Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, May 8, 2015

UKURASA WA 128; Ni Sawa Kama Hutapata Kile Unachotaka.

Kila mmoja wetu ana malengo na mipango yake kwenye maisha, na hiki ndio kitu ambacho kimekuwa kinakusukuma uweke juhudi zaidi kwenye kile unachofanya.

Lakini hakuna ambaye ana uhakika wa kile ambacho kinaweza kutokea kesho. Na hii ndio sehemu muhimu ambayo unatakiwa kujipa ruhusa kwa sababu kushindwa kufanya hivyo utaishi maisha ya majito.

SOMA; Kama Unataka Maisha Yako Yawe Bora Na Yenye Mafanikio, Acha Kufanya Kitu Hiki Kimoja.

Unaweza kuweka malengo na mipango mizuri sana, unaweza kufanya kila ambacho kipo ndani ya uwezo wako, na bado mambo yakaenda vile ambavyo hukutegemea yaende. Ukashindwa kupata kile ambacho ulitegemea kupata.

Na hii ni sawa kabisa.

Ni sawa kama watu hawatakubaliana na wewe kwa kile unachofanya

Ni sawa kama hujui ni nini utafanya baada ya sasa.

Ni sawa kama utashindwa au kufukuzwa au kukataliwa.

Ni sawa kama utaanza biashara na ukapata hasara.

Ni sawa kama hujui unataka uanzie wapi.

Ni sawa kama utafanya baishara na kufanikiwa.

Ni sawa kama utakuwa bilionea.

SOMA; UKURASA WA 80; Utabiri Mzuri Wa Kesho.

Kwa sababu hayo ndio maisha yenyewe. Maisha ni darasa ambalo kila mtu anajifunza, kila mtu yuko kwenye kiwango chake cha mafunzo ambacho hakifanani na mtu mwingine. Ni sawa pia.

Unapoweka mipango na ukashindwa kuifikia kumbuka sio kwamba wewe huwezi, au sio kwamba huna bahati, bali kuna vitu muhimu hujaweza kuvifanya vizuri. Kwa kufanya vitu hivi kwa umakini utajipa nafasi nzuri ya kuwezakufikia kile unachotaka.

Unapoweka mipango yako na ukaweza kuifikia, sio kwamba wewe unaweza sana au una bahati sana, ni kwamba umejua njia unayofanya kazi na umeweza kuitumia vizuri. Endelea kuitumia.

Maisha ni yako na machaguzi ni yako, hakikisha unasimamia machaguzi yako.

TAMKO LA LEO;

Ni sawa kama nitafanya kitu nikashindwa, ni sawa kama nitafanya kitu nikashinda. Najua hakuna aliyeniahidi kwamba kila nitakachogusa kitakwenda vizuri na licha ya mipango ninayoweka bado sijui kesho ni nini kitatokea. Nitajifunza kwenye kila kinachotokea kwenye maisha yangu, ili niweze kuwa bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda.

Tukutane kwenye ukurasa wa 129 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment