Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, March 13, 2015

UKURASA WA 72; Unaenda Mbele Au Unarudi Nyuma?

Katika safari ya mafanikio, kuna hali mbili tu, kwenda mbele au kurudi nyuma. Hakuna kati kati, hakuna kwamba umesimama.

Ni unaenda mbele au unarudi nyuma. Unapanda au unashuka. Unakuwa bora au unakuwa hovyo.

Ndivyo hali ilivyo.

Sasa kila siku hebu jiulize swali hili kabla hujalala, je leo nimeenda mbele au nimerudi nyuma?

SOMA; Mambo Matano Ambayo Viongozi Bora Hufanya Kila Siku.

Kama umaefanya kazi yako au biashara yako kama ulivyofanya jana na juzi basi umerudi nyuma.

Kama hujajifunza kitu chochote kipya basi umerudi nyuma.

Kama hakuna ulichoboresha kwenye mahusiano yako basi umerudi nyuma.

Kama hujagusa maisha ya mtu mwingine kwa hali yoyote ile basi umerudi nyuma.

Kurudi nyuma ni rahisi sana kwa sababu hujui kama unarudi nyuma, wewe unaona tu umesimama kumbe mambo yanakupita kwa kasi kubwa sana.

SOMA; UKURASA WA 63; Usikazane Kushindana, Kazana Kuwa Bora.

TAMKO LA LEO;

Kila siku nitafanya jambo dogo ambalo litanipeleka mbele zaidi. Hata kama ni wka asilimia 1 tu, kadiri nitakavyoendele akufanya ndivyo nitakavyoendelea kuwa bora. Kama sitofanya na nikabaki nimesimama, maana yake narudi nyuma. Ninajua hatari kubwa ya zama hizi ni kurudi nyuma.

Tukutane kwenye ukurasa wa 73 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment