Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, May 27, 2015

UKURASA WA 147; Njia Rahisi Ya Kufikia Uhuru Wa Kifedha.

Kama kichwa cha habari kimekuvutia na ukafikiri hapa utajifunza njia rahisi ya kupata fedha umekosea njia, hapa sikupi njia rahisi ya kupata fedha, haipo, kwa sababu kama ingekuwepo na jinsi ambavyo watu wanaipenda fedha kila mtu asingeijua.
Hapa nataka nikushirikishe njia rahisi ya wewe kufikia uhuru wa kifedha. Unakuwa na uhuru wa kifedha pale ambapo fedha sio changamoto kwenye maisha yako. Yaani una uhuru wa kipato ambacho kinaingia bila ya wewe kufanya kazi moja kwa moja na unaweza kupata mahitaji yako yote bila ya kuwa na changamoto kubwa.
SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.
Leo nataka nikuambie kwmaba uhuru wa kifedha hautegemei kiasi kuwa na kiasi kikubwa cha fedha, ila kuweza kutumia vizuri kiasi cha fedha ulichonacho hata kama ni kidogo.
Leo fanya zoezi hili moja, fikiria ungekuwa na dola bilioni moja kwenye akaunti zako za benki(hii ni sawa na trilioni mbili za kitanzania) ni mambo gani ungefanya. Yaani fikiria fedha sio tatizo, unazo zakukutosha na hata usipofanya kazi bado utakula wewe, watoto wako na wajukuu zako. Je ni vitu gani ambavyo ungefanya?
Orodhesha vitu hivi kwenye karatasi, usiache hata kimoja. Chochote unachofikiria utafanya kiorodheshe. Baada ya kukamilisha hatua hii ya kuorodhesha sasa nenda kwenye hatua ya pili na muhimu zaidi.
Hatua ya pili; kwenye orodha yako ondoa vitu vyote ambavyo ni vya anasa. Vifute kabisa vitu vyote ambavyo ni vya anasa, ambavyo sio muhimu uwe navyo ndio maisha yaende. Kwa mfano kama uliorodhesha kuwa na nyumba tatu za kuishi, huwezi kuishi kwenye nyumba tatu kwa wakati mmoja.
SOMA; Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.
Hatua ya tatu ni kuanza sasa kufanya yale ambayo yamebaki kwenye orodha yako baada ya kuondoa yale ambayo ni anasa.
Kwa kufanya hivi utafikia uhuru wa kifedha kwa sababu; hutakuwa na matumizi makubwa, utafanya vitu ambavyo unavipenda na hutojali sana kuhusu fedha.
TAMKO LA LEO;
Najua uhuru wa kifedha unapatikana pale ambapo ninafanya kitu ninachopenda kufanya na kuwa na matumizi mazuri ya fedha zangu. Kama ningekuwa na fedha za kutosha ningependelea kufanya vitu vifuatavyo, na vitu hivi ndio nitaanz akuvifanya sasa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 148 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment