Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, April 3, 2015

NENO LA LEO; Hapa Ndipo Alipo Anayetaka Kukurudisha Chini.

“Whoever is trying to bring you down is already beneath you.” ― Habeeb Akande

Yeyote anayekazana kukurudisha chini, tayari yupo chini yako.

Angalia kwa makini kwenye maisha yako, kazi yako na hata biashara yako. Angalia wale watu ambao wanajaribu kukurudisha chini, angalia wale watu ambao wanakukatisha tamaa, angalia wale watu ambao wanakuwekea vikwazo. Wote utakuta wapo chini yako.

Ni vigumu sana kwa mtu aliyeko juu yako kukurudisha wewe chini. Hii ni kwa sababu aliye juu anakuwa bize na kuelekea juu zaidi hivyo hawezi kupoteza muda wake kukazana kukurudisha wewe chini. Na kama ukimuomba akuvute juu, atakuwa tayari kufanya hivyo.

SOMA; BIASHARA LEO; Ondoka, Hakuna Aliyekuita Hapa.

Ila kwa walioko chini sasa, kwanza hawaamini wkamba wanaweza kwenda juu, pili hawana kazi kubwa ya kufanya na hivyo wana muda wa kutosha wa kukurudisha wewe chini. Na pia hawapendi kubaki chini wenyewe, hivyo wanahakikisha kila anayejitahidi wkenda juu wanamrudisha chini.

Usisikilize tena mtu anayejaribu kukurudisha chini, huyo ni mtu ambaye yupo chini yako. Usikubali kabisa akurudishe kwenye ngazi zake za chini.

Pambana.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini - 2

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment