Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, April 2, 2015

UKURASA WA 92; Usipoteze Muda Kwa Vitu Vidogo Vidogo.

Tunaishi kwneye dunia yenye kelele nyingi sana. Maendeleo makubwa yaliyokuja kwenye teknolojia pia yameleta usumbufu mkubwa sana. Kwa simu hizi za kisasa tunazotumia, unaounganishwa na dunia nzima kwa masaa 24 kwa siku.

SOMA; BIASHARA LEO; Ondoka, Hakuna Aliyekuita Hapa.

Unaweza kuona ni kitu kizuri, kuweza kupata kila taarifa inayotokea masaa 24 kwa siku kwenye simu yako. Lakini hili ni tatizo kubwa na linalokupotezea muda wako na kukufanya ushindwe kufikia mafanikio makubwa.

Zaidi ya asilimia 90 ya habari na taarifa unazopata kila siku hazina msaada wowote kwako au hata kufikia malengo yako. Halafu mbaya zaidi habari hizi ni hasi na hivyo kukufanya na wewe uwe hasi. Kama unakumbuka vizuri, huwezi kufikia mafanikio kama uko hasi, yaani kama una mtizamo hasi.

SOMA; Jinsi ya kuzuia hatari ya kupata hasara kupitia uwekezaji katika hisa

Unaruhusu muda wako kupotelea kwenye vitu vidogo vidogo ambavyo havina maana yoyote kwako. Unafikiri ni vizuri kwenda na wakati, ila wakati huu unakufanya ushinwe kwend ambali zaidi.

Kwa kuwa umeshachagua ni kitu gani unataka kwenye maisha yako, hebu wekeza nguvu zako zote hapo. Achana na vitu hivi vidogo vidogo, havina msaada wowote kwako zaidi ya kukuacha ukiwa umechoka na usijue ni hatua gani ya kuchukua.

SOMA; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini - 2

TAMKO LA LEO;

Najua kuna vitu vingi vidogo vidpgo vinagombania kutumia muda wangu. Najua kwmaba mud awangu ni muhimu sana ili kufikia malengo yangu. Sitapoteza muda huu kwa kuhangaika na vitu ambavyo havina faida kwangu. Kwanzia sasa naacha kufuatilia habari zote ambazo hazina msaada kwangu kufikia malengo yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 93 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment