Binadamu wote tuna tabia ambazo ni za asili kabisa. Hizi ni tabia ambazo kila mtu anazo. Tabia hizi zinaweza kuwa nzuri au mbaya.
Tofauti kubwa ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni kwenye matumizi ya tabia hizi.
Leo utajiongeza kwa tabia hizi na jinsi ya kuzitumia kufanikiwa.
1. Uvivu
Kwa asili binadamu wote ni wavivu. Ni kutokana na uvivu ndio maana kila siku binadamu wanatafuta njia ya kutahisisha ufanyaji wa mambo.
Tumia uvivu wako sio kwenye kutega kazi bale kwenye kufikiria njia rahisi ya kufanya kazi unayofanya sasa ili kuboresha zaidi.
3. Tamaa
Binadamu wote tuna tamaa, kila mtu anapenda kupata zaidi. Kama kuna kazi mbili ambazo ziko sawa kabisa moja unalipwa milioni moja ja nyingine unalipwa milioni moja na nusu, utakubali ile ya milioni moja na nusu. Hii ni kwa sababu una tamaa ya kupata zaidi.
Unaweza kutumia tabia hii kwenye kazi au biashara na hivyo kuhakikisha yule unayemhudumia ajisikie anapata zaidi ya alicholipia. Hii itakufanya wewe ufanikiwe sana.
3. Ubinafsi
Hata uwe na mtu unampenda kiasi gani, inapotokea hatari kila mtu anafikiria ni jinsi gani ya kuokoa maisha yake. Katika mambo yote mtu hujifikiria yeye mwenyewe kwanza ni jinsi gani ananufaika au kuumia.
Hivyo unapofanya kazi au biashara mpatie mteja wako uhakika wa kuwa bora zaidi kwa bidhaa au huduma unayompa.
4. Ufahari/kujivuna
Kila mtu ana majivuno au kupenda kuonekana yeye ndiye aliyefanya kitu fulani na asifiwe kwa hilo. Tumia tabia hii kuwashawishi watu wakupatie kile unachotaka, kwankuangalia ni kitu gani wanafanya vizuri na wewe kukisifia.
5. Ujinga
Kila mtu ni mjinga kwenye kitu fulani. Profesa wa uchumi ni miinga kabisa kwenye sayansi ya uinjinia. Na hakuna mtu anayeweza kujua kila kitu.
Tumia nafasi hii kujua ni kitu gani unaweza kujifunza ili kuwafundisha wengine ambao wanakihitaji sana.
Tumia tabia hizo tano ili kuweza kufikia mafanikio.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment