Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, May 24, 2015

UKURASA WA 144; Huu Ndio Ukweli Kuhusu Wewe.

Leo nataka nikuambie ukweli kuhusu wewe, ndio wewe hapo una mambo mengi mazuri unayoweza ila unayakwepa. Kuna ukweli mwingi sana kuhusu wewe lakini umeamua kutokuufanyia kazi. Kwa kutojua ukweli huu na kutoufanyia kazi imekuwa kikwazo kwako kuboresha maisha yako.

SOMA; Usijaribu Kumbadili Mtu, Utapoteza Muda Wako…

Huu ndio ukweli kuhusu wewe…

Wewe ni mtu bora sana na wa kipekee,

Wewe ni mtu mzuri, mwaminifu, mkweli na mchapa kazi.

Wewe ni mtu unayewaheshimu wengine na kuwafanyia yaliyo mema.

Wewe ni mtu ambaye umejitoa kwa ajili ya familia yako, ndugu na jamaa zako, pamoja na kazi au biashara yako.

Wewe ni mtu imara, unayejiamini na unayekubali majukumu yako.

Wewe ni mtu ambaye una akili, una ujuzi na una uzoefu mkubwa.

Wewe ni muhimu sio tu kwa watu wanaokuzunguka, bali kwa jamii nzima.

Wewe umezaliwa kwa sababu maalumu na jukumu kubwa la kutimiza hapa duniani.

SOMA; Mambo Madogo Ndio Muhimu Sana.

Huyu ndio wewe, sio mwingine bali wewe unayesoma hapa. Yawezekana mengi kati ya haya huyafanyii kazi kwa sasa, hii ni kwa sababu unaamua kuukataa ukweli kuhusu wewe. Hebu kuanzia leo uanze kuishi ukweli huu na utaona kama maisha yako yataendelea kubaki kama yalivyo.

Ishi ukweli huo, usikwepe hata kimoja. Maana huyo ndio wewe, na ukiwa hivyo ni lazima utakuwa na maisha bora na yenye mafanikio.

TAMKO LA LEO;

Ukweli ni kwamba mimi ni mtu wa kipekee, ni mtu ambaye ninaweza kufanya makubwa kwangu na kwa wanaonizunguka pia. Japokuwa sijaishi ukweli huu kwa asilimia 100, nitaanza sasa kuuishi ili niboreshe maisha yangu na ya wale wanaonizunguka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 145 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment