Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, April 17, 2015

UKURASA WA 107; Sema HAPANA, Hapa Ndio Uhuru Wako Ulipo.

HAPANA ndio neno gumu kusema kuliko maneno mengine yote. Hasa kwa watu ambao ni wa karibu au kwa vitu ambavyo unavipenda.

Lakini neno hili HAPANA ndio limebeba uhuru wako. Yaani uhuru wako upo ndani ya uwezo wako wa kusema hapana.

Kwa nini HAPANA ni muhimu?

Tunaishi kwenye dunia ambayo ina usumbufu mkubwa sana. Ukuaji wa teknolojia umerahisisha karibu kila kitu. Mtu anaweza kukupata kwa muda wowote anaotaka yeye na kwa njia yoyote anayoamua. Kuna vitu vingi sana vya kufanya kwa muda ule ule ambao tumekuwa nao enzi na enzi ambao ni masaa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki na wiki 52 kwa mwaka.

SOMA; Kama Unajiambia Hivi Mara Kwa Mara, Unaharibu sana maisha Yako.

Ili uweze kufanya mambo ambayo ni muhimu kwako, ni lazima uweze kusema hapana kwenye mambo mengi ambayo sio muhimu kwako na kusema ndio kwenye mambo amchache ambayo ni muhimu kwako.

Ni mambo gani ya kusema hapana?

Jambo lolote ambalo haliweki fedha kwneye mfuko wako, haliongezi maarifa kwenye akili yako au haliimarishi mahusiano yako ya kimaisha, kibiashara na kikazi unatakiwa kulisemea HAPANA haraka sana, maana hili linanyonya muda wako.

Hii inakwenda moja wka moja kwenye habari nyingi ambazo unafuatilia, mitandao mingi ya kijamii ambayo unatembelea kila siku na kila mara, mabishano yoyote yasiyo ya msingi, na maombi au mapendekezo ya wengine ambayo hayaingii kwenye mambo ambayo ni muhimu kwako.

Ni mambo gani ya kusema NDIYO?

Mambo yote ambayo yanakusogeza kwenye lengo lako, kazi unayofanya, biashara unayofanya, familia yako, muda wa kupumzika, na vingine ambavyo ni muhimu sana kwako.

SOMA; Ukweli Kuhusu Afya ya Wanaume; Kwa nini Wanaume Wanakufa Wadogo Kuliko Wanawake.

Uwezo wako wa kusema HAPANA, utakuwezesha kununua uhuru wako kwenye dunia ya sasa ambayo ina kelele na vishawishi vya kila aina.

TAMKO LA LEO;

Neno muhimu kwangu ni HAPANA. Nitasema hapana kwa kitu chochote ambacho hakiweki fedha kwenye mifuko yangu, hakiongezi maarifa kwenye akili yangu, au hakiimarishi mahusiano yangu na wale ambao ni muhimu kwangu. Muda ni mfupi na mambo ya kufanya ni mengi, HAPANA ndio uhuru wangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 108 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment