Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, June 10, 2015

UKURASA WA 161; Hiki Ndio Kinachokuzuia Wewe Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako.



Hakuna wakati bora wa kuwa hai kama sasa. Huu ni wakati bora sana kwa mimi na wewe kuwa hai hapa duniani. Hii ni kwa sababu kuna uhuru mkubwa sana wa kuweza kufanya kile ambacho kila mmoja wetu anapenda kufanya.
Huhitaji tena kupewa ruhusa ndio uweze kufanya kile ambacho unataka kukifanya. Unahitaji kujiruhusu wewe mwenyewe na kuanza kufanyia kazi mawazo yako na hatimaye yakakufikisha kwenye mafanikio makubwa sana.
Lakini pamoja na uhuru huu mkubwa bado watu wengi wanashindwa kujipa ruhusa na kusubiri mtu aje kuwapa ruhusa. Hili ni kosa kubwa sana linalowazuia wengi kufikia uwezo mkubwa ambao upo ndani yao.
Kama hutajiruhusu wewe mwenyewe hakuna atakayekuruhusu. Hii ni kwa sababu hao unaosubiri wakuruhusu hawajui ni nini hasa kipo ndani yako. Hivyo kuwategemea waweze kukitoa ni sawa na kupoteza muda wako bure.
Jipe ruhusa ya kuishi maisha ambayo unayataka na kuyafurahia na sio kuishi kwa sababu ndivyo wengine wanataka uishi. Una muda mchache sana hapa duniani, miaka 100 ijayo hutakuwepo hapa tena, hivyo haijalishi watu wengine wanakufikiriaje, haitadumu kwa zaidi ya miaka 100.
Ni afadhali uishi yale maisha ambayo ni bora kwako na huenda ukaacha alama kwenye maisha ya wengine na hata baada ya miaka hii 100 ukaendelea kukumbukwa. Ila kama utakuwa mtu wa kufuata kundi, kufanya kile ambacho kila mtu anafanya au anategemea ufanye hakuna kikubwa utakachofanya na hakuna atakayekukumbuka miaka 100 ijayo.

TAMKO LA LEO;
Najua nisipojipa ruhusa mwenyewe hakuna atakayenipa ruhusa. Ni mimi mwenyewe ninayejijua vizuri na ni kitu gani ninataka na ninaweza kufanya vizuri. Sitasubiri mtu anipe ruhusa, sitafanya kwa sababu kila mtu anafanya na sitafanya kwa sababu watu wanataka nifanye. Nitafanya kwa sababu ndio kitu hasa ninachotaka kufanya na ndio kitu ninachofurahia kufanya kwenye maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 162 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tuesday, June 9, 2015

UKURASA WA 160; Poteza Vitu Vyote Ila Sio Hiki Kimoja Muhimu.



Unaweza ukapoteza vitu vyote kwenye maisha yako, ndio namaanisha vyote. Iwe ni magari, nyumba, fedha zenyewe na kila kitu cha thamani ambacho umetumia nguvu nyingi kukipaya kwenye maisha yako. Ila utaweza kuvipata vyote kama hutapoteza kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiko utajifunza leo hapa baada ya muda mfupi.
Kabla hujajifunza kitu hiko, nikuambie kwamba kama wewe sio mwizi au fisadi na umeweka juhudi na maarifa kupata kile ambacho umekipata, basi una uwezo wa kupata vingine vingi zaidi ya ulivyonavyo sasa. Hii ni kwa sababu wewe una uwezo wa kutengeneza kipato. Wewe una kitu fulani ambacho ukikifanya, watu wanakuwa tayari kukupa wewe fedha. Iwe ni kazi au biashara au hata kipaji fulani unachotumia, lakini watu wanakuwa tayari kukulipa wewe kwa kile unachofanya.
Tunaita kitu hiki uwezo wa kutengeneza kipato na ndio kitu unachotakiwa kukilinda kwenye maisha yako. Poteza kila kitu kwenye maisha yako, lakini usipoteze uwezo wako wa kutengeneza kipato. Maana ukishapoteza uwezo huu, na wewe umepotea. Ila utakapoendelea kuwa na uwezo huu, hata kama utapoteza vitu vingine vingi ulivyonavyo utaweza kuvirudisha.
Kuna faida nyingine kubwa ya kujua uwezo wako wa kutengeneza kipato, hii itakuletea uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako. Kuna watu ambao wanafikiri wameajiriwa kwa huruma tu, na hivyo kuogopa kupoteza ajira zao kwa sababu hawatapata ajira nyingine au kipato kingine. Hii sio kweli kabisa, japo waajiri wanataka wewe uamini hivyo. Kama ungekuwa umeajiriwa kwa huruma ungeshafukuzwa zamani sana, kuna thamani ambayo unaitoa na ndio maana unalipwa. Jua thamani hii na iboreshe zaidi, hata ukiamua kuondoka kwenye ajira hiyo unajua uwezo wako wa kutengeneza kipato bado unao.
Unawezaje kujenga uwezo huu wa kutengeneza kipato? Kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo unajifunza. Na kitu cha kwanza ninachokushauri ufanye, kama bado hujafanya, soma kitabu JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA. Hapa utaweza kujua mabadiliko muhimu kwenye kazi au biashara yako na hivyo kuendelea kukuza kipato chako zaidi. Kama hujasoma kitabu hiki kisome sasa, kama huna mpango wa kukisoma umeamua mwenyewe kukataa uhuru wako.
TAMKO LA LEO;
Hata kama nitapoteza kila kitu, nitalinda kitu kimoja muhimu sana, kitu hiki ni uwezo wangu wa kutengeneza kipato. Hii ndio silaha yangu kubwa itakayoniwezesha kushinda kwenye ulimwengu huu ambao una changamoto nyingi. Nitaendelea kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo najifunza ili nikuze na kuimarisha uwezo wangu wa kutengeneza kipato. Najua nikipoteza uwezo huu ndio nimepoteza kila kitu kwenye maisha yangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Monday, June 8, 2015

UKURASA WA 159; Njia Bora Ya Kuweza Kufanya Kitu Unachohofia Kufanya.



Hofu ni moja ya vitu ambavyo vinawazuia watu wengi kuweza kupiga hatua kwenye maisha yao. Hofu imewafanya watu wengi kushindwa kuzichangamkia fursa zinazowazunguka na hivyo kushindwa kufikia mafanikio kwenye maisha.
Moja ya hofu kubwa zinazowazuia wengi kupata maendeleo ni hofu ya kupoteza. Mtu akishakuwa na kitu, hufanya kila lililo ndani ya uwezo wake ili kulinda kitu hiko. Hakuna anayependa kupoteza kitu ambacho amekifanyia kazi kwa muda mrefu.
Lakini pia kuhofia kupoteza kitu ulichonacho maana yake utashindwa kuchukua hatua kwenye fursa mbalimbali zitakazojitokeza. Kama tunavyojua kwenye maisha, kitu chochote kizuri huwa kinakuja na hatari zake(risk). Hivyo ili upate faida ni lazima ufanye kitu ambacho kinaweza kuwa hatari kwako. Unakuwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza kama ilivyo kwenye kupata.
Unapojikuta kwenye hali ya hofu kama hii, pia kiasi ambacho unaweza kupoteza na pia pima kile ambacho utakipata kama ukichukua hatua. Pia pima ni kitu gani unajifunza kama utachukua hatua na ukapoteza. Pia angalia njia nyingine unazoweza kutumia kupunguza hatari hiyo. Baada ya hapo chukua hatua mara moja.
Watu wengi watakuambia chukua risk, fanya na utajifunza, ila usiingie kichwa kichwa, hakikisha  hata kama utapoteza basi kuna somo utajifunza.

TAMKO LA LEO;
Najua hofu imekuwa inanizuia kufikia malengo yangu kwenye maisha. Hofu ya kupoteza imekuwa inanizuia mimi kuzichangamkia fursa zinazojitokeza. Kuanzia sasa nitakuwa nafanyia kazi fursa inayojitokeza kwa kuhakikisha hata kama ninapoteza kuna somo kubwa ninalojifunza.

Tukutane kwenye ukurasa wa 160 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.