Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, April 3, 2015

UKURASA WA 93; Linda Sana Mawazo Yako.

Maisha yako yanatokana na mawazo yako. Kitu chochote ambacho unakifanya au unakutana nacho, hakitokei tu kwa bahati mbaya, ila kinaanzia kwenye mawazo yako. Mawazo yako yana nguvu kubwa sana ya kuumba. Na ndio yameumba kila kitu kinachoendele akwenye maisha yako.

Kama mawazo yako ndio yanayotengeneza maisha yako, hii ina maana kwamba unatakiwa kuwa makini sana na mawazo hayo. Kama utakuwa na mawazo mazuri yatakutengenezea maisha mazuri. Kama utakuwa na mawazo mabaya ndio maisha utakayokuwa nayo.

Kama waswahili wanavyosema, unapanda ulichovuna, mawazo unayoweka kwenye akili yako ndio matunda unayovuna.

SOMA; BIASHARA LEO; Mwisho Wa Ufalme Wa Mteja.

Mawazo yako haya yako kwenye hatari kubwa sana ya kuharibiwa na hivyo maisha yako kuharibika pia. Tunaishi kwenye jamii ambayo imejaa mawazo hasi, imejaa wakatisha tamaa na imejaa mashahidi wa uongo ambao watakupa kila sababu kwa nini utashindwa.

Linda sana mawazo yako dhidi ya mawazo haya hasi. Usikubali kabisa kuingiza wazo hasi wkenye kichwa chako, ikitokea wazo hili limeingia liondoe haraka kwa kuweka mawazo mengine chanya.

SOMA; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini

Una mawazo mengi chanya unayohitaji kuyafanyia kazi. Weka mawazo yanayoendana na malengo unayotaka kufikia kwenye maisha na utaona fursa nyingi sana za kukuwezesha kufikia malengo yako.

Kama utashindwa kulinda mawazo yako, kila wazo hasi litaingia na litakuwa kikwazo kikubwa kwako kufikia mafanikio makubwa.

TAMKO LA LEO;

Najua mawazo yangu ndio yanatengeneza maisha yangu. Najuaili nifanikiwe nahitaji kuwa na mawazo chanya juu ya maisha yangu na mazlengo ninayotaka kufikia. Najua pia kwamba jamii inayonizunguka imejaa mawazo mengi hasi. Nitalinda sana mawazo yangu dhidi ya mawazo haya hasi. Wazo lolote hasi litakaloingia kwenye mawazo yangu nitalitoa haraka kwa kuweka mawazo mengine ambayo ni chanya.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Tukutane kwenye ukurasa wa 94 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment