Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, July 6, 2015

UKURASA WA 187; Usikubali jua lizame leo kabla hujafanya kitu hiki muhimu.

Siku ya leo kuna watu wengi sana watakaokuudhi. Kuna watu wengi watakukasirisha na wengine watakufanya ujisikie vibaya sana. Kwa hasira inayotokana na watu hawa unaweza kufanya maamuzi ambayo sio mazuri sana kwao na kwako pia.
Ila kumbuka mara nyingi unapokuwa na hasira huwezi kufanya maamuzi ambayo ni sahihi. Na hata kama mtu atakuchukiza kiasi gani, hata kama atakuudhi kiasi gani kwa wewe kuwa na hasira, kwa wewe kuendelea kuwa na kinyongo naye haimuumizi yeye bali inakuumiza wewe mwenyewe.
SOMA; JICHO KWA JICHO; Tutabaki Na Dunia Ya Vipofu.
Sasa leo nataka nikupe kitu kimoja muhimu cha kufanya kabla jua halijazama. Hakikisha jua linapozama umemalizana na kitu hiki ili siku yako ya kesho iwe bora sana.
Kabla jua halijazama leo hakikisha umewasamehe wote waliokukosea leo. hakikisha umeondokana na vinyongo vyote ambavyo unaweza kuwa umejitengenezea kwa siku ya leo. Acha mambo haya yote yazame na jua la leo, ili jua linapochomoza kesho uanze siku yako ukiwa vizuri na uweze kufanya makubwa.
Usikubali jua lizame ukiwa bado na hasira au kinyongo. Vitu hivi havikusaidii chochote zaidi ya kufanya maisha yako kuwa magumu na hata kuharibu afya yako.
TAMKO LA LEO;
Sitakubali siku ya leo na siku nyingine yoyote ipite nikiwa na kinyongo au hasira kwenye moyo wangu. Jua litakapozama nitahakikisha nimeachia yote niliyokumbana nayo siku ya leo. kama kuna mtu ameniudhi, amenikasirisha au amefanya chochote ambacho kimenifanya niwe na kinyongo nitamsamehe. Maisha yangu ni muhimu zaidi ya chuki ninazotaka kutengeneza na watu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 188 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment