Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, May 21, 2015

UKURASA WA 141; Kama Huna Hofu, Una Tatizo Kubwa Sana.

Hofu imekuw akikwazo cha watu wengi sana kufikia mafanikio makubw akwneye maisha yao. Unajua kabisa hutaki kubaki hapo ulipo, unajua unataka uanze biashara, unajua unataka uanze kuweka ubora kwenye kile ambacho unafanya ili uweze kupata mafanikio makubwa.

Unaweka malengo na mipango ya kukuwezesha kufika kule unakotaka kufika naunajua kila hatua unayotakiwa kufuata. Ila unapofika wakati wa utekelezaji ndio changamoto inapoanzia, hofu inabisha hodi, unaanz akufikiria itakuwaje kama ukishindwa, itakuwaje kama watu wakikukataa, watu watakuchukuliaje na mengine mengi yanayokufanya ushindwe kuchukua hatua.

SOMA; Fanya Tukio Hili La Kihistoria Ambalo Litakupa Uhuru Uliopoteza.

Swali je, hofu ni kitu kizuri au ni kitu kibaya? Kwa kuw ahofu imekuwa inakuzuia wewe kupata kile unachotaka utasema hofu ni kitu kibaya, na ndio maana inaendelea kukuandama mpaka sasa. Leo nataka nikuambie kwmaba hofu sio kitu kibaya, ni kitu kizuri ambacho unatakiwa kukifurahia.

Unapokuw ana hofu maana yake unajaribu kufanya kitu ambacho sio cha kawaida kwako. Unataka kufanya kitu ambacho ni cha juu kuliko ulivyozoea na ndio maana unafikiria kama utashindwa itakuwaje. Sasa hebu niambie, mafanikio yanakuja wakati gani? Pale unapofanya vitu ambavyo umezoea kufanya kila siku au pale unapokwenda hatua ya ziada? Wote tunajua hatua ya ziada ndio inayoleta mafanikio.

Hivyo basi tunatakiwa kufurahi sana pale tunapojikuta tunahofia kufanya kitu, kwa sababu hii ni dalili tosha kwamba kitu hiki kina manufaa makubwa kwako.

SOMA; Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu.

Kama huna hofu kabisa, una matatizo makubwa sana. Kuna uwezekano unafanya mambo yale yale ambayo umezoea kufanya. Sasa kwa kufanya hivi huwezi kupiga hatua yoyote, utaendelea kubaki hapo ulipo na kwa kuwa dunia inasonga mbele wewe utakuwa unarudi nyuma.

Sasa niifanyeje hii hofu? Niifurahie tu halafu ndio itanisaidia? Kwa kujua una hofu hapa ndio unapoanza kufanya kazi, chochote unachohofia anz akukifanya kidogo kidogo, gawa kweNye vipande vingi vidogo ambavyo unaweza kuvifanya bila ya kuwa na hofu kubwa. Kwa kuanza kufanya, utaanza kuona kadiri siku zinakwenda na hofu nayo inapotea na mwisho wa siku utaweza kukamilisha kile ulichokuwa unahofia kufanya.

SOMA; Hofu, Matumizi Mabaya Ya Ubunifu Wako.

TAMKO LA LEO;

Najua kwmaba hofu sio kitu kibaya, bali hofu ni dalili kwmaba nataka kufanya kitu ambacho sijazoea kukifanya. Badala ya mimi kuogopa hofu nitaikaribisha na kuanza kufanya kidogo kidogo mpaka nitakapokamilisha kile ninachotaka kufanya. Kutenda ndio dawa pekee ya kuua hofu, nitakuwa mtu wa vitendo kila mara.

Tukutane kwenye ukurasa wa 142 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment