Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, April 14, 2015

NENO LA LEO; Hii Ndio Tiba Ya Muujiza Mkubwa.

Love is the great miracle cure. Loving ourselves works miracles in our lives. -Louise L. Hay

Upendo ndio tiba ya muujiza mkubwa. Kujipenda sisi wenyewe kunaleta miujiza mikubwa kwenye maisha yetu.

SOMA; Sababu Zinazokufanya Wewe Kushindwa Kuthubutu Wazo Lako

Kama una changamoto zozote kwenye maisha yako, kama una matatizo yoyote kwenye maisha yako, hebu anza kw akujipenda wewe mwenyewe kwanza.

Unapojipenda mwenyewe, kwanza unajiepusha na matatizo mengi ambayo yangeendelea kukusumbua. Na pia utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.

Upendo ni tiba kubwa sana na inayoweza kutenda miujiza mikubwa. Unapojipenda mwenyewe, utayathamni  maisha yako, utakuwa na udhubutu na utaweka juhudi na maarifa ili uweze kupata kile unachotaka.

Unapojipenda mwenyewe pia inakuwa rahisi kwako kuwapenda wanaokuzunguka.

Jipende wewe kwanza na mambo mengine yatakwenda vizuri.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Mafanikio Ya Biashara Yanaanza Na Wewe Mwenyewe.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment