Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, May 26, 2015

UKURASA WA 146; Ukiendelea Na Maisha Haya Watu Watakunyanyasa Sana…

Katika moja ya makala za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 tuliona kwmaba wewe mwenyewe ndio unaweza kutoa ruhusa ya mtu kukunyanyasa. Japokuwa ruhusa hii unaitoa pale unapokubali kunyanyasika na kitu anachofanya au anachosema mtu, kuna njia nyingine ya kunyanyasika ambayo hata kama hutakubali kuchukua kile ulichoambiwa au kufanyiwa bado utanyanyasika.

SOMA; Huyu Ndio Mtu Pekee Anayeweza Kukunyanyasa.

Njia hii ni pale ambapo unamtegemea mtu mwingine kwa jambo muhimu sana. Na yeye akawa na nguvu ya kuweza kukupa au kukunyima. Hapa unaweza kuruhusu manyanyaso makubwa sana na yatakayokufanya uishi maisha kama ya mfungwa.

Kwanza kabisa tuelewane kwamba binadamu wote tunategemeana, lakini utegemezi huu unakupokuwa mkubwa kwa upande mmoja ndipo manyanyaso yanapoanzia. Kwa mfano wewe ni mfanyabiashara, una bidhaa na huduma zako, unategemea mteja akupe fedha. Asipokupa anakosa huduma au bidhaa ambazo ni muhimu kwake. Kama wewe ni mfanyakazi ambaye una utaalamu, mwajiri wako anategemea utaalamu wako na juhudi zako na atakulipa kutokana na vitu hivyo.

Sasa fikiria pale ambapo unahitaji msaada wa moja kwa moja na huna kitu cha thamani cha kubadilishana na msaada huo. Hapa ndio unakaribisha manyanyaso makubwa. Tuseme wewe ni mtu mzima, ila maisha yako ni magumu, na una ndugu yako mmezaliwa tumbo moja ila yeye maisha yake ni mazuri sana. Unaona ndugu yako huyu ana jukumu la kukusaidia wewe, ndio anaweza kuwa nalo. Lakini halazimiki kuacha mambo yake yote kwa sababu tu anatakiwa kukusaidia wewe. Na kuna wakati utakuwa na uhitaji mkubwa sana na akakuambia haiwezekani. Utanyanyasika sana katika hali kama hii na unaweza kuona ndugu yako huyo hakujali.

SOMA; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani - 2

Kama hutaki kukaribisha kunyanyasika kwneye maisha yako hakikisha unajitegemea kw akiasi kikubwa sana. Na hata kama unahitaji kitu kutoka kwa mwingine, hakikisha una thamani ya kuwez akubadilishana na kile unachotaka. Vinginevyo utajiona wa chini mara zote na utanyanyasika.

Kama tungekuwa tunaishi kwenye zama za uwindaji ningekuambia, KULA ULICHOWINDA.

TAMKO LA LEO;

Najua njia rahisi ya kukaribisha manyanyaso ni kutegemea msaada wa moja kwa moja kutoka kwa wengine. Nitahakikisha naondoa hali hii kw akuweka juhudi na maarifa kwneye chochote ninachofanya, ili hata wakati ambapo nahitaji kitu cha ziada niwe na thamani ya kubadilishana. NITAKULA NILICHOWINDA.

Tukutane kwenye ukurasa wa 147 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment