Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, April 30, 2015

UKURASA WA 120; Ni Muda Tu…

Nafikiri umewaona watu wengi ambao wamefanikiwa zaidi ya ulivyofanikiwa wewe. Na labda kuna wakati unajiona wewe umeshindwa kwa sababu tu hujafikia viwango vile ambavyo wengine wameweza kufikia. Au labda huna uwezo mkubwa, au labda huna bahati kama waliyonayo wengine.

Yote haya sio ya kweli, hakuna mwenye bahati zaidi ya mwenzake na mafanikio hayatrofautiani kwa uwezo. Kama unafanya kile ambacho unahitaji kufanya ili kuwez akufikia mafanikio unayotaka, basi kuna kipimo kimoja kikubwa kati ya waliofanikiwa na ambao bado hawajafanikiwa, nacho ni MUDA.

SOMA; Sema HAPANA, Hapa Ndio Uhuru Wako Ulipo.

Hata kama una mipango mizuri kiasi gani, hata kama unafanya akzi kwa juhudi na maarifa kiasi gani, hata kama una una nidhamu na uvumilivu mkubwa sana, bado mafanikio hayatakuja haraka kama mvua. Unahitaji muda wa kuyafanyia kazi ndio uweze kuyaona mafanikio hayo.

Watu wote ambao unawaona wamefanikiwa wamekuwa wakifanya kitu hiko kw amuda mrefu na hivyo wameshafanya makosa mengi na  kujifunza. Wameshajijengea uzoefu mkubwa na wanaweza kuutumia vizuri na kuwawezesha kufikia mafanikio.

SOMA; Hivi Ndio Vitu Vinavyopelekea Ongezeko La Thamani Ya Hisa Kwa Mwekezaji.

Usiumie kwa sababu umeanza kufanya kitu mwaka mmja au miwili iliyopita na bado huoni mabadiliko. Bado unahitaji kuweka muda zaidi. Usiingie kwenye biashara leo na kujilinganisha na aliyekuwepo kwenye biashara kw amiaka kumi sasa, tayari yeye ameshatengeneza mzingi imara zaidi.

Chochote unachofanya kwenye maisha yako, jua kwmaba unahitaji muda ili kuweza kufikia mafanikio. Mafanikio ni mkusanyiko wa mambo madogo madogo ambayo yamefanywa kwa muda mrefu. Endelea kufanya mambo madogo madogo kwa ufanisi mkubwa na mwisho wa siku utaona mabadiliko makubw akwenye maisha yako.

SOMA; Usipoteze Muda Kwa Vitu Vidogo Vidogo.

TAMKO LA LEO;

Najua muda ndio tofauti pekee kati ya waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa bado, kama wote wanafanya kile ambacho wanahitaji kufanya ili wafanikiwe. Nitaendelea kuweka juhudi na maarifa kwenye malengo na mipango yangu kwa sababu najua baada ya muda nitakuwa mbali sana na hapa nilipo sasa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 121 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

Wednesday, April 29, 2015

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Biashara Kubwa Kwa Kuanzia Chini Kabisa, Hata Kama Huna Kitu.

Semina ya mafanikio kupitia biashara mwaka 2015 imebaki siku mbili tu ili uweze kujiunga. Kama unapitia changamoto zozote kwenye biashara yako au hata kama huna changamoto ila ungependa kufikia mafanikio makubwa usikose kujiunga na semina hii. Mwisho wa kujiunga ni ijumaa hii tarehe 01/05/2015. Baada ya hapo hutapata tena nafasi ya kujiunga na mafunzo hayo ambayo ni muhimu sana kwenye maisha yako na biashara yako pia. Kujiunga tume fedha ya ada ambayo ni tsh elfu 30 kwenye namba 0717396253/0755953887 na kisha tuma ujumbe wenye jina lako na email yako. Semina itafanyika kwa mwezi mzima wa tano na kwa njia ya email. Kuna vitu unaweza kuvikosa kwenye maisha yako, ila sio semina hii, utakosa mengi na utaendelea kushindwa kufika hatua ya juu kabisa kwenye biashara yoyote ambayo unafanya au unatarajia kufanya.

Kwenye makala ya leo nataka nikushirikishe mbinu ambazo unaweza kutumia na kutengeneza biashara kubwa sana na yenye mafanikio hata kama unaanzia chini kabisa, yaani huna kitu chochote cha kuanzia.

Katika hali ya kawaida watu wengi sana huwa wanalalamika kwamba wanataka kufanya biashara ila hawana mtaji. Wengine wanafikiri wanakosa elimu kubwa ndio maana hawawezi kuingia kwenye biashara. Wengine wanafikiri wangepata ‘connection’ nzuri tu basi biashara zao zingefika mbali sana. Ni kweli vitu vyote hivyo ambavyo watu huwa wanavilalamikia ni muhimu sana ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara. Ila ukweli muhimu zaidi ni kwamba, haimaanishi kwa kukosa vitu hivyo basi wewe umelaaniwa na huwezi kufanikiwa kwenye biashara.

Unaweza kufikia mafanikio makubwa sana kwenye biashara yako hata kama huna mtaji, huna elimu kubwa na hata kama hakuna anayekujua. Inawezekanaje hivyo? Tutajifunza kwa undani sana kwenye semina inayokwenda kuanza wiki ijayo, ila leo hapa nitakuonesha kwa mfano rahisi jinsi gani unaweza kufanya hivyo. Twende pamoja kwenye mfano huu rahisi na unaweza kuutumia kwenye biashara nyingine yoyote.

Tuseme labda wewe ni kijana ambaye umekuwa na wakati mgumu sana kifedha. Unajaribu kutafuta kazi hupati na pia umefikiria sana kufanya biashara ila tatizo limekuwa mtaji. Na pia ukifikiria hakuna mtu yeyote anayeweza kukuunganisha na watu wa kazi au watu wa biashara. Ukifikiria mkopo, hupati jibu kabisa kwa sababu huna chochote cha kuweka dhamana.

Ila kwa kuwa wewe ni mtu ambaye hukatishwi tamaa haraka, unaamua kufikiria zaidi. Unajiuliza ni shida gani ambayo mtu anaweza kuwa nayo na wewe ukaweza kuitatua na akakupa japo fedha kidogo? Kwa kufikiria kwa kina na kutokana na hali uliyonayo, unapata jibu moja ambalo linakuonesha mwanga. Unagundua kwamba sehemu unayoishi watu wana magari, ila hawapati huduma nzuri za kuoshewa magari yao. Unaona hapa ndio unapoweza kuanzia, kuosha magari kwa mtindo tofauti kabisa na wanavyofanya wengine.(Tafadhali usiishie hapa baada ya kuona nakuambia ukaoshe magari, hii ni hatua ya mwanzo tu, utafikia biashara kubwa sana baadae). Baada ya kuwa na wazo hili unaweza kulikuza hatua kwa hatua kama ifuatavyo.

Nenda kwa kila jirani mwenye gari, na mweleze kwamba ungeomba umwoshee gari yake bure kabisa. Unamwambia unataka kuanzisha biashara ya kuosha magari ambayo itakuwa tofauti kabisa na inavyofanyika sasa. Mwambie kwamba kwa ufahari wa huduma hii anafanyiwa akiwa nyumbani kwake, kwa siku ambayo amepumzika. Utahitaji kutoa maelezo ya kina ili uonekane kwmaba unajua kile ambacho unakwend akufanya. Kuna ambao watakataa, ila wengi watakubali, kwa sababu hakuna gharama yoyote wanayoingia na kama umewapa maelezo mazuri, watajaribu kupima waone kama kweli huduma unayokwend akuwapa ni ya tofauti.

Baada ya hapo jifunze kila aina ya gari unaloona majirani zako wanalo. Kama umeweza kusoma hapa, maana yake unawez akufungua mitandao mbalimbali inayohusiana na magari. Jifunze ubora wa gari husika, tafuta kitu chochote unachoweza kukisifia kwenye gari la mteja wako. Jua vitu muhimu unavyoweza kumshauri kuhusiana na gari lake hilo ili liweze kudumu kwa muda na lisimsumbue. Wakati huo huo jifunze kuhusu uoshaji wa magari, Jifunze ni kemikali gani nzuri unazoweza kuzitumia na zisilete madhara kwenye rangi ya gari au vitu vingine kwenye gari. Mambo yote haya muhimu utamweleza mteja wako siku ya kwanza unapoomba kuosha gari bure na hata siku ya kufanya kazi hiyo. Pia waeleze ni jinsi gani itakuwa fahari kwao kw akupata mtu wa kuwaoshea magari huku akiwapatia maelekezo yote ya msingi kuhusiana na magari yao.

Baada ya kupata nafasi ya kuosha gari bure kwa siku ya kwanza, hapa sasa unatoa ofa yako ambayo mteja hawezi kuikataa kutokana na huduma nzuri uliyompatia siku hiyo ya kwanza. Mwambie mteja kwamba unaweza kumfanyia huduma hiyo mara moja kila wiki kwa gharama ya tsh elfu tano tu. Utamfanyia usafi wa uhakika na kumpa maelekezo yote muhimu kuhusiana na gari lake.

Labda tuseme kwenye mtaa unaokaa kuna watu 30 ambao wanamiliki magari yao. Kwa kuongea nao wote 20 wanaweza kukubali kukupa nafasi ya kuwaoshea magari yao bure. Baada ya kutoa huduma hii ya kwanz a bure na kuwapa ofa yako, tuseme 10 ndio watakaosema ndio. Hii ni sawa na tsh elfu 50 kwa wiki, kwa kuanzia, sio mbaya ukilinganisha na sasa ambapo huna kipato kabisa. Na kumbuka huu ni mwanzo tu, unaendelea kuwaambia wengine wengi zaidi, maliza mtaa unaokaa na nenda mtaa mwingine. Na hawa wateja wako waambie wawaambie na marafiki zao kwamba unatoa huduma hiyo. Uzuri ni kwmaba mtu mwenye gari atakuwa na marafiki ambao nao pia wana magari na kama ukiwapa huduma nzuri hawatasita kuwaambia wenzao kwamba kuna kijana anatoa huduma nzuri sana ya kusafisha magari.

Hata kama umepata mteja mmoja, endelea kuongea na wengine wengi. Hata kama wote wamekataa, endele akuongea na wengine wengi, na kama utakuwa unatoa maelezo yako vizuri kuna mtu atakuambia NDIO na huyu ndio wa kumtumia vizuri.

Kumbuka katika mchakato wote huu hujatumia fedha nyingi sana, hujahitaji kuw ana eneo kwa sababu huduma hii unaitolea kwa mteja. Labda utahitaji kuwa na ndoo mbili, na vifaa vingine vya kawaida vya kuoshea na sabuni au kemikali nyingine nzuri ya kuoshea magari ambayo sio ya bei ghali sana. Gharama za vitu hivyo vichache haiwezi kuzidi tsh elfu 20.

Haya yote tuliyojadili hapo juu ni hatua ya kwanza kabisa ya wewe kufanikiwa kwenye biashara, bado kuna hatua nyingi sana ambazo bado hujatumia. Na changamoto kubwa ni kwmaba watu wengi huwa wanaishia hatua hii ya kwanza ndio maana wanakuwa watumwa wa biashara zao. Unakuta mtu anauza duka lile lile kwa kiwango kile kile kwa zaidi ya miaka 10, hakuna mafanikio hapa. Sasa wewe hutaki kuosha magari kwa maisha yako yote. Hivyo unakwenda hatua nyingine muhimu kabisa ya ukuaji wa biashara yako. Anza kutoa huduma za ziada kwenye magari unayoosha, badilisha oil au maji au chochote ambacho kutakuongezea kipato cha ziada kutoka kwa mteja wako ambaye sasa anakuamini sana. Unaweza pia kuchukua jukumu la kuwatafutia fundi wa uhakika kwa matatizo wanayokutana nayo kwenye magari yao. Yaani wewe unakuwa zaidi ya muosha magari kwao, wanapopata shida yoyote kwenye magari yao, mtu wa kwanza kuja kwenye akili yao ni wewe na hivyo kukutafuta uwashauri vizuri.

Baada ya kupata wateja wa uhakika tafuta vijana wengine ambao wapo tu mtaani na hawana cha kufanya. Chagua unaoona wanaweza kufanya akzi kwa uaminifu, wafundishe kile unachofanya na wafenye kuwa wasaidizi wako. Walipe kadiri wanavyoweka juhudi zao kwenye kazi unazowapangia. Endelea kwenda mbele, endelea kukua, endelea kuongeza wateja mpaka unafikia wateja 1000 kwa mwezi ambao wapo tayari kukupa sio chini ya shilingi elfu tano kila mmoja. Hii itakuwa ni milioni tano, ukiondoa gharama zote za uendeshaji, bado utabaki na zaidi ya nusu ya kiwango hiko. Sasa niambie ni nani angekuajiri akupe mshahara wa milioni mbili, ndani ya mwaka wako wa kwanza wa kazi. Kumbuka hapa bado una nafasi kubwa ya kuendelea kukua zaidi na zaidi na hakuna kikomo isipokuwa unachojiwekea mwenyewe.

Hivyo ndio unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kw akuanzia chini kabisa. Maelezo hayo yanaonekana rahisi ila utekelezaji unahitaji moyo, unahitaji muda maana hiyo haitotoke amara moja tu, watu watataka wakuamini kwanza ndio waweze kufanya kazi na wewe. Unahitaji uaminifu wa hali ya juu sana, unahitaji kujitoa na kutokujali wengine wanakuchukuliaje kwa sababu umeamua kuosha magari. Unahitaji uvumilivu, kuna watu watakuambia hapana, kuna wengine watakusumbua kwenye malipo. Lakini kama utakomaa, kama utaweka juhudi na maarifa na ukatoa huduma ambayo mtu hajawahi kuipata kokote, lazima utakuwa na bishara, hata kama hutofikia mamilioni, lakini utapata cha kukutoa hapo ulipo.

Sasa hebu niambie, unafikiri ni kitu gani kinachokuzuia mpaka sasa? Ni wewe mwenyewe tu.

Mfano huu tuliotumia hapo juu unawez akuweka kitu kingine chochote unachoweza kufanya, iwe ni kutangaza biashara za watu wengine kwenye mtandao, iwe ni kutoa huduma ya kukusanya taka taka, iwe ni kutoa huduma ya kufundisha watoto majumbani na mengine mengi. Unachohitaji ni wewe kukaa chini, kuweka mipango na kuanz akuitekeleza mara moja.

Kupitia semina inayoanza wiki ijayo, utajifunza mengi zaidi na jinsi unavyoweza kubadili wazo lolote kuwa biashara itakayokulipa.

Kama wewe ni kijana na huna fedha kabisa ila umependezwa na wazo hilo hapo juu na unafikiria kulifanya, jiunge na semina hii halafu tutapata muda wa kuendeleza wazo hilo na nitakupa nafasi ya kuwa msimamizi wako mpaka biashara yako itakapokomaa. Kwa hiyo unahitaji shilingi elfu 50, elfu 30 ya semina na elfu 20 ya kuanzia biashara yako. Kama kwa kufikiria wkako kote unaona huwezi kupata shilingi elfu 50, fanya hivi, angalia ni vitu gani unavyomiliki ambavyo huna matumizi navyo makubwa na unaweza kuuza na kupata fedha hiyo. Kama huna, angalia katika ndugu zako na watu wengine wa karibu, chagua watu kumi ambao utaomba kuonana nao na utawaomba wakupe shilingi elfu kumi tu kila mmoja, waambie kuna kitu cha tofauti unataka kujaribu na kitakuw ana manufaa kwako. Katika 10 utakaowaomba, hutakosa watano watakao kupatia. Usikubali kirahisi, pambana mpaka uhakikishe umepata kile ambacho unakitaka.

Nikukaribishe sana kwenye semina inayoanza wiki ijayo na mwisho wa kujiunga ni ijumaa hii. Ukiikosa hii, unakuw aumejikosesha mambo mengi sana na mazuri.

Nakutakia kila la kheri katika biashara unayofanya au unayotegemea kufanya.

TUPO PAMOJA

Makirita Amani 

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322

UKURASA WA 119; Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu.

Hebu jiulize kama isingekuwa hofu leo hii ungekuwa wapi? Fikiria mipango yote ambayo umewahi kuwa nayo kwa muda mrefu lakini ilipofika utekelezaji tu, hofu ikabisha hodi na ikakufanya usidhubutu hata kuanza.

Kumbuka jinsi ambavyo umekuwa unahofia kushindwa, umekuwa unahofia kukataliwa, umekuwa unahofia kwamba utapata hasara kubwa. Umeacha kufanya kile ulichopanga kufanya. Lakini je hofu imetosheka? Jibu ni hapana, inaendele akukufuata popote unapokwenda na kwenye jambo lolote unalotaka kufanya.

SOMA; Ukweli Kuhusu Afya ya Wanaume; Kwa nini Wanaume Wanakufa Wadogo Kuliko Wanawake.

Kama unataka kufikia mafanikio makubwa, huna budi kufanya maamuzi magumu na maamuzi hayo ni kuondokana kabisa na hofu ambazo zinakuzuia wewekuchukua hatua kwenye maisha yako. Sasa unawezaje kuondokana na hofu hizi? Leo nitakushirikisha mbinu moja rahisi sana ya kuweza kufanya hivyo.

Njia rahisi na ya uhakika kabisa ya kuondokana na hofu ni kutengeneza tabia ya kufanya lile jambo ambalo unahofia kufanya. Tuseme labda umekuwa unatamani sana kuandika, ila unaogopa kuandika. Sasa fanya kuandika iwe ndio tabia yako unayofanya kila siku. Anza leo kwa kuandika sentensi moja, kesho mbili, keshokutwa aya na endelea hivyo hivyo. Hakikisha hukosi siku hujafanya hivyo. Na sio lazima kile unachoandika umuoneshe mtu.

SOMA; Hizi Ndio Siri 21 Za Mafanikio

Kama unahofia kuongea mbele ya watu, anza kujenga tabia ya kuongea na kila mtu ambaye unakutana naye, ongea na vikundi vidogo vidogo vya watu na nenda hatua ya juu zaidi mpaka utakapofikia kuongea na kundi kubwa kabisa la watu.

Kama unahofia kuanza biashara, anza kidogo, kwa kitu ambacho unajua huwezi kupata hasara na hata ukiipata haitokuumiza, endelea kuongeza kidogo kidogo kila siku, mpaka siku moja unajikuta unamiliki biashara kubwa sana.

Tabia ni dawa ya uhakika ya kumaliza hofu. Usiendelee kuhofia tena, anza kufanya kile ambacho unahofia kufanya na hofu haitakuw ana budi bali kukimbia na kukuachia wewe uhuru wa kufanya kile ulichochagua kufanya.

SOMA; Kitu Hiki Kimoja Ni Muhimu Kuliko Kiwango Cha Fedha Unachotaka.

TAMKO LA LEO;

Najua dawa ya hofu ni kufanya kile ambacho nahofia kufanya. Kuanzia sasa nitakuwa nafanya kile ambacho nahofia kukifanya, nitaanz akufanya kidogo kidogo na mwishowe nitakuwa nimepiga hatua kubwa sana.

Tukutane kwenye ukurasa wa 120 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tuesday, April 28, 2015

UKURASA WA 118; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka…

Kuna watu huwa wanasema kwamba siku zao zina kisirani, wengine husema wameamkia upande mbaya na maneno mengine mengi yanayoashiria kwamba kuna siku mbaya na siku nzuri.

Tuchukue mfano, umeamka asubuhi na kwa bahati mbaya umeamka kwa kuchelewa, hivyo unaanza kujiandaa haraka haraka, unavaa nguo huku unafanya mambo mengine ili tu uokoe muda. Mara asubuhi hiyo ukapishana kauli na mtu wa karibu unayeishi nae, anaweza kuwa mke/mume, mtoto au hata rafiki. Unapata hasira sana na hata kumwambia maneno makali. Unatoka na kufika barabarani, labda unatumia daladala kama usafiri na unakuta daladala hakuna, zinakuja zimejaa na unatakiwa kugombania.

SOMA; USHAURI; Jinsi Unavyoweza Kuondokana Na Changamoto Za Kuendesha Biashara Na Kuweza Kufikia Mafanikio Makubwa

Unagombania na kupata daladala, mara kidogo katika kukaa vizuri mtu anakukanyaga, unamuuliza kistaarabu kwa nini anakanyaga tu bila kuangalia? Anakujibu ungekuwa unataka raha ungepanda teksi au ungenunua gari lako. Maneno hayo yanakuw amachungu sana kwako, mnajibizana tena maneno makali. Wakati huo huo kuna foleni ndefu sana halafu unaona trafic anaita magari mengine kwa muda mrefu ila ya upande mliopo hayaitwi kabisa. Unazidi kupata hasira.

Unafika ofisini, hapo tayari umechelewa. Unakuta bosi wako anakusubiri kwa hamu na kuanza kukusem akw atabia yako ya kuchelewa. Unajaribu kujitetea ndio unawasha moto kabisa.

Sasa hebu niambie kwa siku kama hii unaweza kufanya kazi yoyote ya maana? Kwa hasira zote hizi ulizokusanya kuanzia nyumbani zinakutosha kutangaza kwamba hii ni siku ya kisirani. Na kila kazi utakayojaribu kufanya utakosea au kuibua mabishano na wengine.

Hebu kwanza tuanze na siku ya kisirani, je kuna siku maalumu ambayo ni ya kisirani? Na siku hiyo jua huwa linachomozea upande upi? Na urefu wa siku hiyo unakuwa masaa mangapi?

SOMA; Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 2

Kwa kweli hakuna siku maalumu ambayo ni ya kisirani, siku zote zipo sawa, ila sisi wenyewe ndio tunaamua kufanya baadhi ya siku zetu kuwa za kisirani. Kitu pekee kinachoweza kuharibu siku yako na kuifanya kuwa ya kisirani ni watu. Ila wewe ndiye utakayetoa ruhusa ya watu kuharibu siku yako. Kwa mfano unapoamka umechelewa, tayari umechelewa, hivyo hata kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hakukufanyi uwahi. Kama mtu amekujibu vibaya, huna haja na wewe kumjibu vibaya, huenda na yeye amechelewa kama wewe au ana hasira zake nyingine, sasa wewe unapokubali kuingia kwenye majibishano nae unakuwa umemruhusu aharibu siku yako pia.

Kitu pekee kinachoweza kuharibu siku yako ni watu. Na njia bora ya kuepuka hili ni kutokuruhusu watu walete matatizo yao kwenye siku yako. Kama mtu anafanya jambo lolote la kukuudhi, achana naye, mpuuzie na wewe kazana kuifanya siku yako iwe bora, kwa kufanya kazi yako kwa ubora wa hali ya juu. Kumbuka mafanikio yako hayatokei siku moja, bali ni muunganiko wa siku nyingi ambazo umeishi kwa mafanikio. Linda sana siku yako, usirihusu watu waiharibu.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyokaribisha Ushindani Kwenye Biashara Yako.

TAMKO LA LEO;

Najua watu wanaweza kuiharibu siku yangu kama nitawapa ruhusa hiyo. Kuanzia sasa sitatoa tena ruhusa kwa mtu kuiharibu siku yangu. Nitailinda siku yangu kwa sababu najua kila siku inachangia kwenye mafanikio yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 119kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Monday, April 27, 2015

NENO LA LEO; Linda Siku Yako.

UKURASA WA 117; Huyu Ndiye Mtu Ambaye Umasikini Huwezi Kumbugudhi.

Umasikini unapenda sana kuwabugudhi watu, lakini sio watu wote. Kuna watu ambao umasikini hupenda sana kuwasumbua. Watu hawa huteseka kwa kipindi kirefu wkenye maisha yao mpaka pale yanapokwisha.

Watu hawa wanaishi maisha yao yote wakitamani kwmaba umasikini uondokane nao lakini jambo hilo linashindikana. Watu hao wanaamini kwamba wakipata fedha tu, basi umasikini bai bai. Ni mpaka pale wanapopata fedha na kugundua kwamba bado umasikini unapenda kuwabugudhi.

SOMA; Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 2

Katika hali hii watu hawa huamini kwamba wao walizaliwa ili wawe masikini. Wnakubali kwmaba sio watu wote walizaliwa wawe matajiri na wanatumia kauli nzuri sana kwamba HATUWEZI WOTE KUWA MATAJIRI. Kama kauli hii ni kweli wanashindwa kujiuliza kwa nini wao tu ndio wanaandamwa na umasikini?

Sasa leo nakushiriksiha mtu mmoja ambaye umasikini hauwezi kumsumbua. Mtu huyu umasikini unamuogopa sana na wala hauwezi kumsogelea kwa karibu. Mtu huyu anasifa ambazo hata wewe unaweza kuwa nazo na umasikini ukakuogopa sana.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Kuzingati Ili Kupata Mbegu Bora Kwenye Kilimo.

Mtu huyu ana sifa moja kuu, anaamua kuifanya kazi yake kw aubora wa hali ya juu sana kwa sababu anaipenda na anaweka ubunifu ili kuwa tofauti. Huyu ni mtu ambaye anatoa huduma bora sana kupitia kile anachofanya na kila anayekutana naye anafurahia kazi yake. Mtu huyu anaogopewa sana na umasikini kwan sababu hakuna wakati ambao anakosa kazi nzuri ya kufanya. Na kwa kuw aadui wa umasikini ni kazi, mtu huyu ameumaliza kabisa umasikini wka kupenda kazi yake na kuifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.

SOMA; BIASHARA LEO; PANGA MARA KUMI.

Je wewe unashidnw akuw ana sifa alizonazo mtu huyu? Najua unaweza, hebu anza sasa. Penda sana kazi unayofanya na ifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.

TAMKO LA LEO;

Najua mimi naweza kuw amtu ambaye umasikini unaniogopa sana. Na njia rahisi ya kufanya hivyo ni kupenda sana kazi ambayo ninaifanya na kuifanya kw aubora wa hali ya juu sana kuliko ambavyo imekuwa ikifanywa na wengine. Nitakuwa mbunifu na kuhakikisha kila anayekutana na kazi yangu inamsaidia sana na anaendelea kuwa mteja wangu mzuri.

Tukutane kwenye ukurasa wa 118 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Sunday, April 26, 2015

UKURASA WA116; Usiwasikilize Watu Hawa.

Kuna watu kazi yao ni kupinga tu. Yaani watu wa aina hii hakuna kitu unaweza kufanya waache kupinga au kukosoa. Na hata utaka[ojaribu kujitetea watayapinga maelezo yako pia.

Ni muhimu sana kuwajua watu hawa na kutowapa nafasi kubw akwenye akili yako. Usiogope kuendelea na mipango yako kwa sababu tu mtu amekwambia huwezi, haiwezekani, unapoteza muda.

SOMA; Huu Ndio Uwekezaji Bora Zaidi Unaoweza Kuufanya.

Elewa kwamba wengi wanaokuambia hivi ndio kitu wanachopenda kufanya. Na ukiwachunguza kwa undani utagundua kwamba hakuna kitu chochote kikubwa wamefanya kwenye maisha yao.

Mara nyingi watu hawa wanakuwa hawajiamini wao wenyewe na hivyo hawaamini kama mtu mwingine anaweza kufanya mambo makubwa. Hawa sio watu unaotakiwa kuwasikiliza hata kidogo. Na angalau wangekuwa wanatoa njia mbadala basi ingejua wanajua kile wanachosema. Badala yake wanakukosoa tu halafu hawakupi njia nyingine nzuri.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu The One Thing.

TAMKO LA LEO;

Najua kuna watu ambao kazi yao kubwa ni kukosoa na kupinga. Watu hawa hawajiamini wao wenyewe na hivyi hawaamini mtu mwingine anaweza kufanya mambo makubwa. Sitawaweka kwenye mawazo yangu watu hawa wala yale wanayosema.

Tukutane kwenye ukurasa wa 117 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Tulichozaliwa Nacho Na Tulichojifunza….

Love is what we were born with. Fear is what we learned here. -Marianne Williamson

Upendo ndio kitu ambacho tulizaliwa nacho. Hofu ni kitu ambacho tumejifunza hapa duniani.

Upendo utakuletea furaha kwenye maisha, upendo utakuwezesha kufanya kile unachopenda na kufanikiwa na upendo utakuwezesha kuishi na wengine vizuri.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyodhulumu Maisha Yako Wewe Mwenyewe.

Hofu ndio sumu kubwa ya mafanikio. Hofu itakuzuia wewe kuchukua hatua, hofu itakufanya ujione wewe huwezi, hustahili. Na hofu zote hizi umejifunza hapa duniani.

Usikubali hofu ziendelee kukurudisha nyuma.

Nakutakia siku njema.

Saturday, April 25, 2015

UKURASA WA 115; Hivi Ndivyo Unavyojitengenezea Dharura.

Maisha sio dharura, ila sisi wenyewe huwa tunayafanya yawe dharura. Kama utakuwa na malengo na mipango yako, halafu ukaifanyia akzi kwa wakati, hakuna wakati wowote ambao utaona una dharura.

Ila hutakuwa na mipango na kufanya mambo pale unapojisikia, kuna wakati utajikuta kwneye dharura kubwa sana. Na hapa ndipo matatizo yote yanapoanzia, pale ambapo una mambo mengi ya kufanya lakini muda ulionao ni kidogo sana.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyodhulumu Maisha Yako Wewe Mwenyewe.

Tunaishi kwenye dunia ambayo ina vitu vingi vya kufanya ila muda tulionao ni ule ule. Una smartphone ambayo inamitandao yote ya kijamii, unaweza kupata habari masaa 24 kwa siku. Hata unapolala, ukiamka tu, habari zipo pale zinakusubiri, uanze kuziperuzi.

Kwa utamu wa habari na kufuatilia mambo mengine kwenye mitandao, inakuwa rahisi kwako kuahurisha yale mambo ambayo ni muhimu sana kwako. Na hapa ndipo unapotengeneza dharura kubwa ambayo itakusumbua sana baadae.

Acha kutengeneza dharura, maisha ni mazuri kama utafanya yale ambayo ni muhimu kwa wakati ambapo umepanga kuyafanya. Mengine yote ambayo sio muhimu achana nayo, hayaongezi chochote kwenye maisha yako na yanakuzuia wewe kufikia mafanikio.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Kuzingati Ili Kupata Mbegu Bora Kwenye Kilimo.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba maisha sio dharura japo nimekuwa najitengenezea dharura mimi mwenyewe. Najua dharura sio nzuri kwenye maisha na zitanipelekea kushindwa kufikia mafanikio. Kuanzia sasa nitaacha kufanya mambo ambayo sio muhimu wkangu ili niepuke kujitengenezea dharura.

Tukutane kwenye ukurasa wa 116 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

NENO LA LEO; Ufunguo Mkuu Wa Furaha.

Love is the master key that opens the gates of happiness. -Oliver Wendell Holmes

Upendo ndio ufunguo mkuu unaofungua milango yote ya furaha.

Umesoma vizuri hapo juu, upendo ndio ufunguo wa furaha, sio fedha nyingi, sio umiliki wa mali za kifahari na sio kutoka kwa mtu.

Kama unataka kuw ana furaha kwenye maisha yako, kuwa na upendo. Wapende wote wanaokuzunguka na kubali kupendwa na wengine pia.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Kitu Hiki Kimoja Ni Muhimu Kuliko Kiwango Cha Fedha Unachotaka.

Friday, April 24, 2015

UKURASA WA 114; Tumia Vikwazo Ulivyonavyo Kufikia Mafanikio.

Watu wengi huamini kwamba ili uwezekufikia mafanikio basi unahitaji uwe na vitu vingi sana au uweze kufanya vitu vingi. Hii inaweza kuwa kweli ila kuna ukweli unaotakiwa kuujua na unaweza kukushangaza sana.

Ukiwachukua watu wawili, na mmoja akawa ana vitu vingi na kuweza kufanya vitu mbalimbali, mwingine akawa na vitu vichache na kuweza kufanya vichache pia. Kwa nafasi kubwa mwenye vitu vichache anaweza kufanikiwa kuliko mwenye vitu vingi.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Unajua ni kwa nini? Twende pamoja.

Unapokuwa na vitu vichache au unapoweza kufanya vitu vichache, nguvu zako zote unazipeleka kwenye vitu hivyo vichache. Na siku zote unapoweka nguvu zako zote kwenye vitu vichache, hakuna jinsi mafanikio yanaweza kujificha.

Unapokuwa na vitu vingi au kuwez akufanya vitu vingi, unapoteza muda mwingi kwenye vitu hivyo na hatimaye kushindwa kufanikiwa hata kwenye kimoja.

Badala ya kulalamika kwamba umekosa hiki au umekosa kile ndio maana hufanikiwi, hebu tumia vile vichache au kile kimoja ulichonacho kuwez akukufikisha kwenye mafanikio. Unaweza kupika mandazi tu? Hebu jifunze vizuri kuhusu upishi wa maandazi, hebu pika mandazi matamu sana ambayo watu watayafurahia, hebu yatangaze maandazi yako popote unapokuwa na hebu toa mafunzo ya upishi wa maandazi.

SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Unaweza kulima tu? Hongera. Sasa hebu fuatilia kilimo unachofanya ili ukijue vizuri, hebu jua mbegu bora za kupanda kwa eneo unalofanyia, hebu jua masoko ya mbali zaidi na yenye faida kubwa badala tu ya kukubali kulanguliwa.

Huna miguu? Hebu tumia mikono yako vizuri, kufanya kazi za mikono ambazo zitakuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa.

Unataka kuanza biashara ila huna mtaji? Hapo ndio pazuri pa kuanzia kwa sababu, kwanza huna kitu kingine cha kufanya. Pili huwezi kupata hasara. Sasa ni jukumu lako kujua ile biashara unayotaka kuifanya, kujua kiwango cha chini kabisa unachoweza kuanzia na kuanzakufikiria utawezaje kupata kiwango hiko cha chini

Huna elimu? Safi sana, sio safi kwa sababu huna ila safi kwa sababu hutakuwa na sababu. Pale utakapoamua kuingia kwenye shughuli yoyote hutaanza kufikiria mimi na elimu yangu nafanya hivi! Wewe utachakarika kwa sababu unajua huna tumaini jingine, na utawaacha wenye elimu zao wakishangaa wakati wewe unafanikiwa.

SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

Kikwazo chochote ulichonacho kwenye maisha yako, usikilalamikie, bali kitumie kufikia mafanikio.

TAMKO LA LEO;

Vikwazo nilivyonavyo ni fursa kubwa sana kwangu kufikia mafanikio makubwa. Vinaniwezesha kuweka nguvu zangu kwenye mambo machache ninayoweza kufanya na kwa njia hii mafanikio ni lazima kwangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 115 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Hakuna Uhaba Wa Fursa, Kuna Uhaba Wa Kitu Hiki…

There is no scarcity of opportunity to make a living at what you love; there's only scarcity of resolve to make it happen. -Wayne Dyer

Hakuna uhaba wa fursa za kutengeneza kipato kwenye kile unachopenda; kuna uhaba wa wewe kuamua kufanya hivyo.

SOMA; Njia Ya Uhakika Ya Kufikia Mafanikio Makubwa.

Kitu chochote ambacho unapenda kufanya, kuna fursa nyingi sana za kuwez akutengeneza kipato. Kama unapenda kupika keki, unaweza kutengeneza keki kwa ajili ya kuuza, unawez akuandika kitabu chenye maelezo ya jinsi ya kutengeneza keki nzuri, unaweza kurekodi video ukionesha hatua kwa hatua utengenezaji wa keki na mengine mengi ambayo mtu mwingine atakuwa tayari kulipia.

Lakini yote hayo yatatokea kama wewe utaamua yawe hivyo. Kama utakaa chini na kufikiri na kufungua macho yako ili uweze kuziona fursa mbalimbali zinazokuzunguka.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Sababu Namba Moja Kwa Nini Hufanikiwi Kwenye Kazi Unayofanya.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.

Thursday, April 23, 2015

UKURASA WA 113; Fursa Zinaweza Kukupoteza…

Fursa Fursa Fursa…..

Katika wakati wowote ule kwenye maisha yako na katika jambo lolote unalofanya, kuna fursa nyingi sana ambazo zimekuzunguka. Na kama ukiwa macho ndio fursa zinazidi kuwa nyingi.

Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye unataka kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa inabidi uzichangamkie fursa hizi, si ndio?

Kama utaichangamkia kila fursa, unajiandaa kushindwa kufikia mafanikio. Haijalishi una uwezo mkubw akiasi gani, haijalishi una kiu kiasi gani ya kufikia mafanikio, kujiingiza kwenye fursa nyingi kutakuwa kikwazo kikubwa kwako kufanikiwa.

SOMA; Haya Ndiyo Mambo Yanakukwamisha Na Kukufanya Ushindwe Kufikia Malengo Yako Uliyojiwekea.

Kama utaikimbilia kila fursa ambayo unaiona,  utaishia kukimbiza ndoto za watu wengine huku ukisahau kabisa ndoto zako.

Chagua aina ya fursa ambazo unaweza kuzifuatilia na nyingine zote achana nazo. Mtu anayekimbiza sungura mmoja ana uwezekano mkubwa wa kumkamata. Mtu anayekimbiza sungura wawili hawezi kumkamata hata mmoja.

Hakikisha fursa unazofuatilia zinakuwa sungura mmoja ili uweze kufikia ndoto zako.

TAMKO LA LEO;

Najua kuna fursa nyingi sana zinazonizunguka. Pia najua siwezi kuzikimbilia fursa zote, na kw akujaribu hivyo itanizuia mimi kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yangu. Nitachagua aina ya fursa za kufuatilia na nyingine nitaachana nazo.

SOMA; Dalili Za Kuanguka, Zijue Na Jinsi Ya Kuepuka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 114 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kila Kinachotoke Kwenye Maisha Yako Ni Fursa Ya Mambo Haya Mawili.

I believe that every single event in life happens in an opportunity to choose love over fear. -Oprah Winfrey

Naamini kwamba kila tukio linalotokea kwenye maisha ni fursa ya kuchagua kati ya upendo au woga/hofu.

Kila tukio linalotokea kwenye maisha yako, linaweza kukupeleka mbele au linaweza kukurudisha nyuma. Hii itatokana na kile ulichochagua kati ya vitu hivyo viwili.

Kama utachagua upendo, utaona fursa ya kufaidika na kile kilichotokea.

Kama utachagua woga/hofu hutaona fursa yoyote katika jambo hilo lililotokea.

Je wewe unachagua nini leo?

Nakutakia siku njema.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya

Wednesday, April 22, 2015

UKURASA WA 112; Njia Kuu Mbili Za Kuishi.

Kuna njia kuu mbili za kuishi maisha yako hapa duniani.

Njia ya kwanza ni kuishi kama ambavyo watu wanataka wewe uishi. Ufanye yale ambayo watu wanakutegemea uyafanye hata kama sio yanayokufurahisha au sio muhimu kwako. Ufanye kile ambacho kila mtu anafanya hata kama huna msukumo wowote wa kufanya hivyo. Hii ndio njia ya kwanza ambayo asilimia 99 ya watu kwenye jamii yoyote wanaishi njia hii.

SOMA; Kabla Hujabadili Tabia Zako Badili Hiki Kwanza…

Njia ya pili ni kuishi kama vile ambavyo wewe mwenyewe unataka kuishi. Kufanya kile ambacho ni muhimu kwako na una msukumo wa ndani wa kukifanya. Kufanya kazi wka juhudi na maarifa ili kuweza kufikia ndoto zako kubwa, bila ya kujali wengine wanafanya nini au wanasema nini. Kutokujiwekea ukomo wa wapi unapoweza kufika na kuwajali wale wanaokujali. Hii ni njia ya pili ambayo asilimia 1 ya watu kwenye jamii yoyote wanaishi njia hii.

Umechagua kuishi njia ipi? Huo ni uchaguzi wako. Kama hujachagua au hujui uchaguzi wako ni sahihi au la, nikukumbushe kwamba hii asilimia 1 wanaoishi maisha kwa njia ya pili, ndio wanaofikia mafanikio makubwa sana, wanaokuwa na furaha kwenye maisha yao na ambao hawana majuto kwenye maisha yao.

SOMA; Kama Huwezi Kufanya Miaka 50 Acha..

TAMKO LA LEO;

Najua maisha ni kuchagua, na kuna njia mbili za kuweza kuishi maisha yangu. Mimi nachagua kuishi njia ya ______________ na nitafanya mambo _____________ ili kuhakikisha maisha yangu yanakwenda vile nilivyopanga. (Jaza sehemu iliyoachwa wazi)

Tukutane kwenye ukurasa wa 113 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Najua Umeshasikia Hili Mara Nyingi, Sio Vibaya Ukasikia Tena Na Leo.

I know you've heard it a thousand times before. But it's true - hard work pays off. If you want to be good, you have to practice, practice, practice. If you don't love something, then don't do it. -Ray Bradbury

Najua umeshasikia hili mara elfu moja kabla. Lakini ni kweli- kufanya kazi kwa juhudi kunalipa. Kama unataka kuwa vizuri, unahitaji KUFANYA, KUFANYA, KUFANYA. Kama kuna kitu ambacho hukipendi, usikifanye.

SOMA; Kazi Ndio Msingi Wa Maendeleo.

Hakuna mbadala wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Nafikiri huwa nasema hili karibu kila siku. Ndio moja ya misingi ambayo naisimamia kwenye maisha yangu. Misingi mingine ni UAMINIFU, UADILIFU na NIDHAMU.

Umeajiriwa, tekeleza majukumu yako kwa ufanisi wa hali ya juu sana. Weka juhudi zako zote na ubunifu wako kuifanya kazi yako kuw aya kipekee, usiangalie ni kiasi gani unalipwa, toa kile ulichonacho wewe kwanza na kama aliyekuajiri hataona thamani yako, wengine wataiona.

Umejiajiri au unafanyabiashara, thamani unayozalisha ndio itakufanya uendelee kuwa na kipato. Weka juhudi na maarifa kwenye kile unachofanya, hakikisha wanatumia bidhaa au huduma zako wananufaika sana.

Kuna kitu ambacho hupendi? Achana nacho, usikifanye, usikifuatilie. Tuna ishi kwneye dunia yenye uhuru mkubwa, hakuna anayekulazimisha chochote, halafu muda ni mfupi sana, mpaka uanze kufuatilia kila kitu.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Njia Mbili Za Kukuondolea Matatizo Yako Ya Kifedha.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.

Tuesday, April 21, 2015

Weka Mayai Yako Yote Kwenye Kikapu Kimoja, Halafu Fanya Hivi....

#NENO_LA_BUSARA..
Kuweka mayai yako yote kwenye kikapu kimoja ni hatari.
Sasa weka mayai yako yote kwenye kikapu kimoja na KILINDE SANA KIKAPU HIKO, kama unavyoyalinda maisha yako.
Ni rahisi kufikisha kikapu kimoja chenye mayai kumi sokoni kuliko kufikisha vikapu kumi vyenye yai moja moja.
Uwe na mapambano mema.
TUPO PAMOJA.
www.kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 111; Kama NINGE….

Kama NINGEanza biashara kipindi kile nilipokuwa na kazi na nguvu bado, leo maisha yangu yangekuwa bora sana….

Kama NINGEchagua kuishi maisha ninayotaka kuishi mimi na sio maisha ya kuiga, leo hii nisingejikuta kwenye matatizo makubwa….

Kama NINGEpata muda wa kutosha wa kukaa na wale ninaowapenda, maisha yangu yangekuwa na furaha zaidi….

Kama NINGEchagua kutokukata tamaa, kuweka juhudi na maarifa katika kile nilichochagua kufanya, leo hii ningekuwa mbali sana….

Haya ni baadhi ya mambo ambayo watu wengi huwa wanajutia hasa pale ambapo maisha yao yanakuwa yameshafika ukingoni.

SOMA; KURASA YA 01; Maisha Unayoishi Ni Yako.

Kama unasoma hapa, kuna uwezekano mkubwa bado hujafikia hatua hii ya kuwa na majuto, lakini huenda umejisahau, na miaka 10, 20, au 30 ijayo, utakaa chini na kusema mija ya kauli hizo hapo juu.

Hakuna kitu kinaumiza kwenye maisha kama majuto. Hakuna kitu kinaumiza kama kujua wkamba ulikuwa na nafasi ya kufanya maisha yako yawe bora ila hukuichukua.

Ndio maana leo nakuambia kwamba, acha kutengeneza mazingira ambayo yatakufanya ujute sana baadae.

Chagua kufanya kazi au biashara unayoipenda, katika wakati huu ambao bado una nguvu za kuwez akupambana. Jali afya yako na ilinde sana maana hii ndio kila kitu kwako. Tengeneza mahusiano yako vizuri na watu wa karibu kwako, maana hawa ndio wanaokufanya uwe na maisha ya furaha.

SOMA; Ni Lipi Dhumuni Lako Kwenye Maisha? Langu Ni Hili Hapa.

Usijiweke kwenye mazingira yatakayokufanya wewe uwe na majuto baadae. Utaona maisha yako hayakuwahi kuwa na maana kabisa.

TAMKO LA LEO;

Najua mambo mengi ninayoyapuuza kwa sasa yatakuja kuwa sehemu ya majuto yangu hapo baadae. Kuanzia sas anayabadili maisha yangu, naishi maisha ambayo yana maana kwangu, nitafanya kile ninachopenda, nitajali afya yangu na kujenga mahusiano mazuri na wale ambao ni wa karibu kwangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 112 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuishi Maisha Yako Kwa Ukamilifu.

Work like you don't need the money. Love like you've never been hurt. Dance like nobody's watching. -Satchel Paige

Fanya kazi kama vile huhitaji fedha. Penda kama vile hujawahi kuumizwa. Cheza kama vile hakuna anayekuangalia.

Ukiweza kufanya mambo hayo matatu, utaishi maisha yako na mafanikio yatakuwa yako.

SOMA; Hii Ndio Sababu Kwa Nini Watu Wanafurahia Pale Unapoanguka...

Unapofanya kazi kama vile huhitaji fedha, utaweka nguvu zako zote na ubunifu wako mkubwa. Kwa hali hii utafanya kazi iliyo bora sana na utafikia mafanikio makubwa.

Unapopenda kama vile hujawahi kuumizwa unatoa upendo wako wote na bila ya kuangalia ni nini umewahi kupitia. Ukianza kuleta hisia zako za kuumizwa utaharibu tena mapenzi mapya.

Unapocheza kama vile hakuna anayekuangalia, unacheza vile unavyotaka wewe, bila aibu, bila kufikiria wengine wanakuchukuliaje. Na hivi ndivyo unavyotakiwa kuyaishi maisha yako. Bila kujali sana wengine wanasemaje kuhusu wewe.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

Monday, April 20, 2015

UKURASA WA 110; Ukomo Unaojiwekea Wewe Mwenyewe.

Mimi sio aina ya watu ambao wanaweza kufanikiwa kwenye biashara….

Mimi sio aina ya watu ambao wanapandishwa cheo kazini…

Mimi sio aina ya watu ambao wanaweza kufikia mafanikio makubwa…

Mimi sio aina ya watu ambao wanaweza kufanya mambo makubw akwneye maisha yao.

SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

Hizi ni baadhi ya kauli ambazo umekuwa unajiambia wewe mwenyewe. Unaona mtu amefanikiwa sana kwenye biashara unafikiria wewe utawezaje kufanikiwa kama yeye lakini kabla hujafika mbali unajikuta umeshajipa jibu kwamba wewe sio aina ya watu hao. Kwamba wao walipata nafasi ambayo wewe hujapata.

Unaona wenzako wakipata mafanikio makubwa kwenye kazi zao, wakipandishwa vyeo, unajiuliza wewe utawezaje kufikia ngazi kama hizo, kabla hujapata jibu unajikumbusha kwamba wewe sio aina ya watu hao. Kwanza wao wanabahati, wana ukaribu na wengine, lakini sio wewe.

SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.

Yote haya unayojiambia, kwanza ni uongo na pili unajiwekea ukomo wewe mwenyewe.

Hakuna mtu ambaye amezaliwa kuwa mtu fulani, kila kitu tunajifunz ahapa duniani. Kama kuna kitu chochote ambacho hukipendi kwenye maisha yako unawez akukibadili. Kama kuna kitu chochote ambacho ungependa kuwa nacho wkenye maisha yako unawez akukipata.

Hii ni kama utaondoa ukomo huu unaojiwekea kila siku. Na ukaanz akuchukua hatua, kuendea kile ambacho unakitaka.

TAMKO LA LEO;

Najua nimekuwa nikitu ia kauzli nyingi za kujiwekea kikomo na kukatisha tamaa. Najua kuna kipindi ambapo nimejiona mimi siwezi kwa sababu mbali mbali. Nimegundua huu sio ukweli na sasa nitaendela kile ambacho ninakitaka kwenye maisha yangu. Najua hakuna kinachoshindikana kama kweli nikiamua.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Tukutane kwenye ukurasa wa 111 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

Huu ni wakati ambao karibu kila mtu anahitaji kuingia kwenye biashara. Haijalishi mtu ameajiriwa au hana ajira, haijalishi kiwango cha elimu mtu alichonacho na wala haijalishi umri wa mtu, kwa sasa kila mtu anahitaji kuwa kwenye biashara.

Ajira zimekuwa za shida kupatikana na hata wale wanaozipata bado haziwawezeshi kuyamudu maisha. Changamoto ni nyingi sana. Njia ya uhakika ya kuweza kupambana na changamoto hizi ni kuingia kwenye biashara,

Mazingira ya kuingia kwenye biashara nayo yamebadilika pia. Tofauti na zamani ambapo ilihitaji mtu kuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha ndio aweze kuingia kwenye biashara, sasa hivi unaweza kuingia kwenye biashara kwa mtaji kidogo sana.

Pamoja na umuhimu huu wa kuingia kwenye biashara na urahisi wa kufanya biashara, bado kuna changamoto kubwa sana wkenye biashara. Biashara nane kati ya kumi zinazoanzishwa zinakuwa zimeshakufa ndani ya miezi 18. Na hata zile ambazo zinapona kipindi hiki, nyingi hazifikii mafanikio makubwa.

Watu wengi wanaweka juhudi kubwa sana kwenye biashara ila bado hawaoni mafanikio waliyotarajia. Hili linawaangusha wengi sana na wengi kukata tamaa.

Matatizo haya mengi yanatokana na kukosekana kwa elimu sahihi ya biashara, kukosa mtazamo sahihi wa kufanikiwa kwenye biashara, kutokujua mbinu za mafanikio kwenye biashara na kufanya biashara kwa mazoea.

Ili kuwasaidia wafanyabiashara na wale ambao wanapanga kuingia wkenye biashara kuweza kuondokana na changamoto hizi, AMKA CONSULTANTS imeandaa SEMINA YA MAFANIKIO KWENYE BIASHARA 2015. Semina hii itakupatia wewe elimu sahihi, mbinu muhimu na mtazamo sahihi utakaokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara yako.

Hii sio semina ya kukosa kwa sababu imejaa mambo mengi ambayo hujawahi kuyapata sehemu nyingine yoyote.

Semina hii imeandaliwa kuweza kukidhi mahitaji ya kufanikiwa kwenye biashara kwa mazingira yetu ya kitanzania. Semina hii itakuwezesha wewe kutoka hapo ulipo sasa na kupiga hatua kubwa sana kibiashara.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao na itaendeshwa kwa kipindi chote cha mwezi wa tano.

Washiriki wa semina hii watatumiwa email ya mafunzo kila siku asubuhi, kupata nafasi ya kuisoma na kuweza kuuliza swali popote ambapo hajaelewa. Email hizi zitakuwa na mafunzo yaliyofanyiwa utafiti w akina pamoja na mifano ambayo itamwezesha mshiriki kpata mawazo tofauti anayowez akuyatumia kwenye biashara yake na akafanikiwa sana.

Semina hii itafundisha mambo yafuatayo;

SEMINA YA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA.

Anza, kuza na fanikiwa kupitia biashara.

Yatakayofundishwa;

1. Utangulizi

1.1. Huu ni wakati mzuri wa wewe kuwa kwenye biashara.

1.2. Unawezakufanikiwa kwenye biashara.

1.3. Utakachokipata kwenye kozi hii.

2. Wazo la biashara

2.1. Biashara sahihi kwako kufanya

2.2. Jinsi ya kupata wazo bora la biashara

2.3. Jinsi ya kuboresha wazo lako la biashara

2.4. Baadhi ya mawazo ya biashara.

3. Mchanganuo wa biashara.

3.1. Umuhimu wa mchanganuo

3.2. Vitu muhimu vya kuweka kwenye mchanganuo wako

3.3. Udhaifu na uimara wako

3.4. Utafiti wa biashara yako

3.5. Ushindani.

3.6. Kuajiri wasaidizi bora kwenye biashara yako.

4. Mtaji na vyanzo vyake.

4.1. Aina za mtaji unaohitaji kwenye biashara

4.2. Mtaji wa fedha na vyanzo vyake

4.3. Njia bora za wewe kupata mtaji wa biashara.

5. Urasimishaji wa biashara

5.1. Umuhimu wa kusajili biashara yako.

5.2. Aina za usajili na faida zake

5.3. Hatua za kusajili biashara yako

5.4. Umuhimu na jinsi ya kulinda biashara yako.

6. Thamani ya biashara yako

6.1. Maandalizi ya bidhaa au huduma

6.2. Upatikanaji na upakiaji wa bidhaa au huduma

6.3. Upangaji wa bei.

7. Masoko na uuzaji.

7.1. Chagua soko la biashara yako

7.2. Mpango bora wa kutangaza biashara yako.

7.3. Njia rahisi za kutangaza biashara yako.

7.4. Mbinu za kuongeza mauzo kwenye biashara yako.

8. Mzunguko wa fedha.

8.1. Mauzo na faida.

8.2. Gharama muhimu za biashara

8.3. Gharama za kuepuka kwneye biashara

8.4. Kujilipa wewe mwenyewe.

8.5. Hesabu za fedha na umuhimu wa mhasibu.

9. Huduma kwa wateja.

9.1. Lengo la biashara ni kutengeneza wateja.

9.2. Jinsi ya kutoa huduma bora kwa mteja.

9.3. Mfanye mteja atangaze biashara yako.

9.4. Mteja ni mfalme na mwisho wa ufalme wake.

10. Changamoto za biashara.

10.1. Changamoto zinazoua biashara nyingi

10.2. Umuhimu wa mabadiliko

10.3. Mbinu za kufufua biashara inayokufa.

11. Mafanikio ya biashara yako

11.1. Jifunze kila siku

11.2. Matumizi mazuri ya muda

11.3. Kujihamasisha mwenyewe

11.4. Mafunzo kwa wafanyakazi wako

11.5. Usimamizi mzuri wa biashara yako.

11.6. Kununua uhuru wako kutoka kwenye biashara yako.

Gharama za kushiriki semina hii ni tsh elfu 30(30,000/=), ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii tuma fedha za kushiriki kwa Mpesa 0755953887 au tigo pesa/airtel money 0717396253 kisha tuma majina yako na email kwenye moja ya namba hizo na utaandikishwa kwenye semina hii. Uandikishaji unaanza leo tarehe 20/04/2015 na utasitishwa tarehe 01/05/2015. Wahi kujiandikisha mapema kwani nafasi ni chache na zitakapojaa utakosa nafasi hii adimu ya kupata maarifa ya kukuwezesha kufanikiwa kwenye biashara yako.

Kumbuka semina inafanyika kwa njia ya mtandao hivyo popote ulipo Tanzania na hata nje ya Tanzania unaweza kushiriki semina hii.

Semina itaanza rasmi tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima.

Karibu kwenye semina hii ambayo itakupatia kila unachohitaji ili kufanikiwa kwenye biashara yako.

Kumbuka maarifa ni nguvu, pata maarifa sahihi kupitia semina hii ili uweze kuwa na nguvu za kutosha na zitakazokuletea mafanikio makubwa.

Karibu sana na hakikisha hukosi semina hii kwa sababu yoyote ile.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani 

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322

NENO LA LEO; Kama Hutaki Kuwa Na Maadui Fanya Kitu Hiki Kimoja.

He who falls in love with himself will have no rivals. -Benjamin Franklin

Yule anayejipenda mwenyewe hawezi kuwa na maadui/wapinzani.

SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.

Njia moja ya uhakika ya kuepuka kuwa na maadui ni kujipenda wewe mwenyewe. Unapojipenda wewe mwenyewe utawapenda na wengine pia. Na mtu yeyote anayewapenda wengine bila ya ubaguzi ni vigumu sana kuwa na maadui.

Na hata pale watu watakapolazimisha kuw ana uadui na wewe, hilo halitakuwa tatizo kwa ko kwa sababu hutakuwa na muda wa kufuatilia hayo.

Jipende wewe mwenyewe, utawapenda wengine pia na utaondokana na maadui zako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.

Sunday, April 19, 2015

UKURASA WA 109; Ni Lipi Dhumuni Lako Kwenye Maisha? Langu Ni Hili Hapa.

Licha ya kuwa na malengo na mipango bado maisha yako yanahitaji kuwa na dhumuni. Dhumuni hili ni kile ambacho unataka maisha yako yawakilishe hapa duniani. Hivi ni vile ambavyo unataka maisha yako yawe kuhusiana na kile unachofanya.

Dhumuni lako kwenye maisha ndio litakaloendelea kukumbukwa hata pale utakapokuwa umeondoka kwenye dunia hii. Kwa mfano kama lengo lako ni kuwa na magari mawili, nyumba na mashamba, utakapoondoka kwenye dunia hii hakuna mtu atakayeendelea kusema mnamkumbuka Makirita, yule alikuwa na magari mawili, nyumba na mashamba? Habari kama hizi hazitasikika.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.

Kitakachosikika ni kile ambacho maisha yako yamefanikisha kukamilisha kwa ajili ya wengine. Zile alama ambazo umeacha kwenye maisha ya wengine. Hii itabaki milele na milele hata baada ya kuw aumeondoka kwenye dunia hii.

Dhumini lako kwenye maisha linatokana na maono yako kwenye maisha na linawahusisha watu wengine. Ni nini utakachofanya kwa ajili ya wengine? Hiki ndio kitakachokusukuma kuweza kufikia maono yako na dhumuni lako kwenye maisha.

Katika kazi yoyote au biashara yoyote unayofanya, unaweza kuacha alama kwenye maisha yako, fanya hili liwe dhumuni lako na angalia unaweza kutumia njia gani kufikia hilo.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

“DHUMUNI LANGU KWENYE MAISHA NI KUWASAIDIA WATU KUISHI MAISHA BORA NA YENYE MAFANIKIO KUPITIA MAFUNDISHO YANGU NA MAANDIKO YANGU.” Makirita Amani 

TAMKO LA LEO;

DHUMUNI LANGU KWENYE MAISHA NI _________________________________________________________________________________________________________________________ andika dhumuni lako hapo na uanze kulifanyia kazi kila siku kwenye maisha yako na kazi zako.

Tukutane kwenye ukurasa wa 110 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

NENO LA LEO; Hii Ndio Sifa Muhimu Ya Mtu Unayetakiwa Kumuajiri.

Do not hire a man who does your work for money, but him who does it for love of it. -Henry David Thoreau

Usimuajiri mtu anayefanya kazi yako kwa sababu tu anataka fedha, bali ajiri yule anayeifanya kwa sababu anaipenda.

Fedha sio hamasa nzuri ya kufanya kazi. Hii ni kwa sababu hakuna kiwango cha fedha ambacho mtu anaweza kuridhika nacho. Na mtu anapofanya kazi kwa ajili ya fedha tu, hakuna kitu kingine anachojali.

Ila mtu anayefanya kazi wka sababu anaipenda, ataweka juhudi na maarifa, atakuwa mbunifu na hii itamwezesha kufanya kazi yake kwa ubora wa hali ya juu sana. Katika hali hii atakufanyia kazi bora na yeye atapata kipato kizuri.

Nakutakia siku njema.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Saturday, April 18, 2015

UKURASA WA 108; Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu.

Hofu ni kikwazo kikubwa kwa wengi kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao.

Kama isingekuwa hifu leo hii ungekuwa mbali sana kuliko ulivyo sasa. Ndio nina uhakika kwa sababu wote tumekulia kwenye jamii ambazo zinatujaza sana hofu.

SOMA; Tumia Sheria Ya Mara 2, Mara 3 Kwenye Mipango Yako Ya Biashara.

Watu wengi wana hofu za kushindwa, hofu za kukataliwa, hofu za kupoteza, hofu ya kufa, hofu ya kuzungumza mbele ya watu na hofu nyingine nyingi.

Sasa leo nakushirikisha njia moja ya kuweza kuondokana na hofu yoyote inayokufanya ushindwe kuchukua hatua kwenye maisha yako.

Ili kuondokana na hofu, ijaze akili yako mawazo chanya muda wote. Usitoe nafasi yoyote ya mawazo hasi kuingia kwenye akili yako. Mawazo hasi ndio yanayokufanya ushindwe kujiamini na hatimaye uhofie kushindwa.

Jaza akili yako na mawazo ya upendo, amani, na maelewano. Fikiria kuhusu malengo na mipango yako, pata picha ya jinsi maisha yako yatakuwa mazuri kama ukiweza kufikia malengo uliyojiwekea. Itumie picha hii kukusukuma zaidi ili usirihusu mawazo hasi kukuingia na kukurudisha nyuma.

Kama ukiweza kufanya hivi, akili yako ya ndani itakuletea mazingira mazuri yatakayokupa wewe ujasiri na kukuwezesha kufikia chochote unachotaka kwenye maisha yako.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha Megaliving -By Robin Sharma

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba chanzo cha hofu zangu ni mawazo hasi ambayo yametawala akili yangu. Kuanzia sasa nitakuwa najaza mawazo chanya kwenye akili yangu ili niweze kupata ujasiri wa kuweza kuendea kile ninachotaka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 109 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Njia Ya Uhakika Ya Kufikia Mafanikio Makubwa.

If you want to be successful, it's just this simple. Know what you are doing. Love what you are doing. And believe in what you are doing. -Will Rogers

Kama unataka kufikia mafanikio, ni rahisi kama hivi. Jua ni nini unafanya. Penda kile unachofanya. Na pia amini kile unachofanya.

SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.

Jua kile unachofanya, kama hujui ni vigumu sana kufikia mafanikio. Jua ni nini unafanya na unataka kikufikishe wapi.

Penda kile unachofanya. Unapopenda unachofanya inakufanya wewe kuwa na hamasa kubwa na kuweka juhudi na maarifa hata pale unaposhindwa.

Amini kile unachofanya, mafanikio yanaanza na imani yako. Je unamini unachofanya kitakufikisha wkenye mafanikio, je unaamini kinawanufaisha wengine.

Vitu hivyo vitatu vitakufikisha kwenye mafanikio bila ya kujali ni kitu gani unafanya kwenye maisha yako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Sababu Zinazokufanya Wewe Kushindwa Kuthubutu Wazo Lako

Friday, April 17, 2015

UKURASA WA 107; Sema HAPANA, Hapa Ndio Uhuru Wako Ulipo.

HAPANA ndio neno gumu kusema kuliko maneno mengine yote. Hasa kwa watu ambao ni wa karibu au kwa vitu ambavyo unavipenda.

Lakini neno hili HAPANA ndio limebeba uhuru wako. Yaani uhuru wako upo ndani ya uwezo wako wa kusema hapana.

Kwa nini HAPANA ni muhimu?

Tunaishi kwenye dunia ambayo ina usumbufu mkubwa sana. Ukuaji wa teknolojia umerahisisha karibu kila kitu. Mtu anaweza kukupata kwa muda wowote anaotaka yeye na kwa njia yoyote anayoamua. Kuna vitu vingi sana vya kufanya kwa muda ule ule ambao tumekuwa nao enzi na enzi ambao ni masaa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki na wiki 52 kwa mwaka.

SOMA; Kama Unajiambia Hivi Mara Kwa Mara, Unaharibu sana maisha Yako.

Ili uweze kufanya mambo ambayo ni muhimu kwako, ni lazima uweze kusema hapana kwenye mambo mengi ambayo sio muhimu kwako na kusema ndio kwenye mambo amchache ambayo ni muhimu kwako.

Ni mambo gani ya kusema hapana?

Jambo lolote ambalo haliweki fedha kwneye mfuko wako, haliongezi maarifa kwenye akili yako au haliimarishi mahusiano yako ya kimaisha, kibiashara na kikazi unatakiwa kulisemea HAPANA haraka sana, maana hili linanyonya muda wako.

Hii inakwenda moja wka moja kwenye habari nyingi ambazo unafuatilia, mitandao mingi ya kijamii ambayo unatembelea kila siku na kila mara, mabishano yoyote yasiyo ya msingi, na maombi au mapendekezo ya wengine ambayo hayaingii kwenye mambo ambayo ni muhimu kwako.

Ni mambo gani ya kusema NDIYO?

Mambo yote ambayo yanakusogeza kwenye lengo lako, kazi unayofanya, biashara unayofanya, familia yako, muda wa kupumzika, na vingine ambavyo ni muhimu sana kwako.

SOMA; Ukweli Kuhusu Afya ya Wanaume; Kwa nini Wanaume Wanakufa Wadogo Kuliko Wanawake.

Uwezo wako wa kusema HAPANA, utakuwezesha kununua uhuru wako kwenye dunia ya sasa ambayo ina kelele na vishawishi vya kila aina.

TAMKO LA LEO;

Neno muhimu kwangu ni HAPANA. Nitasema hapana kwa kitu chochote ambacho hakiweki fedha kwenye mifuko yangu, hakiongezi maarifa kwenye akili yangu, au hakiimarishi mahusiano yangu na wale ambao ni muhimu kwangu. Muda ni mfupi na mambo ya kufanya ni mengi, HAPANA ndio uhuru wangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 108 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Unachotakiwa Kusema Na Unachotakiwa Kufanya.

I say what I want to say and do what I want to do. There's no in between. People will either love you for it or hate you for it. –Eminem

Nasema kile ninachotaka kusema na nafanya kile ninachotaka kufanya. Hakuna kuwa kati kati(vugu vugu). Watu watakupenda au kukuchukia kw akile unachosema na kufanya.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.

Usiseme kitu kwa sababu unataka kuwafurahisha watu. Usifanye kitu kwa ajili ya kuwafurahisha watu. Unaweza kuwafurahisha wachache ila pia utawachukiza wengine.

Kama watu watakuchukia kwa jambo ambalo hata wewe hulipendi, maisha yako yanaweza kuwa magumu zaidi.

Ni bora ufanye kile unachotaka kufanya, sema kile unachotaka kusema. Kuna ambao watakupenda kwa hilo na watakupa moyo wa kufanya zaidi. Na kuna ambao watakuchukuia na kukupinga kwa hilo, hawa hawatakusumbua kwa sababu kile ulichosema au kufanya ndio unachopenda au kujali.

Kitu kinapokuwa na maana kwako na kama sio kinyume na sheria na taratibu basi usihofu kuhusu wachache watakaokupinga.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.

Thursday, April 16, 2015

UKURASA WA 106; Usijaribu Kumbadili Mtu, Utapoteza Muda Wako…

Kuna wakati kwenye maisha huwa tunatamani watu wawe kama vile ambavyo sisi tunataka. Tunataka watu wawe na tabia zile tunazotaka na tunataka wafanye kile ambacho tunataka wafanye.

Kwa kufanikisha hili, tunajaribu kuwabadili, tunawawekea masharti fulani ili wabadilike. Lakini je tunaambulia nini? Hatuambulii chochote.

SOMA; Ukweli Kuhusu Maisha Ambao Kila Mtu Anapaswa Kuujua.

Kama kuna kitu ambacho watu hawapendi ni kulazimishwa kubadilika. Kila mtu anataka aone maisha yake ni muhimu kwake na hakuna anayempangia nini cha kufanya. Wewe unapojaribu kumbadili, tena kwa nguvu unamfanya awe mkali sana na ahakikishe uhuru wake anautetea.

Una mke/mume ambaye ana tabia ambazo huzipendi, unakazana kuzibadili. Lakini unaishia kushindwa kufanya hivyo. Una rafiki ambaye ungetamani awe tofauti na alivyo sasa, lakini ukijaribu kumbadili huwezi. Yote hii ni kwa sababu hiyo hapo juu.

Sasa unafanya nini?

1. Wakubali watu walivyo, usilazimishe mtu kubadilika.

2. Kama unaona kuna mabadiliko yanahitajika, mshauri mtu, muoneshe ni jinsi gani ambavyo akifanya kitu kw autofauti itakuwa faida kwake na kwako pia.

3. Usiweke mategemea makubwa kwa watu. Wape watu nafasi ya kukosea. Usiweke masharti kwa watu, kwamba ukifanya hivi ndio nitakupenda, kama unamkubali mtu mkubali alivyo.

4. Badilika wewe kwanza, na utaona mabadiliko makubwa kwa wengine. Hata kama hutabadilika tabia, badili mtazamo wako juu ya wale unaotaka wabadilike.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Na Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi.

TAMKO LA LEO;

Najua ni vigumu sana kubadili watu. Sitapoteza muda wangu kutaka kuwabadili watu, nitawashauri wabadilike kwa sababu itakuwa na faida kwao na kwangu pia. Na hata kama hawatabadilika, sitakuwa na tatizo nao.

Tukutane kwenye ukurasa wa 107 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

NENO LA LEO; Usilenge Mafanikio. Lenga Kitu Hiki Na Mafanikio Yatakuja Yenyewe.

Don't aim for success if you want it; just do what you love and believe in, and it will come naturally. -David Frost

Usilenge mafanikio kama unayataka, wewe fanya kile ambacho unapenda kufanya na amini kwenye kitu hiko na mafanikio yatakuja yenyewe.

Siku zote mafanikio yanakuja kw akufanya kitu ambacho unakipenda. Iwe ni kazi au biashara, hatua ya kwanza ya kufanikiwa ni kukipenda kile unachofanya.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha Megaliving -By Robin Sharma

Unapopenda unachofanya, unakuwa tayari kujitoa kwa moyo wako wote na unakuwa tayari kuweka juhudi, maarifa na ubunifu ili kutoa kilicho bora zaidi.

Unapotoa kilicho bora ndio unatengeneza njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Vipi kama hupendi unachofanya?

Unaweza kufanya mambo mawili.

1. Kipende.

2. Achana nacho na utafute kile unachopenda kufanya.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.

Wednesday, April 15, 2015

UKURASA WA 105; Njia Bora Kabisa Ya Kulipa Kisasi..

Kwanza kabisa, hakikisha hujengi uadui na mtu, jaribu kuishi bila ya kujiingiza kwenye matatizo na watu. Ila kama watu ndio watalazimisha kujiingiza kwenye matatizo na wewe basi leo nakupa njia bora kabisa ya kuweza kulipa kisasi.

Labda kuna watu ambao wanakupinga sana kwa kile ambacho unafanya. Labda kuna watu ambao wanakuwekea vikwazo ili tu ushindwe. Labda kuna watu ambao wanakazana usiku na mchana ili kuhakikisha wewe hufikii kile unachotaka. Na kwa hakika kundi hili ni kubwa sana.

SOMA; NENO LA LEO; Kisasi Bora

Je ni njia gani ambayo unaweza kutumia ili kupambana na kundi lote hili? Je unawezaje kulipa kisasi kwa watu ambao wamekuwa wanakazana kukurudisha nyuma na hata wakati mwingine kukuumiza?

Kwanza kabisa, kulipa kisasi kwa kurudisha mapambano ni sawana kumwaga petroli kwenye moto. Utawapa kila sababu ya wao kuendelea kukufanyia mashambulizi makali.

Njia bora kwako ya kulipa kisasi kwa watu hawa ni kuishi vizuri, kuwa bora zaidi na zaidi. Mtu anayekufanyia kila kitu ili ushindwe ataumia sana pale ambapo ataona unaendelea kufanikiwa sana. Kadiri anakazana kukurudisha wewe ndio unazidi kumuacha, hili linaweza hata likamuua kabisa.

SOMA; Mambo Matano(5) Ambayo Ni Marufuku Kufanya Kwenye Eneo La Kazi.

Ishi vizuri, kuwa bora sana kwenye kile ambacho unafanya. Hii ndio njia bora kabisa ya kulipa kisasi kwa wale wanaokurudisha nyuma, na wanaweza hata kufa kabisa.

Kama kuna chupa yenye tindikali, ikimwagika kidogo bado nyingi inaendelea kuwa ndani ya chupa. Hivi ndivyo ilivyo kwa watu wabaya, wanakumwagia wewe ubaya wao kidogo, ila mwingi zaidi upo ndani yao. Usiogope, jua ubaya umewajaa wao kuliko hata wanaokuonesha wewe. Kazana kuwa bora zaidi na acha wenye tindikali iwamalize yenyewe.

TAMKO LA LEO;

Najua kabisa ya kwamba njia bora ya kulipa kisasi ni kuwa bora zaidi, kuishi maisha mazuri na kuwa na mafanikio makubwa. Najua kwa kuwa na mafanikio makubwa nazidi kuwachanganya wale wanaonirudisha nyuma na wanaweza kufa kabisa. Sina muda w akujibizana na wanaonirudisha nyuma, nina muda wa kuboresha kile ninachofanya na kuishi maisha yangu.

SOMA; Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

Tukutane kwenye ukurasa wa 106 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Jambo Muhimu La Kufanya Kila Siku Unapoamka Asubuhi.

When you arise in the morning, think of what a precious privilege it is to be alive - to breathe, to think, to enjoy, to love. -Marcus Aurelius

Unapoamka asubuhi, fikiria ni jinsi gani ulivyo na bahati ya kipekee kuwa hai – kupumua, kufikiri, kufurahia, kupenda.

SOMA; TABIA ZA MAFANIKIO; Umuhimu Na Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Shukrani.

Kama huwezi kufurahia maisha yako kwa vile tu yalivyo unaweza kuwa na maisha magumu sana na maisha yako yatakwenda hivyo kwa muda mrefu.

Shukuru kwa maisha uliyonayo, kuwa hai ni zawadi ya kipekee kwako. Shukuru kwamba unaweza kupumua, shukuru kwamba unaweza kufikiri, shukuru kwamba umeweza kusoma hapa, shukuru kwamba unapenda na kuna wanaokupenda.

Usianze siku yako kwa kufikiria umekosa nini, kwa kufanya hivyo unakosa shukrani. Anza kwa kushukuru kwa vile ambavyo unavyo, ambavyo ni upendeleo mkubwa kwako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Tuesday, April 14, 2015

UKURASA WA 104; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuibadili Dunia.

Kila mmoja wetu ana uwezo mkubwa wa kuibadili dunia. Kila mmoja ana eneo lake ambalo kama akiweza kulitumia vizuri itakuwa faida kwake mwenyewe na kwa wengi wanaomzunguka.

Je wewe umeshapanga kuibadili dunia? Au unataka kuibadili dunia?

Kama ndio karibu, na kama hujui uanzie wapi basi leo unapata pa kuanzia.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Amua kwamba unakwenda kuibadili dunia kupitia kile ambacho unafanya au unataka kufanya. Kila kitu kinachofanyika na binadamu kina uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kwenye dunia. Iwe ni biashara, kazi au hata huduma yoyote ambayo mtu anaweza kuitoa.

Ukishaamua ni jinsi gani unakwenda kuibadili dunia, wekeza nguvu na jitihada zako zote kwenye kile unachofanya ili kuibadili dunia. Utakapofanya hivi, vitu viwili vinaweza kutokea.

1. Unaweza kufanikiwa kwa kila hatua na hapa tumia mafabikio haya kama motisha wa wewe kuendelea zaidi.

2. Unaweza kukutana na changamoto na kushindwa kwenye baadhi ya hatua, na hapa tumia changamoto hizi kujifunza zaidi ila usiache au kukata tamaa.

SOMA; Huu Ni Uwekezaji Wa Uhakika Ambao Hautakuangusha.

Lengo lako la mwisho ni kuibadili dunia, hayo mengine yote siyo ya msingi, usikubali yakupotezee muda.

TAMKO LA LEO;

Nimeamua sasa nakwenda kuibadili dunia kupitia_______________(sema kile unachofanya au utakachofanya).  Nitaweka juhudi na maarifa katika lengo hili na mafanikio nitakayopata nitayatumia kujihamasisha. Pia changamoto nitakazokutana nazo nitazitumia kama sehemu ya kujifunza. Nitakomaa na lengo langu hili, mengine yote yanaweza kusubiri.

Tukutane kwenye ukurasa wa 105 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.