Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, February 5, 2015

UKURASA WA 36; Mafanikio Sio Kitu Kimoja.

Japokuwa kila mtu ana maana yake ya mafanikio, bado mafanikio si kitu kimoja hata kwa huyo mtu mmoja.

Kwa mfano tuseme wewe maana yako ya mafanikio ni kuishi kwenye nyumba ya kifahari ufukweni, kuendesha gari la kifahari na kuwa na bilioni moja kama akiba.

Sasa mafanikio sio pale unapokuwa na vitu hivi tayari. Na kama unafikiri mafanikio ndio hivyo utapoteza miaka yako mingi sana ya maisha.

SOMA;  NENO LA LEO; Hiki Ndio Unachohitaji Ili Kufanikiwa.

Mafanikio ni jinsi unavyoweza kuishi kila siku yako kwa ubora huku ukijitengenezea nafasi ya kufikia malengo uliyojiwekea. Hii inafanya kila siku inakuwa nzuri kwako na unakuwa na furaha.

Dunia inatuaminisha kwamba mafanikio ni pale unapokuwa na vitu hivyo ambavyo watu wanaviona. Ila kuanzia leo mafanikio kwako ni kuweza kuishi siku ya leo kwa ubora kuliko ulivyoishi jana huku ukitekeleza malengo yako. Kama jana ulipata elfu tano, leo umepata elfu sita, ni mafanikio, na lengo lako ni kuendelea kuongeza kiwango hiko kila siku.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba hakuna siku moja nitakayoamka usingizini na kusema leo nimefanikiwa kwa sababu ninachi kila ninachohitaji. Mafanikio yanatokana na mambo madogo madogo ninayofanya kila siku kwenye maisha yangu. Kuanzia sasa nitawekeza nguvu zangu kwnye mambo ninayofanya ili nifikie mafanikio na kupata furaha.

Tukutane kwenye ukurasa wa 37 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Kesho ni siku muhimu sana kwako, na itumie kufanya jambo hili moja muhimu.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment