Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, April 12, 2015

UKURASA WA 102; Mara Zote Sema Ukweli, Ni Rahisi Kukumbuka.

Kuna usemi maarufu kwamba ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.

Sasa hebu niambie ni mambo gani unayokumbuka uliongea kuanzia mwaka huu umeanza, vipi mwaka jana, na vipi miaka mitano iliyopita? Ni vigumu sana kukumbuka kila kitu ambacho umewahi kuongea.

Hivyo sehemu ya pili ya usemi huo kwmaba uwe na kumbu kumbu haiwezekani kwa sababu tunasahau sana.

SOMA; Siri Ya Kutambua Kampuni Nzuri Ya Kuwekeza Ili Upate Faida.

Hivyo basi ili usije kujikuta kwenye wakati mgumu, ongea ukweli mara zote. Kwa kuongea ukweli hutakuwa na haja ya kukumbuka maana wakati wowote ukweli unabaki kuwa ukweli. Ni vigumu sana kusahau kitu ambacho ni cha kweli.

Kuna usemi mwingine maarufu kwamba njia ya muongo ni fupi. Usitake kuingia kwenye njia hii, kuna siku moja utaumbuka na utajiondolea heshima yako.

Kama una tabia ya uongo iache mara moja, uongo ni tabia ambayo itakunyima fursa nyingi sana. Unaweza kufikiri kwamba ukidanganya ndio watu watakupenda ila watakapogundua umewadanganya watakudharau sana. Sema ukweli hata kama ni mchungu na watu watakuheshimu wakati wote.

SOMA; Huu Ndio Mtaji Mkubwa Ambao Tayari Unao.

TAMKO LA LEO;

Najua uongo ni sumu kubwa sana kwangu kufikia mafanikio. Nitaema ukweli mara zote ili nisije kujikuta kwenye wakati mgumu utakaoniondolea heshima yangu na kuninyima fursa nyingi nzuri. Nitasema ukweli hata kama ni mchungu kwa sababu ukweli siku zote hushinda.

Tukutane kwenye ukurasa wa 103 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment