Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, February 6, 2015

#HADITHI_FUNZO; Zawadi Ya Matusi…

Palikuwa na shujaa mmoja aliyeishi miaka ya zamani. Japo shujaa huyu alikuwa amezeeka, bado alikuwa na uwezo wa kupambana na kumsinda mpinzani wake. Sifa zake zilisambaa sana na wanafunzi wengi walikuja kwake kujifunza.

Siku moja shujaa mwingine kijana alikuja kwenye kijiji cha shujaa yule mzee. Alikuwa ameamua kuwa mtu wa kwanza kumshinda shujaa yule mzee. Alikuwa na nguvu sana na pia alikuwa na uwezo wa kipekee wa kuweza kumsoma mpinzani wake, kujua udhaifu wake na kuweza kumshinda.

SOMA; Sifa TATU Unazohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Pamoja na kushauriwa na wanafunzi wake kwamba asipigane na shujaa yule kijana, shujaa mzee alikubali kupambana na kijana yule ambaye alionekana kuwa na uwezo mkubwa sana kuliko yeye.  Waliingia kwenye uwanja wa mapambano na kijana yule alianza kujitamba huku akimtukana mzee yule matusi. Alimsogelea na kutukana kila aina ya tusi, alimtemea mate usoni. Alifanya hivi kwa muda mrefu, lakini shujaa yule mzee hakufanya kitu chochote zaidi ya kumuangalia usoni.

Baada ya muda shujaa yule kijana alichoka kwa maneno na kuondoka kwa aibu. Wanafunzi wake walimfata shujaa yule mzee na kushangazwa kwa nini alivumilia matusi yote yale na hakumpiga kijana yule. Mzee yule aliwauliza swali moja “Kama mtu akikupa zawadi halafu hukuipokea, zawadi ile inakuwa ya nani?”

SOMA; Mambo matatu yatakayokufanya uishi maisha marefu.

Tunajifunza nini kwenye hadithi hii;

1. Kuonesha udhaifu wako ndio udhaifu mkubwa zaidi kwako. Shujaa kijana alikuwa anamtukana shujaa mzee ili apate hasira na aoneshe udhaifu wake ambapo angemshinda kirahisi.

2. Kama mtu akikupa zawadi, halafu hukuipokea, inabaki kuwa zawadi yake. Mtu akikutukana halafu hukumjibu anakuwa amejitukana mwenyewe.

3………..

4…………

5…………

Jaza mengine matatu uliyojifunza kwenye hadithi hii na washirikishe wengine watano ili nao wajifunze.

TAFADHALI Usiache kuwashirikisha wengine.

SOMA; Hatua TANO Za Kuongeza Uzalishaji Wako Ili Kufikia Mafanikio.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment