Ni vizuri sana kujifunza kutoka kwa viongozi waliofanikiwa maana hapa unapata njia ya vitu gani vya kufanya ili na wewe uweze kufanikiwa kama kiongozi.
Ni vizuri pia kujifunza kutoka kwa viongozi walioshindwa kwa sababu kupitia kushindwa kwao unajua ni vitu gani vimewafanya washindwe na hivyo kuviepuka ili na wewe usiishie kushindwa kama wao.
Leo tutaangalia tabia tatu za viongozi dhaifu na jinsi ya kuepuka kuwa kiongozi dhaifu.
1. Husita kufanya maamuzi magumu.
Viongozi wote hufikia wakati ambao wanahitaji kufanya maamuzi magumu ili kubadili hali ya mambo. Maamuzi haya yanaweza kuwa na madhara fulani ila kutokufanya maamuzi hayo kunaleta madhara makubwa zaidi mbeleni.
Viongozi dhaifu husita na kuchelewa kufanya maamuzi magumu na hivyo kujikuta kwenye matatizo makubwa zaidi.
2. Hulalamika kukosa rasilimali.
Viongozi hafifu hulalamika kila mara kwamba wamekosa rasilimali fulani ndio maana wameshindwa kufanikiwa. Hutumia muda mwingi kulalamikia rasilimali wanazokosa badala ya kutumia rasilimali walizoko nazo katika kufikia mafanikio.
3. Huepuka majukumu.
Viongozi hafifu hukwepa majukumu yao na kutafuta njia rahisi kwao. Kwa kuepuka huku majukumu wanashindwa kufikia mafanikio na kwa kutafuta njia rahisi wanapata njia ambayo inawapeleka kwenye kushindwa.
Epuka tabia hizi tatu za viongozi hafifu ili uweze kuwa kiongozi bora na uweze kufikia mafanikio makubwa.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.
kweli kabisa lazima watu wajifunze jinsi namna ya kuongoza watu wa aina tofauti kulingana na akili zao, ufahamu wao, uelewa wao. tutambue kuwa kumuongoza mtoto ni tofauti na kumuongoza mtu mzima .
ReplyDeleteKwel kabisa
ReplyDelete