Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, April 13, 2015

UKURASA WA 103; Vitu Rahisi Kufanya Ndio Vyenye Matatizo Makubwa.

Tunaishi kwenye dunia ambayo inajaribu kurahisisha kila kitu. Kila mtu anaangalia njia rahisi ya kupata kile ambacho anataka. Kila mtu anataka kupata kitu kwa haraka zaidi na kwa urahisi sana.

Ni kweli maendeleo ni pamoja na kurahisisha vitu na kuharakisha vitu. Badala ya kusafiri miezi sita kwenda ulaya kwa meli unaweza kusafiri wka siku moja kwa kutumia ndege.

SOMA; Mafanikio Ya Biashara Yanaanza Na Wewe Mwenyewe.

Lakini urahisi huu na uharakishaji huu haufai kutumia kila eneo la maisha yetu. Kwenye maeneo mengi unaleta matatizo makubwa sana.

Unataka kula chakula rahisi na cha haraka, lakini vyakula vya aina hii ndio vinavyotengeneza afya mbovu sana.

Unataka kupata njia ya kupata fedha haraka na kw aurahisi, unajiingiza kwenye matendo ambayo yanakupa matatizo makubwa.

Unataka kupata furaha kwa haraka na kwa urahisi, unajiingiza kwenye tabia ambazo zitakuletea matatizo makuwba sana kama ulevi.

SOMA; Fursa katika Kilimo cha Bustani

Kwa chochote unachofanya kwenye maisha yako kumbuka kwamba RAHISI na HARAKA inaweza kukuletea matatizo makuwba sana baadae. Na ubaya wa matatizo haya ni kwamba hayaji ghafla, yanaanza kidogo kidogo na baadae unajikuta kati kati ya matatizo makubwa sana.

Epuka RAHISI na HARAKA hasa katika swala la afya, mafanikio, kipato, furaha, uaminifu na uadilifu.

TAMKO LA LEO;

Najua kwmaba vitu vinavyopatikana kwa HARAKA na URAHISI vinaweza kuniweka kwenye matatizo makubwa sana baadae. Nitakuwa mwangalifu kabla ya kuingia kwenye kitu chochote ambacho ni HARAKA AU RAHISI. Maisha yana changamoto zake, sitaki kujitengenezea nyingi zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 104 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment