Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, May 7, 2015

#NENO_BUSARA; Matumaini Sio Mpango.

Mara nyingi mambo yanapokwenda vibaya, au yanapokuwa magumu mtu huwa na matumaini kwamba hali itabadilika tu.
Sio vibaya kuwa na matumaini, ila nataka nikukumbushe kwamba matumaini sio mpango.
Ukiacha mambo yawe mazuri yenyewe huo sio mpango mzuri kwako na hivyo huwezi kupata kilicho bora.
Kama unataka kuondoka kwenye hali ngumu uliyonayo sasa, au utakayokutana nayo ni lazima uwe na mpango.
Halafu uufanyie mpango huo kazi.
Ni mimi KOCHA WAKO.
Ungana nami kwenye ukurasa wa facebook ambapo nitakuwa nakupa mambo muhimu ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla. Bonyeza Coach Makirita Amani na ulike hiyo page ili usikie kutoka kwangu mara kwa mara. Waalike wengine nao wa-like.
Kila la kheri.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment