tabia moja inayofanana, ukivitumia bila ya kuandika kwenye karatasi unavipoteza.
Kitu muhimu cha kufanya kabla ya kutumia fedha au muda ni kupangilia matumizi hayo kwa kuandika kwenye karatasi au kitabu.
Usipopangilia kwa kuandika, utajikuta umetumia hovyo na hivyo kupoteza muda wako au fedha zako.
Weka mipango kabla ya kutumia muda au fedha.
Itakusaidia kuvitumia vitu hivyo viwili kwa makini.