Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, May 29, 2015

Ukurasa Wa 149; Hawa Ndio Watu Unaotakiwa Kuwafikiria Zaidi.



Utakapoamua kuboresha maisha yako, utakapoamua kufanya tofauti na ulivyokuwa unafanya na utakapoanza kupata majibu ya tofauti na uliyokuwa unapata mwanzo, kuna watu watakuchukia. Nataka nikuambie hilo wazi. Kuna watu watakuchukia wazi wazi na kukuambia huwezi au unapoteza muda wako, na hata ukiweza watakuambia subiri. Na kuna wengine watakuchukia kwa ndani bila ya wewe mwenyewe kujua, ila utaona wamepunguza ushirikiano na wewe.

SOMA; Haya Ndio Makundi Matatu Ya Watu, Je Wewe Upo Katika Kundi Lipi?

Habari nzuri ninazotaka kukupa pia ni kwamba kwa kuamua kufanya hivi kuna watu ambao watakupenda. Kuna watu watafurahia jinsi maisha yako yamebadilika, kuna watu watapenda thamani uliyoongeza na wataendelea kuwa na wewe.
Sasa ni watu wapi ambao atakunyima usingizi, ni wapi ambao utawafikiria zaidi? Kwa hali ya kawaida ya kibinadamu utawafikiria sana wale ambao wanakuchukia au wanakupinga. Ukifikiria ni njia gani unaweza kutumia ili kuwaonesha kwamba wewe ni zaidi ya wanavyofikiria. Kuwaonesha kwamba hawakujui vizuri. Unaweza kufanya hivi ila nataka nikuambie kwamba utakuwa unapoteza muda wako bure. Watu ambao hawakukubali sasa, hawatakukubali milele au huenda itawachukua muda mrefu kufanya hivyo, chochote utakachofanya, watatafuta njia ya kuona kwamba bado huwezi.
 
SOMA; Hiki Ndio Kitu Kikubwa Unachohitaji Kufanya Ili Kuboresha Maisha Yako(Zawadi Yangu Kwako).
Tumia muda wako mwingi kuwafikiria wale ambao wanakukubali na kupenda kile unafanya. Watu hawa wakunyime usingizi ukifikiria ni jinsi gani unaweza kuwaboreshea zaidi kile wanachokipenda na kwa njia hii utawanufaisha zaidi na wao watakunufaisha zaidi na pia watakuletea wengi zaidi wa aina kama yao.
Ukitumia muda mwingi kuwafikiria wale ambao wanakuchukia na kukupinga, unawadhulumu wale ambao wanakupenda na kukuhamasisha. Muda ni mfupi sana kuanza kuhangaika na watu ambao hawajali na hawatojali, fanya kazi na wale wanaojali, na utakuwa na maisha yenye furaha na mafanikio.
TAMKO LA LEO;

Muda wangu ni mfupi sana siwezi kuutumia kuwafikiria wale ambao wananichukia na kunipinga. Nitatumia muda huu kuwafikiria wale wanaonipenda na kunikubali. Nitaendelea kufanya kile ninachofanya kwa ubora wa hali ya juu sana kwa sababu najua ndio kitakachoniletea mafanikio na furaha kwenye maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 150 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment