Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, May 23, 2015

UKURASA WA 143; Wewe Ni Sumaku…

Wewe ni sumaku inayoishi. Nafikiri unaijua sumaku, na unajua tabia za sumaku. Kama umesahau sumaku, ni chuma ambacho kina uwezo wa kuvuta vyuma vingine. Sumaku haiwezi kuvuta kila kitu, ila inaweza kuvuta vile vitu ambavyo vinatabia za kufanana na sumaku. Sumaku itavuta chuma, lakini haiwezi kuvuta plastiki.

Wewe ni sumaku inayoishi na una tabia zote za sumaku. Wewe kama sumaku inayoishi, unavuta kwenye maisha yako, vile vitu ambavyo vinafanana na wewe. Kila kitu ambacho kinaendelea kwenye maisha yako, umekivuta mwenyewe, hakuna mtu aliyekuletea. Mke au mume uliyenaye, marafiki ulionao, maisha unayoishi, kipato unachopata vyote umevivuta wewe mwenyewe.

SOMA; Hatua Saba (7) Za Kuweka Malengo Na Kuweza Kutimiza Ndoto Zako.

Na sio kwamba vitu hivi unavivuta kw anguvu, bali unavivuta kwa mawazo yako. Kile ambacho unawaza kwenye akili yako kwa muda mrefu ndio kinachotokea kwenye maisha yako. Yale mawazo uliyonayo kuhusu kipato chako, kuhusu hali ya maisha yako, kuhusu marafiki zako ndio yanakuletea vitu hivyo.

Kama unataka kubadili maisha yako, kama unataka kuwa na marafiki ambao wanamwelekeo wa mafanikio, kama unataka kuwa na maisha ya mafanikio, basi anza kwa kubadili mawazo yako. Acha kufikiria mawazo ambayo yanakuletea vitu vya chini na waza mawazo yatakayokuletea vitu vilivyobora.

SOMA; Sifa Sita(6) Unazohitaji Ili Kuwa Mjasiriamali Bora.

Na kumbuka kuwaza tu hakutakuletea maisha unayotaka, utahitaji kuweka juhudi pia. Lakini juhudi ukiwa na mawazo yasiyojenga, ni kazi bure. Kuwa na mawazo sahihi, halafu weka juhudi za kutosha. Tutakutana kileleni.

TAMKO LA LEO;

Mimi ni sumaku inayoishi na vitu vyote nilivyonavyo kwenye maisha yangu nimevivuta mwenyewe kutokana na mawazo ambayo nimekuwa nayo. Najua kama nahitaji kubadili eneo lolote la maisha yangu, nahitaji kubadili kwanza mawazo yangu na kuendelea kuweka juhudi ndio nitayaona mabadiliko ya kweli.

Tukutane kwenye ukurasa wa 144 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment