Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, June 30, 2015

UKURASA WA 181; Kitu Cha Kufanya Pale Watu Wanapokuwa Hawakuamini Kama Unaweza.

Kama unataka kufanya jambo jipya, kama unataka kufanya jambo tofauti na wengine walivyozoea kufanya, naweza nikakuhakikishia jambo moja, WATU HAWATAKUAMINI.
Watu hawatakuamini kwamba unaweza kufanya jambo hilo. Watu hawatakuamini kwamba kuna uwezekano wa jambo hilo kufanyika kwa tofauti. Na hapa ndipo watu wengi hukata tamaa na kuamua kuacha. Na hivyo watu wale walioshindwa kuwaamini mwanzo wanakuwa sahihi na wanazidi kupata nguvu ya kuwaambia wengine kwamba hawawezi au haiwezekani.
Leo nataka nikuulize, je unajua unatakiwa kufanya nini pale ambapo watu hawakuamini kwamba unaweza? Au umekuwa mtu wa kukatishwa tamaa mara nyingi na wewe kukubali?
Sasa kuna kitu kimoja muhimu sana unachotakiwa kufanya pale ambapo watu hawakuamini kama unaweza. JIAMINI WEWE MWENYEWE. Wewe ndio umekuja na mawazo hayo uliyonayo, wewe ndiye ambaye umekuwa unafikiria usiku na mchana jinsi unavyoweza kubadili hali ya mambo. Wewe ndiye uliyefikiria na kuona kuna njia mbadala na ambayo inawezekana. Sasa kwa nini ukubali kumsikiliza mtu ambaye amefikiria kwa upande mmoja tu wa kwamba vitu haviwezekani?
SOMA; Hukuja Na Maelekezo Kwa Mtumiaji Na Kwa Nini Ufurahie Hili.
Kama utawasikiliza watu hawa utakuwa hujajitendea haki kabisa, kwa sababu hata watu hawa sio kwamba wana uhakika haiwezekani, ni vile tu hawajawahi kuona mtu mwingine akifanya hicho unachotarajia kufanya.
Kama watu hawaamini kwamba unaweza, huo ndio wakati wa kujiamini na hata kufurahia sana kwenye maisha yako. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu unapoanza kufanya kitu ambacho wengi wanaona hakiwezekani, jua unafanya kitu ambacho sio cha kawaida, unafanya kitu kikubwa. Na mafanikio yanakuja kwa kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba pale ninapopanga kufanya jambo kubwa, watu wengi watashindwa kuniamini. Huu ni wakati muhimu sana wa mimi mwenyewe kujiamini na kuendelea kuweka juhudi. Hakuna mafanikio yanayokuja kwa kufanya vitu ambavyo ni vya kawaida. Hivyo ninapoona watu hawaniamini kwa kitu kikubwa ninachotaka kufanya, najua hapo ndio penye mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 182 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment