Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, May 16, 2015

UKURASA WA 136; Unataka Kubaki Hapo Ulipo Au Unataka Kwenda Mbele?

Unataka kubaki hapoo ulipo au unataka kwenda mbele? Swali rahisi sana na najua kila mtu jibu lake ni NDIO nataka kwenda mbele zaidi.

Lakini tatizo sio kutaka kwenda mbele, tatizo ni kujua kipi kitakufikisha mbele, utawezaje kwenda mbele zaidi ya ulipo sasa?Na hata baada ya kujua kwmaba utakwendaje mbele, je upo tayari kufanya hivyo?

Kama umewahi kuona mtu anayebeba vitu vizito, vyuma, huwa anaanzia wapi? Anaanza na uzito mdogo, anabeba uzito huo mdogo kwamuda halafu anaendele akuongeza kidogo kidogo. Kwa mfano anaanza na kilo 20, baada ya muda anakwenda 25, naadae 30, baadae 50 mpaka anaziti kilo 100.

SOMA; Jinsi Unavyoweza Kutumia Changamoto Kama Fursa Ya Kujifunza Zaidi.

Kwa nini haanzii kilo 100 moja kwa moja? Kwa sababu hawezi. Kwa nini aendelee kuongeza uzito kadiri siku zinakwenda? Kwa sababu ndivyo kukua kulivyo.

Huyu mbeba vyuma kama atabeba kilo 20 tu hata kama ataubeba uzito huu kila dakika ya siku na kila siku kwa miaka yote, bado haitampa uwezo wa kubeba kilo 100. Misuli inakua na kuweza kuhimili uzito mkubwa pale inapoongezewa uzito, pale inapoongezewa changamoto. Kwa kubeba uzito ule ule kila siku, misuli inaendelea kuwa na nguvu ile ile. Ukitaka upate nguvu zaidi unahitaji kuongeza uzito zaidi.

Sasa tuje kwako rafiki yangu wa karibu, wewe upo na tatizo lile lile kila siku, changamoto yako ni ile ile, hudhubutu kujiingiza kwenye changamoto nyingine, je unafikiri unakua? Unafikiri unasonga mbele? Hakuna, hata kama utakaa na changamoto hiyo miaka yako yote, hujakua, hujaenda mbele, umedumaa na umerudi nyuma.

SOMA; KITABU CHA MAY; A Long Way Gone(Historia Ya Kweli Ya Mdhara Ya Vita).

Wewe kila siku unasema unataka kufanya biashara ila changamoto yako ni mtaji, miaka inakwenda lakini bado changamoto yako ni hiyo hiyo, je unafikiri unasonga mbele? Hapana.

Wewe unafanya kazi ile ile kwa mtindo ule ule unaofanya kila siku. Yaani ukienda ofisini leo unarudia kile ambacho ulifanya jana na juzi na wiki iliyopita. Unafikiri unakua kwenye kazi hiyo? Unafikiri unasonga mbele? Hapana. Halafu unaweza kutumambia una uzoefu wa miaka 10 kwenye kazi unayofanya, kweli? Sio una uzoefu wa mwaka mmoja mara 10? Hebu jitathmini vizuri rafiki yangu. Kama kweli upo tayari kusonga mbele au unataka kuendele akubaki hapo ulipo.

SOMA; Upya Wa Biashara Mpya Na Unavyoweza Kuutumia Vizuri…

TAMKO LA LEO;

Najua siwezi kusonga mbele kama nitaendelea kufanya kile ambacho nafanya sasa hivi. Najua siwezi kusonga mbele kama nitaendelea na changamoto niliyonayo sasa hivi. Nahitaji kufanya mambo tofauti, nahitaji kuwa na changamoto mpya.

Tukutane kwenye ukurasa wa 137 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment