Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, May 22, 2015

UKURASA WA 142; Maisha Ni Mafupi, Usiyapoteze Kwa Kufanya Mambo Haya….

Miaka 100 ijayo kila mtu anayesoma hapa sasa hivi atakuwa amekufa. Kitachobaki kwenye dunia hii sio mipango mikubwa uliyokuwa nayo, na wala sio ahadi nyingi ulizoweka, bali ni jinsi gani uligusa maisha ya wengine kw akile ambacho ulikuwa unafanya.

SOMA; Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo..

Kama miaka 100 ijayo hutakuwepo hapa duniani hii ina maana gani kwako? Maana halisi ni kwmaba maisha ni mafupi, dunia ina umri mrefu sana ukilinganisha na miaka chini ya 100 utakayoishi hapa duniani. Hivyo basi hebu muda huu mfupi usioupoteze kw akufanya mambo ambayo hayataacha kumbukumbu pale utakapoiacha dunia hii.

Maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa kufanya kitu ili wengine wakupende. Fanya kitu unachopenda na wale wanaokupeda kweli watakuwa na wewe.

Maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa kuweka mipango mingi ambayo huifanyii kazi kw akigezo kwamba bado hujawa tayari, anza kufanya sasa na mengine utajifunza mbele ya safari.

Maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa kuishi maisha ya maigizo. Kufanya mambo kwa sababu kila mtu kwenye jamii anafanya. Fanya yale ambayo ni muhimu kwako.

SOMA; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani - 2

Maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa kujali ni nini watu wengine wanafikiria au kusema juu yako. Hawana uhakika ni nini unafanya au hata wao wenyewe wanafanya. Hivyo wataongea mengi ya kukukatisha tamaa, usiwasikilize.

Maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa kufikiria ufupi wa maisha, bali yaishi kwa kila siku, kila saa na kila sekunde.

Maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa kugombana na watu, kushindana na watu na mambo mengine ambayo hayaongezi thamani kwenye maisha yako. Yafanye maisha yako kuwa bora kila siku, hayo mengine yatakuwa sawa yenyewe.

SOMA; Fanya Kama Hakuna Anayekuangalia.

TAMKO LA LEO;

Najua maisha ni mafupi na hivyo nitayaishi kw akufanya kile ambacho napenda kufanya na kuacha alama kwenye maisha ya wengine ambayo itaendelea kuonekana hata baada ya kuondoka kwenye dunia hii. Kila siku, kila saa na kila sekunde ninayoishi ni nafasi ya pekee kwangu kufanya lililo jema na kuboresha maisha yangu na ya wale wanaonizunguka.

TAFADHALI TUMA UJUMBE HUU KWA MARAFIKI ZAKO KWA EMAIL NA MITANDAO YA KIJAMII, NI SEHEMU YA WEWE KUACHA ALAMA.

Tukutane kwenye ukurasa wa 143 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment