Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, February 3, 2015

UKURASA WA 34; Jali Mambo Yako.

Katika wakati wowote ule na popote ulipo kuna mambo mengi sana yanayoendelea. Kama utataka kujali kila kitu utashindwa kufikia mafanikio makubwa.

Kama utataka kujua kila kitu kinachoendelea, nani kafanya nini, utakuwa unajali mabo mengine na mambo ya watu wengine na kujinyima muda wa kufuatilia mambo yako.

Kumbuka tulivyosema kwenye kuweka vipaumbele, chagua mambo ambayo yanakuletea faida kubwa na wekeza nguvu zako kwenye mambo hayo machache. Mengine yote achana nayo, ni kelele kwako.

SOMA; UKURASA WA 21; Weka Vipaumbele Kwenye Maisha Yako.

Jali mambo yako, na hayo mengine yatajijali yenyewe. Muda ni mfupi sana kwa wewe kujali kila kitu kinachoendelea.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba mambo yangu ni muhimu kukiko kufuatilia kila kinachoendelea. Nitajali mambo yangu na mambo ambayo yanaweza kuniathiri kwa njia moja au nyingine. Mambo mengine nitaachana nayo yajijali yenyewe.

Tukutane kwenye ukurasa wa 35 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Sifa TATU Unazohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment