Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, June 27, 2015

UKURASA WA 178; Lakini Nitapitwa.... (Sababu Ya Kijinga Inayokufanya Upoteze Muda)

Kama umejitoa ili kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unahitaji kujifunza jinsi ya kutumia muda wako vizuri. Na kwa kuwa siku ina masaa 24 tu na hakuna anayeweza kuyazidisha, hakuna njia ya kuongeza muda ambao tunao.
Kwa kuwa tunahitaji muda mwingi zaidi wa kufanya kile tunachofanya kwa ubora, basi tunahitaji kupunguza mambo mengi tunayofanya ili tuokoe muda mwingi.
Ili kupata muda mwingi nimekuwa nawashauri watu kufanya yafuatayo, ambayo hata mimi nafanya; usifuatilie habari, punguza sana muda unaotumia kwenye mitandao ya kijamii, tenga muda wa kuwa mbali na simu yako pale ambapo unafanya kazi inayohitaji umakini wako.
Watu wamekuwa wakipinga sana baadhi ya mambo haya, hasa kutokufuatilia habari au kukaa mbali na simu. Watu wamekuwa wakisema lakini nitapitwa.....
Najua na wewe unaona usipoangalia au kusoma habari siku moja unaona unapitwa. Yaani unapitwa na habari ya mtu aliyejinyonga huko mpanda, ukishaisikia inakusaidia nini? Utaniambia kuna habari muhimu kuhusu mambo yanayoendelea. Kama habari ni muhimu kweli zitakufikia tu. Kwa mfano kama nchi inaingia vitani, utajua hata kama huangalii habari. Lakini mambo ya mgombea gani kapata wadhamini wangapi sio habari za mtu makini kushabikia, ni kupoteza muda wako.
SOMA; Unacho Kila Unachohitaji Ili Kufanikiwa.
Asilimia kubwa ya watu wanaotumia simu ni kama wamefunga ndoa na simu hizo. Kila dakika mtu upo na simu na hazipiti dakika tano unaangalia kama kuna mtu katuma ujumbe au kapiga hukusikia. Na hata unapokwenda kulala, unaiweka pembeni ya kichwa chako, ili usipitwe. Unapoteza muda mwingi sana, ni vigumu kufanya kazi yenye maana huku unajibu ujumbe wa simu au kupokea simu kila mara. Ni afadhali uweke simu hiyo kimya kabisa na ufanye kazi yako, bila ya kuiangalia. Utasema lakini watu watanipigia na kunikosa, nitakosa dili nzuri. Ukweli ni kwamba, na hapa nakuambia kwa uzoefu, kama mtu ana shida ya kuwasiliana na wewe kweli, atakutafuta hata mara kumi. Ila anayepiga mara moja na kuacha, hata ukija kumpigia baadae hakuna jambo kubwa na la haraka sana alilokuwa anakuambia. Mwingine atasema labda mtoto wangu ataumwa ghafla inabidi nipate taarifa, sawa umeshazipata unafanya nini? Maana hata kama wewe ni daktari huwezi kumtibu mtoto wako, itabidi apelekwe tu hospitali. Sisemi usikae na simu siku nzima, bali masaa machache hivyo taarifa hizi utazipata baadae na utafanya maamuzi sahihi, huku umeshakamilisha kazi uliyopanga kufanya.
TAMKO LA LEO;
Nimekuwa najidanganya kwamba nitapitwa na hivyo kuwa karibu na habari, kuwa karibu na mitandao na kuwa karibu na simu yangu kila mara. Hali hii imekuwa inanipotezea muda wangu mwingi kwa kufuatilia vitu visivyo na maana na kukosa muda w akufuatilia yale ambayo yataniletea mafanikio. Kuanzia sasa natenga muda wangu wa kufanya mambo muhimu na muda huu hautaingiliwa na kitu kingine chochote.
Tukutane kwenye ukurasa wa 179 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment