Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, June 28, 2015

UKURASA WA 179; Unataka Kuwazidi Wengine? Umeshapotea.

Kwanza kabisa nikiri kwamba mimi huwa napinga sana dhana ya kushindana. Ndio kuna wakati ushindani unaonekana ni mzuri, lakini tatizo linakuja kwamba ukishakuwa na akili ya kushindana ndio unadumaa.
Kama unakuwa na akili ya kushindana maana yake lengo lako kubwa ni kuwazidi wengine. Kuwa wa kwanza, kuwa bora zaidi ya wengine.
Sasa tuseme labda unafanya biashara eneo ambalo watu wanafanya biashara kwa mitindo ya kizamani. Mtu akipata faida kidogo siku moja kesho yake analala, anaona amewini maisha. Na wewe ukawa unashindana nao, unafikiri utafika wapi?
Au tuseme unafanya kazi kwenye eneo ambalo kila mtu anakazana kununua gari na wewe ukawa na akili ya kushindana, unafikiri mafanikio yako makubwa kwenye maisha yatakuwa nini. Ukishanunua gari bora zaidi ya wengine tayari umekwisha. Utaonekana wewe ndio wewe na kile kiroho chako cha kushindana kitafurahi, kitakufanya uone maisha umeyamaliza.
SOMA; Sheria Tatu Muhimu Za Kufanikiwa Kwenye Maisha.
Lengo lako sio kuwa zaidi ya wengine, kama unataka kufikia mafanikio makubwa. Bali lengo lako ni wewe kuwa bora zaidi yako wewe mwenyewe. Wewe kuwa bora kuliko wewe mwenyewe. Wewe kuwa mbele yako mwenyewe. Hii ina maana kwamba leo uwe bora zaidi ya ulivyokuwa jana, leo ufanye kazi yako au biashara yako kwa ubora zaidi kuliko ulivyokuwa unafanya siku zilizopita. Leo upate kipato kikubwa zaidi ya ulichopata siku zilizopita. Leo upate mteja mpya tofauti na uliokuwa nao zamani.
Hiki ndio unatakiwa kupigania, hiki ndio unatakiwa kufanya kila siku. Na sio kuingia kwenye mbio za kundi na kujiingiza kwenye mashindano ambayo hujui hata yanakupeleka wapi.
TAMKO LA LEO;
Najua kukazana kuwa bora zaidi ya wengine ni kupoteza muda wangu na kujizuia kufikia mafanikio makubwa. Kuanzia sasa nitakazana kuwa bora zaidi yangu mwenyewe, nitakazana kuwa mbele yangu mwenyewe, kwa sababu najua kuna uwezo mkubwa uliopo ndani yangu ambao bado sijautumia. Nitahakikisha nautumia sasa ili niweze kufika mbali zaidi ya hapa nilipo sasa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 180 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment