Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, March 27, 2015

UKURASA WA 86; Jifunze Kusikiliza.

Tuna masikio mawili na mdomo mmoja kwa sababu moja kubwa sana. Kusikiliza ni bora kuliko kuongea. Yaani unahitaji kusikiliza mara mbili ya unavyoongea.

Lakini kwenye maisha yetu ya kawaida mambo ni kinyume kabisa na hapo. Watu wanaongea mara mbili ya wanavyosikiliza. Kila mtu anakazana kuongea na mwishowe hakuna tena mazungumzo mazuri.

SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.

Maongezi mengi yamekuwa sio ya kujifunza na kuelewa zaidi bali yamekuwa ni maongezi ya mtu kusubiri wakati wake wa kuongea. Yaani wakati mtu mwingine anaongea wewe husikilizi kwa makini kile anachoongea bali unafikiria utamjibu nini au utaongea nini.

Katika hali hii hakuna mawasiliano mazuri kati ya watu wanaongea na hivyo ujumbeuliotakiwa kufika unashindwa kufika.

SOMA; Maswali ambayo huulizwa mara nyingi kuhusu uwekezaji katika hisa.

Hasara za kuongea kuliko unavyosikiliza zipo nyingi sana ila kuna hii moja ambayo ni kubwa sana na yenyewe ni KUTOJIFUNZA. Kama katika maongezi yoyote uliyopo wewe ndio muongeaji sana maana yake unajiambia vitu ambavyo tayari unavijua. Lakini unaposikiliza unajifunza vitu vipya ambavyo hukuwahi kuvijua kupitia wengine wanaoongea.

Punguza kuongea na anza kusikiliza kwa makini, hata kama mtu anakosea, utajifunza ni nini cha kufanya ili na wewe usikosee.

SOMA; Hizi Ndizo Gharama Unazotakiwa Kuzilipia, Ili Uweze Kupata Kile Unachokihitaji Katika Maisha Yako.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia leo nitakuwa nasikiliza mara nyingi ya zaidi ya ninavyoongea. Na katika kusikiliza kwangu nitasikiliza kwa makini ili kujifunza na sio kusikiliza ili nijue kipi cha kujibu. Najua kwa kuongea mimi mwenyewe sijifunzi kitu kipya, ila ninapowasikiliza watu wengine najifunza mambo mengi sana mapya. Nitasikiliza kwa makini sana maongezi yoyote nitakayokuwepo.

Tukutane kwenye ukurasa wa 87 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment