Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, May 14, 2015

UKURASA WA 134; Hukuja Na Maelekezo Kwa Mtumiaji Na Kwa Nini Ufurahie Hili.

Ukienda dunaki kununua kitu chochote utapewa maelekezo kwa mtumiaji. Kwa vitu vidogo vidogo yanaweza maelekezo yasiambatanishwe hii ni kwa sababu kila mtu anajua utumiaji wake.

Lakini nenda kanunue simu mpya leo na ndani ya boksi la simu hiyo kuna kitabu chenye maelekezo kwa mtumiaji, tena kina maelezo rahisi na picha pia. Nenda kanunue kompyuta na utakuta kitabu cha maelekezo kwa mtumiaji. Kanunue tv, redio, friji, na hata gari utakuta ndani kuna kitabu kinachotoa maelekezo kwa mtumiaji.

Kitabu hiki kina nini basi? Najua wengi hatuvisomi kwa sababu huwa tunaona tunajua kile tunachohitaji kufanya. Na kama tukipata matatizo wkenye vifaa vyetu, cha kwanza kuangalia ni kitabu cha maelekezo kwa mtumiaji. Kitabu hiki kinaeleza shughuli unazoweza kufanya na kifaa husika, jinsi ya kukitumia na jinsi ya kukihifadhi. Msisitizo mkubwa upo kwenye matumizi ya kifaa husika na huwezi kukitumia kwa malengo mengine nje ya yale yaliyoandikwa pale, kitaharibika na hata ukiomba kulipwa hutolipwa.

Kwa kufuata maelekezo ya kitabu cha maelekezo kwa mtumiaji, watu wote tunatumia vifaa vyetu kwa aina moja. Kila mtu aliyenunua redio ataitumia kusikiliza mziki, tv kuangalia, simu kuwasiliana.

Lakini sisi binadamu, mimi na wewe hatukuja hapa duniani tukiwa na kitabu cha maelekezo kwa mtumiaji. Iwe mtumiaji ni wewe mwenyewe au wale waliokulea ukiwa mdogo, hukuwa na kitabu cha maelekezo. Ndio maana kila mtoto ana ukuaji wake wa tofauti na hata malezi yao hayafanani. Kwa wenye watoto mnalielewa hili. Mama hata awe na watoto watano, bado akipata mtoto wa sita atampa changamoto . Kwa sababu kila mtoto anakuja tofauti na hakuna anayekuja na kitabu cha maelekezo kwa mtumiaji.

Lakini cha kushangaza tunapokua tunalazimishwa na kujilazimisha kuwa kama kila mtu. Wote tende shuleni tufaulu mitihani, tupate kazi, tuwe na nyumba, gari na madeni, tufanye kazi miaka mingi mpanga nguvu zituishie, tustaafu halafu tufe. Kwa nini tulazimike kwenda na hali hii? Nani alikuja kututengenezea hiki kitabu cha maelekezo kw amtumiaji tukiwa watu wazima?

Hukuja na kitabu cha maelekezo kwa mtumiaji na hii ina faid akubwa sana kwako. Unaweza kuwa chochote unachotaka, unawez akufanya chochote unachotaka, hakuna wa kukuzuia na hakuna wa kukuambia wewe ulizaliwa uwe hiki, au ufanye hiki. Yeyote atakayekuambia hivyo mwambie akupe kitabu cha maelezo kwa msomaji ulichozaliwa nacho. Hakuna kitabu hiki na furahia sana hili.

Fanya kitu kwa sababu ndio kitu unachopenda kufanya, ndio kitu ulichoamua kufanya na sio kwa sababu ndio kila mtu anakifanya. Ukiweza kuishi maisha haya, utakuwa na furaha sana bila ya kujali ni maisha gani unayoishi.

TAMKO LA LEO;

Sikuja duniani na kitabu cha maelekezo kwa mtumiaji na hii ina maana kubwa sana kwangu kwaba sikuzaliwa niwe kama ambavyo watu wananilazimisha niwe. Nimezaliwa nikiwa na uhuru wa kuchagua chohcote ninachotaka na chochote ninachopenda, nitailinda haki yangu hii ya msingi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment