Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, February 2, 2015

SIRI YA 3 YA MAFANIKIO; Mtazamo Wako Utaamua Mafanikio Yako.

Mtazamo wako ni picha ya akili yajo. Ni jinsi ambavyo unaona vitu.
Mafanikio yako yatatokana na kile unachoona, iwe unaona uwezekano au unaona changamoto.
Kuwa na mtizamo chanya hakukuhakikishii mafanikio. Lakini unaookuwa na mtizamo chanya una nafasi kubwa ya kufanikiwa.

“Things turn out the best for the people  who make the best of the way things turn out.” - John Wooden

#HADITHI_FUNZO; Dakika Ya Mwisho Kabla Ya Kufa…

Mtu mmoja alikuwa akipita msituni na hamadi akakutana na chui mkali.  Ili kuokoa maisha yake alikimbia sana. Kwa mbio zake alijikuta kwenye kona ya mteremko mkali sana. Palikuwa na mzabibu uliokuwa unaning’inia kwenye mteremko ule na hivyo akaninginia nao.

SOMA; Kitu Kimoja Cha Kufanya Kila Siku Ili Ufikie Malengo Yako 2015…

Akiwa pale na kujua ndio mwisho wa maisha yake aliona panya wakimega mzabibu ule. Alipoangalia kwa karibu aliziona zabibu, alichuma chache na kuweka mdomoni mwake. Zilikuwa zabibu tamu sana.

Tunajifunza nini kwenye hadithi hii?

1. Hata pale unapofikia wakati wa mwisho kabisa na ukaona hakuna tumaini tena, endelea kuishi maisha yako.

2. Tafuta kitu kizuri hata kama upo katika hali ngumu kiasi gani.

Unaweza kuongeza vingine ulivyojifunza kwenye maoni hapo chini.

SOMA; Je Upo Tayari Kupata Unachotaka? Siri Ni Hii Moja…

UKURASA WA 33; Tengeneza Mtandao Wako Wa Mafanikio.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu yeye mwenyewe. Na hata kwenye mafanikio, hakuna mtu ambaye anaweza kusema amefikia mafanikio yeye mwenyewe kwa nguvu zake mwenyewe tu.

Ili kufikia mafanikio unahitaji ushirikiano wa watu wengi sana.

Ni muhimu sana kutengeneza mtandao ambao utakufikisha kwenye mafanikio. Shirikiana na watu ambao wana malengo ya kufikia mafanikio kama wewe.

Kumbuka mafanikio yako ni wastani wa mafanikio ya watu watano unaokuwa nao kwa muda mrefu. Hivyo kama unashirikiana na watu ambao hawana njaa ya mafanikio na wewe hutofikia mafanikio.

SOMA; SIRI 50 ZA MAFANIKIO.

Mafanikio yako yanategemea ni watu wangapi wenye mafanikio wanaokuzunguka zaidi ya kile unachofanya.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba mafanikio yangu yanategemea sana wale wanaonizunguka. Hivyo kama nataka kufanikiwa zaidi inabidi nizungukwe na wale ambao wamefanikiwa zaidi. Nitajenga mtandao mzuri utakaoniwezesha mimi kufikia mafanikio.

Tukutane kwenye ukurasa wa 34 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA

NENO LA LEO; Hasara Ya Kutokuwa Bora.

“If your're not practicing, somebody else is, somewhere, and he'll be ready to take your job.” Brooks Robinson
Kama hujifunzi na kufanya kazi yako kwa ubora kuna mtu mahali fulani anafanya hivyo na yuko tayari kuchukua kazi yako.
Katika ulimwengu wa sasa ni muhimu sana kujifunza na kufanya chochote unachofanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Iwe ni kazi au biashara, kama unafanya kawaida(hovyo) kuna mtu yuko vizuri sana na atakuondoa kwenye kazi hiyo.
SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…
Chochote unachokifanya kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.
Nakutakia siku njema.

Sunday, February 1, 2015

SIRI YA 2 YA MAFANIKIO; Tumia Chochote Kitakachokuwezesha Kufikia Malengo Yako.

Watu wenye mafanikio mara zote wanatafuta chochote kitakachowawezesha kufikia malengo yao.
Watu wenye mafanikio wanaangalia mbele ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuzitumia fursa zinazojitokeza mbele yao.
Anza kuangalia mbele. Fikiria mbele na panga mbele, utakuwa katika nafasi nzuri ya kutumia fursa zitakazojitokeza wakati wengine wakiwa bado wanasinzia.

“The time to repair the roof is when the sun is shining.”  - John F. Kennedy  

SIRI YA 1 YA MAFANIKIO; AMUA KUFANIKIWA.

Siri ya kwanza kabisa ya wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni kuamua kufanikiwa.
Amua kwamba maisha yako yatakuwa bora zaidi ya yalivyo sasa.
Pia kuwa tayari kulipa gharama ya mafanikio.
Watu waliofanikiwa wanajua ili kufanikiwa kuna gharama unatakiwa kulipa.
Weka malengo, fanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuwa mvumilivu na mafanikio utayafikia.

“Success is to be measured not so much by the position that one has reached in life as by the obstacles which he has overcome while trying to succeed.”  - Booker T. Washington

Kitu Kimoja Cha Kufanya Kila Siku Ili Ufikie Malengo Yako 2015…

Mpaka sasa umeshajifunza mbinu nyingi sana za kukuwezesha kufikia malengo uliyojiwekea kwa mwaka huu 2015.

Kama una malengo na mipango tayari ni muhimu sana kutumia yale unayojifunza ili uweze kufikia malengo yako.

Mpaka kufikia leo kuna watu ambao tayari wameshasahau malengo waliyokuwa wamejiwekea kwa mwaka huu 2015. Hii inatokana na kuweka malengo kishabiki na kutokufuata kanuni muhimu z akuweza kuyafikia.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Ili uweze kufikia malengo yako unahitaji kuyafanya yawe kwenye akili yako kila siku na kila mara. Bila ya kujali ni hali gani unayopitia hutakiwi kuondoa mawazo yako kwenye malengo yako.

Leo utajifunza mbinu moja muhimu sana itakayokuwezesha kuyaweka malengo yako kwenye akili yako kila mara.

Mbinu hii ni kujiwekea utaratibu wa kuandika malengo yako kila siku asubuhi kabla ya kuianza siku yako. Yaani kila siku unapoamka andika malengo yako makubwa kwenye karatasi(ni vyema ukawa na kitabu) na tarehe ambazo utakuwa umefikia malengo hayo.

SOMA; Kozi 1100 Unazoweza Kujifunza Bure Kupitia Mtandao.

Kwa kufanya hivi utaianza siku yako kwa kufikiria ni nini cha kufanya ili uweze kufikia malengo hayo. Malengo yako yanakuwa kwenye akili yako muda wote na inakuwa rahisi kwako kuziona fursa za kukuwezesha kufikia malengo hayo.

Kumbuka kila siku kuandika malengo yako, haitakuchukua muda mrefu, dakika chache tu ila itakuletea faida kubwa. Usione ni kitu kidogo, kina matokeo makubwa kwako.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia malengo yako kwa mwaka huu 2015.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Ni Muda Unaenda Haraka Au Wewe Unaenda Taratibu?

Kufumba na kufumbua mwezi wa kwanza hatunao tena...
Tuko mwezi wa pili na siku sio nyingi tutauanza mwezi wa tatu.
Ni majuzi tu tulikuwa tunasherekea mwaka mpya, sasa hivi ni kama umechakaa.
Muda unakwenda haraka eh?
Hiki ndio kila mtu anachosema, kwamba muda unakwenda haraka sana.
Lakini je ni kweli?
Ni kweli muda unakwenda haraka au sisi tunakwenda taratibu?
Kipimo cha muda tunachotumia ni kile kile ambacho tumetumia miaka mingi iliyopita.
Iwe ni kwa kutumia saa, machweo na mawio na hata mzunguko wa mwezi. Vyote hivi havbijabadilika.
Ila sisi tunaona mabadiliko, muda unakwenda haraka sana.
Kwa dhana hii ya kwamba vipimo vyetu vya muda havijabadilika, ni dhahiri kamba sisi ndio tunakwenda taratibu.
Na kama tusipogundua mapema tutazidi kubaki nyuma.
Tufanye hima, muda hautusubiri.

UKURASA WA 32; Mambo Yanapokuwa Magumu…

Mambo yanapokuwa magumu, huu ni uhakika, yatakuwa magumu, unafanya nini?

Umeshaweka malengo na mipango yako vizuri.

Umeshajitoa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

Umekazana kwa juhudi zako zote, umekuwa mvumilivu lakini mambo hayae kabisa, huoni mabadiliko yoyote.

Unafanya nini? Unakubali kwamba lengo hili haliwezekani na hivyo unaachana nalo? Kosa kubwa sana.

SOMA; Jambo Muhimu La Kufanya Leo Jumapili Usiku.

Hata mambo yawe magumu kiasi gani, usibadili lengo, bali badili baadhi ya mipango au njia ambazo unaona hazizai matunda.

Ukibadili lengo umekwisha, maana hata ukiweka lengo jingine yatajirudia hayo hayo.

Hivyo usibadili lengo, bali badili baadhi ya mbinu au mipango ambayo haionekani kuleta matokeo unayotaka.

TAMKO LA LEO;

Mambo yatakapokuwa magumu sitabadili lengo bali nitabadili mipango na mbinu ambazo hazileti mabadiliko mazuri. Najua nikibadili lengo langu nitakuwa nimejiondoa mwenyewe kwenye safari ya mafanikio.

Tukutane kwenye ukurasa wa 33 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Mambo Matano Ambayo Viongozi Bora Hufanya Kila Siku.

NENO LA LEO; Muda Wa Wewe Kuwa Bora..

”You don't must be great to beginning, but you should start to end up being great” Zig Ziglar

Sio lazima uwe bora wakati unaanza, ila ni lazima uanze ukijua utakuwa bora mwishoni.

Hakuna mtu anayeanza kitu akiwa bora, ila ubora unapatikana kadiri unavyokwenda.

Kama utakuwa mtu wa kujifunza na kutokata tamaa ni lazima utakuwa bora.

Anza sasa na usijali ubora ambao kwa sasa huna.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Mambo Matatu Muhimu Ya Kufanya Siku Ya Jumapili Ili Kuwa Na Wiki Yenye Mafanikio