Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, May 18, 2015

UKURASA WA 138; Nguvu Haipo Nje, Nguvu Unayo Ndani Yako…

Kila mtu anapenda kuwa bora zaidi ya alivyokuwa siku zlizopita. Kila mtu anapend akufikia mafanikio makubwa kuliko aliyonayo sasa. Lakini mbona bado watu wengi wanahangaika bila ya kupata mafanikio wanayotarajia? Kwa nini watu wanashindwa kuongeza juhudi kwenye kazi au biashara wanazofanya ili kuweza kufikia mafanikio makubwa?

Kuna sababu moja kubwa sana ambayo inawazuia wengi kuweza kufikia viwango vya juu kuliko walivyonavyo sasa. Na sababu hii ni kufikiri kwmaba nguvu wanayohitaji ili kuleta mabadiliko iko nje yao na hivyo kupoteza muda mwingi kuitafuta. Watu wengi wanashindwa kujua kwamba nguvu wanayohitaji tayari ipo ndani yao na jukumu lao ni kuanza kuitumia.

SOMA; Kama Umeajiriwa Na Hujaanza Kufanya Hili Jua Kuwa Unapotea.

Kwa mfano kama una kazi ambayo unajua unatakiwa uimalize ndani ya siku fulani, lakini ukawa umechoka sana ni rahisi kujiaminisha kwamba huna nguvu ya kuweza kukamilisha kazi kazi hiyo kwa muda uliopanga. Na hapa utaiahirisha mpaka siku nyingine ambapo utaona utakuwa na nguvu. Lakini ukiwa kwenye hali hiyo hiyo ya kuchoka na ukaambiwa nyumba yako inaungua moto utatoka kasi sana kwenda kufanya jitihada za kuokoa nyumba hiyo. Au kama utaambiwa kuna mtu wako wa karibu amepata ajali utapata nguvu ya haraka ya kwenda kusaidia.

Sasa nguvu hii ya ghafla inatoka wapi wakati wewe ulikuwa umechoka kabisa na kuamua kuahirisha kazi? Nguvu hii ipo ndani yako ila hujaweza kuifikia na kuitumia. Unayo nguvu kubwa sana iliyopo ndani yako. Unaweza kuitumia nguvu hii kama utajua jinsi ya kuifikia.

Ili uweze kufikia nguvu kubwa iliyopo ndani yako, tengeneza hamasa kubwa sana kwenye kile unachofanya. Ona faid akubw aunayoipata kw akukamilisha kile unachofanya na hii itakusukuma kuweza kufanya zaidi ya pale ulipofikia sasa. Kama ni kazi ambayo ni muhimu kwako kuikamilisha ila unaona umechoka, jipe hamasa kubwa itakayokusukuma kuifanya. Ona vile utakavyoboresha maisha yako kwa kukamilisha kazi hiyo. Ona ambavyo utapata muda wa kufanya mambo mengine muhimu kwako kw akukamilisha kazi hiyo. Na ona ambavyo utaweza kupumzika huku ukiwa huna mawazo ya kazi pale ambapo utakamilisha kazi yako kwa wakati.

SOMA; KITABU CHA MAY; A Long Way Gone(Historia Ya Kweli Ya Mdhara Ya Vita).

Nguvu ya kufanya jambo lolote kubwa ipo ndani yako, ni muhimu wewe kujihamasisha na kuweza kuitumia nguvu hii kufanya mambo makubwa.

TAMKO LA LEO;

Najua nina nguvu kubwa sana iliyopo ndani yangu ambayo ninaweza kuitumia kufanya mambo makubwa. Nitajihamasisha kila siku ili niweze kuitumia nguvu hii kuongeza thamani zaidi kwenye shughuli zangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment