Mambo yote yanayotokea kwenye maisha yako yanatokana na tabia ulizojijengea.
Kama maisha yako sio mazuri hii ina maana kuna tabia unazofanya zinazokuletea maisha hayo.
Hizi hapa ni tabia tano unazoweza kujijengea na ukaboresha maisha kwa kiwango kikubwa.
1. Kuamka asubuhi na mapema.
Hii itakufanya kuwa na muda zaidi wa kufanya mambo yako. Anza l
Kwa kuamka saa moja kabla ya muda uliozoea kuamka.
2. Kusoma angalau nusu saa kila siku.
Kwa kufanya hivi utapata maarifa mengi sana.
3. Kufanya mazoezi.
Itaimarisha afya yako na kukuepusha na magonjwa yatakayoweza kukurudisha nyuma.
4. Kunywa maji mengi.
Utakuwa na afya bora na utafanya kazi kwa ufanisi zaidi.
5. Kusema HAPANA.
Huwezi kufanya kila kitu, jinsi utakavyoweza kusema hapana kwa mambo ambayo hayana faida kwako ndivyo utakavyopata muda mwingi wa kufanya mambo yenye maana.
Jenga tabia hizo tano na kila siku tembelea mtandao huu wa JIONGEZE UFAHAMU ili kujifunza zaidi.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment