Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, February 28, 2015

UKURASA WA 59; Kabla Hujabadili Tabia Zako Badili Hiki Kwanza…

Hakuna shaka kwamba huwezi kufikia mafanikio kama utaendelea kufanya kile ambacho unafanya sasa na kwa mtindo ambao umekuwa unautumia miaka yote. Kama utaendelea kufanya kile unachofanya utaendelea kupata matokeo unayopata.

Njia ya kupata matokeo tofauti ni kufanya mambo tofauti au kufanya mambo kwa utofauti.

SOMA; SIRI YA 34 YA MAFANIKIO; Unakuwa Kile Unachofikiria.

Njia moja ya kufanya mambo tofauti au kufanya mambo kwa utofauti ni kubadilika wewe kwanza. Yaani huwezi kupata mabadiliko kwenye maisha yako kama hutabadilika wewe kwanza.

Sasa swali ni je ili kubadilika unahitaji kufanya nini? Wengi watakimbilia kusema kubadili tabia. Ni kweli kubadili tabia kutakuwezesha kubadilisha ila mabadiliko hayo hayatadumu kama hutabadili kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiki ndio unatakiwa kukibadili kabla hujabadili tabia.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Kitu hiko ni utambulisho wako. Ndio kila mtu ana utambulisho wake, wa jinsi anavyojiona mwenyewe na watu wanavyomuona. Utambulisho wako kwako binafsi unaweza kuwa wewe ni mvivu, ni mtu usiyekamilisha mambo, ni mtu uliye na bahati mbaya, au kisirani. Hata kama utabadili tabia, kama utambulisho wako utaendelea kuwa huu, utarudi pale pale na kushindwa kufikia mafanikio.

Anza kwanza kubadili utambulisho wako, anza kujiona wewe ni mtu unayeweza kufikia mafanikio na anza kufanya kazi kulingana na utambulisho wako mpya.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia leo nafuta utambulisho wangu wa zamani ambao hakuwa wa msingi kwangu. Sasa mimi ni mtu ambaye nafanya kazi kwa juhudi na maarifa, naweka na kusimamia malengo yangu, nakamilisha mambo niliyofanya na ni mvumilivu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 60 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Akili Ndogo, Akili za Kawaida Na Akili Kubwa.

Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people. -Eleanor Roosevelt

Akili kubwa zinajadili mawazo; akili za kawaida zinajadili matukio; akili ndogo zinajadili watu.

SOMA; UKURASA WA 40; Amua Kuwa Wewe…

Je wewe unajadili nini?

Ukijikuta unajadili watu, fulani kafanya hiki, fulani kafanya kile na mengine mengi ambayo hayawezi kukusaidia jua una akili ndogo. Kwa kutumia akili hii ndogo sahau kabisa kufikia mafanikio makubwa.

Kama muda mwingi unajadili matukio, nini kimetokea, kimetokeaje, kwa nini kimetokea halafu mara nyingi matukio hayana msaada wowote kwenye malengo yako ujue unatumia akili ya kawaida. Na kama tulivyosema, KAWAIDA = HOVYO. Hivyo ukitumia akili ya kawaida unakuwa hovyo.

SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

Kama muda mwingi unajadili mawazo, wazo gani zuri, jinsi gani ya kuboresha wazo lako ni wazo gani linaweza kuendana na mazingira uliyopo, unatumia akili kubwa. Na mafanikio lazima yawe yako kwa sababu mawazo ndio yanaleta mabadiliko.

Kuanzia leo amua kutokujadili watu wala matukio, JADILI MAWAZO.

Nakutakia siku njema.

SOMA; NENO LA LEO; Hapa Ndio Pa Kuanzia, Hasa kwa mwaka 2015…

Friday, February 27, 2015

SIRI YA 34 YA MAFANIKIO; Unakuwa Kile Unachofikiria.

Unapata kile unachofikiri unastahili kupata kwa sababu wengine wanakuona wewe kama unavyojiona mwenyewe. Kama unafikiria wewe ni wa chini, utafanya hivyo hivyo na watu watakuchukulia wewe ni wa chini.
Jinsi unavyofikiri kunaamua jinsi unavyotenda na jinsi unavyotenda kutaamua wengine wakuchukulieje. Jinsi unavyojiheshimu mwenyewe ndivyo na wengine watakavyokuheshimu.

  “Change your thoughts and you’ll change your world.”  - Dr. Norman Vincent Peale

UKURASA WA 58; Usikubali Kubeba Matatizo Ya Mtu.

Unaruhusiwa kumsaidia mtu, na tunahitaji sana kusaidiana ili tuweze kufikia mafanikio.

Lakini kama njia yako ya kumsaidia mtu ni kuyabeba matatizo yake basi unajiandaa kushindwa. Kuna watu wengi sana ambao unahitaji kuwasaidia kiasi kwamba ukitaka kubeba matatizo yao yote maisha yako yatakuwa hovyo sana.

Unapomsaidia mtu, hakikisha maisha yako wewe hayawi hovyo kuliko ya yule ambaye unamsaidia, ikiwa hivyo msaada wako hautakuwa na maana.

SOMA; NENO LA LEO; Huwezi Kuanguka Kama Hutafanya Hivi.

Msaidie mtu kujisaidia mwenyewe, na hii ndio njia bora kabisa. Maana msaada wa mtu unatoka ndani yake kama ataelekezwa na kuongozwa. Ila kama wewe ndio unataka uyabebe matatizo yote utajikuta kwenye wakati mgumu sana.

Kwa mfano una ndugu yako ambaye ni mlevi sana na kila akipata fedha analewa mpaka anakuwa hajitambui. Halafu akimaliza fedha zote anakuwa na maisha magumu sana kiasi cha kutia huruma. Je ukitaka kumsaidia utampa fedha? Fanya hivyo kununua matatizo zaidi, maana kwanza atakutegemea wewe moja kwa moja wka fedha na utaongeza tabia yake ya ulevi. Fikiria njia bora zaidi.

SOMA; NENO LA LEO; Hiki Ndio Chanzo Cha Furaha.

Hivyo usikimbilie tu kutoa msaada hakikisha msaada huo unakuwa wa maana kwa watu wote wanaohusika.

TAMKO LA LEO;

Niko tayari kuwasaidia watu wanaonizunguka ila sipo tayari kubeba matatizo yao. Kwa kuwa kama na mimi nitakuwa kwenye matatizo hakuna atakayeweza kumsaidia mwenzake. Nitahakikisha namsaidia mtu kujisaidia mwenyewe.

Tukutane kwenye ukurasa wa 59 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; KURASA YA 01; Maisha Unayoishi Ni Yako.

NENO LA LEO; Vitu VIWILI Ambavyo Tayari Unavyo Na Vinavyoweza Kukufikisha Popote Unapotaka KWENDA.

You have brains in your head, and feet in your shoes. You can steer yourself any direction you choose.” Dr. Seuss

Una ubongo kwenye kichwa chako na una miguu kwenye viatu vyako. Unaweza kuenda uelekeo wowote unaochagua.

Tumia akili yako vizuri, kuwaza na kujua ni kitu gani hasa unachotaka kwenye maisha yako.

Tumia mwili wako kukuwezesha kufikia kile unachokitaka.

Kutumia kimoja pekee hakuwezi kukupatia matokeo mazuri, unahitaji kutumia vyote viwili.

SOMA; NENO LA LEO; Umuhimu Wa Kuchepuka…

Na popote unapoelekea sasa ndiko ulikochagua kwenda, hata kama hukuchagua mwenyewe basi umejikuta umeshachaguliwa na wewe unaenda tu.

Kama unataka kubadili uelekeo wako na uende kule ambapo ni bora zaidi kwako anza kutumia akili yako vizuri halafu mwili utatekeleza maamuzi ya akili yako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; KURASA YA 01; Maisha Unayoishi Ni Yako.

Thursday, February 26, 2015

UKURASA WA 57; Dunia Haina Usawa…

Kuna wakati ambao utafanya kila unachotakiwa kufanya na kusubiri upate matokeo uliyotegemea kupata ila huyapati.

Unafanya kila kilicho ndani ya uwezo wako, unakazana sana kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa ila mwisho wa siku hupati kile ulichotarajia kupata.

Unapata kilicho tofauti kabisa, au hupati kabisa, au unaishia kupoteza kabisa.

SOMA; Mwalimu Anakusubiri, Chukua Hatua Sasa…

Ndivyo maisha yalivyo.

Unafanya kazi kwa juhudi na maarifa, unajituma sana unatoa msaada wa kutosha kwenye eneo lako la kazi ukitegemea kupewa cheo kizuri ila cha kushangaza cheo anakuja kupewa mtu mwingine.

Unaamua kufanya biashara yako kwa uaminifu mkubwa, unajituma, unakuwa mbunifu ila unaishia kupata hasara na wale unaoona wanafanya hovyo tu wanapata faida.

Katika hali hii usishangazwe au kuacha kufanya unachofanya, endelea kufanya na kuna siku mambo yatakuwa mazuri tu.

SOMA; Tunarudia Makosa Yale Yale…

Nakupa moyo, usiache kile ambacho ni sahihi kwako kufanya, endelea na siku moja dunia haitakuwa na ujanja bali kukupatia kile unachotaka.

Ila kama utakasirika na kuacha kufanya kile kizuri ulichokuwa unafanya, unaharibu nafasi zako zote za kufanikiwa baadae.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba kuna wakati nitafanya kila kilicho ndani ya uwezo wangu ila majibu yatakuja tofauti na ninavyotegemea. Sitokata tamaa wala kuacha kile ninachofanya. nitaendelea kuweka juhudi mpaka pale nitakapopata na hata nisipopata nitaendelea kufanya kile ambacho ni sahihi kwangu kufanya. Kwa sababu haya ndio maisha niliyoamua kuishi.

SOMA; NENO LA LEO; Hiki Ndio Unachohitaji Ili Kufanikiwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 58 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SIRI YA 33 YA MAFANIKIO; Kuwa Mtu Wa Vitendo.

1 – Lenga kile unachoweza kufanya sasa.
2 – Usisubiri mpaka mambo yote yawe sawa. Kufanya ni bora kuliko kusubiri kila kitu kiwe tayari.
3 – Mawazo tu yenyewe hayana thamani. Mawazo yanayofanyiwa kazi yana thamani kubwa sana.
4 – Kama utatenda sasa na kuzikabili hofu zako, hofu zitapotea.
5 – Usisubiri mpaka ujisikie kufanya kitu. Chukua hatua mara moja na utaanza kujisikia kuendelea kufanya.
6 – Usipoteze muda mwingi kujiandaa kufanya kitu, anza kufanya mara moja.

   “Anyone can do nothing.”  - Ruben Gonzalez

NENO LA LEO; Tatizo La Kuwa Na Machaguo Machache.

To the man who only has a hammer, everything he encounters begins to look like a nail. -Abraham Maslow

Kwa mtu ambaye ana nyundo tu, kila kitu anachokutana nacho kinaonekana kama msumari.

Kama unajua kitu kimoja tu, kila tatizo utakalokutana nalo utajaribu kulitatua kw akile unachojua. Na mara nyingi utatuzi wako unaweza kuzaa matatizo mengi zaidi.

SOMA; JICHO KWA JICHO; Tutabaki Na Dunia Ya Vipofu.

Kama ilivyo kwa mtu mwenye nyundo tu kila atakachokutana nacho kitaonekana kama msumari na ataanza kukigonga au kuking’oa.

Jua vitu vingi, kuwa na machaguo mengi na hapa utakuwa na uhuru wa kuamua utumie kitu gani katika hali gani na kitakachokuletea matokeo mazuri.

Nakutakia siku njema, usiwe na nyundo tu.

SOMA; Kama Hutofanya Chochote…

Wednesday, February 25, 2015

Kama Unataka Kuitawala Siku Yako Ya Kesho Fanya Kitu Hiki Kimoja Kesho Asubuhi.

Unapoamka kesho asubuhi, usiamke kwa kujivuta vuta, wala usiamke kivivu vivu wala usianze kufikiria kama uamke au la.
Muda wa kuamka unapofika, LIPUKA kutoka kitandani.
Yaani lipuka kama bomu, na utaianza siku yako ukiwa na hamasa kubwa na nguvu kubwa.
Na kwa kuianza siku yako kwa mlipuko utaishangaza siku na dunia itakuogopa na kukupatia kile unachotaka.
Usiamke tu kinyonge, LIPUKA kutoka kitandani.

USHAURI ADIMU; Kwa Sababu Umelipia Haimaanishi Utumie Yote.

Siku hizi ukinunua kifurushi cha mawasiliano kwenye mitandao ya simu, unapewa meseji 250 kwa siku.
Ukisema utume meseji zote hizi, hata kama utatumia dakika moja kutuma meseji itakuchukua dakika 250 ambazo ni sawa na masaa manne.
Sasa kama utatumia masaa manne kutuma meseji kwa siku kila siku inabidi uwe unafaidika sana na zoezi hilo.
Lakini vinginevyo hutumi meseji zako zote kwa sababu umezilipia, unatuma zile unazohitaji.
Ukienda kula hotelini, mezani utakuta kuna chumvi, iko pale na unaweza kutumia vyovyote utakavyo. Lakini huwezi kuweka chumvi yote kwenye chakula kwa sababu ipo pale na umeshailipia kwenye chakula.
Chochote unachofanya kwenye maisha usifanye kwa sababu kipo, au kwa sababu kila mtu anafanya. Ila fanya kwa sababu ndicho unachohitaji kufanya.
Nakutakia kila la kheri.

SIRI YA 32 YA MAFANIKIO; Zishinde Changamoto.

Watu waliokata tamaa na maisha yao wana kitu kimoja kinachofanana. Wote walikutana na changamoto ambayo iliwafanya waache kile wanachofanya na watakuwa tayari kukuambia ni jinsi gani hali waliyokutana nayo ilikuwa ngumu kwao. Mara zote wanaendelea kulisha hofu zao.
Watu waliofanikiwa wanatenda tofauti wakati wanapokutana na changamoto. Wanaamka, wanajifunza kwa kilichowaangusha , wanasahau kilichotokea na kuendelea kusonga mbele.

   “It’s not what happens to you. It’s how you handle it.”  - Ruben Gonzalez

UKURASA WA 56; Unajaribu Kumdanganya Nani?

Unajua kwamba maisha yako ni yako, na wewe mwenyewe ndio utaishi maisha hayo mpaka utakapokufa, sasa unajaribu kumdanganya nani?

Unajua kabisa kwamba kazi unayofanya huifurahii, kipato unachopata hakikutoshi, lakini unapokuwa na watu unakazana uonekane unafanya kazi muhimu, na inakupa kipato cha kutosha, unajaribu kumdanganya nani?

SOMA; UKURASA WA 18; Hakuna Anayejali Maisha Yako Zaidi Yako Mwenyewe.

Unajua kabisa kwamba biashara unayofanya inakupa changamoto kubwa, unakazana sana lakini faida unayopata ni kidogo, huna mbinu zozote za kubadili hali hiyo lakini unapokuwa na watu unakazana kuwaonesha kwamba biashara yako ni nzuri, unajaribu kumdanganya nani?

Unavaa nguo nzuri, uonekane umependeza. Unakaa na marafiki mnapiga soga, mnakunywa, unatembelea sehemu nzuri na za kifahari lakini ukirudi nyumbani hakuna amani, ukilala usiku bado unajiona ni mpweke, mtupu. Unajaribu kumdanganya nani?

SOMA; Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Martin Luther King

Imetosha sasa, acha kujaribu kudanganya watu, maana ukweli ni kwamba unajidanganya mwenyewe na hali hiyo haitakufikisha mbali. Maisha yako yataendele akuwa magumu na kuigiza kutakuchosha.

TAMKO LA LEO;

Naamua leo kuacha kuendelea kujaribu kuwadanganya wengine na kujidanganya mwenyewe pia. Naamua kuacha kuishi maisha ya maigizo. Naamua kuishi maisha yangu, kufanya kile ambacho napend akufanya, ambacho ni sahihi kwangu na kwa wanaonizunguka. Sitajaribu tena kuwafanya watu wanikubali, maana nitakuwa nawadanganya na kujidanganya mwenyewe.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

Tukutane kwenye ukurasa wa 57 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SIRI YA 31 YA MAFANIKIO; Inuka Ushinde Mbio.

Maisha ni kama mbio ambapo kila siku unakimbia ili kufikia mafanikio.
Katika mbio hizi kuna kuchoka na hata kuanguka.
Haijalishi umeanguka mara ngapi, unahitaji kujikaza na kuendelea na mbio ili uweze kufikia ushindi.

NENO LA LEO; Kitu Muhimu Cha Kununua Kabla Hujanunua Nguo…

"Wear the old coat and buy the new book." - Austin Phelps

Vaa nguo Ya Zamani na nunua kitabu kipya.

Najua hii ni kauli ya tofauti kabisa, ambayo hujawahi kuisikia na wala hukuwahi kudhani utakujakuisikia. Sawa, tayari umeshaisikia na ifanyie kazi.

SOMA; Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.

Wakati wowote unapotaka kununua nguo, kwanza jiulize nina kitabu kipya? Kama huna usinunue kwanza nguo, nunua kitabu.

Kwa sababu unaponunua nguo unakuwa umefanya uwekezaji kidogo sana na ukizingatia tayari unazo nguo nyingi. Ila unaponunua kitabu unakuwa umefanya uwekezaji mkubwa sana ambao utakulipa mara dufu kwa kutumia maarifa uliyojifunza kwenye kitabu hiko.

Weka kipaumbele kwenye kujifunza, maisha yako yatakuwa bora sana.

Nakutakia siku njema.

SOMA; UKURASA WA 45; Uwekezaji Muhimu Kwako Kufanya Na Unaolipa Sana.

Tuesday, February 24, 2015

SIRI YA 30 YA MAFANIKIO; Uaminifu Unalipa Gawio Kubwa.

Watu wasioona mbali hawaelewi kwamba kila wanachofanya kina matokeo yake.
Matendo mazuri yanapewa zawadi na matendo mabaya yanaadhibiwa.
Ni bora kushindwa na ukabaki na heshima kuliko ukafanikiwa huku ukiwa tapeli.

   “To measure a man, measure his heart.”  - Malcolm Forbes

USHAURI ADIMU; Chukua Ushauri Kwa Mtu Huyu Tu, Achana Na Wengine Wote.

MSOMAJI; Nimekuwa nikisoma baadhi ya makala zako. Naomba nikuulize. Je, mtu unapoamua kufanya biashara fulani,ukaomba ushauri kwa watu,hao watu kwa uoga wao wakakuvunja moyo kuwa utakuwa kwenye risk zaidi. Unaionaje hii?asante,naamini utanijibu niweze kuelewa.

MIMI; Usiombe ushauri kwa mtu ambaye hafanyi biashara, atakudanganya. Usiombe ushauri kwa mtu aliyepata hasara kwenye biashara, atakufundisha makosa yake. Omba ushauri kwa mtu anayefanya biashara yenye mafanikio, na mtu huyo awe tayari kutoa ushirikiano.

Moja ya mawasiliano yangu na msomaji leo. Nimeona inaweza kukusaidia na wewe.
Kila la kheri.

UKURASA WA 55; Usikubali Kirahisi…

Maisha yako hivi, unaweza kuwa unahitaji kitu fulani na ili kupata kitu hiko inabidi umwombe mtu mwingine. Unapoendakumwomba mtu huyo anakupa jibu rahisi, HAPANA, HAIWEZEKANI.

Wewe unachofanya ni nini? Unakubali, unarudi nyuma na kuwa shahidi mzuri, kwamba ulijaribu sana, lakini haikuwezekana, uliambiwa hapana, uliambiwa haiwezekani.

Hapo ndio unapokosea, unakubali kirahisi, kwamba hupewi, kwamba haiwezekani, kwamba hutaweza.

SOMA; UKURASA WA 07; Uvumilivu Ni Nguzo Muhimu.

Leo nakwambia acha kabisa kukubali kirahisi. Ni marufuku kukubali majibu rahisi rahisi tu. Kwa sababu mtu amekwambia hawezi kufanya unachomwambia afanye haimaanishi hawezi kweli, huenda hujampa sababu za kutosha kwa nini inabidi afanye hiko unachotaka afanye.

Kwa sababu umefungua biashara na wateja hawanunui haimaanishi biashara yako haina wateja, bali unahitaji kuwashawishi zaidi kuwapa huduma bora zaidi ili waridhike na kile wanachotoa na kile wanachopokea pia.

SOMA; UKURASA WA 47; Kuwa Na Subira, Hakuna Unachopoteza.

Vyovyote vile usikubali majibu rahisi, chimba ndani zaidi, komaa na utaona vikwazo vyote vilivyokuwa vinajitokeza vilikuwa vinakupima tu kama una kiu kweli ya kupata unachotaka.

TAMKO LA LEO;

Sitakubali tena kupokea majibu rahisi na kukubaliana nayo kirahisi. Nitaendelea kushinikiza, nitaendelea kuhoji na nitaendelea kuchunguza mpaka nipate sababu inayonizuia kupata ninachotaka. Kwa sababu najua vikwazo ninavyokutana navyo haviwezi kunizuia kamwe.

Tukutane kwenye ukurasa wa 56 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA

SOMA; Je Upo Tayari Kupata Unachotaka? Siri Ni Hii Moja…

NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Wivu…

Envy is the art of counting the other fellow's blessings instead of your own." - Harold Coffin

Wivu ni sanaa ya kuhesabu baraka za wengine badala ya kuhesabu baraka zako.

Epuka kuwa na wivu, hauwezi kukusaidia bali unakurudisha nyuma.

Wivu unakufanya ujilinganishe na wengine na hatimaye uone wewe huwezi.

Wivu utakukatisha tamaa na kuona wewe ni wa chini.

SOMA; Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.

Na pia usijidanganye, hakuna wivu wa maendeleo au usio wa maendeleo. Wivu ni wivu na ni mbaya kwa mafanikio yako.

Huhitaji kuona wengine wanafanya nini na wewe ufanye ndio useme una wivu wa maendeleo, unahitaji kuwa na malengo yako ambayo unayafanyia kazi kila siku.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Njia KUMI Za Kuboresha Maisha Yako Ya Kibiashara.

Monday, February 23, 2015

SIRI YA 29 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kupata Furaha.

Huwezi kutafuta furaha.
Furaha ni zao la mambo haya matatu;
1. Ubora wa mahusiano yako na wengine.
2. Kiwango cha udhibiti ulionao kwa hisia zako.
3. Jinsi unavyotumia zawadi na uwezo wako katika kutimiza malengo yako.
Kama unataka kuwa na furaha fanya kazi ya kuboresha mahusiano yako, dhibiti hisia zako na yafanyie kazi malengo yako kwa akili zako na moyo wako wote.

  “Satisfaction lies in the effort, not in the attainment.  Full effort is full victory.”  - Mohandas Gandhi

UKURASA WA 54; Kufa MTUPU….

Moja ya njia zitakazokuwezesha kufanya kazi iliyobora kwa wakati ambao bado unaishi hapa duniani ni kupanga kufa MTUPU.

Kwa lugha ya kiingereza tunasema DIE EMPTY.

Kila mmoja wetu amezaliwa na mziki mzuri sana ambao upo ndani yake. Lakini ni wachache sana ambao wanaweza kuimba mziki huu. Na ninaposema mziki simaanishi mziki wa kuimba bali lile jambo ambalo uko bora kuliko mambo mengine yote.

SOMA; Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…

Hiki ndio kimejaa ndani yako na unatakiw akukitoa bila ya choyo, bila ya kukibania. Kwa sababu huna sehemu nyingine ya kwenda kukitoa tena zaidi ya hapa duniani. Na huna wakati mwingine wa kukitoa zaidi ya leo, zaidi ya sasa.

Hakikisha unajikamua mpaka tone la mwisho la ubora wako. Kama umewahi kuona jinsi ambavyo mtu anakamua juisi ya miwa, ndivyo unavyotakiwa kufanya kwako binafsi.

Na uzuri wetu binadamu ni kwamba jinsi unavyojikamua ndivyo unavyozidi kutoa ubora zaidi.

SOMA; Hatua TANO Za Kuongeza Uzalishaji Wako Ili Kufikia Mafanikio.

Usikubali kufanya tu kazi ya kawaida wakati unaweza kuwa bora zaidi. Usikubali tu kufanya biashara ya kawaida wakati unaweza kuwa bora sana. Mara zote pigania kuwa bora, kwa sababu una uwezo huo na amua kufa MTUPU, uache ubora wote kwa faida ya dunia na vizazi vijavyo.

TAMKO LA LEO;

Naamua kufa MTUPU. Sitaibadia dunia hii ubora ambao upo ndani yangu. Sitaki kuondoka na mziki wangu ukiwa haujachezwa hapa duniani. Chochote ninachofanya nitakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana, kwa ubora wa kiwango cha daraja la kwanza. Kama ambavyo haijawahi kufanywa na mwingine yeyote duniani. Kwa sababu mimi ni wa pekee.

Tukutane kwenye ukurasa wa 55 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA

SOMA; Weka Pamoja Vitu Hivi Vitatu Na Tayari Wewe Ni Mjasiriamali Mwenye Mafanikio Makubwa.

NENO LA LEO; Vitu Vitatu Muhimu Kwenye Maisha Yako.

"In the end, just three things matter: How well we have lived How well we have loved How well we have learned to let go." - Jack Kornfield

Mwishoni vitu vitatu tu ndio vitakuwa muhimu: Jinsi gani ulivyoishi. Jinsi gani ulivyowapenda wengine. Jinsi gani ulivyoweza kukubali mambo yapite.

Maisha unayoishi mwisho wa siku hayatahesabiwa kwa fedha utakazokuwa nazo au magari utakayokuwa nayo.

Maisha yako yatahesabiwa kwa vipengele hivyo vitatu.

SOMA; Siri Kubwa Unayotakiwa Kujua Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara.

Na pia ni vipengele hivi vitakufanya uone maisha yako yamekuwa ya thamani.

Anza leo kuishi maisha yako na uache kujianda akuishi maana siku zinakwenda sana na muda haukusubiri.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Sunday, February 22, 2015

UKURASA WA 53; Hakuna Kinachodumu Milele…

Moja ya siri kubwa unayopaswa kuijua ili kupata uhuru kwenye maisha ni kwamba hakuna kinachodumu milele.

Kama vile ambavyo sisi binadamu hatutadumu milele, siku moja utafikia mwisho, utakufa. Ndivyo ilivyo kwa kila kitu kwenye maisha, kuna wakati kitafika mwisho.

SOMA; Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo..

Matatizo uliyonayo hayatadumu milele, kuna wakati yatafika mwisho, labda wewe mwenyewe uamue kutafuta matatizo mengine tena.

Hata kazi unayofanya sasa haitadumu milele, kuna siku itafika mwisho, utafukuzwa, kupunguzwa au kustaafu.

Biashara unayofanya sasa, hautaendelea kuifanya hivyo hivyo milele. Mambo yatabadilika na kama wewe hutabadilika utaachwa nyuma.

Mafanikio uliyonayo sasa hayatadumu milele, unahitaji kujifunz ambinu za kuendelea kuyaongeza kila siku.

Kwa kujua kwamba hakuna kidumucho milele, unaweza kujiandaa kwa nyakati ambazo ulichonacho sasa hakitakuwepo. Kushindwa kujiandaa ndio unajikuta kwenye wakati mgumu, kwenye matatizo makubwa.

SOMA; Ukurasa Wa 03; KIFO…(Umuhimu Wake Na Jinsi Unavyoweza Kukitumia Kufikia Mafanikio)

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba hakuna kidumucho milele, kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Nitajiandaa vizuri kwa vile vitu ambavyo nahitaji kuendelea kuwa navyo ili visiondoke na nikabaki na matatizo. Pia nitahakikisha vile nisivyotaka vinafika mwisho wake na sivitafuti tena.

Tukutane kwenye ukurasa wa 54 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

NENO LA LEO; Kama Hufanyi Makosa Hii Ndio Maana Yake.

If you're not making mistakes, then you're not doing anything. -John Wooden

Kama hufanyi makosa maana yake hufanyi chochote.

SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.

Katika jambo lolote ambalo utafanya, huwezi kukwepa kufanya makosa. Hasa pale ambapo unafanya mambo mapya, makosa huwa makubwa sana.

Hivyo usiogope pale unapojikuta unafanya makosa, bali jua ya kwamba kuna mambo mapya unayofanya na unajifunza ni kipi hutakiwi kufanya.

Kama ungekuwa huogopi kukosea, kama ungekuwa huogopi kushindwa, je ungekuwa umekamilisha mangapi? Ungekuwa unafanya nini sasa? Anza kufanya.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Saturday, February 21, 2015

SIRI YA 28 YA MAFANIKIO; Tabia Zako Zitakujenga Au Kukubomoa.

Tabia zako zitakupeleka kwenye mafanikio au kushindwa. Ndio maana kuchangamana na washindi na kusoma vitabu vizuri ni muhimu sana. Kwa sababu unakuwa na tabia za watu unaokaa nao muda mrefu. Unaiga tabia zao. Na tabia ndio zinaamua mafanikio yako.

  “The books you read and the people you meet will determine  where you are in five years.”  - Charlie “Tremendous” Jones

SIRI YA 27 YA MAFANIKIO; Amua Kujiendeleza Kila Siku.

Watu waliofanikiwa sana kwenye kila eneo ni watu wanaojifunza kila siku na kila mara. Mara zote wanasoma vitabu, kusikiliza vitabu vya kuwaelimisha na kuhudhuria semina.
Wanajua kwamba kama wakijifunza na kutumia yale waliyojifunza wanazidi oiuwa bora zaidi ya wale wanaoshindana nao.
Kama utatumia dakika 15 mpaka 30 kwa siku kujisomea, baada ya muda utakuwa mtaalamu uliyebobea.
Wekeza kwako mwenyewe na utaongeza kipato chako mara dufu.

“You are what you are and where you are because of what’s gone into your mind. You can change what you are and where you are by changing what goes into your mind.” - Zig Ziglar

SIRI YA 26 YA MAFANIKIO; Mara Zote Weka Malengo.

Dhumuni la malengo ni kutupa umakini na mwelekeo. Akili yako haiwezi kukutafutia majibu kama haijawekwa kwenye uelekeo husika. Pale unapokuwa na malengo thabiti miujiza inatokea. Unaanza kupokea mawazo na fikra zinazokufikisha kwenye lengo lako.
Maisha bila malengo yanakera. Maisha yenye malengo ni kama safari nzuri.
Andika malengo yako kila siku asubuhi. Hiki ni kitendo cha kujitoa kinachokuandalia mazingira mazuri ya kuanza siku ya uzalishaji mkubwa.

“The world has the habit of making room for the man whose words and actions show that he knows where he is going.” - Napoleon Hill

Sababu Namba Moja Kwa Nini Hufanikiwi Kwenye Kazi Unayofanya.

Sababu namba moja kwa nini hufanikiwi kwenye kazi unayofanya ni kwa sababu unaangalia fedha tu.
Yaani wewe kinachokusukuma ufanye kazi ni kwa sababu unapata fedha.
Sasa fedha inapokuwa ndio hamasa kwako utafanya kile tu ambacho kinakuletea fedhq, hutataka kwenda hatua ya ziada na hivyo kujinyima fedha nyinhi zaidi baadae.
Ufanyeje sasa?
Hamasa yako kubwa isiwe fedha bali iwe mapenzi ya dhati kwa kile unachofanya.
Penda sana kile unachofanya na kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.
Kuwa mbunifu na mara zote penda kwenda hatua ya ziada.
Kwa hali hii fedha zitakuja mpaka utashangaa zilikuwa zimejificha wapi. Amini hilo, nakuambia kwa uzoefu.

Do not hire a man who does your work for money, but him who does it for love of it.—Henry David Thoreau,

UKURASA WA 52; Epuka Miluzi Mingine…

Waswahili wanasema miluzi mingi humpoteza mbwa.

Hii sio kweli kwambwa tu, ni kweli hata kwa sisi binadamu.

Kelele nyingi zitakupoteza, achana nazo.

Dunia ina kelele nyingi sana, ambazo unaweza kutamani kuzifuatilia, kujua zaidi kuhusu kelele hizo.

Ila huu wote ni upotevu wa muda, kelele hizi hazina msaada wowote kwa wewe kufikia malengo yako.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

Ukishajua malengo yako ni nini, peleka nguvu zako zote kufanikisha malengo hayo. Kufuatilia mambo mengine yasiyo ya msingi kunakupunguzia wewe kasi ya kufikia malengo uliyojipangia.

Acha sasa kufuatilia mambo yasiyo ya msingi, acha kufuatilia udaku, acha kufuatilia umbea, acha kufuatilia habari yoyote ambayo haikuongezi wewe maarifa ya kufikia unachotaka au huwezi kuiathiri kwa njia yoyote ile.

SOMA; Hizi Ndio Siri 21 Za Mafanikio

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba miluzi mingi humpoteza mbwa. Naelewa kwamba dunia imejaa kelele nyingi zinazinitamanisha kuzifuatilia na kuacha lengo langu kuu kwenye maisha. Kuanzia sasa napuuza kelele hizi, napuuza habari zote ambazo haziwezi kunisaidia au siwezi kuziathiri.

Tukutane kwenye ukurasa wa 53 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

NENO LA LEO; Bado Hujachelewa…

It's never too late - never too late to start over, never too late to be happy. -Jane Fonda

Hakuna wakati ambao unakuwa umechelewa, hujachelewa kuanza tena, hujachelewa kuanza kuwa na furaha.

SOMA; Siri Moja Kubwa Ya Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Kwenye maisha hakuna kuchelewa ila pale unapojua unachotaka ndio wakati huo huo unahitaji kuchukua hatua.

Kama umepata habari za ukombozi wa maisha yako leo, usiseme umechelewa bali chukua hatua leo ili kesho yako iwe bora zaidi.

Unaposhindwa kuchukua hatua pale ambapo unajua ni nini cha kufanya ndio unakuwa umejichelewesha mwenyewe.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…

Friday, February 20, 2015

SIRI YA 25 YA MAFANIKIO; Ni Lazima Upande Kabla Hujavuna.

Ni lazima upande mbegu kabla ya kuvuna mazao.
Unavyopanda mbegu nyingi zaidi ndivyo unavyovuna mazao mengi zaidi.
Ukipanda mbegu kiganja kimoja, utavuna gunia moja, ukipanda bakuli moja utavuna magunia kumi. Mara zote unavuna zaidi ya unachopanda.
Usihukumu kila siku kwa mavuno unayopata, bali hukumu kwa mbegu unazopanda.
Je wewe unapanda mbegu gani? 

   “The man who will use his skill and constructive imagination to see how much he can give for a dollar, instead of how little he can give for a dollar, is bound to succeed.”  - Henry Ford

SIRI YA 24 YA MAFANIKIO; Fanya Licha Ya Kuwa Na Hofu.

Kama utasita kwa sababu ya hofu, hofu itaendelea kukua.
Kama utafanya kile unachohofia hofu itapotea yenyewe. Kwa sababu hofu ni hali ya akili. Ni kama moshi tu.
Usikubali hofu ikutawale. Itokomeze hofu kwa vitendo.
Ujasiri ni kuweza kufanya licha ya kuwa na hofu. Woga ni kukimbia hofu zako.
Je wewe unataka nini? Kuwa jasiri au kuwa mwoga? Uchaguzi ni wako.

“You gain strength, courage, and confidence by every experience in which you really stop to look fear in the face…The danger lies in refusing to face the fear, in not daring to come to grips with it… You must make yourself succeed every time. You must do the thing you think you cannot do. - Eleanor Roosevelt

UKURASA WA 51; Uadilifu, Kioungo Muhimu Cha Kufikia Mafanikio.

Viungo vingine muhimu sawa na uadilifu ni KUFANYA KAZI KWA BIDII NA MAARIFA na UAMINIFU. Ukibonyeza hizo hapo chini unajifunza zaidi kuhusu viungo hivyo viwili.

SOMA; UKURASA WA 06; Kazi Ndio Msingi Wa Maendeleo.

SOMA; UKURASA WA 38; Uaminifu, Kitu Muhimu Kitakachokuwezesha Kupata Unachotaka.

Uadilifu ni kiungo muhimu sana cha wewe kuweza kufikia mafanikio katika jambo lolote unalolifanya. Kukosa uadilifu ni hatari kubwa sana kwenye maisha yako. Hii ni kwa sababu hata ukifanya kazi kwa juhudi kiasi gani unajikuta unaingia kwenye matatizo au huoni mafanikio yoyote.

Uadilifu ni pale ambapo wewe mwenyewe unakuwa na misingi yako uliyojiwekea na kuisimamia kwenye kila jambo na kila wakati. Uadilifu ni pale ambapo unafanya jambo kwa manufaa ya wengi na sio kwa manufaa yako tu.

Kama hujui uanzie wapi kuwa mwadilifu basi anza kuishi kauli hii; USIMFANYIE MWINGINE KILE AMBACHO HUNGEPENDA KUFANYIWA.

Watu wengi ambao wanaingia kwenye matatizo, watu wengi ambao wanatapeliwa, watu wengi ambao wanaua na kuuawa ukichunguza vizuri matatizo yote yanaanzia kwenye uadilifu.

Kuwa mwadilifu, weka mising yako na isimamie.

SOMA; Mwongozo Wa Kujijengea Misingi Yako Ya Kimaisha Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

TAMKO LA LEO;

Najua UADILIFU ni kiungo muhimu sana kwangu kufikia mafanikio. Najua kwa kukosa uadilifu hata nikiweka jitihada kiasi gani nitaendelea kuingia kwenye matatizo makubwa zaidi. Kuanzia leo naishi kwa kauli hii; SITAMFANYIA MTU MWINGINE KILE AMBACHO MIMI SIPENDI KUFANYIWA. Na kazi au biashara yoyote nitakayoifanya itakuwa ya kuwanufaisha wote wanaohusika nayo na sio kuninufaisha mimi tu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 52 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Pale Unapoona Mambo Hayaendi Fanya Hivi.

“When life's problems seem overwhelming, look around and see what other people are coping with. You may consider yourself fortunate.” Ann Landers

Pale matatizo ya maisha yanapoonekana kukulemea, angalia wengine wanakazana kufanya nini na maisha yako. Unaweza kujiona mwenye bahati.

Unaweza kulalamika huna viatu lakini utakapokutana na mtu ambaye hana miguu hali yako utaiona sio mbaya kama unavyofikiri.

Swala sio wewe upate faraja kwamba kuna watu wana hali mbaya kuliko wewe, bali kuona kwamba maisha yako bado yana thamani kubwa.

SOMA; #HADITHI_FUNZO; Mbinu Rahisi Iliyomwezesha Jenerali Kushinda Vita Ngumu.

Haijalishi unapitia magumu kiasi gani, kuna njia ya kutokea. Ukiacha kuangalia matatizo yako na kuumia nayo utaweza kuona njia hiyo na kuweza kuitumia vizuri.

Pia ukijua kwamba wengine wanapitia kama unayopitia na wanaweza kupambana nayo na kusonga mbele unapata hamasa ya wewe kuendelea kupambana.

Nakutakia siku njema.

SOMA; SIRI YA 4 YA MAFANIKIO; Itumie Sheria Ya Wastani Kukuletea Mafanikio.

Thursday, February 19, 2015

SIRI YA 23 YA MAFANIKIO; Kama Una Matumaini Ya Baadae Una Nguvu Leo.

Matumaini yanaona visivyoonekana na kufanikisha visivyowezekana.
Napoleon alisema kwamba kazi ya kwanza ya kiongozi ni kuwapa watu wake matumaini.
Kwa sababu watu wanapokuwa na matumaini, watapigania ndoto zao. Na wanapokosa matumaini wanakata tamaa.
Zungukwa na watu ambao wanakutia moyo, watu watakaopanda matumaini na imani ndani yako na utaweza kuwa chochote unachotaka kuwa.

   “Faith is to believe what we do not see; and the reward of this faith  is to see what we believe.”  - Saint Augustine   

SIRI YA 22 YA MAFANIKIO; Ongeza Kazi Yako Ya kushindwa na Utaongeza Mafanikio Yako.

Watu waliofanikiwa wanakubali kushindwa kama sehemu ya maisha na wamaamua kutymia kushindwa kwao ili kufanikiwa.
Wanaangalia kila kikwazo kama somo la kujifunza ili kufanikiwa.
Wanaelewa kwamba kushindwa ni sehemu ndogo katika mchakato wa kufikia mafanikio na hawakubali iwe kikwazo kwao kufikia mafanikio.  

“Failure is only the opportunity to more intelligently begin again.”  - Henry Ford

Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.

Naweza kusema sasa hivi nimekuwa mlevi wa kitu kimoja, kusoma. Na sio kusoma tu, bali kusoma vitu vizuri ambavyo vinanifanya kuwa tofauti, kufikiri tofauti na hata kupata maarifa zaidi.

Naweza kusema kw akujivunia kwamba chochote ninachofanya sasa kinatokana na maarifa makubwa ninayoyapata kwa kusoma vitabu. Nasoma vitabu vingi na kwa sasa nasoma angalau vitabu viwili kwa wiki, wiki nyingine nasoma zaidi ya hapo ila nahakikisha kila wiki sishuko chini ya hapo.

Mwaka huu 2015 lengo langu ni kusoma vitabu visivyopungua 150, ukichanganya na vingine zaidi ya 200 nimesoma kwa miaka miwili iliyopita, maarifa yangu yataongezeka maradufu.

Leo siandiki haya kukuonesha kwamba nasoma sana ila nataka nikushirikishe faida kumi ninazozipata kwa kusoma, ukiacha kuongeza maarifa ambacho ndio kila mtu anafikiria.

SOMA; Mambo Yamebadilika, Hatari Sio Hatari Tena, Salama Ndio Hatari...

1. Burudani.

Kusoma ni burudani na ni burudani ambayo haina madhara yoyote kwenye mwili wako au maisha yako. Kuna baadhi ya vitabu unapovisoma unapata hisia nzuri za kiburudani na unaona uzuri na utamu wa maisha.

2. Kuhamasika.

Tunaishi kwenye dunia ambayo inakatisha tamaa sana. Kila jambo ambalo unajaribu kufanya kuna watu watakuambia haiwezekani au kuna watu watajaribu kukuwekea vikwazo. Unapokuwa unasoma vitabu unapata hamasa kubwa sana ya kufanya kile unachotaka kufanya. Unaposoma maisha ya wengine na kuona jinsi walivyopitia magumu, unapata moyo kwamba inawezekana.

SOMA; USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

3. Mshauri(mentor)

Ni muhimu sana kuwa na mshauri wako, ambaye anakuonesha wapi pa kupita ili uweze kupata kile unachotaka. Mara nyingi mshauri huyu inabidi awe ameshapitia unakopitia wewe. Katika mazingira yetu ya kitanzania ni vigumu sana kupata mtu wa aina hii, na hata ukimpata anaweza asipate muda mwingi wa kwenda na wewe sawa. Ila vitabu, vitabu ni mentor mzuri sana. Unaweza kusoma maisha ya watu ambao wamefanikiwa kwenye kile unachofanya na wakakupa mwongozo mzuri sana.

4. Kuwa bora zaidi.

Licha ya kuongeza tu maarifa, kusoma kuna kufanya unakowa bora zaidi katika kila eneo la maisha yako. Kabla sijajingea tabia ya kujisomea nilikuwa mtu wa kuhukumu, kukwazika, kuchukia, kubishana na mengine mengi. Lakini yote hayo nimeyaacha sasa, sina tena muda wa kuhukumu kwa sababu najua kila mtu ana matatizo yake, kila mtu anachagua maisha yake. Sikwaziki tena wala kukasirishwa na mtu kwa sababu najua anayetaka kukukasirisha anataka na wewe uwe na matatizo kama aliyonayo yeye, nishakuwa mjanja, sinunui tena matatizo ya watu. Na kilicho bora zaidi sibishani, zamani nilikuwa nikiwa na wazo langu na mtu akalipinga, nabishana nae mpaka nihakikishe amekubaliana nami, lakini sasa sibishani tena, kwa sababu nimejifunza kama wazo lako ni sahihi huna haja ya kulipigania, maana mwisho wa siku ukweli utashinda. Na kama wazo lako sio sahihi pia huna haja ya kubishana maana hakuna atakayekusikiliza au kujali.

5. Kuishi maisha tofauti tofauti.

Mtu anayesoma vitabu anaishi maisha zaidi ya 1000 kabla hajafa, mtu asiyesoma vitabu anaishi maisha mamoja tu mpaka anakufa. Sasa unafikiri ni yupi ambaye anakuwa na maisha mazuri kati ya hawa wawili? Kitabu kinaweza kukutoa hapa na kukupeleka kwenye mapiramidi ya misri, kikakupeleka marekani, kikakupeleka china na kadhalika.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

6. Kuandika.

Moja ya faida kubwa ninazopata kwa kusoma vitabu ni kuandika. Ndio huwezi kuandika kama husomi, nazungumzia kitu ambacho kinaweza kuwasaidia wengine. Huwa naandika kila siku, zamani ilikuwa maneno 1000 ninapoamka asubuhi lakini sasa ni zaidi ya maneno 2000. Fikiria pale unapohitaji kuandika kila siku, jumatatu mpaka jumatatu, mwaka mzima, ni kazi ngumu eh? Kuna siku naweza kuamka sijisikii kabis akuandika, nachukua kitabu na kuanza kusoma, nusu saa baadae nakuwa nimepata mawazo zaidi ya matano ya kitu ninachotaka kuandika. Mara nyingi mawazo hayo hayatoki kwenye kitabu hiko ninachosoma, ila kile kitendo cha kukaa na kuanza kusoma ni kama milango ya akili inafunguka na kuanza kumwaga mawazo mazuri. Napenda sana hii hali.

7. Kutunza muda.

Unapoanz akujijengea tabia ya kujisomea, moja kwa moja unaanza kujijengea tabia ya kutunza muda. Hutapoteza tu muda na kuona huna cha kufanya kwa sababu muda wote una kitabu cha kusoma. Na pale ambapo una kitu cha kukusukuma umalize kitabu haraka kila dakika chache utakazopata utazitumia vizuri kusoma.

8. Kupunguza gharama.

Unapojijengea tabia ya kujisomea, muda wako mwingi unautumia kusoma hivyo hutapata mawazo ya nifanye nini sasa na kujikuta umeenda kufanya jambo ambalo linakuingiza kwenye gharama ambazo sio za msingi. Naweza kuhitaji kubadili mazingira nikachagua kwenda kwenye hoteli kubwa, nikiwa na kitabu nasoma, naagiza maji ya kunywa. Natulia na kusoma hata kwa masaa mawili bila ya kufanya kingine chochote. Ila ukiend akwenye hoteli ya aina hii na huna kitu cha muhimu cha kufanya, utajikuta unatumia gharama kubwa sana.

SOMA; Acha Kuifanya Hali Mbaya Kuwa Mbaya Zaidi.

9. Kuepuka umbea na majungu.

Angalau watanzania tumebobea kwa hili. Kama unapenda kufuatilia umbea na majungu sikulaumu kwa sababu kama huna kingine cha kufanya utafanya nini sasa? Yaani umeamka asubuhi huna ratiba yoyote ya siku zaidi ya kwenda kazini kama ulivyoenda jana. Utaanza kuangalia I nini kinaendelea, Diamond ana mpenzi gani mpya, kampa mimba nani, kavaa viatu vya shilingi ngapi au valentine alitumia kiasi gani cha fedha. Sawa, sikukatazi kufuatilia, ni burudani, lakini kabla ya kuipa burudani hii kipaumbele je maisha yako umeyapa kipaumbele?

10. Kuongeza kipato.

Hii ipo karibu sana na kupata maarifa maana maarifa ndio yanafanya kipato chako kuongezeka. Lakini nimetaka niiweke yenyewe ili kuonesha msisitizo zaidi. Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, nilisoma kitabu cha Robin Sharma, na moja ya vitu alivyoshauri ni hiki; KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA MBILI, ONGEZA KUSOMA KWAKO MARA TATU. Nikasema nafanyia kazi hilo, kadiri ninavyojisomea ndivyo kipato changu kinaongezeka, mpaka wakati mwingine nashangaa nilichelewa wapi sikuanza mapema kama miaka kumi iliyopita.

Hizo ndio faida kumi za kujijengea tabia ya kujisomea. Anza kujisomea leo, na utaanza kunufaika na hayo na mengine mengi ambayo sijayaandika hapa. Nina uhakika na haya ninayokuambia hapa, hebu anza kufanya na lazima utaona mabadiliko.

SOMA; Habari Za Kusikitisha; Kila Kitu Kinabadilika…

KARIBU KWENYE KUNDI LA KUJISOMEA;

Kama unataka kujijengea tabia ya kujisomea na ungependa kupata kitu cha kukusukuma uweze kusoma nakukaribisha kwenye kundi la kusoma vitabu. Kundi hili linaitwa VORACIOUS READERS, katika kundi hili tunasoma vitabu viwili kwa wiki na ni muhimu kila mwanachama kusoma na kujadili angalau kitabu kimoja. Kupata maelezo zaidi ya kundi hili bonyeza maandishi haya.

MUHIMU; Usitake kujiunga na kundi hili kwa sababu tu umehamasika, ni muhimu sana utenge muda wa kujisomea na usome kweli, usipofanya hivyo unaondoka kwenye kundi.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

TUPO PAMOJA.

UKURASA WA 50; Njia Mbili Za Kukuondolea Matatizo Yako Ya Kifedha.

Tunaweza kusema matatizo yote duniani chimbuko lake ni fedha. Au kama sio yote basi sehemu kubwa ya matatizo inaanza na matatizo ya fedha.

Sina haja ya kurudia hapa kusema kwa nini fedha ni muhimu, kila mtu anajua na ndio maana tunaitafuta kwa nguvu.

Pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuongeza elimu na hata kulalamika na kugoma bado watu wanajikuta kwenye matatizo ya kifedha kila siku. Haijalishi umri au uzoefu, mtu aliyepo kazini mwaka mmoja na aliyepo kazini miaka kumi wote wana matatizo ya kifedha.

Hii fedha ni mdudu gani ambaye anamshinda kila mtu?

Leo tunajifunza mbinu mbili za kuondokana na matatizo ya kifedha.

Mbinu ya kwanza; tumia pungufu ya kipato chako. Yaani kama kipato chako ni laki moja basi hakikisha hutumii yote.

Mbinu ya pili; Weka akiba. Unapotumia chini ya kipato chako kile ambacho hutumii unaweka akiba, halafu unawekeza hii akiba ili iweze kukuzalishia zaidi.

SOMA; Maazimio Matano Muhimu Ya Fedha Kwa Kila Kijana Kuweka Mwaka Huu 2015.

Ni rahisi kama hivyo, lakini kwa nini watu wengi hawawezi kufanya?

Kwa sababu wanakubali kipato chao ndio kipange matumizi, yaani kipato kikiongezeka na matumizi yanaongezeka. Na pia wanasubiri watumie halafu kitakachobaki ndio waweke akiba, matumizi hayaishi.

TAMKO LA LEO;

Najua ili niweze kupata uhuru wa kifedha nahitaji kuanza kuujenga mwenyewe. Nitaujenga uhuru huu kwa kuongeza kipato changu, kuweka akiba nakuwekeza akiba hii. Kila kipato nitakachopata, sehemu fulani nitaweka akiba. Na baada ya muda akiba hii nitaiwekeza ili iweze kunizalishia zaidi.

SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.

Tukutane kwenye ukurasa wa 51 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kama Bado Hujaipata Fursa Fanya Hivi…

”If opportunity doesn’t knock, build a door” Milton Berle

Kama bado fursa haijagonga hodi, tengeneza mlango.

Unaweza kuwa unalalamika kwamba fursa haijaginga hodi kwako, kumbe huna hata mlango wa kutoa nafasi kwa fursa hiyo kugonga. Hivyo acha kulalamika na tengeneza mlango ambapo fursa itagonga.

SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.

Fanya maamndalizi ambayo yatakuwezesha kutumia fursa  mbali mbali zinazokuzunguka.

Tatizo sio uhaba wa fursa, fursa zipo nyingi sana, swali ni je umejiandaa kuzitumia?

Fanya maandalizi, tumia fursa, boresha maisha yako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Maswali Matatu Muhimu Ya Kujiuliza Kwenye Wazo Lako La Biashara.

Wednesday, February 18, 2015

SIRI YA 21 YA MAFANIKIO; Tegemea Kilicho Bora.

Pale unapoamini jambo linawezekana na kulifanyia kazi ipasavyo, dunia yote itakusaidia kufanya ndoto zako, malengo yako na mipango yako kuwa kwenye uhalisia.
Wale wanaoshinda ni wale wanaofikiri wanaweza.
Amini unaweza, tegemea makubwa, yafanyie kazi na utayapata.

  “If you paint in your mind a picture of bright and happy expectations, you put yourself into a condition conductive to your goal.”  - Norman Vincent Peale

UKURASA WA 49; Uelekeo Ni Muhimu Kuliko Mwendo Kasi..

Kama hujui unakokwenda, kuongeza mwendo hakutakufikisha unakotaka kufika.

Kuongeza mwendo kutazidi kukupoteza, kukupeleka mbali zaidi na huenda ukawa mbali zaidi na unakotaka kufika.

Hivyo jukumu lako kubwa kwenye maisha sio kuongeza mwendo bali kujua kwanza unakokwenda ni wapi.

SOMA; Sababu 5 Kwa Nini Ni Marufuku Wewe Kukata Tamaa.

Ukishajua unakokwenda ni wapi, hapo ndio unapoweza kuongeza mwendo na ukaweza kufika pale.

Ila kwenye maisha watu wengi wanaongeza mwendo bila ya kujua uelekeo wao na hivyo kujikuta wanapotea zaidi.

Unaanza kufanya kazi ambayo hujaiwekea malengo, unapofika katikati unapotea. Unapoongeza juhudi na maarifa kwenye kazi hiyo unazidi kupotea, unazidi kuharibu.

SOMA; Mambo 5 Muhimu Ya Kufanya Kabla Hujalala Leo.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba uelekeo ni muhimu zaidi kuliko mwendo kasi. Mara zote nitahakikisha nipo kwenye uelekeo sahihi wa kufikia malengo yangu kabla sijaongeza mwendo. Maana kwa kuongeza mwendo bila ya kujua uelekeo ni kuendelea kupotea zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 50 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Biashara 5 Unazoweza Kuanza Kufanya Bila Ya Kuwa Na Mtaji.

NENO LA LEO; Kitu Muhimu Zaidi Kwenye Maisha…

“The most important thing in life is not to capitalise on your successes - any fool can do that. The really important thing is to profit from your mistakes”. William Bolitho

Kitu muhimu zaidi kwenye maisha sio kunufaika na mafanikio yako, hata mjinga anawea kufanya hivyo. Kitu muhimu kweli ni kunufaika na makosa yako.

Unapofanya makosa, unaweza kuchagua yakurydishe nyuma au yakusogeze mbele.

Ukishaweza kutumia makosa yako kusonga mbele, kupata mafanikio zaidi hapa ndio umekomaa kweli kuweza kufikia mafanikio.

SOMA; Ushauri Kwa Wajasiriamali Kutoka Kwa Mwanzilishi Wa Facebook.

Wanasema ubora wa nahodha haupimwi kwa utulivu wa bahari.

Wakati mambo ni mazuri kila mtu anaweza kufanya vizuri. Mambo yanapokuwa mabaya ndio wale hasa waliojipanga kweli kufanikiwa wanapoonekana.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Mambo 10 Unayotakiwa Kujua Kuhusu Uwekezaji.

Tuesday, February 17, 2015

SIRI YA 20 YA MAFANIKIO; Iendee Dhahabu...

Watu waliofanikiwa sana sio watu wanaokubali kuwa kawaida. Hawakubali kuwa bora wa piku.
Hawaridhishwi na kufanya vitu kama kila mtu anavyofanya.
Washindi siku zote wanaongeza kiwango chao.
Wanataka kufanikiwa zaidi na wanataka kila wanachofanya kuwa cha daraja la kwanza.
Wanakwenda hatua ya ziada.
Wanaweka jitihada zisizo za kawaida kwenye kile wanachofanya.
Wanafanya kila kitu kwa ubora na wanajijengea sifa ambayo inawapeleka juu zaidi.

  “The kind of people I look for to fill top management spots are the eager beavers, the mavericks. The guys who try to do more than  they’re expected to do. They always reach.”  -Lee Iacocca

UKURASA WA 48; Ni Marufuku Kubadili Lengo…

Kuna usemi unakwenda, ujinga ni kufanya jambo lile lile na kw anjia ile ile halafu ukategemea majibu tofauti.

Yaani kama unalima shamba lako na unapanda mbegu fulani na kutumia mbolea fulani na ukanyeshea vizuri, kama usipopata mazao mazuri, hata wakati mwingine ukilima hivyo hivyo utapata kama ulivyopata.

SOMA; UKURASA WA 20; Geuza Changamoto Kuwa Fursa.

Kama unafanya kile kitu ulichopanga lakini bado hupati majibu unayotarajia, kuendelea kufanya hivyo hivyo ni vigumu kupata kile unachotaka. Kwa maana hiyo ni kwamba kuna vitu ambavyo unatakiwa kubadili.

Ila ni marufuku kubadili lengo lako kuu unalofanyia kazi kwenye maisha. Badili njia unazotumia kufikia lengo lako, ila usibadili lengo.

Kukubali kubadili lengo maana yake umekubali kushindwa na hata utakapokwenda kuanza lengo jingine itakuwa rahisi kwako kuliacha pia.

Changamoto hazikosekani kwenye jambo lolote unalotaka kufanya, ila ukikubali zikufanye uache kile unachotaka utashindwa katika kila jambo unalofanya kwenye maisha yako.

SOMA; UKURASA WA 42; Usitafute Sababu, Chukua Hatua…

TAMKO LA LEO.

Najua kwamba kuna wakati mambo hayatakwenda kama nilivyopanga. Katika wakati huu nitabadili mbinu ninazotumia, ila sitabadili lengo langu kubwa kwenye maisha.

Tukutane kwenye ukurasa wa 49 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Furahia Kupingwa…

“Great spirits have always encountered violent opposition from mediocre minds”. Albert Einstein

Mawazo makubwa mara zote hukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mawazo ya kawaida(hovyo).

SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

Usiogope pale unapofanya jambo ambalo wewe unajua ni sahihi ila kuna watu wengi wanakupinga au wanakukatisha tamaa.

Jua kwamba wewe unaona mbali zaidi yao, unafikiria makubwa zaidi yao na utafikia mafanikio makubwa zaidi yao.

Ila ukikubaliana nao, utaendelea kuwa kama wao, utakuwa kawaida na kama tulivyosema maana ya kawaida ni hovyo, basi utakuwa hovyo.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.

Monday, February 16, 2015

UKURASA WA 47; Kuwa Na Subira, Hakuna Unachopoteza.

Wenye busara walisema; haraka haraka haina baraka.

Hawakuishia hapo, waksema tena, pole pole ndio mwendo.

Lakini dunia ya sasa inatufanya tuone tuna busara zaidi, kwamba hatuna muda wa kusubiri, nataka hiki na nakitaka sasa hivi. Huku ni kujidanganya.

Kwa sababu mwaka huu 2015 umeamua kubadili maisha yako haimaanishi utaanza kuona matokeo mara moja, itakuchukua miezi na hata miaka ndio uone kile ambacho unakitaka.

SOMA; UKURASA WA 07; Uvumilivu Ni Nguzo Muhimu.

Usilazimishe mambo, kwa kufanya hivyo utajiondoa kabisa kwenye njia inayokupeleka kwenye mafanikio.

Kama ambavyo mwanamke atachukua ujauzito kwa miezi tisa ndio aweze kuzaa mtoto mwenye afya nzuri na anayeweza kuhimili hali ya dunia. Na kama ilivyo kwmaba huwezi kuharakisha mchakato wote huu wa ujauzito mpaka kupatikana kw amtoto. Ndivyo ilivyo kwmaba mafanikio yanakuja kwa wakati sahihi, kama utaendelea kufanya kile kilicho sahihi bila ya kuacha.

Unahitaji subira kubwa na uvumilivu pia ili uweze kupata unachotaka.

TAMKO LA LEO;

Najua ninahitaji subira ili niweze kupata kile ninachotaka. Najua siwezi kuharakisha sana bila ya kuleta madhara. Nitaendelea kufanya kile ambacho ni sahihi, nitaendelea kuweka juhudi na maarifa, nitaendelea kuwa mwaminifu na nitaendele akupenda kile ninachofanya. Kwa kufanya hivi bila kuchoka najua ya kwamba mafanikio yatakuja kwa wakati wake yenyewe.

Tukutane kwenye ukurasa wa 48 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…

NENO LA LEO; Faida Tatu Za Kazi…

“Work spares us from three evils: boredom, vice, and need”. Voltaire

Kazi inatuepusha na mambo matatu mabaya; kuchoka kwa kutofanya lolote, maovu na mahitaji.

Unaweza kuona kama kazi ni kitu kibaya sana ambacho kinakutesa.

Na wakati mwingine kutamani kwamba hata kazi zisingekuwepo.

Ila jiulize kama usingekuwa na kazi, usingechoka tu kukaa bila kufanya chochote?

SOMA; Sifa TATU Unazohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Je ungepataje mahitaji yako? Usingeshawishika kuiba au kuchukua vya wengine ili utimize mahitaji yako?

Kazi ni kitu kizuri sana ambacho tunatakiwa kukipenda.

Kwa sababu kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ndio msingi wa maendeleo na mafanikio.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Tabia Mbaya KUMI(10) Zinazopunguza Ufanisi Wako.

Sunday, February 15, 2015

UKURASA WA 46; Kuwa Mtaalamu Uliyebobea..

Katika fani yoyote ile, watu wanaolipwa sana au wanaopata kipato kikubwa ni wale ambao ni wataalamu sana na waliobobea.

Hawa ni watu ambao wamechagua kufanya kitu na kujifunza kuhusu kitu hiko nje ndani.

Wanajua mbinu zote za kuweza kufanya kazi iliyobora na wakitoa kazi yao kila mtu anaifurahia na kuipenda.

Hawa ni watu ambao wakigusa kitu kinabadilika, kama ni jiwe linakuwa dhahabu.

SOMA; UKURASA WA 14; Kataa Kupokea Chochote Kizuri, Na Kubali Hiki…

Hawa ni watu ambao mtu yeyote mwenye shida hafikirii kutafuta mtu mwingine bali wao.

Unapokuwa mtaalamu, unapobobea kila mtu atataka kufanya kazi na wewe, kila mtu atataka kupata huduma au bidhaa unayotoa.

Kwa chochote unachofanya, iwe ni kazi au biashara hakikisha unaijua vizuri kushinda mtu mwingine yeyote duniani, na unaifanya kwa ubora wa kipekee kuliko mtu yeyote alivyowahi kuifanya dunia nzima. Sitanii, namaanisha dunia nzima uwe wewe tu unayetoa unachotoa, na inawezekana kama ukianza leo.

SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

TAMKO LA LEO;

Naamua kuwa mtaalamu niliyobobea kwenye hiki ninachofanya. Nitaijua kazi/biashara hii kwa undani na nitatumia ujuzi wangu kutoa huduma/bidhaa ambayo ni bora sana kwa yule anayekwenda kuitumia. Nitahakikisha mtu hawezi kupata huduma hii sehemu nyingine yoyote, ila kwangu tu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 47 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Jinsi Unavyoweza Kutumia Uwezo Mkubwa Wa Akili Yako

”Without inspiration the best powers of the mind remain dormant. There is a fuel in us which needs to be ignited with sparks”. Johann Gottfried Von Herder

Bila ya hamasa nguvu kubwa ya akili yako inadumaa. Kuna mafuta yako ndani yetu ambayo yanahitaji kuwashwa na cheche.

Akili yako ina uwezo mkubwa sana, ila huwezi kuutumia kama huujui.

Njia nzuri ya kuweza kutumia uwezo huu ni kujihamasisha kila siku.

SOMA; SIRI 50 ZA MAFANIKIO.

Jihamasishe kwa kujifunza na kujisomea

Jihamasishe kwa kuhudhuria semina na mafunzo mbalimbali.

Jihamasishe kwa kuamini kwamba unaweza na kujikumbusha hivi kila mara.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Sifa TATU Unazohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Saturday, February 14, 2015

UKURASA WA 45; Uwekezaji Muhimu Kwako Kufanya Na Unaolipa Sana.

Kila mtu anatafuta fursa nzuri sana ya kuwekeza.

Watu wanafikiria ni biashara gani nzuri wakifanya watapata faida kubwa.

Wengine wanafikiria ni kilimo gani wakifanya watapata faidia na kufikia mafanikio.

Wengine wanafikiria ni hisa za kampuni gani wakinunua watapata faida kubwa.

Yote haya yatawezekana kama utafanya uwekezaji wa msingi sana ambao utakuletea faida kwenye mambo mengine yote unayofanya.

Uwekezaji tunaozungumzia hapa ni kuwekeza kwenye akili yako.

Akili yako ndio kila kitu, kama utaiweka katika hali nzuri utaweza kupata chochote unachotaka. Kama ikiwa katika hali ya hovyo utahangaika sana lakini hutaona mafanikio.

Unawekezaje kwenye akili yako?

Kujifunza. ifunze, jifunze, jifunze. Siwezi kuchoka kukuambia ni jinsi gani ilivyo muhimu kwako kujifunza.

Tulishajadili hili tena kwenye umuhimu wa kujifunza kila siku.

SOMA; UKURASA WA 13; Jifunze Kila siku.

Leo hii nakuambia umuhimu wa kuwekeza zaidi kwenye akili yako, pamoja na kujifunza kila siku kw akujisomea, hudhuria semina kubwa ambazo zinatoa mafunzo makubwa, jiandikishe kwenye kozi zinazohusiana na kazi au biashara unayofanya na unazoweza kujifunza kwa muda ulionao. Fanya chochote ambacho kitakupatia maarifa zaidi na kitakuwezesha uweze kuzitumia fursa zinazokuzunguka zaidi.

SOMA; Kozi 1100 Unazoweza Kujifunza Bure Kupitia Mtandao.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba uwekezaji muhimu na bora sana kwangu ni kuwekeza kwenye akili yangu. Maana akili yangu ikiwa vizuri nitaweza kuzitumia vizuri fursa zinazonizunguka ili kufikia mafanikio. Nitahudhuria semina na kujiandikisha kwenye kozi ambazo zitaniongezea maarifa zaidi.

Washirikishe watu watano unaowapenda habari hii nzuri ambayo itawawezesha kubadili maisha yao.

Tukutane kwenye ukurasa wa 46 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kila Mtu Ni Mwekezaji…

“We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities”. Ralph Waldo Emerson

Sisi wote ni wawekezaji, kila mmoja anafuata uelekeo wake, akiongozwa na ramani yake mwenyewe ambayo haifanani na ya mwingine. Dunia ni milango yote na fursa zote.

Kuna fursa nyingi sana duniani, nyingi kama ilivyo idadi ya watu.

Hii ni kwa sababu watu hatufanani na hivyo kila mtu akiweza kutumia uwezo wake mkubwa na wa kipekee walionao, anaweza kutengeneza fursa itakayomnufaisha kwa kiasi kikubwa sana.

SOMA; NENO LA LEO; Tengeneza Maisha Yako Hivi…

Anza sasa kutumia uwezo wako ambao ndio ramani inayokuongoza na utafikia fursa ambayo itakuwa ya kipekee kwako.

Wekeza kwenye akili yako, jifunze, jifunze, jifunze…

Nakutakia siku njema.

SOMA; Hakuna Anayejua Anachofanya, Na Huo Ndio Uzuri Wa Maisha.

Friday, February 13, 2015

UKURASA WA 44; Usiondoe Macho Kwenye Zawadi…

Vikwazo ni kile unachokiona pale unapoondoa macho yako kwenye malengo yako.

Kauli hii ni ya kweli kabisa. Unapoacha kuangalia kile unachotaka, unapoacha kuweka msisitizo kwenye kile unachotaka kupata ndio unaanza kuona vikwazo, ndio unapoanza kuona changamoto na ndio unapoanza kupata mawazo ya kukata tamaa.

Kama kweli unataka kupata unachotaka, fanya maamuzi ya kutoangalia kitu kingine chochote, angalia kile unachotaka tu. Kwa kufanya hivi hata utakapokutana na vikwazo itakuwa rahisi kwako kupata ufumbuzi na kuendelea kusonga mbele.

Maana hakuna kikwazo kisichokuwa na ufumbuzi, hakuna mafumu yasiyokuwa na mwisho.

SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Lakini kama utaanzakupepesa macho yako, na kuangalia vitu vingine, utaanza kuona vitu vingine ni bora kuliko unachofanya na utashawishika kuacha unachofanya na kwenda kufanya hivyo ulivyoangalia.

Utastuka pale utakapoanza kuvifanya na kugundua kwamba vina changamoto pia.

TAMKO LA LEO;

Nitaweka macho yangu, akili yangu na nguvu zangu zote kwenye malengo yangu. Sitapoteza muda wangu kuangalia mambo mengine maana kwa kifanya hivi naweza kushawishika kuacha malengo yangu na kuparamia vitu vingine ambavyo vitanifanya nishindwe.

SOMA; UKURASA WA 20; Geuza Changamoto Kuwa Fursa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 45 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

NENO LA LEO; Haijalishi Umeshindwa Mara Ngapi…

“Ever tried. Ever failed. No matter. Try Again. Fail again. Fail better”. Samuel Beckett

Umewahi kujaribu. Umewahi kushindwa. Haijalishi. Jaribu tena. Shindwa tena, Shindwa Vizuri.

Hijalishi umejaribu na kushindwa mara ngapi, kukata tamaa hakutakufanya upate ulichotaka.

Endelea kujaribu tena na tena na tena na kadiri unavyoshindwa ndio utafikia mafanikio yako. Cha msingi usirudie makosa na jifunze kila unaposhindwa.

SOMA; UKURASA WA 10; Umetengeneza Ulimwengu Wako Mwenyewe.

Kushindwa ndio kunawatengansiha wenye mafanikio na wasiokuwa na mafanikio.

Je wewe unataka mafanikio, kuwa tayari kushindwa.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Mambo Matano Ya Uongo Uliyojifunza Shuleni.

NENO LA LEO; Haijalishi Umeshindwa Mara Ngapi…

“Ever tried. Ever failed. No matter. Try Again. Fail again. Fail better”. Samuel Beckett

Umewahi kujaribu. Umewahi kushindwa. Haijalishi. Jaribu tena. Shindwa tena, Shindwa Vizuri.

Hijalishi umejaribu na kushindwa mara ngapi, kukata tamaa hakutakufanya upate ulichotaka.

Endelea kujaribu tena na tena na tena na kadiri unavyoshindwa ndio utafikia mafanikio yako. Cha msingi usirudie makosa na jifunze kila unaposhindwa.

SOMA; UKURASA WA 10; Umetengeneza Ulimwengu Wako Mwenyewe.

Kushindwa ndio kunawatengansiha wenye mafanikio na wasiokuwa na mafanikio.

Je wewe unataka mafanikio, kuwa tayari kushindwa.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Mambo Matano Ya Uongo Uliyojifunza Shuleni.

Thursday, February 12, 2015

SIRI YA 19 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kuongeza Kipato Chako Mara Mbili.

Chukua wastani wa kipato cha watu watano unaokaa nao muda mrefu na utapata kipato chako.
Asilimia tisini ya mafanikio yako yanaamuliwa na watu unaokaa nao muda mrefu.
Unajua ni kwa nini?
Kwa sababu watu wenye mafanikio wanafikiri tofauti na watu wasiofanikiwa na wewe unafikiri kama wale wanaokuzunguka wanavyofikiri.
Kama unataka kuongeza kipato chako mara mbili, anza kukaa karibu na watu ambao kipato chao ni mara mbili ya kipato chako. Na waruhusu wakufundishe jinsi ya kushinda zaidi.
Kumbuka watu wenye mafanikio wanapenda kuongelea mafanikio.

“You are a product of your environment. So choose the environment that will best develop you toward your objective. Are the people and things around you helping you toward success – or are they holding you back?” - W. Clement Stone

UKURASA WA 43; Ushauri Wa Bure Una Gharama Kubwa.

Ushauri wa bure hauna gharama mpaka pale utakapoanza kuutumia.

Siku hizi kila mtu anajua kutoa ushauri, kuwa makini sana kabla hujatumia ushauri wowote unaopewa. Hasa ushauri unaotolewa na kila mtu.

Kuna maneno rahisi ya mtaani utasikia biashara fulani inalipa kweli, fulani kaanza kuifanya na sasa hivi yuko vizuri. Au utasikia kilimo fulani kinalipa kweli, watu wanaofanya wananufaika sana.

SOMA; Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…

Mara nyingi utakuta wanaokupa ushauri wa aina hii wala hawafanyi hiko wanachokushauri.

Utakuja kujua ukweli pale unapojiingiza kwenye kitu hiko kinachoshauriwa, utakutana na changamoto ambazo hukuambiwa na kama hutakuwa imara unaweza kukata tamaa.

Kabla ya kufanyia kazi ushauri wote unaopewa, fanya utafiti wa kutosha, jua changamoto na vikwazo utakavyokutana navyo na unapoamua kuingia ingia moja kwa moja ukiwa na lengo moja tu, KUSHINDA.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba ushauri unaotolewa na kila mtu sio ushauri mzuri sana kuufuata. Kabla sijafuata ushauri wowote ninaopewa, hasa wa bure, nitafanya utafiti ili nijue kwa undani kila kinachoendelea. Na nitakapoamua kufanyia kazi ushauri huo, sitarudi nyuma.

Tukutane kwenye ukurasa wa 44 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA

SOMA; Hatua TANO Za Kuongeza Uzalishaji Wako Ili Kufikia Mafanikio.

SIRI YA 18 YA MAFANIKIO; Fanya Kitu Unachopenda...

Tafuta uwanja unaopendelea kufanyia kazi.
Fanya kitu ambacho unakifurahia.
Fanya kitu ambacho uko tayari kukifanya bure.
Maisha ni mafupi sana kufanya kitu ambacho hukipendi.
Kama utapenda kazi/biashara unayofanya, hakuna kitakachokuzuia kufikia mafanikio.

   “I never did a day’s work in my life. It was all fun.”  - Thomas Edison

SIRI YA 17 YA MAFANIKIO; Una Hamu Kiasi Gani Ya Kufikia Ndoto Yako?

Hamu kubwa unayokuwa nayo kwenye kitu unachotaka ndio inapima kama utaweza kukipata.
Kama una hamu kubwa sana ya kupata kitu, hakuna kitu kitakachoweza kukuzuia kukipata. Hata utapokutana na changamoto lazima utapata njia.
Hamu kubwa ya kupata kitu inakupa nguvu ya kulipa gharama ya mafanikio.
Unaweza kujitengenezea hamu, kuichochea hamu na kuiendeleza hamu kwa kujijengea picha ya kile unachotaka na kujihusisha na watu ambao wana hamu ya mafanikio.

“Nothing can resist a will which will stake even existence  upon its fulfillment.” - Benjamin Disraeli

NENO LA LEO; Kampuni Zinazokufa Na Kampuni Zinazofanikiwa….

“Companies that solely focus on competition will ultimately die. Those that focus on value creation will thrive.” Edward de Bono

Kampuni zinazoweka mkazo kwenye kushindana zinakufa mara moja. Kampuni zinazoweka mkazo kwenye kutengeneza thamani zinastahimili.

Ni vigumu sana kushinda kwenye kushindana, maana unapoingia kwenye mchezo wa ushindani kila mtu anatumia kigezo kimoja kushindana.

Njia bora ya wewe kujiweka pembeni na ushindani na hata kuweza kufanikiwa ni kutengeneza thamani kubwa ambayo haipatikani sehemu nyingine yoyote.

Watu watafuata thamani hiyo.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Weka Pamoja Vitu Hivi Vitatu Na Tayari Wewe Ni Mjasiriamali Mwenye Mafanikio Makubwa.

Wednesday, February 11, 2015

SIRI YA 16 YA MAFANIKIO; Jifunze Kutokana Na Makosa Yako Na Jipange Kufanikiwa.

Fursa zinakuja na kuondoka.
Maisha yana nyakati ambazo zinakuja na kuondoka kama mawimbi ya bahari.
Mwogeleaji anapokosa wimbi moja hakai chini na kujutia, bali hujifunza kutokana na makosa yao na kujiandaa vizuri kwa wimbi lijalo.
Kuwa kama mwogeleaji kwa kuangalia fursa, jiweke kwenye nafasi ya kushinda.

“Luck is the sense to recognize an opportunity and the ability to take advantage of it…The man who can smile at his bad breaks  and grab his chances gets on.”  - Samuel Goldwyn

SIRI YA 15 YA MAFANIKIO; Mafanikio ni Hatua Kwa Hatua.

Hakuna kitu kama mafanikio ya haraka.
Ni lazima uweke misingi siku kwa siku na kwa muda mrefu sana.
Ni lazima uweze kusinda mapambano madogo madogo mengi kabla ya kukutana na mapambano makubwa.
Nyumba zinajengwa tofali moja baada ya jingine.
Mashindano ya mpira yanasindwa kwa mechi moja baada ya nyingine
Biashara inajengwa kwa mteja mmoja baada ya mwingine.
Mafanikio yoyote makubwa, ni muunganiko wa mafanikio madogo madogo.

   “Do not despise the bottom rungs in the ascent to greatness.”  - Publilius Syrus

UKURASA WA 42; Usitafute Sababu, Chukua Hatua…

Katika jambo moja ambalo tunaweza kukubaliana wote ni kwamba kwa chochote unachofanya ni lazima utakutana na changamoto.

Kama tulivyowahi kujifunza, kitu pekee ambacho tuna uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika. Unapanga vizuri jinsi biashara yako itakuletea faida, unaishia kupata hasara. Unapanga vizuri jinsi utafanya kilimo chako na upate mazao mazuri unaishia kukosa mazao kabisa.

Changamoto ni sehemu ya maisha yetu, hakuna njia ya kuzikwepa ila kuna njia ya kuzivuka na kuendelea mbele.

SOMA; Matatizo Yote Kwenye Maisha Yako Yanatokana Na Kitu Hiki.

Unapokutana na changamoto yoyote una mambo mawili ya kufanya;

Jambo la kwanza na ambalo ni rahisi kufanya ni kutafuta sababu kwa nini imetokea na jinsi gani wewe huhusiki na changamoto hii. Kama ni hasara basi utapata sababu kwamba uchumi sio mzuri, wateja hawanunui na kadhalika. Kama ni kilimo utasema hakukuwa na mvua, uliowapa kazi hawakufanya vizuri n.k. Baada ya sababu hizi kinachotokea ni wewe kukata tamaa, mwisho wa mchezo.

Jambo la pili unaloweza kufanya ambalo ni gumu na ndio linatofautisha wanaofanikiwa na wanaojaribu tu ni kuangalia ni wapi ulikosea. Baada ya kuona mchango wako kwenye changamoto hiyo unaamua kuchukua hatua na wakati huu ukiwa na funzo tayari kutoka kwenye changamoto uliyopitia.

TAMKO LA LEO;

Najua changamoto yoyote ninayopitia inaweza kunifanya niwe imara zaidi au inaweza kunipoteza kabisa. Nachagua kuwa imara kw akila changamoto ninayopitia. Sitotafuta sababu za kuniridhisha kwamba changamoto ninayopitia sikutengeneza mimi, bali nitajifunza kutokana na mchango wangu kwenye changamoto hiyo na baadae nitafanya kwa ubora zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 43 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; UKURASA WA 20; Geuza Changamoto Kuwa Fursa.