Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, May 31, 2015

UKURASA WA 151; Je Unazalisha Au Wewe Ni Mtumiaji Tu?



Katika dunia tunayoishi, kuna makundi mawili ya watu. Kuna kundi la watu ambao ni wazalishaji, hawa ni watu ambao wanatuletea vitu vyote tunavyotumia. Simu, tv, vyakula vizuri, vitabu, makala tunazosoma, nguo tunazovaa, magari na vingine vingi. Kundi la pili ni la watumiaji. Hawa ni watu ambao wanatumia vitu hivi vinavyotolewa na wazalishaji.
Kwanza kabisa kila mmoja wetu ni mtumiaji wa kitu kinachotengenezwa na wengine. Huu sio ulimwengu ambao unaweza kujitegemea wewe mwenyewe kwa kila kitu. Unategemea vitu vingi sana kutoka kwa wengine ili maisha yako yaweze kwenda vizuri.
Swali kubwa la kujiuliza ni je wewe unazalisha nini? Ndio umekuwa mtumiaji mzuri, lakini ni kitu gani ambacho unazalisha kwa ajili ya wengine? Unatumia simu nzuri na kuifurahia ila kumbuka kuna mtu amekaa chini, usiku na mchana kutengeneza simu hiyo nzuri unayoipenda leo. Je wewe ni kitu gani kimekuchukua usiku na mchana kufanya na kikafika kwenye mikono ya watumiaji wakafurahi sana? Unavaa nguo nzuri na kujiona unakwenda na wakati, umependeza, lakini kuna watu ambao wamefanya kazi kubwa sana mpaka wakaweza kuja na nguo hizo.
Kazi yako au biashara yako ilikuwa iwe sehemu nzuri sana ya wewe kuzalisha, lakini je unazalisha kupitia hiko unachofanya? Ni kweli unahangaika usiku na mchana kuhakikisha kile unachozalisha kikimfikia mtu atakifurahia sana? Je unatoa kile kilicho bora sana na kujisukuma zaidi ili kufanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi? Kama ambavyo wengine wanafanya kwenye maisha yako?
Wakati mwingine unapoangalia kitu kizuri unachotumia, jiulize ni kitu gani wewe umezalisha na mtu anayekitumia anafurahia kama wewe unavyofurahia kilichozalishwa na wengine. Hii ikupe hasira ya wewe kuzalisha kilicho bora zaidi. Usikubali kuwa mtumiaji tu, kuwa mzalishaji pia.

TAMKO LA LEO;
Nimechoka kuwa mtumiaji na kufurahia vitu vilivyozalishwa na wengine tu. Sasa na mimi nitakuwa mzalishaji ambaye natoa vitu wengine watavifurahia na kuboresha maisha yao. Nitafanya hivi kupitia kazi au biashara ninayofanya. Najua sijayaishi maisha yangu kama sijaweza kuyabadili maisha ya mwingine kupitia ninachofanya.

Tukutane kwenye ukurasa wa 152 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment